Matumizi ya Kamusi
Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye
msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa
katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo wasomaji wanaweza
kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika karatasi au nakala tepe
yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na maelezo mengine na
kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wowote wa
kielekroniki.
Kamusi huweza kuwa ya lugha moja,
yaani orodha ya maneno pamoja na maelezo yake yakiwa katika lugha moja
Example 5
Mfano:
chatu,ni nyoka
mkubwa na mnene
Kamusi nyingine huwa za lugha mbili
yaani orodha ya maneno ipo katika lugha moja na maelezo ya maana ya maneno hayo
yapo katika lugha nyingine.
Example 6
chatu, npython
Kamusi ni hazina ya lugha
inayohusika, kwani tofauti na vitabu vingine vya lugha, huwa na orodha ya
maneno mbali mbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha ile pamoja na maana
zake. Japokuwa wingi wa maneno hutegemea ukubwa wa kamusi, kitabu hiki kina
manufaa makubwa kwa mtumiaji wake kwani humpatia msamiati asioufahamu pamoja na
maana zake au humpatia maana zaidi ya maneno anayoyafahamu.
Taarifa zinazopatikana katika kamusi
Awali kamusi zilipoanza kutungwa
zilikuwa ni orodha ya maneno magumu pamoja na maana zake. Kamusi za siku hizi
huwa na taarifa zaidi ya maana. Miongoni mwa taarifa ambazo kamusi huwa nazo
ni:
- tahajia za maneno mfano. Tasinifu Vs Tasnifu, Burangeti
Vs Blanketi, Kula Vs Kura, -ingine vs -engine
- matamshi
- sarufi ya lugha kama inavyojitokeza katika kila neno
kama vile maumbo ya wingi wa nomino, vinyambuo vya neno kama vile chezesha,
chezeka, chezea, mchezo, mchezajin.k ambavyo vinatokana na kitenzi cheza
- maana
- etimolojia ya neno (asili ya neno husika)
- matumizi ya neno
Jinsi ya Kutumia Kamusi
Maneno yanayoingizwa katika kamusi hupangwa
kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno yanayoanza na herufi a, yote huwekwa
chini ya herufi A. Maneno yanayoanza na herufi fulani nayo hupangwa
katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi ya pili, ya tatu, nne au
tano ya neno kama mfano hapa chini unavyoonyesha.
Example 7
Mfano:ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi.
Maneno yote yanaanza na herufi [j].
herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya tatu ni [b] na [d]. Kwa kuwa
[b] hutangulia [d] katika mpangilio wa alfabeti maneno yenye [b] kabla ya yale
yenye [d]. Kwa kuwa maneno yenye herufi [b] ni mawili itabidi tutazame herufi
ya nne ya hya maneno ili tuchague litakaloorodheshwa mwanzo. Neno ‘jabali’
litaorodhewshwa kabla ya ‘jabiri’ kwa kuwa [a] (herufi ya nne) ya ‘jabali’
hutangulia [i] ya ‘jabiri’ ambayo pia ni herufi ya nne. Kisha tunatazama maneno
yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya nne ili kubaini
neno litakaloandikwa mwanzo kati ya ‘jadhibika’ na ‘jadi’. Kwa kuwa [h]
hutangulia [i] basi ‘jadhibika’ huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na ‘jadi’.
Kwa hiyo hivi ndivyo unavyopaswa
kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi ya neno unalotafuta alafu
litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya kwanza kuorodheshwa.
Neno linaloorodheshwa kwenye kamusi
ili lifafanuliwe linaitwakidahizo.Kidahizo huandikiwa maelezo ya
kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana ya kidahizo, kategoria
ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo n.k. Kidahizo pamoja na
maelezo yake ndio huitwakitomeo cha kamusi.
Example 8
Kitomeo cha kamusi
Dhabihu (kidahizo)nm (kategoria ya neno) mahali pa kuchinjia
wanyama (maana ya neno).
Taarifa Ziingizwazo katika Kamusi
Fafanua taarifa ziingizwazo katika
kamusi
Maana za maneno
Kwa mfano:Dhabihunm
mahali pa kuchinjia wanyama.
Kategoria za maneno
Kategoria za maneno kama vile
kielezi (ele), kitenzi (kt), kivumishi (kv), nomino (nm), kihisishi.
Mifano ya matumizi
Kwa mfano, Waiziraeli huwapeleka
koondo wao kwenye dhabihu kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Lengo la kutoa
mifano ni kumsaidia msomaji asiye fahamu vyema neno husika aelewe jinsi neno
hilo linavyotumika.
Uingizaji wa nomino
Nomino nyingi katika lugha ya
kiswaili zina maumbo ya umoja na wingi.
Mfano:dume nmma-
mkopo;nm mi-
Viambishi ambatishi huwekwa kando ya
nomino kuashiria umbo la wingi la nomino.
Ngeli za nomino
Mfano:mkopo nmmi- [u-/i-]
Kutafuta maana unayoitaka
Neno linaweza kuwa na maana moja au
zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji kamusi hana tatizo kwani hiyo
ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno linapokuwa na maana zaidi ya moja,
mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi aichague. Ili kupata maana inayosadifu
itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana ambayo inahusiana na muktadha wa neno
linalotafutwa.
Mfano:kifungo nm vi-
- kitu cha kufungia
- kitu kinachotumiwa kufungia vazi kama vile shati,
gauni, suruali n.k
- adhabu ya mtu kuwekwa jela kwa muda fulani
Iwapo mtumiaji aliona neno ‘kifungo’
kwa muktadha wa: “Juma alihukumiwa kifungo cha miaka kumi baada ya kupatikana
na hatia ya kubaka….” Maana ya mukatadha huu itakuwa ni ile maana ya 3 kwa
sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo neno kifungo limetumika na wala
sio maana ya 1 wala ya 2.
No comments:
Post a Comment