MADA YA TATU:
FASIHI KWA UJUMLA
Dhima ya Fasihi
Dhana ya Fasihi
Fasihi; ni sanaa ya lugha inayoshughulikia masuala yanayomhusu
binadamu matatizo yake, ndoto zake, matumaini yake, migogoro yake na jinsi
anavyoingiliana na mazingira yake. (Wamitila, 2004).
Fasili hii imejaribu kufafanua
vizuri kile ambacho fasihi inajihusisha nacho, kimsingi fasihi inajihusisha na
wanadamu. Vitu vya msingi tunavyoviona katika fasili hii ni kwamba fasihi ni
sanaa, na fasihi inatumia lugha lakini zaidi fasihi inajihusisha na wanadamu.
Dhima za Fasihi katika Jamii
Dhima za fasihi katika jamii ni
pamoja na hizi zifuatazo:
- Kuburudisha jamii:Pamoja
na mambo mengine fasihi inalenga kuburudisha jamii. Kupitia takribani
vipera vyake vyote, fasihi huwa na kusudi la kufurahisha, kutumbuiza na
kusisimua hadhira, kwa mfano kupitia nyimbo, hadithi, mashairi na
kadhalika.
- Kuelimisha.
Fasihi hutumika kama nyenzo ya kuelimisha jamii, kupitia fasihi wanajamii
wanaweza kuelimishwa juu ya mambo mabalimbali, kama vile juu ya umuhimu wa
kuishi kwa amani, umuhimu wa kijikomboa kifikra, umuhimu wa kujikomboa
kiuchumi, ubaya wa ufisadi na kadhalika.
- Kuonya jamii.
Fasihi ina jukumu la kuhakikisha wanajamii wanakaa katika mstari wa
maadili ya jamii husika. Kupitia fasihi wanajamii wanapewa mwongozo wa
jinsi ya kufuata mwelekeo unaokubalika katika jamii.
- Kuunganisha jamii.
Fasihi huleta watu katika jamii. Watu huunganishwa kupitia kazi mbalimbali
za kifasihi, kwa mfano, kupitia nyimbo, miviga, vichekesho na kadhalika.
- Kukuza lugha.Fasihi
hutumia lugha kufikisha ujumbe wake katika jamii, lugha ya fasihi huwa ni ya
kisanaa zaidi na hivyo kuifanya iwe yenye mvuto kwa wasikilizaji au
wasomaji. Mtu anaposoma au kusikiliza kazi ya fasihi anapata ujuzi wa
lugha. Lakini pia fasihi yenyewe inaweza kutumika kama chombo cha kukuza
lugha. Wasimulizi na waandishi wa fasihi huhitaji kuwa na utajiri mkubwa
wa lugha.
- Kuhifadhi mila, tamaduni na itikadi za jamii. Kupitia fasihi simulizi, tamaduni na mila za jamii
husika huhifadhiwa. Kwa mfano kupitia methali, misemo, nahau na
vitendawili unaweza kujua mila na tamaduni za jamii husika.
- Kukuza uwezo wa kufikiri. Vipera vingi vya fasihi huwachochea hadhira kufikiri
sana ili kupata suluhisho. Kwa mfano, vitendawili, ngano za mtanziko na
kadhalika.
Aina za Fasihi
Kuna tanzu mbili za fasihi, ambazo
ni fasihi andishi na fasihi simulizi.
Dhana ya Fasihi Simulizi
Fasihi Simulizi ni utanzu wa fasihi
ambao unawakilisha sanaa ya lugha inayopitishwa kutoka kwa kizazi hadi kizazi
kwa njia ya maneno/masimulizi ya mdomo.
Sifa na Dhima za Fasihi Simulizi
Sifa za Fasihi Simulizi
- Hupitishwa kwa njia ya mdomo
- Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo
wa msimulizi, au wahusika.
- Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia
na hali
- Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa
katika fasihi simulizi.
- Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au
mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.
- Aghalabu huwa na funzo fulan
Dhima za Fasihi Simulizi
- Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira
- Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo
unaotarajiwa katika jamii.
- Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazingira
yao
- Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana
na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo.
- Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii
- Kuunganisha watu - huleta watu pamoja
- Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia
mbinu mbalimbali za lugha.
- Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.
- Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi
hutumika kupitisha muda.
- Fasihi simulizi ni chombo cha mawasiliano hususani
kupitia ngomezi.
Dhana ya Fasihi Andishi
Fasihi Andishi ni aina ya sanaa
ambayo hutumia maneno ya maandishi kupitisha ujumbe kwa hadhira.
Kuna tanzu kuu nne za Fasihi
Andishi:
- Hadithi Fupi
– Hii ni kazi ya fasihi andishi yenye kisa kimoja na mhusika mkuu mmoja na
maudhui yake sio changamani.
- Riwaya –Ni
kazi ya fasihi andishi yenye wahusika wengi na muundo changamani ni ndefu
na maudhui yake ni mapana.
- Tamthilia-
ni kazi ya kisanaa yenye muundo wa kiugizikaji inayowasilishwa katika
maandishi.
- Mashairi
- mashairi yakiwa yamechapishwa pia hutambulika kama fasihi andishi.
Sifa na Dhima za Fasihi Andishi
Sifa za Fasihi Andishi
- Hupitishwa kwa njia ya maandishi
- Ni mali ya mtu binafsi
- Haiwezi kubadilishwa papo kwa papo
- Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa katika
uwasilishaji wake.
Dhima za Fasihi Andishi
- Kukuza lugha
- Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi
- Kuburudisha
- Kuelimisha
- Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii
- Kuonya, kuelekeza, kunasihi
Tofauti
kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi
Zifuatazo ni tofauti kati ya Fasihi
Simulizi na Fasihi Andishi kama zilivyobainishwa katika jedwali hapa chini:
FASIHI SIMULIZI
|
FASIHI ANDISHI
|
|
1.
|
Huwasilishwa kwa njia ya mdomo
na/au matendo.
|
Huwasilishwa kwa njia ya maandishi
|
2.
|
Ni mali ya jamii.
|
Kazi andishi ni mali ya mwandishi
(na mchapishaji)
|
3.
|
Msimulizi anaweza kubadilisha
sehemu Fulani
|
Kitabu kilichoandikwa hakiwezi
kubadilishwa
|
4.
|
Huhifadhiwa akilini
|
Huhifadhiwa vitabuni
|
5.
|
Kazi simulizi hubadilika na wakati
|
Kazi andishi haibadiliki na wakati
|
6.
|
Huhitaji msimulizi na hadhira yake
wawe mahali pamoja wakati wa masimulizi
|
Msomaji anaweza kusoma kitabu cha
hadithi peke yake, mahali popote, wakati wowote
|
7.
|
Mtu yeyote anaweza kutunga na
kusimulia
|
Ni lazima mwandishi na msomaji
wawe na uwezo wa kusoma
|
8.
|
Hutumia wahusika changamano
(wanyama, watu, mazimwi n.k)
|
Hutumia wahusika wanadamu.
|
No comments:
Post a Comment