MADA 2 : MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI UWASILISHA NA
UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa,
kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji wake.
AU
Ni sanaaa ambayo hutumia mazungumzo na matendo katika
kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa kwa watazamaji au wasikilizaji.
Mazungumzo hayo huwa katika mfumo wa masimulizi kwa kuumbwa,
kutambwa, kuganwa au kutongolewa.Fasihi simulizi hueleza jamii kiutamaduni,
kiuchumi na kisiasa, fasihi huzungumzia juu ya yale mambo ambayo huzunguka
jamii husika, fasihi simulizi huathiriwa sambamba na mabadiliko ya jamii na kwa
hiyo nayo hubadilika kimaudhui na kifani kufuatia mabadiliko ya mifumo ya
kisiasa, kiuchumi, na kijamii.
Fasihi simulizi ni utanzu wa Sanaa ambao hukua na kubadilika
kutokana na mabadiliko ya wakati na mifumo ya jamii.
VIPENGELE MUHIMU VYA FASIHI SIMULIZI
(a) Msimulizi (fanani)
Huyu huwa ni mtu
ambaye anaitamba hadithi, kuimba wimbo, kusimulia au kutoa vitendawili au
methali.
(b) Wasikilizaji au watazamaji (Hadhira)
Hawa ni washiriki katika kutazama au kusikiliza fani ya fasihi simulizi
na mara nyingine huwa wanatumiwa na fanani kama wahusika katika fani yake
(c)
Mandhari
Hili ni jukwaa au mahali ambapo tukio la kifasihi (fasihi simulizi)
litatendeka.Pahali au mahali hapo yaweza kuwa nyumbani, uwanjani, kuzunguka
moto, baharini n.k.
(d)
Tukio/Dhana
inayotendeka
Hili huwa ni tendo linalotendeka kwa jukwaa la fasihi simulizi. Tendo
hili kaweza kuwa ni usimulizi wa hadithi, kutega vitendawili, kuimba nyimbo au
wimbo au kutoa methali.
SIFA ZA FASIHI SIMULIZI.
1.
Fasihi simulizi ina sifa ya utendaji ambao
hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati mmoja.Hii humfanya fanani aweze
uonyesha baadhi ya matendo katika usimulizi wake kama vile kutumia viungo vya
mwili kwa kuchezesha midomo, kukunja uso, kubinya macho, kuchezesha mabega n.k.
2.
Fasihi
simulizi ina sifa ya kuwepo kwa fanani ambaye huweza kusimulia kwa kuimba,
kusoma kwa sauti au kubadilisha mtindo wa usimuliaji wake,fanani huweza kufanya
yote hayo kama akiona hadhira yake imechoka kusikiliza.Pia ana uwezo wa kuona
kama ujumbe wake umeeleweka au la!
3.
Fasihi simulizi ina sifa ya kuwepo kwa
washirikishwaji wa fanani na hadhira, hadhira hushiriki kwa kuuliza maswali
kupiga makofi kuimba kutegemea jinsi atakavyoishirikisha.
4.
Fasihi simulizi zina sifa ya kwenda na wakati na
mazingira tabia hii inatokana na jinsi fasihi simulizi inavyoenea wasikilizaji
huwa wengi na hata kama tanzu za fasihi simulizi zilipitwa na wakati zinaweza
kubadilishwa na fanani ili zisadifu mazingira maalumu ya wakati huo.
5.
Fasihi simulizi huzaliwa, hukua, huishi hata
kufa hii inasababishwa na mabadiliko ya mazingira ambayo hufuata mfumo wa
kihistoria wa jamii, mfano kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya
kuhifadhi fasihi simulizi katika maandishi ya fasihi simulizi huonekana chapwa
kwa sababu ya mambo kama vile miondoko au ngoa, vinakuwa havimo.
6.
Fasihi simulizi ina sifa ya kuwa na uwanja
maalumu wa kutendea. Fasihi simulizi huwa na sehemu kwa ajili ya aina fulani ya
fasihi simulizi itakayofanyika na wahusika mfano tambiko huwa na sehemu maalumu
ya kutambikia kama vile sehemu yenye pango,kwenye mti mkubwa kama vile mbuyu,
njia panda, makaburini n.k.Hivyo ni wazi kwamba fasihi simulizi inahitaji
uwanja wa kutendea yenye kuhusisha vitendo.
7.
Fasihi simulizi ina sifa za kuwa mali ya jamii
nzima.Tangu zake zote zikishatendwa humilikiwa na jamii kwa pamoja na hii ndiyo
inayopatiwa uwezo wa kurithishwa kizazi kimoja hadi kingine.Hivyo huwafikia
watu wengi hata wale wasiojua kusoma na kuandika.
UWASILISHAJI NA UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
(a) UWASILISHAJI WA FASIHI SIMULIZI
Uwasilishaji
hutumiwa kuelezea njia au mtindo unaotumiwa kufanya kazi ya kifasihi iwafikie
walengwa .Mfano uwasilishaji wa maigizo ni kutendwa kwake jukwaani mbali ya
hadhira ya watazamaji.Tangu zamani, uzalishaji wa tanzu za mbalimbali za fasihi
simulizi huwasilishwa kwa masimulizi ya mdomo na matendo.
Mattemi
(1983:27) Anasema fasihi simulizi ni fasii ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa
watumiaji wake hutegemea nyenzo mbalimbali za kuonekana na kusikikia zitumiwazo
na binadamu katika kujieleza binadamu hutumia Sanaa hii yam domo kuwa mwangaza
juu ya maisha yake ya kila siku.Hubuni hadithi, nyimbo, methali n.k.
zinazobaini hisia zao mbalimbali kuhusu maisha na mazingira yao.Fasihi simulizi
pia inaweza kuzungumzia historia ya watu wa jumuiya Fulani itikadi zao na mambo
mengine mengi wanayoyathamini katika kuishi kwa pamoja.
Kwa kuwa fasihi
simulizi haiandikwi kuhifadhiwa kwake kunategemea kuelimishana kwa mdomo kutoka
kizazi kimoja hadi kingine kwa njia hii kizazi kimoja kinaweza kuwasilisha
kizazi kingine yale mambo muhimu ambayo kinataka yaendelee katika jamii hiyo
mambo ambayo yamefungamana na mazingira yao maisha yao utamaduni wao na itikadi
zao.
(b)UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
UENEZAJI:
Ni dhana
inayotumiwa kueleza uhusiano unaokuwako kati ya hadithi za jamii
mbalimbali.Dhamira ya kimsingi ya nadharia hii ni kuonyesha kuwa inawezekana
kuwa jamii zinazohusika ziliingiliana kihistoria au kutokana na ukaribu wao wa
kijiografia kuingiliana huku kunaweza kuwa msingi wa kuwako kwa hadithi
zinazosimuliwa ambazo zinafanana
Mfano utenzi wa
Fumo Liyongo unapatikana katika jamii kadhaa za pwani ya Kenya kama waswahili,
wapokomo, wabajuru n.k. Inawezekana kuwa hupatikana huku ni tokeo la ueneaji
hasa kwa kuwa hizi ni jamii zinazokaribiana kijiografia za zilizohusiana
kihistoria
SABABU ZA KUENEA KWA FASIHI SIMULIZI.
a) Kuanzishwa kwa vikundi vya Sanaa na muziki.
Vikundi mbalimbali vya Sanaa na muziki vilianzishwa ambavyo
kazi yake ni kuendeleza tanzu mbalimbali za fasihi simulizi hapa nchini.Vikundi
vya Sanaa za maonyesho, Vikundi vya taarabu na muzikivinafanya kazi kubwa ya
kueneza na kuendeleza fasihi simulizi hapa nchini.
b) Muingiliano na fasihi andishi.
Kuenea kwa kazi ya fasihi simulizi kwa asili ni kwa mdomo na
masikio yaani usimulizi, hata hivyo maendeleo ya watu yamefanya baadhi ya kazi
za fasihi simulizi zienee kwa maandishi.Maandishi ni jitihada za kuhifadhi kazi
ya fasihi simulizi na kuifikisha mahali ili ikatambuliwe au isumimuliwe.Hadithi
mbalimbali kama vile
-Hekaya za Abunuasi
(1915)
-Hadithi za Esopo
(1890)
-Fasihi simulizi ya
mtanzania.Hadithi (1977) TUKI
Hizi zote zimehifadhiwa na kuenezwa kwa maandishi.
Fasihi andishi inatumia vipengele mbalimbali vya fasihi
simulizi katika uandishi wao na hivyo kuviendeleza vipengele hivyo kama vile
-Matumizi ya semi
mbalimbali
-Matumizi ya nyimbo
-Matumizi ya
hadithi ndani ya hadithi
-Matumizi ya mianzo
na mishilizo ya hadithi za fasihi simulizi
-Matumizi ya
majigambo, utani n.k.
Kwa sasa methali, vitendawili, nahau, vimewekwa katika
maandishi kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye na hivyo vinaenezwa kwa njia ya
maandishi.
c) Ufundishaji shuleni na vyuoni
Mfumo wa Elimu nchini nao umesaidia kueneza fasihi simulizi
kwa kiasi kikubwa hapa nchini kwa sasa fasihi simulizi ni somo linalofundishwa
toka darasa la kwanza hadi ngazi za juu (chuo kikuu)
Vile vile kuna vyuo hapa nchini vinavyofundisha baadhi ya
tanzu mbalimbali za fasihi simulizi kama vile Sanaa za maonyesho na muziki.
Mfano chuo cha Bagamoyo, Butimba, Nyegezi na chuo kikuu cha Dar-es-salaam.
d) Mabadiliko ya kiteknolojia.
Kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa sasa
fasihi simulizi inaenezwa kwa vyombo vya habari kama vile kaseti, redio, video,
luninga, mtandao wa kijamii n.k.Mfano Redio Tanzania (TBC) kupitia kipindi
chake cha “Mama na Mwana” “Watoto Wetu” vimesaidia sana kueneza fasihi simulizi
hapa nchini Tanzania katika vipindi hivi watu husimuliana hadithi mbalimbali
walizopatwa kusimuliwa hutegemea vitendawili humalizia methali kwa nyimbo
Luninga nazo zimesaidia sana kueneza fasihi simulizi nchini
kupitia vipindi mbalimbali vya michezo ya kuigiza.Hivyo mabadiliko ya Sayansi
na Teknolojia hayawezi kuwa fasihi simulizi
Mwingiliano wa mataifa mengine.
Katika mwingiliano muziki umesaidia sana kukuza fasihi
simulizi.Hali hii imesaidia kuleta muziki wa kizazi kipya (muziki wa kutoka
toka) pamoja na Rege vijana wa kizazi
kipya wamechota miundo na mitindo ya muziki kutoa nje na kuendeleza muziki wao
ingawa madhui bado wanajadili yale yale yaliyojadiliwa na wanamuziki wa zamani.
Matumizi ya fasihi simulizi katika Sayansi na Teknolojia
yamesaidia sana kuenea kwa fasihi simulizi kwani fasihi simulizi inapata
hadhira kubwa kwa wakati mmoja lakini hadhira hiyo haiyonani ana kwa ana na
fanani wao kwa kutumia vyombo hivyo vya Sayansi na Teknolojia.
ATHARI ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA UWASILISHAJI NA
UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Mwanzo fasihi simulizi iliwasilishwa na kuenezwa kwa njia ya
masimulizi ya mdomo hivyo fanani na hadhira walikuwa ana kwa ana wakati wa
uwasilishaji lakini zama hizi za Sayansi na Teknolojia, uwasilishaji na
uenezaji unaotumia vyombo vya habari kama vile redio, video, televisheni, kanda
kunasia sauti, mtandao na hata kompyuta, mara nyingi hasa hadhira haiwi ana kwa
ana na fanani hutokea hadhira ikawa inaangalia luninga au sinema au tamthiliya
jukwaani kwenye mazingira kama hiyo si rahisi hadhira kushiriki kikamilifu
katika utendaji.
Kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia fasihi
inaathiriwa katika vipengele vifuatavyo:-
1. Uwasilishaji. Mwanzoni fasihi simulizi inawasilishwa kwa njia ya
masimulizi yam domo hivyo fasihi na hadhira walikuwa wanaonana ana kwa ana
wakati wa uwasilishaji lakini katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia,
uwasilishaji wa fasihi simulizi unatumia
vyombo kama, vile redio, luninga, video, kanda, mtandao na hata kompyuta na sio
msanii awapo.
2. Uhifadhi, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia sasa fasihi
simulizi inaweza kuhifadhiwa vizuri Zaidi kuliko inavyofikiriwa na wanamapokeo.
Lakini leo hii fasihi simulizi inaweza kuwekwa katika mkanda wa kompyuta (flash
disc) CD, DVD, Maandishi n.k na ikaendelea kuwepo kwa miaka mingi sawa sawa na
fasihi andishi hata zaidi.
Kwa upande wa
video na DVD, uhifadhi wake huendelea kuonyesha vitendo na sauti huweza kudumu
hata zaidi ya maandishi katika fasihi andishi itatungwa vizuri.
3. Wakati na mahali, zamani fasihi simulizi ilifanyika sana saa za jioni,
kando ya moto au barazani. Aidha kwa vile fasihi simulizi hutolewa redioni
inaweza kusimuliwa wakati wowote na mahali popote ambapo kipindi kinasikika na
kwa saa na wakati huo. Majumbani, mijini watoto hawazunguki moto tena, bali
husubiri wakati kipindi kinaporushwa kwani siku maalumu na wanaizunguka luninga
au redio.
4. Hadhira au ushirikishwaji wa hadhira, zamani hadhira ya fasihi
simulizi ilikuwa inaonana ana kwa ana na fanani wake wakati wa uwasilishaji
wake. Hadhira iliweza kuchangia kazi ya fasihi hiyo na hata kuathiri uumbwaji
wake, ikaitwa hadira tende. Lakini katika muktadha wa maendeleo y sayansi ana
kwa ana na msimuliaji na sio lazima iathiri usimuliaji.
UHIFADHI WA KAZI ZA
FASIHI SIMULIZI
Kwa sasa fasihi simulizi inaweza kukusanywa na kuhifadhiwa
kwa njia zifuataz:-
a)
Kichwa, uhifadhi wa fasihi simulizi
ni katika vichwa vya watu kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Jambo hili
limekuwa likifanyika kwa muda mrefu sana. Hivyo kutokana na kuhifadhiwa katika
vichwa ndio maana fasihi simulizi itakuwa ikirithishwa katika kizazi kimoja
hadi kizazi kingine.
b)
Maandishi, Tangu maandishi
yagunduliwe baadhi ya kazi za fasihi simulizi zimekuwa zikihifadhiwa kwenye
maandishi kwa ajili ya kumbu kumbu ya baadaye. Kazi za fasihi simulizi
zikihifadhiwa katika maandishi inaweza kufanya watu wasijue ni simulizi au
andishi. Hata hivyo vidokezo kadhaa husaidia kazi za fasihi simulizi huwana
mianzo ya “Paukwaa! Au hadithi…….hadithi njoo” n.k. Aghalabu fasihi simulizi
huwana mtiririko wa moja kwa moja usio na urejeshi.
c)
Kanda za kunasia sauti (tepu rekoda),Hii
ni njia moja wapo inayotumika kuhifadhi tanzu mbali mbali za fasihi simulizi.
Kanda hizo hushika sauti pamoja na vidokezo vyake, kwa hiyo wasikilizaji ili
wapate wanachokitaka lazima wanunue kanda hizo.
d)
Kanda za video, luninga na filamu z
sinema CD, DVD na Kompyuta.
e)
Mtandao, pichaza video hurekodi sura na
sauti,Picha hizo hutebeana kuonyeshwa kwenye skirini ya video na
lunnga. Picha za sinema hupigwa kwa aina maalumu za kansera ambazo hupiga picha
za mfululizo katika utepe maalumu. Picha hizo huonyeshwa kwa mashine na
huonekana na zinatembea, kamera nyingi za sinema za siku hizi zina mitambo ya
kurekodi sauti pia. Hivyo kwa kutumia filamu za sinema na video tunaweza
kuhifadhi na kuonyesha kazi za fasihi simulizi.
ATHARI ZA MBINU MBALI MBALI ZA
UHIFADHI WA FASIHI SIMULIZI
KICHWANI
Uhifadhi wa kichwani una matatizo
yafuatayo:-
i)
Kumbukumbu za akili zinaweza kupungua au kufifia
au fanani kufa kabisa. Hali hii ikitokea fasihi simulizi hupotea.
ii)
Mtu anayehifadhi kichwani anaweza kubadilisha
mambo muhimu katika simulizi na hivyo kugeuza kiini cha masimulizi hayo.
iii)
Kutokana na mazingira pamoja na mabadiliko kuna
tatizo la kupata watu wanaoweza kuhifadhi kazi hiyo.
MAANDISHI
Uhifadhi
kwa kutumia maandishi una matatizo yafuatayo:-
Ø
Kuna mambo ya msingi ambayo hayawezi kuhifadhiwa
katika maandishi. Mambo hayo ni yale yanayohusiana na utendaji, sauti, vitendo,
toni, kuimba, muziki n.k. Matokeo ya kukosekana kwa vitu hivi ni kwamba ladha
au athari ya kazi inayowasilishwa hupungua.
Ø
Katika maandishi fasihi simulizi haina sauti kwa
hiyo msomaji anapaswa atie sautinna mahadhi yake mwenyewe. Shughuli hii inaweza
kuharibu au kufanya kazi ya fasihi ipungue ubora wake.
Ø
Hakuna uhusianao kati ya fanani na hadhira kwa
hiyo hadhira inashiriki kwa kuona maandishi.
Ø
Haibadiliki kutokana na wakati na mazingira.
Hivyo huweza kudumu katika hali ile ile kwa muda mrefu kama ilivyo fasihi
andishi.
Ø
Inakuwa ya ubaguzi au watu wachache yaani wale
wanaojua kusoma na kuandika. Wale wasiojua kusoma na kuandika itawawia vigumu
kuelewa fasihi hiyo iliyoko katika maandishi.
Ø
Ni gharama kubwa kuhifadhi masimulizi katika
maandishi, hii ni kwasababu uandishi hutumia kalamu na karatasi. Hivyo hapa
zinahitajika pesa za kununulia kalamu na karatasi na gharama za uchapaji.
KANDA ZA KUNASIA SAUTI
Uhifadhi huu una
matatizo yafuatayo:-
Ø
Kanda za kunasia sauti husikika sauti tu.
Matendo hayawezi kushikwa na hii kuathiri tena uhifadhi na utoaji wa kazi za
fasihi simulizi.
Ø
Hakuna ushirikishwaji wa hadhira kwani fanani na
hadhira hawaonani ana kwa ana kwa hiyo hadhira inashiriki kwa kusikiliza kanda
tu, sikio huathirika lakini jicho halioni.
Ø
Ni gharama kuhifadhi fasihi simulizi kwa njia
hii kwani kununua tepurekoda pamoja na kanda zenyewe, betri, spea hupatikana
kwa shida na kwa bei ghali licha ya hiyo si wote wenye uwezo wa kununua tepurekoda
hivyo ni watu wachache sana wenye uwezo wa kuhifadhi fasih simulizi kwa kutumia
chombo hiki.
Ø
Haitabadilika kulingana na wakati au mahitaji ya
hadhira. Huweza kudumu katika hali ile ile kwa muda mrefu kama ilivyo fasihi
andishi.
KANDA ZA VIDEO, LUNINGA, FILAMU ZA SINEMA, CD, DVD, VCD NA
KOMPYUTA
Njia hii ina matatizo yafuatayo:-
v
Upungufu wa ushirikishwaji wa hadhira,Hadhira
haiwezi kushiriki ila inasaidia kufanya fasihi simulizi kupata hadhira kubwa
ingawa hadhira hiyo haionani ana kwa ana na fanani wao.Kanda hizo huwa
zinatazamwa na watu wengi hivyo kupata hadhira wengi kwa wakati mmoja ambao
hawasiliani na fanani wao.
v
Ni gharama,kwani vitu hivyo vinahitaji pesa
nyingi za kununulia vifaa hivyo na watu wachache wenye uwezo wa kununua vifaa
hivyo.
v
Haitabadilika kulingana na mahitaji ya jamii au
hadhira au wakati.Huweza kudumu katika hali ile ile kwa muda mrefu kama ilivyo
fasihi andishi
v
Kanda hizi na vifaa hivyo vinahitaji mahali
pazuri ambapo panaweza kutunza vyombo hivyo kwa muda mrefu, endapo haitofanyika
hivyo kuna hatari ya kupoteza kilichohifadhiwa katika vyombo hivi.
KUHAKIKI KAZI ZA FASIHI SIMULIZI.
Kazi za fasihi simulizi zinaweza kupimwa na kuonekana kama
zinafaa au hazifai. Kazi hizi hupimwa kwa kuzingatia uhusiano wake na hali
halisi ya jamii.
Pia vipengele vya fasihi simulizi huangaliwa kwa kupima
ubora wa jinsi vilivyotumika.Upimaji wa ubora wa kazi ya fasihi simsulizi
hujumuisha umuhimu wa mambo yaliyosemwa katika jamii inayohusika au namna mambo
hayo yanayosemwa .
Hivyo mhakiki atajiuliza maswali kama:-
Ø
Ujumbe utolewao hapa ni wa kweli na una manufaa
au la!
Ø
Je maadili yatolewayo hapa yanalingana na wakati
tulionao?
Ø
Je nahau, misemo, methali na tamathali za semi
zinalingana na jambo linalosemwa au la!
Ø
Je mtiririko wa matukio unasaidia msikilizaji
kuelewa kisa au unamchanganya?
Maswali ya namna hiyo yanamsaidia mhakiki kuelewa ubora wa
kazi ya fasihi simulizi.Pia yaweza kutumiwa na mtunzi wa kazi ya fasihi
simulizi ili kurekebisha kazi yake na kuifanya iwe bora Zaidi.
FANI KATIKA FASIHI SIMULIZI
Wataalamu wengi wamejaribu kufafanua dhana fani katika
fasihisimulizi.Baadhi ya maoni ambayo yametolewa na Senkoro (1982:8) ni kuwa
fani katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaotumia msanii katika kazi yake
Mulokozi na kahigi (1978:53) wanasema, kutokana na maelezo
haya ya Senkoro inaeleweka kuwa fani ni ustadi au ubingwa au mbinu ambazo
msanii wa kazi ya fasihi hutumia katika kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira
yake.
Mulokozi na kahigi (1970:53) wanasema fani ni Sanaa na jumla
ya vipengele vya lugha vilivyowekwa katika mpangilio mahususi ili kutoa kwetu
maana Fulani kwa hadhira.
Taasisi ya ukuzaji mitaala (1988:168) wanasema fani ni umbo lililosanifiwa
ili kueleza hisia za fanani.
Kutokana na maelezo haya fani ni jinsi msanii
anavyojikanyaga umbo fulani na umbo hapa ni tanzu au aina ya Sanaa ili kueleza
hisia zake kwa lugha ya ufasaha.
Kwa mujibu wa watalamu tuliowanukuu,fani ni majumuisho ya
vipengele vyote vya fasihi ambavyo msanii hutumia katika juhudi za kuelezea
hisia au maoni yake kwa njia ya ufasaha.
VIPENGELE VYA FANI
1. TUKIO.
Kaika tanzu za fasihi simulizi mara nyingi ni lazima pawe na
jambo au tukio ambalo huchukuliwa kama kiini au chanzo cha utanzu
utakaohusishwa fani au utanzu unaotumiwa na msanii havubuki tu hivi hivi.Tukio
huwa ndio kishawishi cha fanani wa fasihi simulizi
Mfano: Nyimbo za unyago huibuka katika mazingira yake
methali za kutuliza zaweza kutumiwa pale ambapo pana mahonzi ya aina fulani kwa
hiyo ni lazima pawe na tukio ambalo kitachukua chemichemi ya utanzu
utakaotumiwa na fanani kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira.
2. MAZINGIRA/MANDHARI
Mazingira ni pale ambapo matukio ya fasihi simulizi
yaliibuka ama yalitokea.Ufundi wa kuchora mazingira unatoa picha halisi, picha
inayoonekana waziwazi juu ya mazingira yaliyohusika.
Fasihi simulizi hutegemea sana muktadha au mazingira maalumu
hivyo tungo za fasihi simulizi huwa zimejikita katika utamaduni wa jamii
zinamoibukia vifaa ambavyo vinatumika katika fasihi simulizi vinategemea
mazingira yanayohusika, mfano msanii anapodhaminia kutoa picha ya kuogofya
anatumia mazingira ambayo yanaogofya kama vile mazingira ya misituni na
wahusika kama majitu ili kuleta dhana ya hofu katika mazingira yake.
3.
MUUNDO
Katika fasihi
simulizi muundo ni mpangilio na mtiririko wa kazi ya fasihi simulizi kwa upande
wa visa na matukio.
Katika muundo
tunazingatia jinsi fanani alivyofuma na kuunda hata alivyounganisha tukio moja
na linguine kitendo kimoja na kingine wazo na wazo, ubeti na ubeti na mstari wa
beti na mwingine kuna muundo mbalimali katika tanzu mbalimbali za fasihi
simulizi kuna miundo kama vile muundo wa moja kwa moja na kuna miundo
changamano
Katika mashairi
kuna miundo mbalimbali ambayo hutumiwa kuainisha mashairi kwa kufuata idadi ya
mistari katika kila ubeti, miundo hii ndiyo hutupa mashairi ya tabria,
tathilitha, takhmisa na n.k.
Katika hadithi
na hata katika tamthiliya waweza kuwa na muundo ambao fanani ameanza kutokamwanzo
akaenda katikati na baadae kumalizia kisa chake aina hii ya muundo unaitwa
mtiririko visa au vitukio mbalimbali na vinaweza kuongezwa na kupunguzwa bila
kupoteza maana ya hadithi au tamthiliya.
4.
MTINDO
Katika kazi ya fasihi ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi yake na
huipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni na kaida zilizofuatwa
kama zilizopo ni za kimapokeo na ni za kipekee kwa mkururo wa maelezo hayo
unaweza kusema kuwa mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi
kwa njia ambayo hatimaye huonyesha nafsi na labda upekee wa mtunzi wa kazi
hiyo.
Mtindo huwa na sehemu kuu mbili
i)
Maudhui na fani
ii)
Nafsi ya msanii ambayo hujitokeza katika mfano
kati ya fani na maudhui
Hapa tunatumia nafsi
kwa maana ya maafikiano baina ya wazo linaloelezwa na mwelezaji wa wazo hilo.
Kinachosisitizwa ni kuwa ikiwa watunzi wawili watashughulikia
mada moja, mitindo yao itakuwa tofauti na hapo ndipo tunafikia kauli kuwa
“mtindo mtu” mtindo ndio unawawezesha watazamaji, wasikilizaji na hata wasomaji
kungamua mtunzi wa kazi hata bila kumwona ama kusoma jina lake.
5. LUGHA.
Hiki ni kipengele muhimu cha fani ya fasihi, lugha ndiyo
malighafi ya fasihi.Lugha inayotumika katika kazi ya fasihi ni lugha ya kisanaa
inayopambwa na inayokusudiwa kuibua hisia fulani kwa hadhira yake.Inaweza
kuathiri moyo ya hadhira na kulingana na jinsi inavyotumiwa kwa lengo la kuchekesha,
kukejeli, kubeza, kuchokoza, kutia hamasa au kushawishi
Matumizi ya lugha fasaha, uteuzi wa misamiati na matumizi ya
misemo na methali zinazosadifu mazingira ya jaini inayohusika kufanya kazi hiyo
ya fasihi simulizi kuwa sumaku ya kuvutia msomaji, msikilizaji au mtazamaji.
Tamathali za semi za aina mbalimbali hutumika kujenga picha
mfano ya tamathali za semi ni kama vile sitiari, tashhisi, kejeli, kijembe,
tabaini, tuniaba, tashibiha n.k.
Taswira ni lugha ambayo huchora pichaza watu, vitu au mahali
kwa kutumia ishara katika taswira unaweza kubainisha maelezo ambayo jinsi
yanavypangwa na msanii huweza kufanya hadhira zipate aina mbalimbali za hisi za
kunusa, kusikia, kuona na kugusa.Mara nyingi hutumiwa na wasanii ili kunasa
hisia zao kwa hadhira.
Hivyo wasanii hutumia maneno ambayo huumba picha kamili ya
kitu, hali, wazo, dhana au uzoefu fulani wa jamii inayohusika.
Mara nyingi matumizi ya picha huenda sambamba na ishara
mbalimbali ili kuwakilisha vitu, dhana au mawazo mengine.
6. UPEO
Katika fasihi simulizi upeo ni kama kilele cha kazi yenyewe,
kuna upeo wa aina mbili
Upeo wa juu.Ni
zile sehemu za kazi hiyo ambazo hutosheleza hoja za wasikilizaji au watazamaji
katika sehemu hii hadhira hupata majibu muhimu ambayo kazi hiyo imecheleweshwa
kwa kutumia taharuki mbinu rejeshi, mtindo wa kiutelezi n.k.
Mara nyingi watunzi wa kazi za fasihi huweka kipeo cha juu
mwishoni mwa kazi zao hata ingawa si lazima kuwa na kipeo kimoja tu wakati
mwingine waweza kupata kazi ya fasihi simulizi ambayo haina kipeo kabisa
Katika kazi mbalimbali za fasihi wasanii hujenga mgogoro
ambao hujtokeza na kukua jinsi kazi hizo zinavyokuwa, kipeo cha juu utokea
ambapo pale msanii hujaribu kutoa suluhisho kwa mgogoro uliojengwa katika kazi
yake.
Upeo wa chini.Ni
sehemu ambayo matatizo yaliyounda kazi ya fasihi yanatatuliwa.Upeo wa chini ni
pale ambapo haja na mataajio ya hadhira hayakukidhiwa katika baadhi ya kazi za
fasihi vipeo vya chini huwadhihirisha la udhaifu wa kazi hiyo lakini katika
kazi nyingine upeo wa chini huwa umekusudiwa hivyo na mtunzi.Hali hii ya pili
hujitokeza hasa katika kazi ya fasihi ambayo upeo wa chini hutumiwa kwa lengo
la kushangaza hadhira.
7. UCHESHI
KATIKA KAZI ZA FASIHI
Ucheshi ni kipengele muhimu cha kifani katika kazi ya fasihi
hasa fasihi simulizi.Ucheshi ni mbinu ya kifani ambayo watunzi hutumia katika
kazi zao za fasihi kwa lengo la kuchekesha na kurudisha hadhira na kuondolea
uchovu.
Wasanii mbalimbali hutumia mbinu tofautitofauti kuleta
vichekesho katika kazi zao.Baadhi yao hutumia vitendawili ili kujenga, kejeli,
dhihaka, n.k. vichekesho pia huweza kutumiwa ili kujenga maudhui.
8. WAHUSIKA.
Ni viumbe ambavyo hutumiwa na wasanii katika mtiririko wa
matukio kuelezea visa vyake.Wahusika wanaweza kuwa watu, miti, wadudu, mizimu, misitu
na wanyama wahusika huwa ni viumbe ambavyo vinatenda na kutendewa wanatumwa na
msanii kusimamia hali mbalimbali za binadamu katika jamii wanamoishi.
Hawa ndio uti wa mgongo wa fani ya fasihi simulizi,
Bilawahusika mtiririko wa matukio au visa hukosa pahali pa kujishikiilia
wahusika si viumbe maalumu wa mtunzi kwa vile ndiyo wanaotumia kutoa picha au
kuwasilisha mawazo na fikra zake kwa jamii inayowakilishwa na wahusika hao.
VIPENGELE
VYA MAUDHUI KATIKA FASIHI SIMULIZI
MAUDHUI
Ni jumla ya mambo yote yanayosemwa na msimuliaji au
mwandishi katika kazi yake.Vipengele vya maudhui au umbo la ndani la kazi ya
fasihi ni kama vile
Ø
Dhamira,
Ni kusudio la mtunzi wa kazi ya fasihi inaweza kuwa na dhamira kuu pamoja na
dhamira ndogondogo.Ubainishaji wa dhamira hufanywa na hadhira,hivyo dhamira
hufahamika kutokana na fasihi za wasikilizaji au wsomi wa kazi ya fasihi.
Ø
Ujumbe: Ili
dhamira ya mtunzi itumie, msanii hutoa taarifa fulani fulani kwa hadhira
yake.Taarifa hizo huitwa ujumbe. Ujumbe unaweza kutamkwa wazi au kwa uficho.
Kwa mfano methali ya “Asije la mkuu huvunjika guu” ina ujumbe huu ukidharau
maonyo ya wakubwa utapatamatatizo.Siku za mwizi ni arobaini ujumbe wa methali
hii chenye mwanzo kina mwisho kwa kawaida kazi moja ya fasihi inaweza kuwa
taarifa Zaidi ya moja.
Ø
Mafunzo: Ni
mafundisho au nasaha mtunzi katika kazi ya fasihi.Mafunzo pia huwa na maana
kulingana na fasihiya hadhira.Hadhira katika hadithi jinsi askari alivyopambana
vikali na jambazi, aghalabu kukusudia kukemea uhalifu lakini baadhi ya
wasikilizaji funzo ni ule utupaji wa ngumi na mateke.Mafunzo humfikiria
msikilizaji au msemaji kwa njia ya ujumbe.Mfano katika ujumbe huu zakaiba
akafungwa hapa funzo ni tusiibe wakati mwingine kazi za fasihi inaweza kutoa
mafunzo mabaya (maadili) mtunzi anaweza kukusudia hivyo au kutokusudia hivyo
Ø
Migogoro:
Hii huelekeza kisa lakini hujizatiti juu ya migogoro ya maisha anayosimulia
fanani.Baadhi ya kazi za fasihi huonyesha ukinzano uliopo baina ya makundi ya
watu au hali ya aina moja dhidi ya hali nyingine kuna aina nyingi za migogoro
lakini Zaidi ni ile ya kisiasa, kiuchumi na kitamaduni au ile ya kibinafsi
mfano: matatizo yanayosababishwa na uzembe dhidi ya watetezi wa kazi (viongozi)
dhidi ya usasa katika mila na desturi husababisha mgongano wa kiutamaduni.
Ø
Falsafa: Ni
mafunzo makuu ya msanii (mtunzi) kuhusu maisha. Mawazo haya hutokana na
uchanganuzi wa kimantiki na huwa ndio hekima na busara za msanii (mtunzi)
huyo.Ni Imani ya mwandishi au fanani katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo
katika jamii.
UMUHIMU NA UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI SIMULIZI.
Fani ni jumla ya mambo mengi yanayoijenga kazi ya
fasihi.Mambo haya ni kama vile muundo, mtindo, mandhari na matumizi mbalimbali
ya lugha.
Maudhui ni jumla ya mawazo au dhamira, msimamo mtazamo,
falsafa na ujumbe katika kazi ya fasihi.
Kwa ujumla fani na maudhui ni vitu vya muhimu sana katika fasihi simulizi kwa
sababu mtunzi hutumia vipengele hivi katika kujenga kzai yake anayotaka
kuwasilisha kwa jamii inayohusika.Maudhui ni kila kina kinachosemwa na fani ni
namna kinavyosemwa.
Fani na maudhui ni vitu ambavyo vinahusiana, vinaathiriana,
hutegemeana na kukamilishana katika kujenga kazi ya fasihi simulizi na kila
kipengele kimo ndani ya kingine
Mudhui hujumuisha viungo mbalimbali vya kazi ya fasihi
simulizi na fani ni mbinu za kisanaa zinazotumiwa na msanii ili kuvifanya
viungo hivyo viyasawili maisha kwa njia ivutiayo hadhira kila kigezo (fani na
maudhui) kimo ndani ya kingine huku vikishirikiana na kuathiriana katika
kujenga au kubomoa kazi ya fasihi simulizi.
KUTUNGA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Utungaji ni uundaji wa mawazo na kuyapanga maneno
yakuwasilisha ama kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi.Utungaji unweza
kutolewa kawa njia mdomo aqu kwa njia ya maandishi.
Mambo ya kuzingatia
katika kutunga kazi ya fasihi simulizi.
i)
Kuwa na jambo lakuelezea (tukio).Mtunzi
anapaswa kuwa na jambo ambalo unaona kuwa linasababisha mivuto katika
jamii.Jambo lazima litoke katika jamii inayohusika na isiyo nje ya jamii hiyo.
ii) Kuteua
utanzu atakaotumia.Mtu ni vyema kujua ni utanzu upi utakaotumia katika
kuwasilisha jambo hilo kwa jamii.Kwa kawaida fasihi simulizi ina tanzu nne
ambazo ni hadithi, ushauri, semi na Sanaa za maonyesho (maigizo).
iii) Kuteua
vipengele vya maudhui, mtunzi anapaswa aangalie nini dhamira yake, kuna ujumbe
gani kwa hadhira, hadhira upata maadili gani na je migogoro ipi na uwasilishe
vipi ili isipotoshwe lengo zima la kazi yake.
iv) Kuteua
kipera kitakachotumika katika uwasilishaji wa kazi yake kwa hadhira, mfano kama
mtunzi ameamua kutumia utanzu wa hadithi bila kuchagua kipera kimoja wapo kati
ya ngano, soga, vigano, visasili au tarihi (visakale)
v) Uteuzi
wa vipengele vya fani. Baada ya kubaini vipengele vya maudhui, msanii anapaswa
aangalie namna atakavyowasilisha maudhui hayo kuwa jamii.Hapa atatumia au atashughulika
na vipengele vya fani ambavyo atavitumia katika kuwasilisha ujumbe
wake.Vipengele hivyo ni muundo, mtindo, wahusika, matumizi ya lugha na
mandhari.Sehemu hii ndiyo ambayo mtunzi anatakiwa kutuma ufundi na ubunifu wa
hali ya juu ili kazi yzke ieleweke, ielimishe na kusisimua hadhira.
Kazi nzuri, hongera
ReplyDeleteShukran
ReplyDelete