
Nadharia kama Usomaji Kimfumo
Kuna mwelekeo unaoshikilia kwamba ili kazi va fasihi ishughulikiwe katika vipengele vvake vvote, inapaswa kuhakikiwa kimfumo. Mwelekeo huu unaongozwa na mtazamo kuwa mtunzi anapotunga kazi va sanaa, kila neno, kishazi, sentensi na alama va uakifishaji ina lengo maalumu. Kila kipashio kimewekwa katika kazi hivo kimaksudi. Hivvo basi, hakuna chochote kinachostahili kuupuzwa. Moja kati va njia za zamani za kusoma kazi za fasihi na zilizosifika sana ni ile inavogawa fasihi katika mawanda mawili; vallvorno na jinsi valivorno vanavvowasilishwa, Nadharia inachukulia va kwamba shairi, tamthilia na shairi ni kazi za fasihi ambazo zina vipengele mbalimbali. Kila kipengele kinapaswa kuelezwa katika muktadha wa vipengele vingine. Bila kuwepo uhusiano huu wa kujengana na kukamilishana, kazi va fasihi haitakuwa kamili. Mtazamo wa aina hii unapalilia wazo kwamba kazi va fasihi imejitosheleza na haihitaji muktadha wa nje ili kuikamilisha. Hatirnave dhana va ufu wa mwandishi imetokana na nadharia hii. Uhakiki unaornnvirna mwandishi nafasi muhimu katika ufahamu wa kazi vake vilevile unaikengeusha hivo kazi kutokana na muktadha ulioizalisha. Hapa itikadi inaikabidhi sanaa lengo la kiujumi bila kuhusisha ule ujumi na maswala va kidhamira va mwandishi. Fikra kwamba lengo la kazi va fasihi linaweza kutofautiana na dhamira va mwandishi wa kazi hivo inatokana na mtazamo huu. UKweli ni kwamba ufasiri wa kutegemewa wa kazi ya fasihi utafafanua dhamira na mtindo wa kazi inayohusika katika vipengele karibu vvote. Haiyumkiniki kuwa kati va vipengele hivvo, mhakiki atakosa kutaja alivokusudla mtunzi asilia asilani. Kazi zote za fasihi ni aina fulani va majazi vaani zinaweza kufahamika katika viwango mbalimbali vVa ufasiri. Kuna mkufu wa kuashiria na kumaanisha kutegemea miktadha tofauti anavorejelea mhakiki. Miktadha hivo inaning'inia kati va lugha dhahania na lugha tendakazi anavoiturnia mwandishi. Nadharia va baada-ukoloni miongoni mwa nadharia nvingine za kisasaleo inathamini mwandishi na muktadha uliomchipuza kwa arnbavvo inarejelea mitazamo va kiutamaduni na va kibinafsi ambayo inapatikana nje va matini ilivoandikwa. Maana zinaweza kuwa nyingi na tofauti lakini zitakuwa na dhima kubwa kwa waliokusudiwa kwa kufasiriwa kimkutadha. 1.10. Nadharia kama Usemaji Unaolenga Kutawala Ujuzi Katika mataifa mengi ya zama hizi, nadharia za uhakiki wa fasihi zimekuwa usemaji unaotumiwa na wanajamii kuwatawala wanajamii wengine. Wananadharia kama Michel Foucault, Jacques Derrida, Jacques Lacan, Homi Bhabha, Gaytri Spivak, Edward Said, Achilles Mbembe, Valentin Mudimbe, Anthony Appiah (Werbner & Ranger, 1996L wanafikiria kwamba njia teule za usemaji zikiwemo nadharia za uhakiki wa fasihi zimeumbwa ili zitumiwe kuutawala ulirnwengu, Kama ambavyo watawawala hujiteua na kujitenga katika matabaka maalum, njia za kuzungumzia ulirnwengu pia zimegawanywa katika matabaka maalum. Katika kazi za wananadharia walioorodheshwa hapo awali, juhudi zinafanywa kutukuza usemaji ambao hapo kabla ulikuwa umedhalilishwa, kudunishwa na kupuuzwa. Kwa kufanya hivyo, njia mbalimbali za kufikiria (yaani nadharia) zimepewa nafasi sawa za kuwatetea wanajamii ambao kwa kawaida hawana majukwaa ya kujitetea. Mfumo wa ukoloni ulitanguliwa na kuandamana na maandishi na masimulizi mengi kuhusu maeneo yaliyolengwa kuwa makoloni. Waandishi kama Friedrich Hegel, Daniel Defoe na Conrad waliandika maandishi yaliyosifu utu wa walionuia "kujitoa mhanga" na "kuyaokoa" maeneo yaliyolaaniwa, maeneo yaliyokaliwa na II wana wa kambo" wa Mwenyezi Mungu. Wakati huohuo, maandishi have yalionyesha uduni wa maisha ya waliolengwa kutawaliwa katika mfumo wa ukoloni. Mwandishi na mhakiki anayepinga mtazamo kama huu anapaswa kujihami na usemaji teule (nadharia) ambao utahalalisha kuwepo kwake na utu wake. Ngugi wa Thiong'o (1998) na Chinua Achebe (1988) wamekuwa katika mstari wa mbele wa kuunda kauli zinazotetea utu wa Mwafrika. Kwa kuunda kauli hizo wamejaribu kuratibisha usemaji unaopaswa kutawala mtazamo wa maisha katika maeneo vallvotawaliwa chini ya mfumo wa ukoloni na ambayo yanaendelea kuathiriwa na matokeo ya matendo yaliyofanywa wakati wa ukoloni. Nadharia za kifeministi zinapatikana katika mkumbo huu wa kufikiria vilevile. Kwao wafeministi, nadharia za uhakiki wa fasihi ni vichochoro vya mikabala ya kubainisha na kueleza jinsi wanawake na wanaume wanavyohusiana katika jamii ambazo kwa muda mrefu zimeongozwa kibabedume. Kama wanavyosema Belsey na Moore: Kwa mujibu wa wanachuo na wasomaji wa kifeministi kila usomaji una mwelekeo maalum juu ya matini inayosomwa. Uchanganuzi wa aina yoyote una malengo na mielekeo ya kisiasa. Usomaji ama unashadidia mabadiliko katika kizazi cha mtu au kusitisha mchapuko wa kutokea kwa mabadiliko hayo (1997:1). Kama inavyodhihirika katika haya maelezo, nadharia za kileo hasa zile ambazo zinaelekeza usomaji na uchanganuzi wa fasihi baada ya umuundo na umaumbo zinakusudia kuumbua matamshi mateule ya kimapokeo kuhusu fasihi na maudhui yake. Baada-ukoloni na ufeministi ni mifano michache ya nadharia hizi. Hata hivyo, isidhaniwe kwamba nadharia zinazojengua uteule wa baadhi ya masimulizi kuhusu hali ya binadamu zinalingana katika vipengele vyake vyote. Ijapokuwa uumbuzi unapiga mwangwi katika Baada-ukoloni na ufeministi, malengo ya baada-ukoloni na ufeministi yanapiku uumbuzi. Hizi nadharia zina malengo ya kisiasa na kiitikadi. Hivyo basi, waumbuzi hawakubaliani kwa kila jambo. Mawazo ya Belsey na Moore kuhusu malengo ya kwanza ya udenguzi yanalishadidia jambo hili: ... tokea mwanzo, uhakiki wa kiumbuzi kuhusu jinsia ulikusudia kulikengeusha swala la uana kutokana na utamaduni na ujumi au sanaa kwa ujumla (1997:9). Maoni ya wahakiki hawa ni kuwa kwa kulipuuza swala la jinsia, uumbuzi ulikuwa unaendeleza itikadi ya kibabedume. Ijapokuwa ufeministi unashirikisha na kutumia baadhi ya mihimili ya uumbuzi, malengo yake ni tofauti kabisa kutokana na malengo ya uumbuzi. Uumbuzi unahusu zaidi udenguzi wa lugha na mifumo wa uashiriaji wake bila kuzingatia amali mbalimbali zinazobebwa na hiyo lugha. Kinyume na haya, ufeministi unatilia mkazo lugha kama kiashiria kinachotumiwa kuelezea mahusiano ya wanajamii katika misingi ya jinsia. Maswala ya kisiasa na ya kijamii hayawezi kuepukika katika usomaji wa kifeministi. 1.11. Nadharia Katika Siku za Halafu Nadharia zitaendelea kuwepo na kuratibu na kuhamasisha usomaji na ufundishaji wa fasihi. Hata hivyo zitabadilika kila kukicha endapo maswala mapya yatazuka ambayo yatahitaji maelezo ya kipekee na kivyake kinadharia. Hayo maswala mapya yatakuwa ya kiitikadi Hatimaye, ikidhihirika kwamba nadharia zilizopo hazina manufaa kiitikadi, zitalazimika kusalimu amri (kuhifadhiwa katika makavazi) ili nadharia nvlnglnezo zichipuke na kutimiza haja za walimwengu waliopo. Baadhi va nadharia zinazungumziwa na jamaa ambao wamekengeuka kutokana na jamii au vikoa wanavvowakilisha. Wengi wa wananadharia wanaozungumzia Baada-ukoloni hawaishi katika miji mikuu va maeneo vanavornilikiwa na ukoloni na athari zake na arnbavo wavaendelea kunvonvwa na mfumo wa kibepari wa kimataifa. Nadharia hazitazungumziwa kiakademia peke vake: zitapaswa kuhusishwa na hali thabiti wanamoishi watu. Kwa sababu va tofauti za kiuchumi kati va watu na kwa sababu va maonevu va aina nvingi vanavcendelea kuonveshwa na mtu dhidi va mtu mwingine, nadharia zinazotalii mahusiano kati va watu zitaendelea kushamiri. Nazo nadharia ambazo hazijakita katika maisha va watu na kuathiri hali halisi za maisha vao kama uumbuzi zitaendelea kufifia. Lakini baadhi va mikakati vake va kuutazama ulimwengu haitafutika. 1.12. Tamati Katika makala hava tumeonvesha va kwamba itikadi inaendelea kuathiri namna va kusoma na kuchanganua kazi za fasihi. Matamshi mateule arnbavo wahakiki wametongoa kuhusu nadharia za uhakiki vamefumbatwa katika itikadi kwa malengo vasivohusiana moja kwa moja na fasihi. Marejeleo Abdalla, A. (1976). Utangulizi. Diwani ya Nyamaume. Nairobi: Shungwaya Abdullah, M. na wengine (2014). "Dialectical Materialism". Ecyclopedia Britannica (Mtandao) Abedi, K. A. (1979). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: Kenya Literature Bureau. Achebe, Chinua (1988) Hopes and Impediments. London: Heinemann. Althusser, Louis (1971). Lenin and Philosophy and Other Essays. Monthly Review. Bakhtin, Mikhail (1989). The Dialogic Imagination: Four Essays. Trans. Michael Holquist & Katerina Clark. Austin: University of Texas Press. Belsey, Catherine & Jane Moore ed. (1997). The Feminist Reader. London: Macmillan. Blamires, Harry (1990). A History of Criticism. London: Macmillan. Bradford, Richard (1997). Stylistics. London: Routledge. Buffon, G (1930). Buffon's Discourse on Style. Paris: Librarie Hatier Publishers. Cohen, Ralph (1989). The Future of Literary Theory. New York &London: Routledge. Daiches, David (1986). Critical Approaches to Literature. London: Longman. Dorsch, S.T. (1965). Classical Literary Criticism: Aristotle/Longinus/ Horace. Harmondsworth: Penguin. Eagleton, Terry (1991). Ideology: An Introduction. London: Verso. Forgacs, David (2000). The Gramsci Reader: Selected Writings 1916-1935. New York: New York University Press Forster, Thomas (2003). How Read to Read Literature Like a Professor New York: Harper Collins. Foucault, Michel (1999). "Space, Power and Knowledge". The Cultural Studies Reader. Ed. Simon During. London: Routledge Gramsci, Antonio (1971). Selections from Prison Notebooks. New York: International Publishers. Harland, Richard (1999). Literary Theory: From Plato to Barthes: An Introductory History. New York: St. Martins. Keesey, D. (2003). Contexts for Criticism. London: Toronto Mayfield. Kezilahabi, Euphrase (1974). Kichomi. Nairobi: Heinemann. Kitsao, Jay (1982). An Investigation of Themes in Swahili Literature & the Application of Stylostatistics to Chosen Texts. Unpublished PhD thesis, University of Nairobi. Mulokozi, Mugybuso & Kahigi K. (1995). Malenga wa Bara. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press. Mulokozi, Mugyabuso & Kahigi K.(1979). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. Njogu, K. & R.M. Wafula (2007). Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation. Shihabuddin, C. (1970). Utangulizi. Malenga wa Mvita. Nairobi: Oxford University Press. Shihabuddin, C. (1977). Utangulizi. Malenga wa Mrima. Nairobi: Oxford University Press. Wafula, R.M. (2014). Uhakiki Kama Mchakato wa Kutaalamisha Usomaji wa Fasihi. Journal of Language Education and Linguistics Vol.8 Number 2. Dept. Of Foreign Languages: University of Dar es Salaam. Wamitila, K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus. Wa Thiong'o, Ngugi (1998). Penpoints Gunpoints and Dreams. Oxford: Clarendon. Wellek Rene & Austin Warren ( 1986). Theory of Literature. Harmondworth: Penguin. Werbner, Richard & Terence Ranger ed. (1996) Postcolonial Identities in Africa. London & New Jersey: Zed Books. Kitawasifu Dkt. Richard Makhanu Wafula ni mhadhiri katika Chuo kikuu cha Kenyatta ambapo anafundisha Nadharia za Uhakiki wa Fasihi, Fasihileo na Fasihi Linganishi.
ACHA KUTUMIA KAZI ZA WENYEWE BILA KUREJELEA. HUO NI UPWAGU WA KIUSOMI
ReplyDelete