MADA: ITIKADI NA UFUNDISHAJI WA NADHARIA ZA UHAKIKI WA FASIHI










Itikadi na Ufundishaji wa Nadharia za Uhakiki wa Fasihi Ikisiri UFUNDISHAJIwa nadharia za uhakiki wa fasihi ulipoanza, ilifikiriwa kwamba hatimaye fasihi imefanikiwa kupata silaha za kiuhakiki na kiakademia za kutegemewa. Wahakiki na wananadharia wa Kimagharibi kama Wellek na Warren (1946) walifikiria kwamba nadharia ya uhakiki wa fasihi ilikuwa moja popote fasihi iliposomwa. Hivi sasa katika kame ya 21, nadharia ni nyingi na zinaendelea kuundwa kuendana na mazingira anuwai ambamo wahakiki wanapatikana. Makala haya yananuia kuonyesha kwamba wingi wa nadharia zilizopo unaashiria mchomozo wa itikadi zinazoratibisha kuwepo kwa nadharia hizo . Japo Wellek na Warren walikuwa wakizungumzia kuhusu nadharia katika umoja wake, walikuwa wakiitikia maswala ya kiitikadi. Jambo hili linahusu fasihi ya Kiswahili vilevile. Maneno muhimu: nadharia, uhakiki, itikadi Abstract It was assumed that the teaching of theories of literary criticism ushered in an era when literature had begotten its ultimate critical and academic weapons. Western critics and theorists such as Wellek and Warren (1986) thought that theory was always singular and its rale uniform wherever it was applied. Now, in the zi" century, there a praliferation of many theories and what is more, others are being churned out and applied congruent to the home environments in which critics find themselves. The intention of this paper is to show that ideology in its various guises has played and continues to playa crucial role in the formulation of those theories. Even as Wellek and Warren were talking about the singularity of theory, they were in fact being ideological. This applies to Kiswahili literature as well. Keywords: Theory, Criticism, Ideology. 1.1. Utangulizi Lengo la makala haya ni kuonyesha dhima ya itikadi katika ufundishaji wa nadharia za uhakiki wa fasihi. Itikadi kama inavyoeleweka sasa ina uwezo mkubwa wa kuifinyanga nadharia ili nadharia hiyo ipondokee mtazamo maalumu na mahsusi. Kabla ya kuonyesha jinsi itikadi inavyoweza kuathiri mwono wa nadharia, inajuzu kujifahamisha japo kwa kifupi maana ya itikadi. 1.2. Maana ya Itikadi Itikadi ni istilahi ya kimsingi katika nyugo za kiutamaduni, za fasihi na taaluma zinazohusu filamu. Maana ya istilahi 'itikadi' kiasilia inatokana na maandishi ya mwanafalsafa wa Kijerumani, Karl Marx na mwenzake Friedrich Engels (Abdulla, Mansur na wenzake, 2014). Katika uchanganuzi wao wa kimsingi wa jamii, walifafanua itikadi kama dhana na imani za tabaka tawala katika kipindi maalumu. Dhana na imani za tabaka tawala ndizo hutamalaki taratibu za kuunda fikra, mawazo na mielekeo ya wanajamii kwa ujumla. Kwa hivyo, mfumo wote wa fikra za tabaka tawala ndio unajenga itikadi ya jamii fulani. Kulingana na Marx na Engels, dhima ya itikadi ni kuhuisha upya zana za kuzalisha mali na Kuhakikisha kwamba tabaka tawala linajiimarisha. Kwao,itikadi hupotosha na kuharamisha ukweli. Ijapokuwa mgawanyo wa jamii kati ya watawala na watawaliwa umeundwa na mtu kwa minajili ya kuhudumia mfumo wa kiuchumi, itikadi huhalalisha na huthibitisha mgawanyo huo. Watawaliwa hukubali hali ya ukengeushi ambayo kwa kawaida wangeasi dhidi yake. Hali hii ya ukengeushi imediriki kuitwa "ung'amuzi"potoshi"(Eagleton, 1991). Dhana ya itikadi kama ilivyofikiriwa na kuwasilishwa na Marx na Engels imesailiwa na Kupanuliwa ili itangamane na mabadiliko ambayo jamii imepitia tangu karne ya 19. Mabadiliko makubwa ambayo yamefanyika ni kwamba uchumi kama kigeu imara kisichobadilika na ambacho hutegemeza mgongano wa kitabaka umepoteza mashiko yake. Wahakiki wa kiutamaduni hasa wale wanaohusishwa na mkondo wa kisasaleo wanasema kwamba vigeu vya kukiritimba mamlaka na uchumi ni vingi vikiwemo jinsia, mfumo wa kuumeni na kukeni rangi ya mtu, kabila lake na taifa anamotoka. Naye mwanafalsafa wa Kitaliano anayeitwa Antonio Gramsci (1971) ameinyambua dhana ya itikadi vingine. Kinyume na kutumia kishazi cha " ung'amuzi potoshi" kama walivyodai Marx na Engels, anaunda na kutumia dhana ya hegemonia. Gramsci anadai kwamba itikadi hupata mamlaka na uhalali kutokana ikibali ya hiari wala si kwa kutumia nguvu. Juu ya haya, anafikiria kwamba itikadi ni seti ya mawazo na matendo wanayofanya wanajamii ili kuhalalisha mfumo unaotawala. Miongoni mwa mawazo haya ni kaida zinazochukuliwa kuwa mazoea ya kila siku ya mtu( Forgacs, 2000). Kwa hakika usuli wake ukisakwa, itabainika kwamba mawazo hayo yaliundwa ili kuhudumia kikundi mahsusi. Mfaransa Louis Althusser aliyanyambulisha mawazo ya Gramsci na kung'amua kwamba kuna zana aina mbili za kuchipuza na kuendeleza utawala; nazo ni zana nyamazishi na zana za itikadi za taifa(1971}. Zana nyamazishi au zana gandamizi ni kama jeshi, polisi na jela. Kwa upande mwingine, zana za itikadi za taifa ni kama vyombo vya habari, mfumo wa elimu, dini na familia. Itikadi na usemi (diskosi) ndio msingi wa kuwasilisha dhana, imani na kaida. 1.3. Itikadi na Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Baadhi ya mikondo ya kuelezea itikadi imeathiri jinsi nadharia zilivyoundwa na zinaendelea kuundwa na kushughulikiwa kiusomi. Itikadi ni zana yenye mamlaka makubwa ya kuratibisha usemaji wa kinadharia katika uhakiki wa fasihi. Maana mbalimbali za nadharia na viashiria vingine vinavyohusishwa nazo vikichunguzwa kwa upekuzi, itagunduliwa kwamba nadharia zimeingiliwa pakubwa na itikadi. Masuala kama nadharia ifikiriwe katika hali ya umoja au hali ya wingi, nadharia kuwa mwongozo wa uhakiki, nadharia kuwa sheri a za uhakiki, nadharia kuwa mikakati ya kusoma, nadharia kuwa usomaji unaozingatia ujarabati, nadharia kuwa uhakiki wa kimfumo, nadharia kuwa muktadha wa kazi ya fasihi husika na nadharia kama usemaji unaolenga kumiliki aina nyingine za usemaji yanategemea itikadi katika viwango anuwai ambavyo watalaamu wameainisha. Tutaonyesha jinsi itikadi imeathiri ufasiri na ufundishaji wa nadharia katika aya zifuatazo hivi karibuni. 1.4. Umoja na Wingi katika Ufasiri wa Maana ya Nadharia za Uhakiki Wahakiki wa fasihi hasa wale walioandika katika miaka ya 1920 hadi miaka ya 1960 kama Wellek na Warren walifikiria kwamba dhana ya nadharia ya uhakiki wa fasihi ni moja. Kwa Mujibu wa mawazo yao, nadharia ilitazamiwa kueleza na kufafanua maana ya fasihi, dhima ya fasihi na viwango mbalimbali vya ubora wa fasihi. Mtazamo wa Wellek na Warren ulifikia kilele wakati wa umuundo, Uhakiki Mpya na umaumbo. Ijapokuwa nadharia ya Uhakiki Mpya ilichipuka kipekee na kivyake inashabihiana kwa sifa nyingi na umuundo na umaumbo. Waasisi na waitifaki wa nadharia hizi zote walifikiria kwamba lugha ya fasihi ina sheria mahsusi za kipekee popote inapotumiwa. Lugha hiyo ya fasihi hujirejelea yenyewe kwa kuzitangaza sifa zake. Wellek na Warren waliandika kitabu chao, Theory of Literature (1986) kuashiria mtazamo na mwelekeo huu. Kwao, nadharia ilikuwa moja tu. Dhamira yao ilikuwa kutafuta msimbo wa kibia wa kuchanganulia fasihi. Isitoshe, kwao kazi za sanaa ni minara inayosifika kwa vile imehifadhiwa kimaandishi. Fasihi simulizi haikuwa moja kati ya taaluma mashuhuri katika mitaala yao. Hii ilikuwa itikadi ya kukiritimba uainisho na usomaji wa fasihi. Ndio sababu wataalamu waliokulia kwa ziwa la Wellek na Warren walipoanza kutembea hasa barani fasihi za kienyeji hazikuwashugulisha asilani ijapokuwa zilikuwa zimeimarika vya kutosha katika vyuo vikuu vya Kimagharibi . Uamuzi wa kutofundisha sanaa za Kienyeji kifasihi ulikuwa wa kiitikadi. Hata hivyo, njia nyinginezo za kuudurusu ulimwengu zilipozuka wahakiki wengi hasa wa pembezoni (Dunia ya Tatu) walikatikiwa Kung'amua kwamba maadamu kuna washindani chekwachekwa katika medani ya kusoma, Kufikiria, na kutathmini, basi kuna njia nyingi za kuzungumzia utaalamu tofauti tofauti. Nadharia za uhakiki ni kama njia nyingi teule za kuzungumzia ujuzi wa kifasihi, zimo mashindanoni na zinazoshinda kidesturi ndizo huhesabiwa kuwa teule zaidi kadamnasi ya nyinginezo. Nadharia zinazoshinda kwa kurejelewa mara kwa mara na kutumiwa si lazima ziwe sahihi na kuhudumia wanajamii wote kwa mafanikio. Kwa hivyo, hivi sasa nadharia ni nyingi na hutumika Kutegemea mahitaji mbalimbali vikundi anuwai vya wanajamii. 1.5. Nadharia kama Mwongozo wa Kuhakikia Nadharia inaweza kuchukuliwa kama mwongozo wa kumsaidia msomaji kufahamu kazi ya sanaa vizuri zaidi. Nadharia ni mkataba usiokuwa rasmi kati ya msomaji na mtunzi. Mhakiki kama msomaji anapoyaweka mawazo ya mtunzi katika utaratibu mahsusi ili yaweze kutathminika pasi kuweka masharti maalum, basi nadharia yake itakuwa kama mwongozo. Katika ushairi wa Kiswahili, wahariri na wahakiki kama Shihabuddin Chiraghdin na Abdilatif Abdalla wanazungumzia ~itanzu vya mashairi kimaudhui pasi kuonyesha mipaka yake mahsusi. Idadi ya vitanzu inategemea masuala yanayoendelea kuibuka. Katika utangulizi wake wa Malenga wa Mvita (1970), tungo zilizosanifiwa na Juma Bhalo, Chiraghdin hazungumzii muundo wa ushairi. Suala la muundo ni kaida na halimshughulishi asilani. Alipouandika utangulizi wake, muundo tengemano wa shairi kama alivyofahamu hakukuwa umetishwa wala kuvurugwa na yeyote. Alilirejelea tu pale alipowajibika kuwaonya na pengine kuwaelekeza washairi chipukizi. Kwa hivvo, Shihabuddin Chiraghdin alivaainisha mashairi va Ahmad Nassir katika rnagawanvo manne: Mbinu za Lugha, Mawazo na Maliwazo, Baina va Mume na Mke, na Majonzi na Makiwa. Uainisho huu ni ithibati tosha kuonvesha kwamba si lazima ushairi wa Kiswahili ufikiriwe kimuundo kila mara mijadala va kinadharia inapozuka. Diwani ya Ustadh Nyamaume navo iliandikiwa uhariri wake na Abdilatif Abdalla. Abdalla anashabihianana Chiraghdin katika kubainisha ushairi wa Nvamaume kimaudhui. Hata hivvo, rngawanvo wa Abdilatif haufanani sarafu kwa va pili na rngawanvo wa Shihabuddin Chiraghdin. Ana mashairi vanavohusu: Kuusemea Ushairi, Malimwengu, Kushauri na Kunasihi, Kuimbana Kishairi, Kufumba na Kupiga Mifano na Kutoa Heko. Kutokana na ukweli huu tunaweza kuhitamidi kuwa uainisho wa ushairi wa Kiswahili kimaudhui ni rnnvumbufu kwa vile maudhui rnapva vanawezakuibuka na kusababisha uundaji wa makundi rnapva va ushairi kimaudhui. Kwa upande mwingine mijadala kuhusu muundo wa shairi la Kiswahili ilianza kudhihirika kwa makali baada va kutungwa kwa diwani va Euphrase (1974), Kahigi na Mulokozi (1976) na Mulokozi na Kahigi (1979). Shihabuddin Chiragdin alilihisi wimbi la watunzi hawa ambao kwa wakati huo walikuwa wakereketwa kiasi na kusemezana na ushairi wao katika utangulizi wa Malenga wa Mrima (1977). Sasa mashairi havakuainishwa kimaudhui kama ilivvofanvwa kingaubaga katikaMalenga wa Mvita. Mhariri wa Malenga wa Mrima alijipa fursa va kushambulia mashairi vasivofuata arudhi. Jambo hili Iilishadidiwa na Hassan Msami katika tahakiki vake va Malenga wa Vumba (1982) . Katika tahakiki hivo, alitambua kueleza sifa za bahari kumi na nne kimuundo. Bahari Hizo ni: kikai, msuko, sakarani, mtiririko, ukara, ukaraguni, kikwamba, msuko wa kikai, tathlitha, tarbia, takhmisa, ukemi, pindu na utenzi. Ulinganifu na tofauti zilizokuwepo kuhusiana na mgao wa ushairi katika makundi mbalimbali ulisababishwa na itikadi va wasomi na wadau wengine waliohusika. Itikadi inatuwezesha kuelezea utamaduni, elimu na aina nvlngine za usemaji uliozowewa ulioratibu uainisho wa ushairi. Katika mazingira va sanaa za Kimagharibi nadharia kama mwongozo inadhihirika katika matamshi va Aristotle katika tahakiki vake va Poetics (1965). Aristotle aliorodhesha na kufafanua sifa na mazoea va Wavunani kuhusu utunzi wa tamthilia. Alifanva hivvo bila kuwashinikiza watunzi na wahakiki kufuata alivovashuhudia. Aristotle aliishi katika demokrasia kiasi na inawezekana kwamba ukosefu wa shinikizo katika tahakiki vake inadhihirisha itikadi hii. 1.6. Nadharia kama Sheria ya Kutunga na Kuhakiki Nadharia kama sheria za kutunga na kuhakiki kazi za fasihi zilipigiwa debe na mhakiki wa kiroma, Horace Katika tahakiki yake Ars Poetica na kufufuka katika kipindi cha urasimi mpya wa Kimagharibi. Katika wakati wa Horace, milki ya Uroma ilikuwa na nguvu nyingi za kisiasa. Lakini Kwa upande wa utamaduni, milki ya Uyunani ambayo ilikuwa imedidimia na kuporomoka iliendelea kukiritimba ushawishi mkuu. Yaani Uyunani iliendelea kuutawala ulimwengu wa Kimagharibi kiutamaduni. Katika mawanda ya fasihi, Waroma waliiga mitindo ya kiutunzi na kiuhakiki wa Kiyunani. Katika kipindi chote ambacho Waroma waliutawala ulimwengu wa kale, lugha ya kiyunani lIikuwa wa pili na ya lazima miongoni mwa Waroma walioelemika. Lakini kiitikadi, Waroma Waliongozwa kwa amri. Juliasi Kaizari na watawala wote waliokuja baadaye walikuwa madikteta. Jambo hili lilidhihirika katika mfumo wa elimu na wa kiusomi wa kipindi kile. Alipokuwa akiwafundisha wanawe Piso katika Ars Poetica, Horace alionya: nitamfundisha mshairi kazi yake na majukumu yake. Nitamfundisha mahali atakapopata malighafi ya kazi yake, yale yatakayokuza na kupapalia kipawa chake cha kutunga ushairi, yale ambayo anapaswa kufanya na yale asiyopaswa kufanya, mahali ambapo njia nzuri itamwelekeza na mahali ambapo njia mbaya itampeleka ( Horace, Ars Poetica katika Dorsh, 89-90) Horace anaendelea kuwaonya wanafunzi wake kwa kusema kwamba: Ukitaka tamthilia yako kufurahiwa na kuigizwa mara nyingine, tamthilia hiyo isiwe na matendo yanayozidi au yanayopungua matano. Matendo yanayosababishwa na majaliwa au nguvu za kiungu yasiingizwe katika tamathilia isipokuwa hali ngumu itokee inayoshurutisha maingilio ya mkono wa kiujiza. Na usiwe na wahusika wanaozidi watatu kwenye jukwaa kwa wakati mmoja (Horace, Ars Poetica, katika Dorch, 85) Ni bayana kwamba kauli hizi ni amri, ni sheria inayohusu namna ya kushughulikia sanaa va kutunga na kuihakiki tamthilia. Hizi ni sheria za Horace. Zinatofautiana pakubwa na jinsi Aristotle alivvoonvesha mchakato wa kutunga na kuihakiki tamthilia. Mazingira va Horace aliithiri jinsi alivvolurnba kauli zake. Yaani, itikadi va kutoa amri arnbavo ilikuwa imekolea katika usemaji wa Makaizari uliingilia moja kwa moja kauli za Horace. 1.7. Nadharia kama Mkakati wa Kusoma Itikadi inaweza kuathiri nadharia na kuikabidhi nadharia hiyo sura va mkakati wa kusoma. Kazi mbalimbali za sanaa zinaweza kuhakikiwa kwa kutumia nadharia ile ile moja. Lengo la kufanva hivvo ni kutathmini uwezo wa nadharia moja katika ufafanuzi wa kazi mbalimbali za fasihi. Hali alivorno msomaji katika kiwango hiki ni mathalan va maabara ambapo mikakati va kusoma inajaribiwa na ile isivohitajika hudumazwa ilhali inavothaminiwa na msomaji hupewa uchomozo zaidi. Mbali na havo, nadharia anuwai zinaweza kutumiwa kukisoma na kukichanganua kitabu kimoja kwa nia va kuonvesha na ipi inavofaa zaidi katika usomaji wa kitabu fulani na ni ipi haifai. Kaida hii va uhakiki inapotumiwa wachanganuzi watachukulia va kuwa baadhi va nadharia zina ushawishi mkubwa hata kabla va kufanviwa majaribio katika mazingira vovote. Katika tasnifu nvlngi zilizoandikwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi katika mwongo wa 7 na mapema mwongo wa 8 wa karne ilivopita, nadharia llivotumlka zaidi kuhakikia kazi za fasihi ilikuwa va uhalisia wa kijamaa au Umarx. Pamoja na hava, maswala valivohusu ubia na upekee wa fasihi valitazamwa katika darubini va Uleninisti. Jambo hili halikufanvwa kwa kuzingatia uwajibikaji wa uhakiki bali ulitilia maanani zaidi fahari ilivohusishwa na kufikiria kimaendeleo au kimapinduzi. Wakati mwingine, watafiti walifanva uchanganuzi kwa kutumia silika zao ijapokuwa walikuwa wametimiza masharti va mapendekezo kwa kupachika uhalisia wa kijamaa au upembuzi wa kimarx katika sehemu ilivohitaji kujalizwa nadharia. Itikadi va ujamaa ilikuwa njia sahihi va kufikiria na hakuna , hata asivekuwa mjuzi alivethubutu kuachwa nvurna wala nje katika rnparanvo huu. Hili lilikuwa swala la kiitikadi. 1.8. Usomaji unaozingatia Ujarabati Huu ni usomaji ulioathiriwa na mielekeo na mitazamo ya kufikiria yenye mashiko katika sayansi asili. Ujarabati ni ufafanuzi wa ujuzi unaozingatia tu mambo halisi yanayoonekana, yanayoshikika na yanayohisika kwa fikra na mishipa ya fahamu ya mtu. Mhakiki anapotumia nadharia zenye mwelekeo huu, huwa kama mchunguzi wa majaribio yanayojaribiwa kwenye maabara. Nadharia za umaumbo na vipera fulani vya nadharia za kimtindo hasa zile zinazotegemea uthibitisho wa kitakwimu ni za kijarabati. Marehemu Jay Kitsao (1982) alitumia nadharia ya kimtindo na kitakwimu kiuchangamano kuandaa tasnifu yake ya uzamivu. Katika muktadha huu, usanii unaainishwa kwa idadi ya jazanda na vipengele vingine vya uchomozo alivyovitumia mwanasanaa. Isitoshe mwanasanaa bi nafsi anaweza kutambulika kwa matumizi ya msamiati, urefu wa sentensi na hata uradidi wa kipekee. Mwelekeo kama huo ndio uliwalifanya wahakiki kama Buffon( 1930) kung'amua kwamba mtindo ni mtu. Vilevile, hii ilikuwa kaida ya kusoma fasihi kisayansi na wana-maumbo wa Kirusi. Kigezo cha uchomozo kilisisitizwa zaidi na wana-maumbo wa Kirusi katika kubainisha tanzu za fasihi. Ushairi ulihusishwa na usanii zaidi kuliko riwaya na tamthilia kwa kuwa una sifa bainifu zaidi kama vina, mizani na wizani. Kuna dhana ya "uhuru wa kishairi" ambao hauhusu ushairi peke yake bali tanzu zote za fasihi. Kwa mujibu wa wana-maumbo wa Kirusi ukiushi ulikuwa ushahidi wa kuwepo kwa usanii na ulitambulika zaidi katika ushairi. Mambo haya yalitokea kwa sababu za kiitikadi. Pengine wahakiki hao walikuwa wanajaribu kuepukana na maswala ya kiharakati kwa sababu za kiusalama au walifikiria kwamba kuchopeka usayansi asilia katika uhakiki wa fasihi kuuliiletea fasihi fahari na umashuhuri.
Share:

No comments:

Post a Comment

ONLINE VISITORS


Labels

Blog Archive

Recent Posts