MADA YA
SITA: UANDISHI
Insha za Hoja
Insha za hoja ni insha zinazoelezea
jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo fulani
alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia. Hoja ni maelezo
bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake.
Katika uandishi wa insha za aina
hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo analiunga mkono na ni
lipi ambalo hakubaliani nalo.
Ili hoja zote zipate kueleweka ni
sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi kwamba mtu
aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana msimamo gani
kuhusu mada hiyo.
Muundo wa Insha za Hoja
Elezea muundo wa insha za hoja
Katika uandishi wa insha, muundo
wake unakuwa na vitu vifuatavyo:
- Kichwa cha insha;
kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako. Kwa
mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k
- Utangulizi;
Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno
muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika
insha yako.
- Kiini cha insha;katika
kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha
yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja
ulizonazo katika mjadala wako.
- Hitimisho;
hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha
au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.
Barua Rasmi
Dhima ya Barua Rasmi
Elezea dhima ya barua rasmi
Barua rasmi ni barua zinazohusu
mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni kutoa taarifa, kuomba kazi au
huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano kwa kiongozi fulani wa nchi,
kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au marejeo.
Muundo wa Barua Rasmi
Elezea muundo wa barua rasmi
Barua rasmi au barua ya
kiofisi/kibiashara huzingatia mtindo rasmi wa barua. Kwa kawaida huwa na sehemu
zifuatazo:
- Anwani ya mwaandishi -huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa
karatasi.
- Tarehe ya barua hiyo-
tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi
- Anuwani ya mpokeaji-
Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa karatasi, na
huwekwa msitari mmoja chini ya tarehe.
- Salamu-
Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama
bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza
hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => taja jina lake ikiwa mnajuana na
unayemwandikia. Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia
bw/bi
- Mada-
Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na
maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa
na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya
barua kiukamilifu.
- Utangulizi–
Hukaa chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya
moja ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo.
- Ujumbe-
Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.
- Tamati–
mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako mwaminifu,
[jina], Sahihi
Simu
Dhima ya Simu ya Maandishi
Elezea dhima ya simu ya maandishi
Simu za maandishi ni aina ya barua
fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana kuliko barua za kawaida.
Simu hizo huandikwa kwenye fomu
maalumu ambazo hutolewa na shirika la posta. Simu za maandishi hujulikana kama
telegram.
Kwa kawaida simu za maandishi
hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika simu za maandishi ni njia ya haraka
ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya kuandika simu yako ujumbe humfikia
huyo unayemtumia katika muda usiozidi siku tatu.
Gharama za simu za maandishi hutozwa
kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika. Kwa hiyo ujumbe unaotumwa huandikwa
kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama kubwa.
Example 1
Mfano wa simu ya maandishi:
MUSA KINGAMBE SLP 5299 DSM
NJOO HARAKA
DADA MGONJWA LINGIDO
Kuandika Simu za Maandishi kwa
Kuzingatia Muundo na Taratibu za Uandishi
Andika simu za maandishi kwa
kuzingatia muundo na taratibu za uandishi
Muundo wa kuandika simu za maandishi
una mambo yafuatayo ya kuzingatia ambayo ni anwani ya mpelekewa taarifa, ujumbe
na jina la mwandishi au mtuma simu. Mambo mengine ya kuzingatia ni kuandika
maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha usomaji na kuandika simu ya
maandishi katika karatasi maalumu ambayo hutolewa na posta.
Activity 1
Andika simu za maandishi kwa
kuzingatia muundo na taratibu za uandishi
Kadi za Mialiko
Kadi za mialiko ni aina ya karatasi
ngumu zinazopeleka taarifa fupi za kumwomba mtu ahudhurie katika sherehe fulani
kama vile harusi, ubatizo mahafali n.k
Muundo wa Kadi ya Mialiko
Fafanua muundo wa kadi ya mialiko
Mambo muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa
katika kadi ya mwaliko:
- Jina la mwandishi au mwalikaji
- Jina la mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama
vile: Profesa, Bi., Bw. Bw&Bi n.k
- Lengo la mwaliko
- Mahali pa kufanyika shughuli
- Tarehe ya mwaliko
- Wakati wa shughuli
- Jina na anwani ya mtu atakayepelekewa majibu.
Mialiko huweza kuandikwa kwa namna
mbili yaani kama barua au kadi. Jina la mwalikwa katika kadi ya mwaliko
hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama vile Bwana….Bi…..au Ndugu…ikiwa
waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na Bwana na Bibi.
Example 2
Mfano wa Kadi ya Mwaliko
Familia ya Manyama na Joseph
Wanapenda kukualika/kuwaalika
Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi……… kwenye harusi ya kijana wao mpendwa
Benny Joseph itakayofanyika huko Kiabakari katika ukumbi wa simba siku ya
Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana hadi saa 3.00 usiku
Kufika kwako ndio mafanikio ya
sherehe hii.
Majibu kwa (wasiofika tu)
Emmanuel Joseph
Simu: 0786 67 54 62
Uandishi wa Dayalojia
Dhana ya Dayolojia
Elezea dhana ya dayolojia
Dayalojia ni mazungumzo au
majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanaozungumza kwa kupokezana. Kama
zilivyo kazi nyingine za utunagaji, dayalojia inaweza kuwasilishwa kwa nijia ya
mazungumzo au maandishi.
Katika kutunga dayalojia mtunzi hana
budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza anapaswa kutafakari
kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo
kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu
kulingana na matendo yao. Kwa mfano kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa,
vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali
ya mkulima halisi.
Mambo ya kuzingatia katika dayalojia
ni pamoja na haya yafuatayo:
- Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili
kumfahamisha
- Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati
ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
- Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya
kusisimua
- Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia
maneno ili dayalojia iwe na uhalisia.
Example 3
Mfano wa dayalojia
Wambura:
|
(Anaonekana mwenye furaha,anamwita
rafiki yake, Anna)Wow, Anna! Tumekutana tena, siamini macho yangu! (wanakumbatiana
wote wakiwa na nyuso za furaha).
|
Anna:
|
(Anatabasamu huku ameshikilia
mkono wa kulia wa Wambura, anaonesha shauku kuu)Wambura! Bado unanikumbuka? Nina furaha sana kwa kweli, ni
muda mrefu sana.
|
Wambura:
|
(Anachekelea)Aaaah, nahisi kama naota Neema, siamini kama nimekutana na
wee leo hii ni muda mrefu sana, nimefurahi kwa kweli.
|
Anna:
|
(Anachekelea)
|
Wambura:
|
Mbona wachekelea tu….
|
No comments:
Post a Comment