MADA 1
: FASIHI KWA UJUMLA
MADA NDOGO -1; NADHARIA YA FASIHI
Nadharia ni Imani au kanuni zinazofuatwa na watu
Fulani au jamii katika kushughulikia jambo Fulani mahsusi.
Nadharia za fasihi ni muongozo au kanuni zinazofuatwa
na wataalamu (wanazuoni) mbalimbali katika kuteua fasili/maana halisi ya
fasihi.
Fasihi ni nini?
Wataalamu mbalimbali wamefasili/Maana ya dhana ya fasihi,
maana hizo ni kama zifuatazo:-
1. Fasihi ni kioo cha jamii (maisha),fasili hii inamaana kwamba mtu
anaweza akajitazama akaona taswira yake na akajirekebisha . Fasili hii ina
udhaifu kwani kioo hakiwezi kumweleza mtu jambo la kufanya ili hali yake iwe bora zaidi
. Pia si sehemu zote takazojiona kwenye kioo(F.Mkwera , 1978)
2. Fasihi ni hisi,Fasili hii ina maana kuwa lazima pawe
na mguso fulani wa wahusika ndipo mtu aweze kuandika na kueleza jambo fulani,’Sengo
na kiango Wanasema “hisi ni kama kuona
njaa, baridi, joto, uchovu pengine kuumwa. Hapa swali la kujiuliza ni kwamba,
je fasihi ina maana moja kati ya hiyo? Uamuzi wa kutenda jambo huja wakati
umeguswa?. Je hizo hisia ziko wapi? Je mtu ambaye haguswi sana moyoni hawezi kuwa mwanafasihi mashuhuri? Je mwanamuziki ambaye huusifu uzuri
wa mwanamke anaguswa moyoni? Je mwandishi kama Shaban Robert, E. Kazilahabi wameguswa mara ngapi? Vile vile
kivipi waguswe Zaidi ya wengine? (Sengo
na Kiango) hivyo bado fasili hii ina udhaifu
3.
Fasihi ni
mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha ya hadhi na taadhima.Fasihi hii ina
maana kwamba mwamvuli humkinga mtu katika mvua na jua na fasihi huhifadhi na
kukinga amali za jamii zisiharibike maana hii ni nzuri kwani inasisitiza
utunzaji wa kile kizuri kwa maana kuwa jamii inachambua kuwa makini na kuona
amali za jamii zinazohifadhiwa. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba jamii itasaidiwa?
Jamii haitulii kama maji katika mtungi bali hubadilika mara kwa mara kutokana na
nguvu za migongano, hivyo kitu kipya huzaliwa na cha zamani hufa kwasababu
jamii haitulii, hivyo hakuna haja ya kuhifadhi amali za jamii chini ya
mwamvuli. Zipo mila na desturi zilizohifadhiwa na makabila mengi ambazo hazina
nafasi leo. Hali ya mabadiliko ya jamii kutokana na siasa, utawala, uchumi,
elimu, sayansi na teknolojia vyote hivi katika maendeleo vitatoboa mwamvuli na
kuziharibu amali zilizohifadhiwa (Sengo na Kiango 1973)
4. Fasihi ni sanaa ya uchambuzi wa lugha
yoyote kadri inavyosemwa,inavyoandikwa na kusomwa,Hii ni kweli kuwa fasihi lazima
itumie lugha kwani lugha ndicho chombo muhimu kitumiwacho na fasihi na si
fasihi tu bali taaluma zote hutumia
lugha.Udhaifu wa fasili hii ni kwamba maana hii imejikita katika uchambuzi wa
Lugha kana kwamba hakuna vipengele vingine vinavyochambuliwa katika fasihi
zaidi ya lugha na hii ni sawa na kusema umeme ni waya wa shaba kwa vile umeme umepita
kwenye waya huo.Na hii ni si kweli kwani Hisabati,fizikia au historia si fasihi
ingawa hutumia lugha.
5.Fasihi ni kielelezo cha hisia za
mwandishi juu ya mambo yanayomwathiri yeye,kikundi au jamii nzima anamoishi na
kwamba lengo lake ni kustarehesha au kufunza wasomaji.Fasili(maana) hii ni nzuri kwa ujumla
lakini mapungufu yake ni kwamba imemuwekea mwandishi kama chanzo pekee cha
uumbaji wa Sanaa na hasa akili yake pia maana hii imetokana na falsafa ya kidhaanifu kwa kuhusisha uchambuzi
wa mambo katika fikra bila kutazama hali
halisi ya maisha ya watu na vitu.
6. Fasihi ni chombo cha utetezi wa maslahi ya
tabaka moja au jingine na kwamba mwandishi ni mtumishi wake anayejijua au
asiyejijua atake asitake mwandishi huyu analengo au dhamira fulani anayotaka
kuionesha.Wasomaji
wanaweza kuyakubali au kuyakataa maudhui ya kazi yake na pengine jamii
kufuatana na msimamo juu ya itikadi ya siasa (napengine amali za jamii) inayotawala
kwa kipindi kile na jinsi mwandishi
anavyooanisha maandishi yake na itikadi hiyo.Fasili au maana hii ni nzuri sana
kwani kwa kifupi ni kwamba fasihi ni mojawapo ya silaha nyingi zinazotumiwa na
tabaka moja kutetea maslahi yake katika mapambano ya kudumu dhidi ya matabaka
mengine.
Hitimisho kwa ufupi fasihi ni taaluma inayotumia Sanaa
maalumu ya lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii inayohusika.Fasihi hutueleza
uzuri wa maandishi au mazungumzo ambayo huonekana katika mashairi ,historia za
maisha ya watu ,tenzi,hadithi za kusisimua na insha mbali mbali.
DHIMA YA MWANAFASIHI KATIKA JAMII
Maana ya mwanafasihi/mtunzi wa kazi ya fasihi
Ni mtu yeyote anayejishughulisha na uandishi au
utungaji wa kazi za fasihi yaani fasihi andishi na fasihi simulizi.
DHIMA ZA MWANAFASIHI
1. .Kuelimisha jamii,Katika kuelimisha jamii mwanafasihi ;
(a)Huchambua
na kuchochea umma kuwafumbua macho,hufichua wazo au uchafu uliomo
katika jamii,wagandamizaji hufichuliwa na wagandamizwao hupewa muongozo sahihi
ili waitambue hali yao dhaifu.Mfano”Duka la Kaya”imechambua na kuchochea jamii
ili iweze kupambana na hali mbaya ya maisha.
(b).Kupiga vita kwa hali na mali mazingira yote ya
ujinga,maradhi,njaa na umaskini,Mfano mwandishi wa tamthiliya ya Hawala ya fedha
anapambana na maovu kama vile ujinga na uvivu na Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe
anajadili na kupiga vita uzembe na
mengineyo.
(c).Kukosoa jamii,Mwanafasihi anaikosoa jamii katika vipengele mbalimbali vya
maisha.Mfano riwaya ya “ Vuta n’kuvute”inakosoa mila na desturi zilizopitwa na
wakati “Raha karaha na Mashairi ya Chekacheka”mwandishi wa diwani hizi
anaikosoa jamii ya Tanzania kwa mapana kama vile Uongozi mbaya,kukithiri kwa
rushwa n.k.
(d).Kutia hamasa na kumfanya mtu asikate tamaa,Mfano S.Kandoro anaeleza hamasa ya
wananchi waliokuwa wameungana kama “Siafu ili kumtoa nyoka pangoni katika
shairi liitwalo ‘Siafu wamekazana’’.Mwandishi kwa hamasa
amewaita waafrika njooni “au” kwetu ni kwa nini’.Hivyo ni wazi kuwa kazi hizi
zinajitahidi kuendeleza mapambano dhidi ya ukoloni mambo leo.
(e)Mwandisi anadhima kujenga misingi na fikra za usawa na
demokrasia miongoni mwa umma wa wakulima na wafanyakazi,Mwanafasihi huyu huwatukuza wakulima
na wafanyakazi pamoja na amali zao.
(f) Mwanafasihi hueneza mawazo na falsafa za jamii,Kwa mfano katika shairi na ngonjera
za Mathias Mnyapala ametangaza sana siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa kutumia
ngonjera za UKUTA 1 & 2 vile vile riwaya kama vile mfaa na utu,njozi za
usiku,ndoto yandaria ,jero si kitu n.k zimetangaza sana siasa ya ujamaa na
kujitegemea hapa nchini Shaban Robert aliwahi kueneza falsafa juu ya kweli kwa
kiasi kikubwa katika mashairi yake.
(g)Mwanafasihi hutoa mwongozo kwa kuikomboa jamii kutoka
fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na kujikomboa ili iweze kupata
haki na usawa,Mfano Riwaya ya kiimbila “Ubeberu Utashindwa” na
tamthiliya ya E.Mbogo “Tone la Mwisho” G Husseni “Kinjekitile”
2.Kuburudisha,zipo kazi mbalimbali za fasihi
zinazoburudisha.Msomaji au msikilizaji wa fasihi huburudisha yaani husisimsha
mwili na akili na huvutiwa kihisia na kazi ya fasihi anayoisoma au
kusikiliza.Tabia ya msomaji au msikilizaji huweza kujengwa kutokana na mafunzo
na mifano bora ya matendo ya kuigwa anayoyapata katika fasihi.
3.Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii,Amali za jamii ni pamoja na mila na
desturi mtindo wa maisha,Imani, historia jiografia,visasili na visakale ni
urithi wa maarifa ya kijadi kwa mfano tiba, sayansi ya kilimo,mbinu za
uwindaji,ufundi wa aina zote n.k.Amali hizo huweza kuhifadhiwa na kuendelezwa
na mwanafasihi na hivyo kurithishwa kwa vizazi vijavyo.
Kwa mfano tamthiliya ya Kinjikitile inahifadhi mengi kuhusu
hali ya maisha wakati wa ukoloni wa kidachi,Kurwa na Doto (1969) ni
riwaya yenye kuhifadhi japo kwa kejeli,mila,desturi na itikadi za jadi za
waunguja,Riwaya ya Bwana Mnyombokero na Bibi Bugonoka;Ntuhanalwo na
Buliwali iliyoandikwa na Anicet
Kitereza imehifadhi mila,Imani,mtindo wa maisha,ufundi na taaluma mbalimbali za
jadi za wakerewe mengi yaliyoeleza humo siku hizi hayapatikani popote isipokuwa
katika riwaya hiyo, vile vile Mzishi wa Baba ana Radhi (1967)
kinaeleza mila na desturi za wapangwa.
Watunzi hasa nyimbo na visasili hukoleza pia shughuli za
kijadi za kiutamaduni kwa mfano Ibada,matambiko,sherehe,katika shughuli za aina
hiyo nyimbo licha ya kuwa kiburudisho hubeba ujumbe wenye kuhusiana na tukio hilo.
4.Kudumisha na kuendeleza lugha,Kwa kadri lugha inavyotumiwa na
kufinyangwa na watunzi ndivyo inavyokuwa na kupevuka.Maneno mengi yatumiwayo
leo katika lugha mbalimbali yalibuniwa na kuenezwa na watunzi wa
mashairi,riwaya,nyimbo na tamthiliya katika Kiswahili.Mifano mizuri ni maneno
mengi yahusuyo Sanaa ya ushairi(vina, mizani, beti, mishororo, miwala,
tathlitha, takhimisa, tarbia n.k)
Katika jadi ya ushairi wa kiswahili inadaiwa kuwa
ushairi ulikua ni ghala ya maneno.Washairi walitumia maneno magumu au
yasiyokuwa ya kawaida makusudi ili kuyahifadhi ysipote.katika tamaduni nyingine
kazi hiyo hufanywa na kamusi pamoja na vitabu viitwavyo Hazina ya maneno kwa kuwa
waswahili hawakuwa na kamusi kazi ya kuhifadhi maneno ilifanywa na ushairi.
DHIMA ZA MHAKIKI WA
KAZI ZA FASIHI
Uhakiki ni kazi au kitendo cha kuchambua au kufafanua kazi ya
fasihi, kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo katika maandishi ya mwandishi asilia.
AU ni sayansi maalumu ya
kuchambua na kuona ubora wa kazi hizo kwa kutumia vipengele mbalimbali vya fani
na maudhui na kuangalia uwiano na uhusiano ama kuathiriana kwake. Uhakiki ni
elimu na ujuzi wa kuipembua kazi ya sanaa inayohusika kimaudhui na kifani.
Uhakiki ni daraja ya juu ya maelezo ya kisanii yenye
kuwalenga watu wa aina tatu:- wasomaji wa
kawaida walio nyumbani na shuleni, waandishi asilia wa kazi za sanaa na
wahakiki.Msomaji hupata mwongozo wa namna bora zaidi ya kumwezesha
kuifahamu kazi ya sanaa kutokana na viwango tofauti vya uhakiki juu ya kazi za
sanaa.
Mhakiki ni nani?
Mhakiki ni mchambuzi na mfafanuzi wa maandishi ya kisanaa
hasa yale ya kifasihi. Ni jicho la jamii kwa vile anagundua mazuri yaliyomo
katika kazi ya fasihi na pia ndiye anayeona hatari ya maandishi hayo kwa jamii.
Mhakiki ni bingwa wa kusoma na kuchambua maudhui, maadili na ujumbe uliomo
katika maandishi ya fasihi.
Ni mtu mhakiki anajihusisha na maandishi ya waandishi asilia na hungalia kwa jinsi
gani mwandishi anawakilisha hali halisi ya jumuiya ya watu. Kwa upande
mwingine, mhakiki anashughulikia uwanja wa fasihi andishi pamoja na ule wa
fasihi simulizi.
Sifa za mhakiki
·
Mhakiki anatakiwa ajue historia na
mazingira yaliyomkuza mwandishi.Mhakiki ili aweze
kuifanya kazi yake vizuri anapaswa aelewe vema historia ya mwandishi na
jamii yake inayohusika. Aelewe asili ya mwandishi, historia yake na utamadumi
wake kwa ujumla. Kutokana na hali hii, mhakiki anaweza kuelewa kama mwandishi
amefanikiwa kueleza ukweli wa maisha ya watu, yaani jamii inayohusika.
·
Mhakiki anatakiwa kuelewa historia na
siasa ya jamii inayohusika.Hii itamwezesha kuyaelewa matatizo ya jamii hiyo. Mhakiki lazima
aifahamu barabara jamii ambayo mwandishi aliandikia juu yake ili aweze kuandika
uhakiki imara, ama sivyo atakwama na kuandika uhakiki dhaifu. Mhakiki anapaswa
kuelewa historia ya watu ambao maandishi hayo yanawahusu, bila kuifahamu
historia yao, itakuwa vigumu kwake kueleza bayana baadhi ya mambo ambayo
mwandishi aliandika na kwa nini aliandika hivyo. Uhakiki wake ukisomwa na watu
wanaoishi katika jamii hiyo si ajabu kusema yeye si mhakiki. Mhakiki huangalia
jinsi gani mwandishi alivyoiwakilisha hali halisi ya jumuiya na historia ya
watu hao.
·
Mhakiki awe amesoma kazi mbali mbali za fasihi na
siyo ile tu anayoifanyia uhakiki. Hii itamsaidia kuwa na ujuzi zaidi katika uwanja wa uhakiki.
·
Mhakiki
anatakiwa asome tahakiki za wahakiki wengine katika uwanja wa fasihi na hata
nje ya jamii yake ili kupata upanuzi zaidi katika kazi ya uhakiki. Hii
itamsaidia kutoa uhakiki bora zaidi, kwani atakuwa amejifunza yale yaliyo
mazuri na kuepuka makosa waliofanya wengine.
·
Mhakiki
lazima awe na akili pevu sana ili aweze kung’amua mambo na akishayang’amua
ayaandike kwa lugha rahisi ili mawazo yake yasomeke na kila mtu kwa urahisi,
yaani atumie lugha ambayo itawatumikia wasomaji wake.
·
Mhakiki
lazima ajiendeleze katika taaluma mbali mbali ili aweze kuwa na mawazo mengi
ambayo yatamsaidia kuhakiki maandishi mbali mbali. Mhakiki hodari huichonga
jamii yake kimawazo. Huiimarisha isitetereshwe au kupofushwa na waandishi
wapotoshaji.
·
Mhakiki
anapaswa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kisayansi bila kuonyesha hisia za
wasomaji. Asiwe na majivuno na
awaheshimu anaowahakiki na anaotaka wasome uhakiki wake. Asichukie au
kusifia tu kazi za waandishi kwa sababu zake binafsi bila kueleza ukweli wa
kazi hiyo. Mhakiki ni rafiki wa mwandishi na wasomaji . Kwa hiyo, mhakiki ni
lazima awe fundi katika kutoa hoja zake na lazima ziwe zinagonga, zenye kuibua
udadisi na kuathiri.
·
Mhakiki
anapaswa asiwe mtu wa kuyumbishwa na maandishi au maneno ya wahakiki au watu
wengine. Tunatarajia aseme kweli kuhusu kazi hiyo. Uhusiano baina ya mhakiki na
mwandishi usiathiri uhakiki wake.
TAHAKIKI
NI NINI?
Ni kitabu kinachotolewa na mhakiki kinachambua vitabu mbali
mbali vya maandishi asilia. Tahakiki hutoa uchambuzi na uhakiki wa vitabu vya
hadithi/tamthiliya/ushairi kwa kuzingatia vipengele vya fani na maudhui. Mfano
wa tahakiki ni kama vile:- Senkoro(1988).
Ushairi: Nadharia na Tahakiki. DSM: DUP,Kiango, Msokile na Sengo (1987),
Uhakiki wa vitabu vya Fasihi Sekondari na vyuo. NPA, n.k.
Dhima
ya mhakiki
· Kuchambua na
kuweka wazi mafunzo yanayotolewa na kazi za fasihi:Hapa mhakiki
anatoa ufafanuzi wa kimaudhui wa kazi ya fasihi. Mhakiki husoma kwa uangalifu
kazi ya fasihi.Baada ya kusoma kwa makini, hutafakari na kuchunguza maudhui,
maadili na ujumbe ambao mwandishi amekusudia kuwafikishia wasomaji wake na
jamii inayohusika.
· Kuchambua na
kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi:Mhakiki
huwasaidia wasomaji ili wasishindwe kuyaelewa maudhui barabar kutokana na
kukanyagwa na usanii. Matumizi, mathalani ya ishara ni baadhi ya mbinu ambazo
zinaweza kumkanyaga msomaji ambaye hajapata utaalamu mkubwa wa kuchambua.
Mhakiki wa kufichua ishara fulani ina maana kuwa amemsaidia msomaji kupata
ujumbe kikamilifu.
Kuhusu
matumizi ya picha, kwa kawaida, lugha ya picha ina mguso sana na huibua hisia
aina na hata kuchekesha au kuwafanya watu walie machozi. Mhakiki sharti
awaambie kwamba, matumizi ya picha ni mbinu mojawapo inayosaidia maudhui
kuwaganda wasomaji. Picha inayochekesha, kufurahisha, kukejeli, n.k. Haikomei
pale tu, kwani baada ya kucheka, n.k. msomaji huathiriwa sana kinafsi na
aghalabu huachiwa mafunzo fulani. Hivyo mhakiki lazima achambue na kuyaweka
wazi mafunzo yanayotolewa na picha hiyo.
·
Mhakiki ana dhima ya kumshauri mwandishi ili afanye
kazi bora zaidi:Mhakiki
anamfundisha mwandishi juu ya yale anayoyasema yanavyoweza kupokelewa na jamii.
Humwonyesha msanii uzuri na udhaifu wa kazi aliyoisaini. Kitendo hiki humfanya
msanii ajifunze mambo yapi ni mazuri na yapi ni mabaya kama anavyoelekezwa na
mhakiki, na hivyo humfanya awe na nafasi nzuri ya kuirekebisha kazi hiyo
atakapoishughulikia kazi nyingine. Kwa msingi huo, mhakiki anaweza kulaumu au
kusifu/kumpongeza mwandishi wa kazi yoyote ya kisanaa.
·
Mhakiki ana dhima ya kumwelekeza msomaji ili apate
faida zaidi kuliko ile ambayo angeweza kuipata bila dira ya mhakiki:Mhakiki huifunza
jamii namna ya kupokea na kuifurahia kazi ya sanaa. Vilevile mhakiki huwasaidia
wasomaji kuyabaini maandishi yaliyo sumu kwa jamii. Mhakiki lazima ayafichue
maandishi hayo ili yasieneze sumu kwa jamii. Mhakiki lazima ayafichue maandishi
hayo ili yasieneze sumu kwa jamii inayohusika.
·
Mhakiki ana dhima ya kukuza kiwango cha utunzi na
usomaji wa kazi ya fasihi:Kutokana na ushauri anaopata mwandishi
kutoka kwa mhakiki, humfanya awe makini zaidi wakati wa kushughulikia kazi
nyingine.Vilevile wasomaji wanakuza kiwango chao cha usomaji kwa kufuata
mawaidha ya mhakiki.
·
Mhakiki ana dhima ya kusema wazi kuhusu kiwango cha
maandishi anayohakikiwa:Akisema wazi kwamba, maandishi hayo yako
katika kiwango cha chini, mara mwandishi huyo asilia atakapoamua kutunga tena,
atashawishika kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu zaidi. Na
waandishi wengine watapatiwa msukumo wa kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango
cha juu zaidi. Na waandishi wengine watapatiwa msukumo wa kuandika maandishi
yaliyo kwenye kiwango cha juu pia. Na hivi ndivyo mhakiki anavyosaidia kukuza
na kuendeleza maandishi ya taifa lake.
·
Mhakiki anatakiwa kuheshimu na kuthamini kazi za
waandishi na kuzifanyia haki:Jamo la msingi (lazima) kuzingatia na
kuwa, mhakiki afanyapo kazi yake huwa vitani. Mhakiki anapaswa kujua namna ya
kuwanasa wasomaji bila wao kujitambua na kuwa na uwezo au kuchambua kisayansi
mambo bila kutoonyesha hisia za wasomaji. Anatakiwa asiwe na majivuno na
aheshimu anaowahakiki na anaowataka wasome uhakiki wake. Awachukue hatua kwa
hatua kifalsafa hata waone vigumu, na kwamba haiwezekani kupigana naye.
MISINGI YA UHAKIKI WA KAZI
ZA KIFASIHI
Uhakiki
wa kazi za kifasihi hufanywa kwa kuzingatia vipengele vya fani na maudhui. Fani
na maudhui ni kama masanduku makubwa ambayo mhakiki huyafungua na kuanza
kuchunguza vilivyomo ndani yake. Kila moja lina vipengele vidogovidogo ndani
yake.
(a)Fani
Fani
ni mbinu au ufundi anaobuni na kutumia mtunzi wa kazi ya kifasihi ili kufikisha
ujumbe kwa hadhira yake iliyokusudia.
Fani ina vipengele mbalimbali. Vipengele hivyo ni pamoja na wahusika, mandhari,
lugha, muundo na mtindo.
1)Wahusika
Wahusika
wa kazi ya kifasihi ni viumbehai au wasio hai; halisi au wa kubuni, ambao
wanatenda matendo mbalimbali ndani ya kazi ya kifasihi. Wahusika wanaweza kuwa
ni binadamu, mawe, miti, malaika, miungu na mizimwi. Kwa kawaida, wahusika
katika kazi ya kifasihi hutumika kuwakilisha au kubainisha maisha halisi ya wanadamu.
Aina za wahusika
Wanafasihi
mbalimbali wamewagawa wahusika katika makundi tofauti. Hata hivyo, sisi
tutawagawa katika makundi makuu mawili, yaani wahusika wakuu na wahusika
wadogo.
· Wahusika wakuu
Mhusika
mkuu ni mhimili wa kazi ya kifasihi na huonekana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa
kazi ya kifasihi. Mhusika mkuu ndiye wa muhimu kabisa kuliko wote. Huyu ndiye
anayehusiana zaidi na dhamira kuu ya kazi inayohusika.
· Wahusika wadogo
Hawa
ni wahusika wanaomsaidia mhusika mkuu kufikisha ujumbe wa mtunzi kwa hadhira.
Kwa kawaida, wahusika wadogo huchomoza hapa na pale kwenye kazi ya kifasihi,
kisha huweza kutoweka kwa muda au kutoweka kabisa. Kwa mfano, mhusika mdogo
masikini anaweza kupambanishwa na mhusika mkuu ili kubainisha ukarimu au uchoyo
wa mhusika mkuu, kisha huyo mhusika mdogo hatumwoni tena. Wahusika, wawe
wakubwa au wadogo, wanaweza kuwa duara, bapa au shinda:
§ Wahusika
duara
Wahusika
duara (au mviringo) ni wahusika wenye sifa halisi za ubinadamu, yaani
wanaonekana ni binadamu halisi. Hii ni kwa sababu wanabainisha katika maisha
yao uzuri na ubaya – wema na uovu, ujasiri na woga, ushindi na kushindwa. Pia,
wanabadilika kiakili, kimtazamo na kimaadili kadiri wanavyokutana na changamoto
za kimaisha kama ilivyo kwa binadamu halisi.
§ Wahusika
bapa
Hawa
ni wahusika ambao hutokea wakiwa na tabia ya aina moja kuanzia mwanzo hadi
mwisho.Wao hawakui au kubadilika,bali hubakia na msimamo au mtazamo ule ule walioanza
nao. Kama ni mchoyo, anakuwa ni mchoyo kuanzia mwanzo hadi mwisho.
§ Wahusika
shinda
Hawa
ni wahusika ambao wako katikati ya wahusika duara na bapa. Wahusika hawa
wanaweza kubadilika, lakini si kutokana na misimamo yao, bali ni kwa sababu ya
kuyumbiswa na wahusika wengine. Ni wahusika ambao hawajitegemei kimawazo.
Tunaweza
kuonyesha aina za wahusika kwenye mchoro kama ifuatavyo:
Wahusika
|
Duara
|
Shinda
|
Bapa
|
Wadogo
|
Wakuu
|
Shinda
|
Duara
|
Bapa
|
2. Mandhari
Mandhari
ni mahali ambako matukio ya kwenye kazi ya kifasihi yanatokea.Mandhari yanaweza
kuwa halisi au ya kubuni tu. Kwa mfano, mtunzi anaweza akawaweka wahusika wake
kwenye Jiji la Dar es Salaam. Haya ni mandhari halisi. Vilevile, anaweza
kuwaweka wahusika kwenye nchi iliyoko chini ya bahari au kwenye jua. Hayo
yanakuwa si mandhari halisi bali ni ya kufikirika au ya kubuni tu.Kwa hiyo, mandhari yanaweza
yakawa mjini au kijijini, msituni au baharini, chini ya ardhi au angani.
3
.Lugha
Lugha
ndiyo malighafi kuu inayotumiwa na mtunzi kuzalisha kazi ya kifasihi. Lugha ya
kifasihi ni lugha yenye mvuto kwa vile husheheni maneno ambayo yameshibishwa
taswira au picha, yaani ni lugha ya picha.Lugha ya kifasihi ni ya picha kwa
kuwa ina mambo yafuatayo:
(a) Nahau
Haya ni maneno, aghalabu mawili au
zaidi, ambayo maana yake ya jumla ni tofauti na maana ya neno mojamoja ndani ya
nahau hiyo. Kwa mfano, kuvunjika kwa moyo si kitendo cha moyo ulio ndani ya
mwili kukatika vipande, bali ni kukata
tama.Nahau hunogesha na kunakshi lugha, hivyo huongeza mvuto na kuupa uzito
ujumbe uliokusudiwa.
(b)Methali
Huu
ni usemi mfupi wa hekima ambao kwa kawaida huwa umerithiwa kutoka vizazi vya
nyuma, na ambao umebeba maana pana iliyojificha. Kwa mfano, kidole kimoja hakivunji chawa.
(c)Tamathali za semi
Hii
ni misemo ambayo hutumiwa kutoa maana tofauti na maana ya maneno yake. Zipo
aina mbalimbali za tamathali za semi. Zifuatazo ni baadhi yake:
Ø Tashibiha
Huu
ni ulinganishaji wa vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno: kama, mithili ya, sawa na, utadhani na,
mfano wa.Kwa mfano:
· Ametulia
kama gogo la mnazi.
· Tumbo
limetangulia mithili ya ngoma ya
gwaride.
· Ana
macho makali utadhani matone ya
gongo.
Ø Sitiari
Huu
ni ulinganishaji wa vitu au hali mbili moja kwa moja bila kutumia maneno: kama,
mithili ya, utadhani na mfano wa.
Kwa mfano:
· Kichwa
chake ni benki ya majina ya shule nzima.
· Maji
ya kifuu ni bahari ya chungu.
· Huyu
mtoto atakuwa kiboko ya wote.
Ø Mubalagha
Huu
ni uelezaji wa jambo kwa kutia chumvi
kuliko hali halisi ilivyo.
Kwa mfano:
· Yaani
Yule ana tumbo kama gunia.
· Huyu
dada anaweza kuongea hadi simu ikaishiwa chaji.
· Kwa
njaa niliyo nayo, naweza kumaliza hata mbuzi wawili.
Ø Tashihisi
Hii
ni njia ya kuvipa vitu visivyo binadamu sifa za ubinadamu, kwa mfano sifa za
kuongea, kufikiri, kucheka na kutoa hoja.
Kwa mfano:
· Jua
lilitudokolea jicho lake kali na kututemea moto wake hadi tukaenda kujificha
chini ya dari.
· Homa
ile ilimng’ang’ania kwa makucha yake huku ikimvutia gizani,lakini alipambana
nayo hadi ikatimua mbio.
· Mlango
ule ulitukaribisha kwenye tumbo la nyumba ile huku madirisha yakitukodolea
macho kwa mshangao.
Ø Taashira
Hii
ni njia ya kutaja kitu fulani kwa lengo
la kuwakilisha kitu au jambo jingine.
Kwa mfano:
· Mwanafunzi
Yule si kama wengine. Yeye ameweka kitabu
mbele.(Kitabu kinawakilisha masomo.)
· Ni
vema kwa kuwa ameamua kuishi maisha ya jembe.
(Jembe
linamaanisha kilimo.)
Ø Taniaba
Hii
ni njia ya kutumia jina fulani kwa namna ya ulinganisho ili kumaanisha kitu
kingine. Hivyo viwili vinakuwa na tabia fulani linganifu.
Kwa mfano:
· Kiongozi
Yule amekuwa ni Iddi Amini wanchi ile.
· Sisi
tunafuga mbuzi tu. Hawa ndio ng’ombe wetu.
Ø Majazi
Hii
ni aina ya tamathali ambayo hutaja sehemu tu ya kitu kwa lengo la kumaanisha
kitu kizima.
Kwa mfano:
· Masomo
haya yanahitaji vichwa kwelikweli.
(kichwa = mtu mwenye akili)
· Ajali
ile imepoteza roho saba. (roho = mtu kamili)
Ø Dhihaka
Haya
ni maneno yenye maana kinyume na vile yanavyosema, ambayo hutolewa kwa lengo la
kudunisha au kushusha hadhi.
Kwa mfano:
· Kijana
huyu asione chakula; macho humtoka na miguu humwasha. Domo hujaa mate tele kama
fisi aliyeona nyama.
· Bosi
wetu alikaa kwenye kiti chake, utadhani kakumbatia tungi la pombe ya kienyeji.
Ama kwa hakika bosi kajaliwa tumbo. Tumbo hilo ni shimo refu ambamo zinaishia
fedha za kampuni na jasho letu.
Ø Tasfida
Haya
ni maneno ya heshima yanayotumika ili kupunguza ukali wa jambo linalosemwa,
ambalo aghalabu, huwa aibu kulitamka mbele ya watu.
Kwa mfano:
· Sehemu
za siri
· Amechafua
hewa
· Yuko
uani
Ø Shtihizai,
Hii
pia huitwa kejeli. Haya ni maneno ambayo yamekusudiwa kuleta maana kinyume na
maana ya kawaida ya maneno hayo. Kwa mfano, kumwita mtu mweusi tii mzungu au cheupe; au mtu mwembamba sana kumwita bonge ni shtihizai au kejeli.
(i)
Ritifaa
Katika
tamathali hii, mtu huzungumza na mtu au kitu ambacho hakipo pamoja naye kama
kwamba yuko nacho.
Kwa mfano:
· “Nyerere
na Karume, mlitupenda wanenu; mkatuwekea misingi ya upendo na amani. Ona sasa
wameingia mbweha na fisi ulingoni. Ninajua kabisa hamngekuwa radhi nao hata kwa
dakika moja!”
Mbinu nyingine
Kuna
mbinu nyingine za kifasihi ambazo msanii anaweza kuzitumia, ambazo si tamathali
za semi. Mbinu hizo ni pamoja na:
v Takiriri
Hii
ni mbinu ya kurudiarudia manenokwa lengo la kusisitiza jambo.
Kwa mfano:
· Wewe
utafungwa, utafungwa utafungwa tu!
· Ukifika
pale ni kula, dansi; kula, dansi!
· Rudi
mwanangu; mwanangu rudi; rudi tu mwanangu; nitakupokea.
Takriri,
pia inaweza kuwa ni kurudia sauti ileile katika neno zaidi ya moja ambayo yanafuatana
karibu karibu.
Kwa mfano:
· Matata
alitamka maneno matano matamu. (sauti ma)
· Sili
wali ilhali ukali wa pilipili uko mbali. (sauti li)
· Alipanda
kwenye kitanda akajitanda shuka lake. (sauti nda)
v Tanakali
sauti
Hii
ni mbinu ya kuiga sauti fulani. Pia, hujulikana kama onomatopea.
Kwa mfano:
· Kakachakakacha
za kutembea kwao ziliniamsha usingizini.
· Mara
tulisikia ngo, ngo, ngo, mlangoni.
· Kabla
hatujakaa sawa, gari lile lilipita kama mshale, fyaaaa!
v Tashtiti
Katika
mbinu hii, msanii huuliza swali ambalo jibu lake liko wazi.
Kwa mfano:
· Kaka
alipofika pale, alimwona rafiki yake akiondoka. “Unaenda kweli?” aliuliza kwa
kutoamini.
· “Ya
nini kujisumbua? Ah! Acha nikalale zangu,” alijisemea Mawazo.
· “Mara
hii umesharudi?” Nilimuuliza kwa mshangao.
v Mdokezo
Hii
ni mbinu ya kuanzisha mazungumzo au wazo,kisha unaishia njiani bila
kulimalizia. Hii ni kwa sababu,kwa namna fulani, sehemu ambayo haikumaliziwa
inaeleweka kutokana na muktadha wa mazungumzo au maelezo yenyewe.
Kwa
mfano:
Mama:
Yaani Doto, umevunja tena kikombe?
Njoo
hapa! Leo nitaku……..!
Doto: Mama nisamehe. Bahati mbaya.
v Mjalizo
Hii
ni mbinu ya kupanga maneno katika mlolongo bila kuweka viunganishi kati yake.
Kwa
mfano:
· Wewe
lia, cheka, imba, lakini hutoki hapa!
· Yule
bwana alikaa chini, alisisimama, alijilaza chini, lakini maumivu yalibaki
palepale.
· Sisi
tulifanya kila njia. Tuliita, wapi! Tukatafuta, wapi! Tukapiga simu, wapi!
Mwishowe tukasema, liwalo na liwe!
v Taswira
Utengenezaji
wa taswira katika kazi za kifasihi ni mbinu inayojitegemea,bali huambatana na
mbinu nyingine, kwa mfano, tamadhali za semi. Taswira ni picha zinazoumbika
akilini ambazo tunazipokea kana kwamba ni kupitia kwenye milango ya fahamu.
Kwa mfano:
· UKIMWI
unabugia watu katika domo lake na kuwatafuna bila huruma.
Ifuatayo ni mifano ya
taswira mbalimbali:
Taswira za kuona
Kwa mfano:
· Ana
tumbo kubwa kama mtungi.
· Uso
wake umetokeza mbele utadhani wa tumbiri.
· Nyumba
ile ilikuwa kama kilima kikubwa chenye mapango ndani yake.
Taswira za kusikia
Kwa mfano:
· Kicheko
chake ni kama radi
· Kelele
za watu ukumbini zilikuwa kama maporomoko ya maji mengi.
· Njaa
husababisha tumbo langu kunguruma kama pikipiki.
· Taswira
za mguso
Kwa mfano:
· Mikono
ilikuwa inaparua kama msasa.
· Alikuwa
na ngozi nyororo kama kikombe cha
udongo.
· Maneno
yake yanachoma kama misumari ya moto.
Taswira za kunusa
Kwa mfano:
· Ungemhurumia
kwa vile ambavyo mguu ule ulitoa harufu kama mzoga wa paka.
· Huyo
bwana usimkaribie aongeapo ni kama unachungulia kwenye debe la pombe ya mnazi.
Taswira ya kuonja
Kwa mfano:
· Mwonekano
wake ulileta uchachu ndani ya akili yangu.
· Ana
maneno makali kama pilipili.
4. Muundo
Ni mpangilio na
mtiririko wa kazi hiyo kwa upande wa visa na matukio. Hapa tunachunguza jinsi
msanii wa kazi ya fasihi alivyofuma, alivyounda na alivyounganisha tukio moja
na jingine, kitendo kimoja na kingine, wazo na wazo, sura moja na nyingine,
ubeti na ubeti, hata mstari wa ubeti na mwingine.
Aina za miundo
(a)
Muundo wa msago,huu ni muundo wa
moja kwa moja ambao tunafatilia matukio mbalimbali tangu la kwanza hadi la
mwisho kwa mbinu ya utelezi. Kwa mfano, mhusika huzaliwa, hukua, huchumbia au
kuchumbiwa, huoa au kuolewa, huzaa watoto, huzeeka, hufa. Riwaya ya kuli (1978)
imetumia muundo huu. Katika riwaya hii tunamwona Rashidi akizaliwa, akikua,
anaanza kazi, anaoa, anaanza harakati za kudai haki za makuli na mwisho
anafungwa.
(b)
Muundo wa kioo,huu ni muundo wa
kimchangamano utumiayo mbinu ambayo huweza ama kumrudisha nyuma msomaji wa kazi
aya fasihi katika mpangilio wa matukio yake au kuipeleka mbele hadhira ya kazi
hiyo. Riwaya ya Zaka la Damu
(1976) imetumia muundo huu.
(c)
Muundo wa rukia,huu ni muundo
ambao visa hupandana. Katika muundo huu kunakuwa na visa viwili ambavyo
hupandana katika kusimuliwa kwake, na mwisho visa hivi huungana na kujenga kisa
kimoja. Mfano ni riwaya ya Njama
(1981).
Katika ushairi
muundo tunaangalia idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi. Kuna miundo ya
aina mbalimbali:
(i)
Muundo wa
Tathnia – kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari miwili.
(ii)
Muundo wa
Tathlitha – kila ubeti unakuwa na mistari mitatu.
(iii) Muundo wa Tarbia – kila ubeti unakuwa mistari minne.
(iv) Muundo wa Takhimisa – kila ubeti unakuwa na mistari
mitano.
(v)
Muundo wa
Sabilia
– kila ubeti unakuwa na mistari sita na kuendelea.
5.
Mtindo,ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi
hiyo na kuipa sura ambayo kifani na maudhui huainisha kanuni au kaida
zilizofuatwa kama ni zilizopo au ni za kipekee.Mtindo ni upangaji wa fani na
maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hatimaye hutokeza au huonyesha
nafsi na labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo.
Dhima ya mtindo
-
Humwezesha
msomaji kujua hisia za msanii kuhusu analiandika.
-
Humsaidia
msomaji kutafiti thamani ya maudhui na namna ya kuyapima au kuyathamini.
-
Hudokeza
kiasi cha hisia na mwamko wa wahusika katika hadithi, na vilevile kuonyesha
maendeleo yake.
-
Ni
kiungo muhimu cha mtiririko wa matukio.
-
Huiumbua
dunia ulimwengu wake ambapo yale maono ni ya msanii, lakini mtindo ndiyo
unaojitokeza kwa watu wengi ili wajue msanii anaandika kitu gani.
Katika mtindo
kinachotazamwa ni:Matumizi ya lugha,Nafsi alizotumia msanii,Matumizi ya
monolojia (maelezo), masimulizi na dialojia (mahojiano)
(b)
Maudhui
Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla
ya mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.
Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii
hadi akatunga na kusaka kazi fulani ya fasihi.
Vipengele
vya maudhui
·
Dhamira,Hii ni wazo kuu au mawazo mbalimbali
yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira hutokana na jamii. Kwa kawaida
dhamira huweza kuwa za kisiasa, kiutamaduni au kiuchumi. Katika dhamira, kuna
dhamira na dhamira ndogondogo.
·
Mtazamo,ni hali ya kuyaona mambo katika maisha
kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe. Wasanii wana mitazamo ya
aina mbili:
-
Mtazamo
kiyakinifu
– Huutazama ulimwengu au mazingira yanayomzunguka binadamu na mfumo wa
kihistoria. Mtazamo huu humfanya msanii kuutazama ulimwengu kama kitu dhahiri
katika uhalisi wake.
-
Mtazamo wa
kidhanifu
– Huu huchukulia ulimwengu kama kitu kinachobadilika kulingana na matakwa ya
Mungu. Msanii mwenye mtazamo huu, atawasilisha hivyo katika kazi yake.
·
Msimamo,hii ni hali ya mwandishi kuamua kufuata
na kushikilia jambo fulani.Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na
wengi,lakini yeye atalishikilia tu. Msimamo wa msanii ndiyo unaosababisha kazi
ya sanaa iwe na mwelekeo maalumu na hata kutofautiana na kazi za wasanii wengine.
·
Falsafa,huu ni mwelekeo wa imani ya msanii.
Msanii anaweza kuamini, kuwa mfano, mwanamke si chombo duni kama wengine
wanavyoamini. Au, kwa wale wapinga usawa, wanaweza kuwa na falsafa ya kumwona
mwanamke kuwa kiumbe duni.
Kwa hiyo,
falsafa ya kazi ya fasihi inatakiwa ichambuliwe kwa kuzingatia jinsi kazi hiyo
ilivyoutazama ulimwengu na kuueleza ukweli juu ya mambo mbalimbali. Ukweli huo
lazima uhusishwe na binadamu.
·
Ujumbe na maadili
Ujumbe katika
kazi ya fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya
fasihi.
·
Migogoro
Migogoro ni
mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Katika migogoro kuna
migogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, familia zao, matabaka yao,
n.k. Na migogoro hii mara nyingi hujikita katika uhusiano wa kijamii. Migogoro
yaweza kuwa ya:Kuichumi,Kiutamaduni,Kisiasa,Kinafsia
MADA NDOGO-2; MAENDELEO YA FASIHI
CHIMBUKO LA FASIHI NA SANAA.
Kuna mitizamo mikuu minne ya kiulimwengu inavyotokeza katika suala la
chimbuko la fasihi .Mitazamo hiyo ni
kama ifuatayo;
1. Mtazamo wa kidhanifu.
Mtazamo wa kidhanifu wa misingi yake
katika kudhani tu kwa hiyo kufuatana na mtazamo huu inaaminika kuwa fasihi na
Sanaa kwa ujumla kutoka kwa Mungu kwa hiyo mwanasanaa huipokea ikiwa imekwishapikwa
na kuivishwa na Mungu huyo.
Mtazamo wa namna hii ulijitokeza
tangu zamani sana wakati wanafalsafa wa mwanzo wa kigiriki na kinenzi kama vile
Socrates Plato na Anstotle,walipoanza kuingia katika ulimwengu wa nadharia ya
Sanaa. katika uwanja wa nadharia ya fasihi/Sanaa ya Kiswahili kuna mifano mingi
ya wahakiki wa mwanzo waliokuwa na mitazamo sawa naya wanafalsafa hao mfano F.Nkwera
(1970), insha yake ya fasihi
inadhihirisha uaminifu wake wa mawazo ya kidhanifu kwa kudai “fasihi
ni Sanaa ambayo huanzia kwa muumba humfikia mtu katika vipengele mbalimbali -ni
hekima ambayo mtu ameshirikishwa apate kumtambua muumba wake”.Nkwera ameungwa mkono na
wahakiki wengine ambao wanasisitiza mtazamo huu kwa kusema “Mtengenezo ya Sanaa huonekana
kuwa ni shughuli ya kiungu yenyekumwiga Mungu ambaye ndiye msanii wa kwanza”
John Ramadhani pia katika makala yake ya fasihi ya Kiswahili
anasisitiza kuwa.“Zaidi ya kwamba fasihi ni hisia vile vile kitengo cha mtu cha kubaini
kazi ya Sanaa ni uigaji wa Mungu ambaye ndiye mfalme wa Sanaa zote”.Mawazo
haya ya akina Nkwera,John Ramadhani na wengine yamejaa mwangwi tu wa mawazo yaliyochakaa ambayo
yalikwisha kutajwa na kushughulikiwa na
wahakiki wa zamani tuliowataja kwa msimamo huu wa kidhanifu,Sanaa au fasihi
havijifinyangwi kwa jitihada za akili za mikono ya mtu bali
hupokelewa kutoka katika mikono mbayo mtu hana uwezo wa kuiona.
Udhaifu, mtazamo huu umepotosha maana halisi kwa kuchanganya Imani
na taaluma,pia unajaribu kumtenganisha msanii na jamii yake kwani unatoa
nadharia inayomwinua msanii na kufanya aonekane kuwa mtu wa ajabu aliyekaribu na Mungu kuliko watu
wengine wa kawaida.
2.
Mtazamo wa kiyakinifu
Kulingana na mtazamo huu Chanzo cha fasihi ni sawa na chanzo cha binadamu wenyewe yaani Binadamu
na mazingira yake ndio Alfa na Omega ya fasihi.Iwe kwa kuumbwa au mabadiliko
kuanzia chembe hai ambayo imepitia maendeleo kadha ya makuzi hata kufikia mtu
binadamu alioanishwa na kazi ili kuyabadili mazingira yake.Katika harakati zake
za kujiendeleza kiuchumi kila mara alijaribu hiki na kile alichokiona kinafaa
alikiendeleza Zaidi na kukidumisha katika hali hii hadithi(ngano),methali,vitendawili,nyimbo,tenzi(mashairi)
n.k vyote hivyo vilitungwa na kusimuliwa kwa madhumuni ya kufunza,kukosoa,kuadhibu,kuchokoza fikra
na kuliwaza jamii baada ya kazi.
Sanaa hii ilirithishwa toka kizazi hadi kizazi kwa njia ya
masimulizi na binadamu alivyozidi kujiendeleza kisayansi na kiteknolojia
akahifadhi taaluma hii katika maandishi.Ndiyo sababu tunasema chanzo cha fasihi
ni sawa na chanzo cha binadamu mwenyewe na jinsi binadamu alivyozidi na
atakavyozidi ndiyo taaluma hii ilivyokuwa na kuendelea.
3. Fasihi inatokana na sihiri,Istilahi Sihiri’ ina maana ya Uwezo au nguvu ya
kimiujiza inayotumiwa na watu kusababisha matokeo fulani.Watalaam hawa wanadai kuwa chimbuko la fasihi ni haja ya mwanadamu
kukabiliana na kujaribu kuyathibiti
mazingira yake. Haja hiyo haikutimilika ipasavyo katika hatua zake za mwanzo za maendeleo ya mwanadamu kwani uwezo wa
kisayansi na kiteknolojia wa mwanadamu wa wakati huo bado ulikuwa kiwango cha
chini sana.Hivyo Imani au miujiza ilichukua nafasi ya sayansi na ugunduzi.Fasihi
ilichimbuka kama chombo cha sihiri hivyo
katika kujaribu kuyashinda mazingira,Mfano Wawindaji walichora picha ya mnyama
waliyetaka kumuwinda kabla ya kwenda kuwinda,kisha walichoma mkuki au mshale kwa
kuamini kuwa kitendo hicho kitatokea kuwa kweli watakapo kwenda kuwinda. Nyimbo
walizoimba wakati wa kufanya sihiri hiyo ndiyo fasihi ya mwanzo.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inachangnya dhima na chimbuko kwani kutumika kwa
nyimbo au ushairi katika sihiri hakuthibitishi kuwa sihiri ndiyo chimbuko lake.Sihiri
ni amali moja tu kati ya amali nyingi za wanadamu wa mwanzo zilizotumia
ushairi.
4. Nadharia ya Mwigo,Wataalam wa nadharia wanadai kuwa
Fasihi imetokana na mwigo(Uigaji),Katika nadharia hii inaeleza kuwa mwanadamu alianza
kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile yaliyomzunguka.Hivyo sanaa za mwanzo mara
nyingi zilijaribu kusawiri vitu vilivyomo katika mazingira ,mfano wanyama,ndege,miti,watu.Nadharia
hii ni kale,ilianzisha na wataalamu wa kiyunani
na walioieneza zaidi ni Plato
(Republic) na Aristotle (Poetics) Plato anahusisha mwigo na dhana ya
uungu.Anaeleza kuwa Maumbile na vilivyomo ni mwigo tu wa sanaa ya kiungu.Sanaa
ya Mwanadamu (Hususani ushairi) ambayo huiga tu mambo hayo yaliyomo katika maumbile haiwezi kuwa na ukweli au uhalisi wa kuwa inaiga maumbile ambayo na
yenyewe yanaiga kazi ya Mungu.Hivyo
alishauri aina fulani za ushairi zipigwe marufuku kwa sababu zinapotosha
ukweli.
Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inasisitiza mno uigaji na kusahau
suala la ubunifu katika sanaa na fasihi.Kama wasanii wangeig maisha na
mazingira tu,sanaa yao ingepwaya sana na haingekuwa tofauti na picha ya
fotografia au maelezo ya matendo ya mazingira na matendo ya kila siku ya
mwanadamu.
FASIHI NI SANAA.
Sanaa ni uzuri unajitokeza katika umbo lililosanifiwa umbo
ambalo mtu hulitumia kuelezea hisia zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au
vielelezo vyenye maana maalumu.
Aina za Sanaa
Ø Sanaa za Uonyeshi,ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza
katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake
kuonyeshwa wakati wowote. mfano uchoraji, uchongaji, kutarizi, ufinyanzi, n.k.
Sanaa ambazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotarizwa,
vyungu n.k.
Ø Sanaa za Ghibu,ni sanaa ambazo uzuri wake
haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia mfano ushairi,
uimbaji, upgaji muziki, n.k. Uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
Ø Sanaa za Vitendo,ni sanaa ambazo uzuri wake umo katika
umbo la vitendo. Uzuri wa sanaa hizi umo
katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo
vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa (mtendaji) na
mtazamaji(Hadhira) wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja, ama sivyo sanaa
haikamiliki. Hali hii ndiyo inayosababisha sanaa hizi za vitendo kuita sanaa
za maonyesho kwa sababu lazima wakati zinapototendeka awepo mtu wa
kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.
SIFA ZA SANAA ZA
MAONESHO
-
Dhana
ya kutendeka (tendo)
-
Mtendaji
(fanani)
-
Uwanja
wa kutendea/jukwaa maalumu
-
Watazamaji
(hadhira).
Hivyo sanaa za maonyesho ni dhana zilizo kwenye umbo
linalotendeka na ili dhana hii itendeke
inahitaji mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huhitaji uwanja wa kutendea hiyo
dhana, na wakati akiitenda hiyo dhana wanakuwepo watazamaji.
Tanzu za Sanaa za Maonyesho
1)Tambiko, ni sadaka inayotolewa kwa miungu au mahoka, mizimu,
pepo, n.k. wakati wa kusalia
miungu.Matambiko yalikuwa na umuhimu mkubwa katika jamii za babu zetu kuliko
siku hizi. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo yaliyowashinda kama vile magonjwa,
ukame, au kukosa mtoto, n.k. walifanya tambiko na kusali ili miungu yao
iwasaidie. Wakati fulani walifanya matambiko kwa ajili ya kuomba radhi au kutoa
heshima na shukrani.
Mara nyingi matambiko haya huandamana na kafara kama sadaka
inayotolewa na jamii kwa wahenga wao. Kafara inaweza kuwa ya kuku, kondoo,
ng’ombe, mbuzi au chakula. Katika jamii nyingi za Kiafrika kabla ya ukoloni
walitoa kafara ya binadamu.
Fani katika tambiko
Ø Sanaa
Katika tambiko sanaa inayotendeka ni ule ufundi wa kutenda vitendo
kwa ukamilifu kwa kutambika kwa kutumia ufundi wa aina fulani.
Ø Wahusika
Wahusika wa tambiko ni wale wazee maarufu walioteuliwa na
jamii kuendesha shughuli hizi za matambiko. Si watu wote katika jamii huhusika.
Ø Mazingira (Mahali)
Tambiko linaweza kufanyika porini, makaburini, njia panda,
kwenye mti mkubwa au mahali popote kutegemeana na aina ya tambiko lenyewe.
Umuhimu wa Tambiko
ü Hujenga imani kama chombo cha
kutatulia matatizo ya jamii. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo ilifanya
tambiko na kusali ili miungu iwasaidie kuondokana na tatizo hilo.
ü Tambiko husaidia kuendeleza mila na
desturi za jamii.
ü Tambiko hujenga na kuimarisha
mahusiano miongoni mwa wanajamii.
ü Matambiko huiongoza jamii katika
mapambano dhidi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Hasara za Tambiko
ü Hujenga dhana potofu katika jamii
kwani watu huamini nguvu fulani bila kuwa na uhakika au uthibitisho wa
kisayansi.
ü Huleta hasara kubwa kwa jamii kwani
kafara ya tambiko inahitaji mnyama au chakula, ambapo watu hutumia hela nyingi kuvipata
vitu hivyo.
2) Mivigha,ni sherehe zinazofanywa na jamii katika kipindi
maalumu cha mwaka. Mivigha hufanywa kwa
lengo la kufundisha jambo fulani maalumu kwa maisha ya jamii. Sanaa za
maonyesho katika kundi hili zinahusu kuingizwa kwa mwanajamii kwenye kundi la
watu wa aina fulani kutoka kundi la watu wa aina nyingine. Mfano jando na
unyago, harusi, kutawazwa chifu, n.k.Katika jando na unyago mtu hutoka kundi la
watoto kuingia kundi la watu wazima, mtu aliyeoa anatoka kundi la makapera
kwenda kundi la waliooa au kutawazwa chifu, mtu anatoka kundi la raia na
kuingia kundi la watawala n.k.
Kutoka kundi moja kuingia kundi jingine ni hatua iliyopewa
umuhimu mkubwa katika jamii ya asili. Umuhimu huu uliambatana na madaraka mapya
yaliyo mkabili mwanajamii kuingia katika kundi jipya. Kila kundi la watu
lilikuwa na madaraka fulani mbayo kutekelezwa kwake ndiko kulikoleta maendeleo
ya jamii .
Fani katika
Mivigha
Ø Sanaa
Sanaa katika mivigha ni ule ufundi wa kutenda kikamlifu na
kiufundi katika kudhihirisha yale yanayotendeka.
Ø Wahusika,Katika mivigha wahusika ni wa aina
tatu:
a)Mtendaji/watendaji,ni wale wote wanaoshiriki kutenda ile dhana ya kuwatoa
watu kutoka kundi moja na kuwaingiza katika kundi lingine. Vitendo hivyo
huambatana na nyimbo, michezo mbalimbali n.k.
b)Watazamaji ,ni wale wanaoingia kutoka kundi moja na kwenda kundi lingine.
Hawa ndio watazamaji, kwa sababu maneno, nyimbo, vitendo, ngoma, n.k. vyote
vinafanyika ili wao wavione na wajifunze na baadae watekeleze yale
waliyojifunza.
c)Waangaliaji, ni wale wanaoangalia mambo yanayotendeka bila wao kushiriki
katika kucheza au kuimba au kutoa mafunzo, wanaangalia tu. Hawa kwa upande wa
sanaa za maonyesho sio watazamaji kwa sababu yale yafanywayo hayawasilishwi
kwao. Wakiwepo au wasiwepo bado vitendo vinatendeka tu bila maana yake kupotea.
Hawa wanaitwa “waangaliaji”
d)Mahali /Mandhari,kwa upande wa mivigha uwanja wa kutendea ni mahali sherehe
zinapofanyika. Inaweza ikawa ndani ya nyumba, au porini, kwenye uwanja wa nje
ya nyumba,milimani au mapanngoni, n.k.
Umuhimu wa mivigha
ü Mivigha hufundisha umuhimu wa kazi
kama vile kilimo, uwindaji, uhunzi, ufinyanzi, ushonaji, n.k.
ü Mivigha huhimiza umuhimu wa ujasiri
katika maisha.
ü Mivigha hufundisha suala zima la unyumba na malezi
kwa ujumla mfano umuhimu wa uzazi na
malezi bora.
ü Mivigha husisitiza umuhimu wa umoja
na ushirikiano katika jamii.
Hasara za Mivigha
ü Hugharimu pesa nyingi sana ambapo
huwaacha wenye sherehe kwenye madeni makubwa.
ü Sherehe huweza kusababisha ugomvi,
chuki, dharau, tamaa, n.k.
ü Huleta ushindani na matokeo yake
husababisha baadhi ya watu wasio na uwezo hujiingiza katika wizi, utapeli,
ujambazi, n.k.
3. Majigambo, ni masimulizi ya kujigamba kwa mtu
kuhusu mambo ya kishujaa aliyopata kuyatenda maishani mwake. Majigambo hayo
husimuliwa katika lugha ya kishairi na masimulizi yake huambatanishwa na
vitendo vya mjigambaji mwenyewe.
Mtambaji anapotamba katika sanaa hii, kwa kawaida huwa na
tabia ya kujivuna au kujitapa kuwa yeye ni bora kuliko wengine wote.Wakati wa
utambaji mazingira humtawala fanani. Pengine fanani alikuwa akitamba kuonyesha
utukufu wake kwa mfalme wao. Au alikuwa akitamba wakati wa kujiandaa kwenda
vitani.
Fani katika Majigambo
Ø Sanaa
Sanaa katika majigambo ni ule ufundi anaoutenda mjigambaji,
kwa kujigamba kwa ufundi huku akionyesha vitendo waziwazi alivyopata kuvitenda
maishani mwake.
Ø Wahusika
Hapa
kuna mtendaji na watazamaji
· Mtendaji ,ni yule anayejigamba mbele ya
wenzake, yaani Yule anayejigamba kuhusu mambo yake ya kishujaa aliyoyatenda
maishani mwake.
· Watazamaji,ni wale
wanaotazama vitendo vinavyotendwa na mtendaji.
Ø Mahali/Jukwaa maalum
Uwanja
wa kutendea ni mahali popote ambapo majigambo yanaweza kufanyikia. Hapa inaweza
kuwa kwenye uwanja mkubwa ambapo sherehe hizo zinafanyikia au kwenye ukumbi.
Ø Matumizi ya Ngoma katika Majigambo
Majigambo vile vile yaliambatana na ngoma, wakati mwingine
ngoma zilichezwa na katikati ya ngoma mjigambaji mmoja alijitokeza na kuanza
kujigamba, alipomaliza alirudi kucheza ngoma na mwingine alijitokeza tena
Umuhimu wa Majigambo
ü Hudumisha utu wa mwanaume katika
jamii.
ü Hudumisha ari ya kuwa wakakamavu,
shujaa na jasiri katika jamii.
ü Huburudisha jamii yaani mtendaji na
wasikilizaji.
Hasara za Majigambo
ü Hukuza na kuendeleza ubinafsi kwani
fanani huonekana ni bora zaidi kuliko watu wengine.
ü Mkusanyiko wa hadhira hutumia pesa au
vyakula kwa wingi, hivyo husababisha umasikini .
ü Majigambo husababisha unafiki kwa
sababu fanani huonyesha mafanikio yake tu na sehemu alizoshindwa hagusii
kabisa, kitu ambacho si cha kweli katika maisha ya mwanadamu.
4.Michezo ya Watoto
Ni mchezo mbalimbali inayochezwa na watoto, na michezo hiyo
hufungamana na hali ya utamaduni, uchumi na siasa ya jamii inayohusika. Mchezo
hii husaidia watoto waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii
yao. Kwa njia hii watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji kama vile
kilimo, kupika chakula, kuwinda, n.k. Vile vile hucheza mchezo wa baba na mama.
Hapa mtoto mmoja anakuwa mama, mwingine baba na wengine watoto. Mchezo huu
huakisi mambo halisi ya nyumbani.
Fani katika Michezo ya Watoto
Ø Sanaa
Sanaa katika michezo ya watoto wadogo ni ule ufundi wa
kutenda vitendo kikamilifu na kuonyesha ujuzi mkubwa katika utendaji huo
Ø Wahusika
Kuna watendaji na watazamaji. Watendaji ni watoto wenyewe
wanaocheza michezo hiyo, yaani wavulana na wasichana. Idadi ya watendaji
inategemea aina ya mchezo wenyewe.Watazamaji ni wale wanaotazama mchezo huo.
Hapa wanaweza wakawa watoto wenyewe
ambao hawachezi au jamii inayowazunguka watoto hao.
Ø Mahali
Uwanja wa kutendea michezo ya watoto ni sehemu yoyote
itakayochaguliwa na watoto wenyewe kulingana na michezo unaohusika. Kwa mfano,
wanaweza kucheza uwanjani, chini ya mti, barabarani, chumbani, sebuleni, kando
ya nyumba, n.k.
Umuhimu wa Michezo ya Watoto
·
Huwasaidia
watoto wadogo kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia
hii watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, utamaduni na siasa
ya jamii yao.
·
Huwasaidia
watoto kujifunza kuwa na ujasiri, ushujaa, udadisi wa mbinu mbalimbali za
kupambana na matatizo yanayojitokeza katika jamii.
·
Hurithisha amali za jamii toka kizazi kimoja
hadi kizazi kingine. Michezo hii hurithisha mila na desturi za jamii fulani kwa
kucheza michezo hiyo.
·
Michezo
hiyo huburudisha watoto. Katika kucheza michezo hiyo, watoto huburudika na
kustarehe.
·
Huwasaidia
watoto huimarisha viungo vya mwili kwa watoto wanaocheza michezo hiyo.
Hasara za Michezo ya Watoto Wadogo
·
Watoto
huweza kuumizana kutokana na michezo hii.
·
Ikiwa
wazazi wa watoto hawa wana tabia chafu kama ile ya kugombana, kutukanana ovyo,
vivyo hivyo watoto hawa watarithi tabia chafu kutoka kwa wazazi wao na wanaweza
kuwaambukiza wenzao.
5. Utani, Ni hali ya kufanyiana mizaha pasipo
kuogopa na kushtakiana au utani ni uhusiano wa kutaniana au kufanyiana masihara
ambao ni tofauti na desturi za kutokuheshimiana. Madhumuni yake makubwa ni
kupunguza na kuondoa kabisa uhasama na chuki iliyokuwepo baina ya makundi
fulani ya watu.
Fani katika Utani
Ø Sanaa
Sanaa katika utani ni ule ufundi na
uwezo wa kutaniana baina ya wahusika wanaohusika na utani huo.
Ø Wahusika
Katika utani, washiriki wanaweza kuwa
mtu na mtu, familia na familia, kabila na kabila, ukoo na ukoo au nchi na nchi.
Ø Mahali
Uwanja wa kutendea inaweza kuwa mahali popote ambapo utani
unaweza kufanyika. Inaweza ikawa kwenye harusi, msibani, kwenye pombe wakati
watu wanakunywa, n.k.
Umuhimu wa Utani
·
Kutoa
maadili na mafunzo fulani kwa jamii.
·
Kuimarisha
umoja na ushirikiano miongoni mwa wanajamii (kujenga undugu)
·
Kuhimiza
ujasiri na juhudi katika maisha.
·
Kuhimiza
upendo katika maisha.
·
Hukuza
na kuimarisha mila na desturi za jamii.
Hasara za Utani
·
Husababisha
ugomvi katika jamii.
·
Huleta
hasara za kuchukuliana vitu bila malipo.
·
Huvunja
au kuvunjiana heshima miongoni mwa wahusika.
Muziki
|
Ufumaji
|
Utarizi
|
Uchoraji
|
Fasihi
|
SANAA
|
Ufinyanzi
|
Uchongaji
|
Maonyesho
|
Ususi
|
Kila kipengele cha Sanaa kinatofautiana na kingine kwa umbo na matumizi. Fasihi ni
kipengele cha Sanaa kinachotumia maneno kuumba huo uzuri wa kisanaa.
TOFAUTI KATI YA FASIHI NA TANZU NYINGINE ZA SANAA
1.
Lugha ,
kazi zote za kifasihi zinaundwa kisanaa kwa kutumia lugha inayotumika au
kuandikika. Lugha hiyo hubeba maana Fulani (ujumbe) kwa jamii Fulani.Hivyo
lugha ndiyo inayotufautisha fasihi na Sanaa nyingine. Kwa mfano, uchoraji
kipengele chake muhimu kalamu, rangi na kipande cha nguo au karatasi. Ufinyanzi
lugha yake ni udongo , uchongaji wa vinyago lugha yake ni gogo la mti n.k.
Fasihi si maelezo ya kawaida kawaida kama vile matangazo, taarifa ya habari au
barua, fasihi ni maelezo yenye mguso kisanaa. Kazi za kifasihi, huumbwa
kimafumbo hutumia nahau au misemo , methali, tamathali za semi, taswira na
ishara mbali mbali. Kazi za fasihi hufikirisha mtu huweza kutumia akili ili
aweze kugundua kazi ya kifasihi aliyosoma au kuisikia kuwa ina maana gani.
2.
Wahusika,kazi
yeyote ya fasihi inakuwa na wahusika wake ambao matukio mbali mbali yanayohusu
jamii huwazungukia wahusika ni watu ama viumbe, waliokusudiwa wawakilishe tabia
za watu katika kazi za fasihi. Kwa upande mwingine wahusika ni muhimu sana
katika kutoa na kufikisha dhamira kwa hadira iliyokusudiwa na mwandishi.
3.
Mandhari,
kazi ya fasihi inakuwa na mandhri ambayo huonyesha tukio linaponyika. Mandhari
hiyo inaweza kuwa ya kubuni au ya kweli.Mandhari husaidia kujenga hisia
inayokusudiwa na mwandishi.
4 . Utendaji, utendaji hasa katika
fasihi simulizi hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati mmoja. Vile vile
utendaji humfanya fanani aweze kuonyesha baadhi yamatendo katika usimulizi
wake.
5 Fani na maudhui,kazi za
fasihi zina sehemu mbili yaani fani na maudhui na sehemu hizi zinafungamana.
Maudhui ni kile kinachosemwa na fani ni namna kinavyosemwa. Kazi nyingine za
Sanaa vile vile zinafanikisha ujumbe kwa hadhira lakini mbinu na vifaa
vinavyotumika ni sehemu ya fasihi. Kwa ujumla kazi za kifasihi, fani na maudhui
yake ni ya hali ya juu sana ukilinganisha
na Sanaa nyinginezo.
KWA VIPI FASIHI NI SANAA ?
Usanaa wa fasihi hujitokeza
katikavipengele mbali mbali kama ifuatavyo:-
1.
Mtindo,
Sanaa katika fasihi hujidhihirisha katika namna kueleza jamii (mtindo) katika
kueleza jambo kunakuwa na aina fulani ya kiufundi ambao mwanafasihi huutumia
katika kufikisha ujumbe kwa jamii yake. Taarifa inayotolewa inaweza kufichwa
katika fumbo, shairi, kitendawili, tamthiliya au hadithi.
2.
Muundo (mpangilio maalumu wa matukio),katika kazi ya fasihi, matukio
yanapangwa kiufundi ili yaweze kuwasilishwa vizuri kwa jamii husika. Matukio
hayapangwi ovyo ovyo tu bali yanakuwa na mpangilio maalumu.
3.
Utenzi mzuri wa lugha iliyojaa nahau, misemo, methali, tamathali za semi,taswira na ishara mbali mbali
unaonyesha wazi usanaa wa fasihi. Lugha itumikayo katika fasihi ni ya kisanaa.
Ni lugha iliyopambwa na inayokusudiwa kuibua hisia za namna Fulani kwa hadhira
yake. Lugha hiyo inaweza kuchekesha, kukejeli, kubeza, kuchokoza, kutia hamasa
au kushawishi. Matumizi ya lugha yako ya aina tofauti, kuna tamathali za semi,
misemo, nahau, methali. Lugha ya wahusika hasa lahaja zao, uchaguzi wa
msamiati,ufundi wa kutoa maelezo hasa ya wahusika ya mandhari na matukio,
uteuzi wa lugha yenyewe itumiwayo.
4.
Uundaji wa wahusika, wahusika huwa na tabia zinazotofautiana kati yao. Wanaundwa
kiufundi sana na msanii anaweza kuamua anataka wahusika wanaowakilisha tabia na
matendo fulani tu katika jamii na kwa hiyo atawaumba wahusika hao ili
kukamilisha nia na lengo lake.Katika kutofautisha tabia na hali za wahusika,
mwandishi analazimika kutumia mbinu ya kuwapa majina wahusika wake. Wahusika
wanaweza kuumbwa kinafsi au kiakili na kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii
mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani na nje au anaweza kuonyesha mabadiliko
yake kila anapokutana na mazingira tofauti.
5.
Ujengaji mzuri wa Mandhari, fasihi hujengwa katika mazingira maalum. Mandhari husaidia
sana kujenga hisia inayokusudiwa na mwandishi. Mandhari yanajengwa kiufundi na
mwandishi ili yasaidie katika kujenga kazi nzima ya fasihi.
FASIHI KAMA CHOMBO CHA UKOMBOZI
Ukombozi ni harakati za jamii yoyote zenye lengo la kuitoa
jamii hiyo kwa nguvu (kwa silaha) au kwa mazungumzo kutoka katika makucha ya
watumwa kisiasa,kiuchumi,kimawazo na kiutamaduni.Jamii inaweza kuwa ni ya
kitumwa kisiasa ikiwa haitakuwa na fursa ya kushika hatamu ya uongozi wao na
badala yake ikategemea uongozi kutoka kwa jamii nyingine jamii itaitwa ya
kitumwa ,kiuchumi,ikiwa haitakuwa na haki ya kuendesha njia mbalimbali za
uzalishaji mali.Pia jamii isiyoweza kufikiri na kuamua wala kutokuthamini
mawazo yake yenyewe na badala yake ikawa katika mgawanyiko wa ibada na itikadi
za kigeni ni jamii isiyo huru kimawazo vile vile jamii haitakuwa huru
kiutamaduni ikiwa itakosa kuthamini uaminifu,uumbaji na ugunduzi wake yenyewe
badala yake ikasujudu amali zilizo na chimbuko kutoka nje.Nyanja za ukombozi wa
jinsi fasihi ya Kiswahili ilivyozitazama mpaka leo
(a)Kisiasa
Ukombozi wa kisiasa unapatikanaje?
Unapatikana tu baada ya kupigania uhuru wa bendera kuwa ndio
wa kwanza kupatikana kwa nchi ambayo iko katika harakati za kujikomboa.Katika
maandishi ya mengi fasihi ukweli huu unajitokeza kwa mfano katika utenzi wa uhuru
wa kenya msanii anatuonyesha
juu ya vita vya kumng’oa mkoloni kutoka katika kiti cha uongozi kwanza
baada ya mwafrika kupandisha bendera yake mambo mengine yafuate vilevile katika
utenzi wa uhuru wa Tanganyika na utenzi wa jamhuri ya
Tanzania “mwandishi anasisitiza uhuru wa bendera ukielezwa kuwa kabla ya
ukombozi wa aina nyingine kufuata.
Kwa hiyo ukombozi huu wa mwanzo (uhuru wa bendera) husababisha
uhuru wa kisiasa wanchi kisha uhuru wa kisiasa huwa ni jukwaa la ukombozi wa
uchumi na mambo mengine,vitabu vingine vinavyozungumzia ukombozi wa kisiasa ni mzalendo,F.E.MK
Senkero) Ubeberu Utashindwa(J.K Kiimbila),Tone la Mwisho(E.Mbogo),Kinjikitile
na Mashetani(E.Hussein),Nuru mpya(R.Rufeshobya)
(b)Kiuchumi
Uhuru wa bendera ni sehemu ya mwanzo tu wa ukombozi wa jamii
nchi zinaweza kujidai ni huru kumbe uchumi wake bado ungali mikononi mwa nchi
nyingine.Nchi nyingi zinazoendelea bado ziko katika harakati hii ya kutaka
kujikomboa kiuchumi.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili wamezungumzia sana suala la uchumi katika mfano ‘’Mashairi ya Azimio la
Arusha’’ mwandishi anaonyesha na kushambulia unyonyaji ambao ni adui wa
uhuru wetu.
Vilevile waandishi wanasisitiza kufanya kazi kama njia ya
kuimarisha uchumi.Pia wameeleza kuwa unyonyaji unaweza kukomeshwa kwa
kutaifisha njia zote za uzalishaji mali na kuwa mikononi mwa umma. Pia Katika
tamthiliya ya “Bwana Mkubwa” (J.P Mbonde) mwandishi ameonesha
kuwa kwa sasa shabaha yetu sisi ni kupigana na ukoloni mambo leo ili kupata
uhuru kamili.Ukoloni mambo leo ni kikwazo cha ukombozi wa kiuchumi. Kwa sababu
ya ulegevu wa uhuru wa kisiasa nchi inaweza kuwa na mali lakini ikizembea kufanya kweli ipasavyo
yaweza kufanyiwa njama na ukoloni ndio maana upo umuhimu wa bidii katika kazi
na uzalishaji wa mali kisha linafuata swala la ulinzi wa mali hiyo.
Kuzikomboa njia za uzalishaji mali hakutoshi kwani kila hila
zao zisizoisha wakoloni wanaweza wakatupora mali hiyo tunapaswa kuwa
macho.Katika utenzi wa “Zindiko la ujamaa” mwandishi anaeleza
utaifishaji wa njia kuu za uchumi na uhalali wa utaifishaji huo. Mwandishi
anaonyesha kuwa utaifishaji huo ulifanywa si kwa kuwaona wakoloni kuwa wanadhuluma
bali kama njia moja wapo ambayo itaongeza kwenye ukombozi wa kiuchumi katika
jamii. Lengo moja ni kufuta ubinafsi ambao unapelekea tofauti za kitabaka na
badala yake manufaa ya umma kwa ujumla.
Ukombozi wa kiuchumi si utaifishaji wa njia za uzalishaji
mali tu na wala si kukomesha ukabaila na ubepari bali ni kuongeza juhudi katika
kazi mbali mbali ili kuongeza kiasi cha pato la kitaifa. Waandishi wengine
wanazungumzia ukombozi wa kiuchumi ni kama vile, “Nuru mpya” (G. R. Ruteshubya)
“Mashetani” (E. Hussein) “Sauti ya dhiki” (A. Abdallah) “Kasri ya mwinyi fuad”
(Shafi Adam Shoji) Zetu bora mkulima na wasifu wa sili binti saad(S. Robert).
C) Kimawazo
Ukombozi wa kimawazo ni uhuru wa mtu katika upeo wa
fikra pasipo kutegemea mtu mwingine. Hapa mtu aliye huru awe anajiamini
mwenyewe na awe mtu kama watu wengine. Awe mwenye uwezo wa kuwaza, kuamua na
kutenda, kuchanganua na kupanga kama watu wengine. Mtu aliye mtumwa wa kimawazo
anaweza kufananishwa na mnyama wa kufugwa. Mnyama wa kufugwa daima ni mtumwa na
bwana wake wakati wote huongojea amri kutoka kwa bwana wake.
Maandishi ya fasihi yanazungumziakwa upana swala hili
la uhuru wa mawazo . Katika riwaya ya “Njozi za usiku” dhana hii ya utumwa wa
kimawazo ipo ndani ya watu wengi ambao wanashikilia hasa baada ya maajilio ya
elimu iliyokuja pamoja na ukoloni na ikatumika kwa upotofu. Katika riwaya hii
msanii anaonyesha kuwa wale waliosoma walidharau kazi zote za mikono,
walifikiri kuwa kazi za mikono zinafaa kwa wale ambao hawakusoma. Wao wanafikiri
kuwa kazi ya mtu aliyesoma ni kushika kalamu na kuandika tu au kuwasimamia
ambao hawakusoma.Tangu uhuru wa Tanzania kumekuwa na harakati za kufutilia mbal
ukanganyifu wa namna hii katika mawazo ya watu. Mawazo ya namna hii ndio
yamekuwa yakiwafanya watu wengi wa hali ya chini waamini kuwa uchumi walionao
wamepewa na Mungu.
Vile vile kimawazo watu waliamini kwamba kila jambo
lilitokana na watawala wa kizungu lilikuwa ni bora kabisa. Kwa mfano hata
majina yliletwa toka Ulaya nay a kwetu
ya asili kuachwa. Haya yanajadiliwa wazi katika tamthiliya ya “Bwana mkubwa”
(J. P. Mbonde)
Katika ukombozi wa kimawazo kuna swala la ukombozi wa
mwanamke na swala la dini.Katika suala la ukombozi wa mwanamke watu wengi
wanalitazama kirahisi jambo hili. Wengi wanadhani kuwa mwanamke hana haki ya kujibagua
kutoka kwa wanaume na kujipigania haki yake. Watu hawa hawaelewi ni mapinduzi
gani ambayo hawa wanapigania.Katika fasihi ya Kiswahili Shaban Robert amewatetea
wanawake katika kazi zake mbali mbali ikiemo Diwani ya”Wasifu wa siti binti saad” na siku
ya watenzi wote. Shaban Robert amemtazama mwanamke kama mtu
anayestahili utu kama watu wengine
wowote wale.
Katika kitabu cha “Wasifu wa Siti binti Saad” msanii au
mwandishi anaeleza wazi jinsi jamii ilivyomfanya mwanamke kama chombo cha
kutunzwa utawani ili kiwe kizuri kipate kuwavutia wanaokitafuta na baada ya
kutoka utawani kikawa mikononi mwa mwanaume kikamtegemea kwa hiyo mwanamke
alikuwa ni mtu aliyechukuliwa kama hana wajibu wowote wa maana Zaidi ya kuwa
mtegemeaji. Lakini Shabn Robert aliona kuwa ( uk 23) “Ukimdumisha mtu leo utamuona juu
ya kilele cha utukufu kesho.
Mawazo ya mwandishi ni kwamba wanawake ni vyema watazamwe
katika hali zao za maisha katika ubaya na uzuri kama wanaume. Kuhusu suala la
dini linajitokeza katika riwaya ya “Kichwa maji” ambapo mwandishi anaona
dini imeanzishwa na waoga ambao hutawaliwa na milango yao ya fahamu badalaya
kutawaliwa na akili au bongo zao.
Jambo muhimu katika kumkomboa mtu kimawazo ni kwamba ikiwa
dini itaendelea kuwepo isiwe na mtazamo duni na finyu na athari zake ambazo alikuja
nazo mkoloni akidai kuwa tamaduni zetu ni za kishenzi. Sharti elimu ndiyo iwe
ya kutafakari na kugeuza mfumo wa maisha ya jamii.
Katika dini pia kuna madhehebu mbali mbali ambayo kati yao
kuna uhasama mkubwa, muislamu anadai kuwa yeye ni bora Zaidi kuliko mkristo na
mkristo anajiona yeye ni bora kuliko muislamu. Madhehebu yote haya yamechimbuka
huko mashariki ya kati…….katika kitabu cha “Bwana mkubwa” (uk 18-19”)……kwanini
basi mlitutenganisha katika vikundi vidogo vya madhehebu tofauti kati ya
wakristo na waislamu iwapo Mungu ni yule yule mmoja leo mnatueleza tuombe
kuungana, utengano alianzisha nani? na kwa faida ya nani?........mbona babu
zetu walimwabudu Mungu wao toka zamani kabla ya ujio wa wazungu.
Kwa ujumla dini imechangia kwa kiasi kikubwa sana katika
kudumisha mtu kimawazo na kumfanya atumie fahamu tu kwa hiyo katika kumkomboa
mtu kimawazo sharti suala la dini litupiwe jicho kali fasihi inazidi kuona
jicho lake.
(d)Kiutamaduni.
Kwa ujumla utamaduni wanchi zilizotawaliwa na ukoloni
umeathiriwa sana na ukoloni huo watu wa nchi hizo wanazipoteza kidogo kidogo
thamani za utamaduni zao.Katika fasihi ya Kiswahili ukweli huu wa mambo yameoneshwa
katika kitabu cha “Njozi za Usiku” mwandishi
wa riwaya hii ameelezea namna vijana wote hasa waliosoma hawataki kabisa kusikia
kuhusu mila na desturi zao (uk 51).Hadi leo vijana wengi wakiwa kwao (vijijini)
na ikatokea kwamba kuna ngoma za kienyeji zinachezwa wao husimama mbali au
kando wakitazama kwa dharau mambo yanayotendeka mbele yao.Wanaamini kabisa kuwa
ngoma hizo ni za kishenzi ngoma ambazo zinafaa kuchezwa na watu wasiosoma watu
wasio staarabika.
Katika riwaya ya “Kichwa maji” mwandishi ameonesha
jinsi isivyo kawaida kwa msomi au watu
wenye cheo serikalini kucheza ngoma za kienyeji lakini vijana hao hao mwanzoni
wasomi wenye mwazo ya kisiasa wakisikia sehemu fulani kuna mziki au disko
watajitahidi sana ili wasikose kufika huko.Kwa sasa kuna mtindo mwingine wa
kupaka madawa ya kujichubua ngozi waonekane weupe na wengine huvaa nywele za
bandia au maiti ili kuficha nywele zao za kipilipili.Huu wote ni utumwa wa
kimawazo kwa upande fulani watu hawa wanaamini kuwa uzungu ndilo shina la
maarifa, watu hawa hawajui kwamba kuna wazungu wengine ni maskini zaidi hata
kuliko sisi wenyewe.Hivyo ili tujikomboe katika nyanja hizi ni lazima tuondoe
ubinafsi, uroho wa madaraka na ulevi wa madaraka hapa nchini.
KAZI ZA FASIHI KATIKA MIFUMO MBALIMBALI
Kwa kuwa mwanadamu ni alfa na Omega wa Fasihi ni dhahiri kuwa
maendeleo yake yanahusiana na maendeleo ya fasihi.Hata hivyo sio kila maendeleo
huwa na mafanikio mazuri na hivyo si kila fasihi inatoa mawazo mema.Fasihi kama
zao la jamii huenda sambamba na maendeleo
ya jamii yanayotokana na kazi na
fasihi hujitokeza katika Nyanja zote za kimaendeleo ziwe za kisiasa,kiuchumi,na
kiutamaduni.Safari ndefu ya kimaendeleo imo katika mifumo mitano (5) ya
uzalishaji mali.Mifumo hiyo ni kama ifuatayo:
Fasihi katika mfumo wa Ujima
Huu ni mfumo wa mwanzo
kabisa wa maisha ya binadamu.Fasihi ya kipindi hiki ilikuwa fasihi ya
uzalishaji mali.Mfumo wa ujima haukuwa na matabaka ya watu hivyo fasihi ya
wakati huo ilijishughulisha na manufaa na maslahi ya watu wote Katika
jamii.Katika mfumo huu fasihi na sanaa ni vitu vilivyokuwa vimefungamana na
mahitaji ya kukidhi haja ya lazima ya watu. Fasihi katika kipindi hiki ililea
amali za jamii ambazo zilikuwa ni KAZI
na USAWA yaani Fasihi ililinganishwa na kazi.Hata hivyo kutokana na uduni wa
uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia,Fasihi ya wakati huo iliilea jamii katika
jamii katika kutawaliwa na nguvu za jamii na mazingira.Katika kipindi hiki
fasihi haikuwa kitu cha anasa.Mazingira ya wakati huo yalikuwa ya kiuhasama
sana,hayakuruhusu kuwepo na anasa ya aina yeyote ile.Kutokana na mazingira hayo
Fasihi ilizuka kuwa silaha mojawapo ya mapambano hayo.
Fasihi
katika mfumo wa Utumwa,
Mfumo huu ulitawaliwa na utabaka ambapo kulikuwa na
mabwana na watumwa wao.Mfumo huu uliruhusu baadhi ya watu kuishi kwa jasho la
wengine.Watu hao waliishi maisha ya anasa kutokana na ziada ya mali iliyozalishwa
na watumwa wao.Katika mfumo huu uzalishaji mali umewekwa migongoni mwa watu wa
tabaka la chini la watwana.Katika shughuli za kisanaa,mfano upande wa ushairi
,watu wa matabaka ya mabwana waliwekewa
watwana na kuwaburudisha kwa
kuwaimbia nyimbo na mashairi.Fasihi nyingi zilikuwa zaile za kuwatukuza
mabwana;zinazotukuza utumwa.Fasihi nyingi za wakati huu zilitumiwa ili
kuendeleza itikadi za kibwana.
Pia kulikuwa na
fasihi inayopinga mfumo huu wa kinyonyaji.Watumwa wanaotumiwa kuwa vyombo vya kuzalisha
mali,wanatunga visa,hadithi,mashairi na nyimbo za kupinga mfumo wa kitumwa.Mara
nyingi mabwana wenye watumwa iliwabidi
wawasake na kuwatenganisha watumwa wenye historian a lugha moja iliyowaruhusu
kutunga fasihi ya pamoja iliyelea hoja na hisi zao za kupinga unyonywaji huo.
Kugunduliwa kwa maandishi kulileta sura mpya kwa
upande wa fasihi ya wakati huo.Uandishi ulikuwa kwa watu wa tabaka la mabwana
tu;nao ulielekezwa katika kutoa kazi za fasihi zinazotetea maslahi ya tabaka
hilo.Kutokana na ugunduzi wa maandishi watunzi walianza mfano kukaa na kupanga
juu ya vina na mizani katika ushairi.Kalam na karatasi zilitumika keneza
mitazamo na itikadi za kibwana.Falsafa na mitazamo ya kiulimwengu wakati huo
ilielekezwa huko katika kuulinda na kuuhalalisha mfumo wa kitumwa.Kwa
mfano,mwanafalsafa Aristotle,katika falsafa zake,alisisitiza na kuhalalisha
utumwa kwa kueleza kuwa kuwa ilikuwa amri ya MUNGU kwamba watu wengine wawe
watumwa na wengine wawe mabwana.
Hatimaye mfumo huu wa kitumwa ulianza kutetereka kwa
mikinzano mbalimbali.Biashara ambayo hustawi sana katika hatua za mwanzo za
mfumo huu zilianza kufilisika .Wakati huo huo watumwa hujizatiti na kupinga
vikali sana utumwa wao.Watu ambao hapo awali walikuwa na mali zao chache kama
vile mashamba na ambazo walinyang’anywa na mabwana wenye watumwa,nao waliungana
pamoja na watumwa katika harakati za kuupinga utumwa.
Katika hatua hii ya kukata roho kwa mfumo huu wa
kitumwa ,ulitumika kama chombo kimojawapo cha kiitikadi cha kupinga mfumo
huo.Tanzu mbali mbali za fasihi kama vile hadithi,ushairi,nyimbo n.k
zilielekezwa katika harakati hizo.
Fasihi
katika mfumo wa kikabaila (Kimwinyi)
Ni mfumo ambao uhusiano wa kitabaka unakuwa kiwango cha juu kabisa.Tabaka tawala
la makabaila linamiliki njia zote za uzalishaji mali yaani kiuchumi na
kiutamaduni.Njia za kiuchumi hutawaliwa
kwa mbinu mbalimbali za kukodisha
mashamba.Mfano aliyekodishwa anapangiwa kutoa fungu kuba sana kwa mwenye shamba
wakati wa mavuno.Mtwana wa wakati huu hutofautiani sana na mtumwa wa kipindi
cha mfumo utumwa.Fasihi ya wakati huu anatawaliwa na falsafa zinazojaribu
kuhalalisha uhusiano huo wa wenye mashamba na njia nyingine za uzalishaji mali
na wale wasio na chochote isipokuwa jasho lao.Fasihi ya kipindi cha ukabaila
iliweka msisitizo kuusu mapambo yasiyo na maana;msisitizo ambao unaathiri kazi
ya fasihi pia.Mfano katika utenzi wa Al-Inkishafi(1810)
mwandishi anasema;
37. Nyumba
zao mbake zikinawiri,
Kwa taa
za kowa na za sufuri,
Masiku
yakele kama nahari,
Haiba na
jaha iwazingiye.
38.
Wapambiye sini ya kuteuwa,
Na kula kikombe kinakishiwa,
Kati watiziye kuzi za kowa,
Katika mapambo yanawirije.
Katika
utenzi huu,Sayyid Abdallah A.Nassir anatuusia kuhusu maisha na ametumia lugha
ya picha ya maisha ya uozo wa wafalme wa Pate kama kielelezo cha uzuri usio na
kifani wa maisha ya hapa duniani.Halafu anaonyesha jinsi ambavyo maisha haya
anayoyaona kuwa uzuri mwingi yanamalizikia katika kaburi ambako miili ya hao
wafalme inakuwa chakula kikubwa cha funza.Uozo wa maisha ya mamwinyi wa
pate umeibua Fani na Maudhui ya Al-inkishafi
(1810)
Pia katika Utendi wa mwanakupona (1962) mwandishi
anamuusia binti yake kuwa ajikubali kuwa pambo mbele ya mume wake.Anasema;
38. Na kowa na kuisinga,
Na nyee zako kufunga,
Na asmini kutunga,
Na firashini kutia
39 Nawe ipambe libasi
Ukae kama arusi,
Maguu tia kugesi,
N mikononi makoa.
41.
Pete sikose za ndani,
Hina sikome nyaani,
Wanda sitoe matoni,
Na inshini kuitia
Katika utendi huu mwandishi anamuasa mwanamke aweke na
kuelekeza akili yote kwenye kujipamba ambapo kwa kufanya hivi kumemfanya
mwanamke abaki katik nafasi duni sana katika jamii;nafasi ya chini ya
kuonekana,kujiona na kujikubali kuwa pambo la kuufurahisha moyo na jicho pamoja
na uchu wa mwanamume.
Pia mfumo huu
unamdanganya akubali kumtumikia na kumtii mume wake bila kumbishia wala kumjibu
kwa lolote lile atakalosema.Mwanamke anaaswa kwamba amtii na amuogope mume
wake;
28. Keti naye kwa adabu,
Usimtie ghadhabu,
Akinena simjibu,
Itahidi kunyamaa,
36. Mpumbaze apumbae,
Amriye sikatae,
Maovu kieta yeye,
Mungu atakulipa.
Katika ubeti wa
36 wa utenzi huu inaonyesha wazi kuwa dini ilitumika kama taasisi kubwa ya
kudumisha na kuhalalisha unyonyaji na mgawanyiko wa jamii katika matabaka ya
watu.Katika utenzi huu,binti anausiwa kuwa afuate yote anayoambiwa na
anayoamriwa na mume wake kwani yote ni
amri ya MUNGU.Hapa tunagundua athari za kitabaka zilizojikita katika dini na
mafundisho yake.Athari hizo zinazidi kumdidimiza na kumkandamiza zaidi na kumfanya mtu duni
sana.
Katika mfumo
huu maisha huwa ya kibiashara na yaliyozingwa na imani kubwa juu ya
pesa.Pesa zinaanza kuabudiwa katika
mfumo huu,nazo hujitokeza katika nyuso
mbalimbali za rundo la utajiri wa makabaila.Katika utenzi wa sundiata jambo
hili linajitokeza waziwazi mwandishi anaelezea kuhusu utajiri wa wafalme kama
vile Mansa Mussa.Mfumo huu wa kikabaila haukuendelea kuwapo muda wote.
Mikinzano ambayo daima huwapo baina ya wanyonyaji na wanyonywaji ,pamoja na
nguvu za vibwanyenye uchwara ambao walikwishaumbika katika harakati za
kitabaka.Upande mmoja wa harakati hizo
walikuwepa wakulima wanyonywaji pamoja
na vibwanyenye ambao daima wamekuwa wakijitahidi kuangusha mfumo huu wa
kikabaila ili badala yake wakite mizizi ya kibepari.Nguvu zote hizi za kiuchumi
na kisiasa hatimaye kuuangusha mfumo wa
kikabaila.
Katika kipindi
hiki pia fasihi ilikuwa chombo kilichosaidia kuendeleza harakati za kuuangusha
mfumo wa kikabaila wakati makabaila waliitumia fasihi kueneza na kuendeleza
itikati zao za kikabaila,papohapo wanyonywaji nao pia walitunga fasihi yao
inayoeleza hisia zao,taabu zao na umuhimu wa kujikomboa.Kwa wakulima fasihi yao
ilikuwa ndiyo silaha ya kifasihi na kwa vibepari uchwara piawalikuwa na fasihi
yao ya kupinga ukabaila na kutetea umuhimu wa kuwa na mfumo mpya wa maisha
yaani mfumo wa kibepari.Mfano wa fasihi ya Kiswahili ya wakati huo ni kama
vile; Utenzi wa fumo liyongo (1913)
ambap awali utenzi huu ulielezwa kwa njia yam domo tu.Kwa watu wa tabaka la
chini waliosimulia kisa hiki cha liyongo kilionekana kuwa cha kusifu ushujaa wa
mtu huyo lakini papo hapo liyongo alikuwa mtetezi na mpenda watu wanyonge.
Fasihi
katika mfumo wa kibepari
Fasihi ni zao la jamii na hufungamana na mfumo wa
maisha ya jamii na pia ulifungamana n mapambano ya kudumu dhidi ya mazingira
,yaani kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.Katika mapambano hayo dhidi ya mazingira
kulikuwa na mitazamo tofauti ya fasihi.Pia fasihi ilionekana kuwa ni silaha
mojawapo kati ya silaha nyingi zilizotumiwa na tabaka moja kutetea maslahi yake
kwenye mapambano ya kudumu ya kitabaka katika jamii
Katika ubepari kuna matabaka mawili ya watu yaani
wenye mali wanaoshikilia rasilimali zote na wanyonge wasio na kitu.Fasihi ya
kibepari ilielezea uzuri wa fedha kwa sababu pesa iliabudiwa sana katika mfumo
huu.Waanii wa kipindi hiki ni wale walionuia kupata pesa,wasanii hawa walivaa
uso wa udanganyifu huku tegemeo lao kubwa ni gunia la fedha,unyang’anyi na
umalaya.Mfumo hu umefanikiwa kuwatenga waandishi na jamii zao.Wengi wametunga
kazi zao za fasihi ambazo maudhui yake,dhamira na lengo lake pamoja na
fani kama vile Mzimu wa watu wa kale
(1958),Kisima cha giningi (1958),Siri ya sufuri (1974),Duniani kuna watu
(1973),Mwana wa Yungi hulewa (1976), na Kosa la Bwana Msa (1984) zaidi
wasanii hawa walishighulikia suala la kusisimua msomaji na kumpumbaza kwa visa
vya upelelezi.Fasihi ya kibepari iliifumba macho jamii isiione machungu yanayoisakama jamii.Fasihi hii huwafumba
macho watu (jamii) ili wasione udanganyifu ulioshamiri katika jamii
hiyo.Huwaficha wagandamizaji na kuwapa nguvu za kumiliki jamii kisiasa
,kiuchumi,na kiutamaduni ili kuendeleza matabaka yanayo wanufaisha wachache.
Fasihi ya
kibepari haikomboi watu kimawazo ili waweze kuchambua na kutambua jamii yao kwa
jicho pevu.Haiwachochei wanaogandamizwa kukataa machungu yanayosababisha na
wagandamizaji wachache.Katika mfumo huu fani huwa kubwa kuliko maudhui
yaliyopatikana humo.Kazi a fasihi iliyo nzuri ni ile ambayo fani na maudhui
huwa katika uwiano ulio sawa.Fani isaidie kuyaweka maudhui katika hali nzuri ya
kueleweka kwa jamii.
Fasihi katika
mfumo wa kijamaa
Mfumo huu huu ulibuniwa na Marx na Angels ambao
walidai kuwa mfumo huu utatetea na kuleta kheri kwa umma.Fasihi ya mfumo huu
itakuwa ya kunufaisha umma na kulinda amali na hali ya jamii.Matunda ya kazi
huwa kwa faida ya wote.Usawa,utu na kuheshimiwa ndiyo msingi wa fasihi ya
kijamaa.Fasihi ya kijamaa ni ya jamii nzima ambapo huiangalia jamii
kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.Huyamulika matatizo ya jamii.Ni chombo cha
kuunganisha,kuadibu,kuhimiza,kuongoza na kushauri jamii katika lake la kufuta
unyonge na uchafu unaoikabili jamii.
Fani na maudhui
katika fasihi ya kijamaa ni vitu ambavyo hufungamana kwa mtazamo wa
jumla.Fasihi lazima iwe wazi ili watu wa ngazi zote waweze kuelewa na
kuzichukua fikra nzuri zilizomo.Uhuru wa kuikosoa na kuichambua jamii ni wazi
kwa fasihi hii,tofauti na fasihi ya kibwenyenye ambayo uhuru huu haupo.Hivyo
basi, fasihi iliyo ya kweli ni ile inayoelewesha umma katika mapambano yake
dhidi ya mazingira,kuikosoa jamii,na kuielekeza jamii katika ukombozi wa
kweli.Fasihi ya dhati ni sharti iendeleze shabaha zilizofikiwa na umma yaani
wakulima na wafanyakazi.
MADA
NDOGO-3; UHURU WA MWANDISHI/MTUNZI WA
KAZI ZA KIFASIHI
Dhana ya uhuru wa mwandishi ni pana sana na inatazamwa kwa
kuangalia vipengele kadhaa kama ifuatavyo:
Mosi,uhuru wa
mwandishi uko katika utashi,Bila utashi mwandishi atakuwa mwoga na mwepesi wa kukata
tamaa.Atayumbishwa haraka kutoka kwenye msingi wa falsafa yake na Imani aliyo
nayo juu ya mabadiliko yatokeayo katika jamii.Makombora ya wahakiki na
wanasiasa huweza kumyumbisha, lakini kwa mwandishi mwenye utashi makombora hayo
humkomaza.
Baadhi ya waandishi walioonyesha utashi wao katika Afrika ni ‘Ole
Soyinka na Ngugi wa Thiongo waandishi hawa wameshambuliwa sana na
wahakiki, lakini misimamo yao ni ile ile, pia wamewahi kufungwa na walipotoka
kifungoni hawakubadili misimamo yao na wamekuwa hivyo kwa sababu ya utashi wa
falsafa zao katika fasihi ya kiswahili, waandishi wenye utashi wapo na msingi
wa kuwepo kwao ni kutoyumbishwa na matamshi ya jukwaani na wahakiki ambao
hawajapevuka.
Pili,uhuru wa mwandishi umo katika kuwa na falsafa moja
inayoeleweka,
Falsafa ifanyayo maandishi ya mwandishi
moja yawe na kitu kijulikanacho kama lengo.Waandishi waliotajwa hapo juu yaani Ole
Sanyika na Ngugi wa Thiongo ndio wanaongoza kuwa na falsafa zao
zinazojulikana. Katika fasihi ya Kiswahili tunaona waandishi wachache wenye
falsafa zao inayojulikana wengi tulio nao wanaandika kufuatana na jambo fulani
au tukio la wakati huo bila kulinganisha leo ataandika juu ya mapenzi, kesho
juu ya upelelezi na kesho kutwa mapinduzi mwishowe anakuwa na orodha ndefu ya
vitabu visivyokuwa na lengo.Waandishi wachache tulio nao ambao wameelekea kuwa
na falsafa inayoongoza maandishi yao ni kama Shaban Robert, G.Kezilahabi na
Mohamedi Suleiman.Bila kuwa na falsafa maalumu ni rahisi sana mwandishi kuyumbishwa.
Tatu,uhuru wa mwandishi umo katika kuitawala vema Sanaa yake,kama unaandika riwaya na hujui
misingi ya Sanaa ya aina hiyo atajikuta katika kikwazo,utajikuta uhuru wa
kisanaa unaweza kujaribu, lakini kazi utakayoitoa itakuwa hafifu.Kazi nzuri ya
kisanaa ni ile inayounganisha vema ubunifu na uhalisia.Mwandishi akielemea sana
katika ubunifu anazua matatizo mengine kazi ngumu aliyonayo mwandishi ni katika
kupata barabara msitari huo.Mwandishi mwenye vitabu vingi anaweza kuwa na
kitabu kimoja tu kilichoupatia vema mstari huo. Katika fasihi ya Kiswahili
waandishi walioupatia msitari huo tunao ni kama vile Ebraim Hussein,Penina
Mhando,Mohamed Suleiman, C.G Mng’ong’o na J.A.Safari.Msanii anayeweza
kuitawala vema Sanaa yake anaunganisha
vizuri Sanaa na maudhui yake.
Mwisho, uhuru wa mwandishi umo katika lugha anayotumia,ili msanii
atawale vema Sanaa yake nilazima ajue lugha anayotumia.Lugha ndicho kiungo maalumu kati ya
Sanaa na kazi ya kifasihi mwandishi kama hajui vema lugha anayotumia atajikuta
hana uhuru wa kukisema anachotaka kwa hiyo lugha ndiyo nguzo ya nne katika
uhuru wa mwandishi, waandishi wa Kiswahili
waliokwisha kutajwa wanakitawala Kiswahili sanifu,Kiswahili sanifu ndiyo
msingi wa fasihi ya Kiswahili.
Ni kweli kuna uhuru wa mwandishi?
Uhuru wa mwandishi ni nini?
Ni ile hali ya mwandishi wa fasihi kuwa huru na wazi
katika kutoa mawazo au hisia zake kwa jamii.Ni uhuru wa kuandika na kulikosoa
tabaka lolote katika jamii bila kupata matatizo yoyote.
Mwandisihi ni nani?
Ni mtu yoyote atumiaye muda wake mwingi kuandika na kuzungumzia jamii yake kwa njia
ya maandishi.
Je kuna uhuru wa mwandishi?
Kwa ujumla uhuru wa mwandishi ni uhuru ikiwa hakufaulu
kudhuru tabaka tawala hii ni kwa sababu suala la uhuru wa mwandishi ni la
kitabaka na lilianza pale jamii ilipogawanyika katika matabaka kwa maana hii
uhuru wa mwandishi unaamuliwa na tabaka tawala
Kuanzia enzi za utumwa, maandishi ya liyovumbuliwa katika fasihi andishi ya mwanzo ilikuwa ya wateule
wachache tu na wenye vyeo vyao.Hao mabwana, wamwinyi na mabepari walihakikisha
kila mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa maandishi ili kuendeleza na kulinda
utawala wao.
Naye B.Goya (1974-78) anasema kuwa mwandishi hana uhuru
kwa vyovyote vile kwa sababu yeye ni tokeo la jamii Fulani, kila jamii ina
mipaka yake ambayo mtu hatakiwi kukiuka kwa vyovyote vile mwandishi huyu
amebanwa na mipaka hiyo asivuke.Pindi avukapo mipaka hiyo atapambana na jamii
hiyo (tabaka tawala) vitabu vya mwandishi huyo vitapigwa marufuku au vitabu
vikitolewa havitanunuliwa au serikali itavikusanya na kuvifanyia mipango
mwingine. Katika Afrika kuna mifano
mingi ya udhibiti wa waandishi mfano mzuri ni mwandishi maarufu wa Kenya Ngugi
wa Thiongo ambaye kazi zake hasa ya “Ngaahika Ndeenda”(I will marry
when I want)- Nitaolewa Nitakapotaka, ilimgombanisha na vyombo vya dola
hadi akawekwa kizuizini, Ngugi ni mwandishi wa kwanza kufichua siri za mfumo wa
kibepari kwa watu wanyonge aliliuzi tabaka tawala la jamii yake ambalo
halikusita kutumia udhibiti na vyombo vyake vya Mabavu.
Baada ya uhuru vitabu vingi sana viliandikwa kwa kudhibitisha
maandishi mbalimbali uliojitokeza waziwazi E.Kazilabi aliandika riwaya “Rosa
mistika”(1971),kitabu hiki kilipigwa marufuku kisitumike mashuleni na
wala kisiuzwe waziwazi madukani.Ilidaiwa na waliokipiga marufuku kuwa kilikiuka
maadili ya jamii kwa kueleza mambo ya aibu kwa wazi.Sura ya kumi ndiyo hasa
ilitolewa mfano wa uchafu wa kitabu hiki.Udhibiti huo ulifanywa na Wizara ya
Elimu na ulizusha maswali mengi kwa wasomaji.Wasomaji walianza kujiuliza, Je si
kweli uchafu uelezwao katika “Rosa mistika” umo ndani ya jamii ya
Tanzania? Je upotofu na uongozi mbaya ulifuchuliwa na riwaya hiyo hii si upo
kati yetu? Kwa baadhi ya wasomaji ilielekea kuwa suala la uchafu wa maelezo
yatokeayo kitandani baina ya wakuu wa chuo na wanafunzi wao lilitumika kama
kisingizio tu cha kudhibiti ukweli wa masuala mengine nyeti yaliyowagusa
viongozi yaliyowakilishwa na watu kama vile Bwana Maendeleo Deogratius
anayeshiriki katika kuwaharibu vijana.
Vitabu vingine ambavyo havieleweki vinasema nini, maudhui,
falsafa na ujumbe wa mwandishi ni mashetani(E.Hussein) “Aliyeonja
Pepo”(F.Topan) na “Ayubu” Paukwa theatre Association.Na hivi viko kwa
kukwepa mkono mrefu wa tabaka tawala.
DHIMA YA UHURU WA MWANDISHI.
· Mwandishi atakuwa huru kuikosoa jamii au tabaka lolote litakaloenda
kinyume na utaratibu wa jamii bila matatizo.Mwandishi atakuwa huru
kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili unaofanywa katika jamii na tabaka lolote
bila matatizo yoyote.
· Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka
pamoja na utashi wake.Hii itamfanya mwandishi awe na msimamo
unaoeleweka.Msimamo wake utamsaidia
kuifundisha na kuielimisha jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na
ataonesha jamii njia za kufikia haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga
· Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo
katika jamii kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa
na kuonewa na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa
tabaka ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.
· Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii huacha tabia
ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii makasuku huandika
mambo bila kufikiri na kurudiarudia
mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa majukwaani bila fikra mpya kwa
hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na uhuru wa mwandishi wa kutosha hali
hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi ataandika mambo mbalimbali
yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au kujipendekeza kwa tabaka
tawala lenye mamlaka yote katika jamii.
· Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi
fasihi inakuwa chombo cha kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na
kifikra (kimawazo). katika jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na
hutumia fasihi kutetea na kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii
nzima inatumiwa na jamii hiyo katika kuwakomboa wanajamii wote.
· Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi,
mwandishi anakuwa huru kuichokoza na kuisukasuka (kuichochea)
jamii
bila matatizo yeyote. Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na
wafanyakazi kufikiri ili waweze kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na
kutoa hadharani uozo uliopo katika kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na
kunyanyaswa na tabaka tawala
· Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na
kuishauri jamii katika mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila
woga.Mwandishi ataishauri jamii kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na
ichague mambo gani yanafaa kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa
huru kuirekebisha jamii bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni
mabovu yanayotendeka katika jamii
MADA NDOGO-4;MASUALA YA KIITIKADI NA DHANA YA UDHAMINI
KATIKA KAZI ZA FASIHI
Maana ya Itikadi
Itikadi ni Imani ya watu au jamii fulani juu ya kitu fulani.
Itikadi kisiasa ni mfumo wa mawazo na Imani ambao umewekwa na tabaka tawala/
tawaliwa au tabaka lolote lenye nguvu katika jamii inayohusika ikiwa na lengo
la kulinda, kutetea na kuendekeza matakwa na maslahi yake. Utaratibu huo
unaambatana na umilikaji wa njia kuu za uchumi na umilikaji wa mapato ya ziada
yatokanayo na jasho la wazalishaji mali hizo, nyenzo za kitaaluma kama vile
elimu ni nyenzo zisaidia kuimarisha itikadi kama vile dini vinatumika kutetea
utaratibu uliowekwa na tabaka tawala.
Kimsingi kuna mitazamo miwili ya
kiitikadi:-
i)
Itikadi
inayotetea na kulinda maslahi ya watu wchache tu katika jamii (utumwa, ukabaila
na ubepari)
ii)
Itikadi
inayotetea na kulinda maslahi na matakwa ya watu wengi katika jamii (ujima na
ukomunisti).
Vile
vile tunapojadili juu ya itikadi katika fasihi na usemi kwa ujumla pia
tunaongelea juu ya utabaka uliopo katika jamii inayohusika . Kuna matabaka ya
aina mbili:-
a) Tabaka tawala
b) Tabaka tawaliwa
·
Tabaka
tawala linamiliki vyombo vya dola na kwa kutumia vyombo hivyo na kwa kutumia
waandishi, tabaka tawala linaunda, linaendeleza na kutetea maslahi yake.Vile
vile tabaka tawala lina nguvu za kiakili na za kielimu kwa manufaa yao.
Mwandishi kwa ujumla hawezi kuepukana na mfumo huo wa kitabaka. Tabaka fulani
huwadhamini waandishi kwa njia mbali mbali.
UDHAMINI
Ni hali ya watu au shirika fulani kutoa fedha kwa ajili ya
kugharamia kitu fulani . Mdhamini au wadhamini ni kundi la watu wenye shabaha
zinazofanana wenye kusimama kama ufadhili wa mradi fulani. Katika fasihi hawa
ni wale wanaosimamia makundi maalumu kipropaganda na kiitikadi.
AINA ZA UDHAMINI
Kuna udhamini wa aina
mbili:-
i)
Udhamini
wa ushawishi
ii)
Udamini
wa nguvu
Ø UDHAMINI WA USHAWISHI
Ni aina ya udhamini ambao mdhamini huwashawishi na kuwanunua waandishi
au wasanii. Matokeo yake ni kwamba msanii anafungwa na matakwa ya mdhamini.
Ø UDHAMINI WA NGUVU
Huu ni udhamini unaotumia vyombo vya dola kama vile jeshi,
polisi, magereza kumdhamini mtunzi au mwandishi n.k.Hakuna hiari katika
udhamini wa nguvu, kila kitu kinaendeshwa kama vile mashine tu. Kwa ujumla
mwandishi akidhaminiwa kwa nguvu za serikali huwa kama kasuku aimbaye na
kuutukuza mfumo wa maisha uliopo katika jamii hata kama roho na moyo wake viko
mbali sana na mfumo huo. Lakini msanii anapodhaminiwa kutetea umma, lazima
kutakuwa na madhara yake katika jamii yake inayohusika.
Mwandishi wa fasihi katika kila nchi atakuwa na udhamini
unaolingana na mazingira yake kwa mfano katika nchi ya Tanzania, mwandishi
anaweza kuandika kwa udhamini wa jamii yake inayohusika.Mdhamini anaweza kuwa mtu
binafsi mwenye fedha, shirika, chombo cha serikali, chama fulani au kundi la
mataifa kwa ushirikiano. Pia mdhamini ni mwakilishi wa wenye mamlaka juu yake,
kwa mfano katika serikali yaTanzania chuo kikuu ni mwakilishi wa serikali na
serikali ni mwakilishi wa tabaka tawala. Hivyo msanii anayedhaminiwa na chuo
kikuu ambacho ni chombo cha serikali hatimaye anajikuta anafanya kazi ili kuendeleza
maslahi ya tabaka tawala.
SABABU ZA UDHAMINI
Ø Uhaba wa fedha kwa waandishi za
kuendeshea shughuli zao za uandishi katika uandishi wa kazi za fasihi. Pesa
zinahitajika kwa ajili ya kununulia karatasi, kalamu, uchapaji n.k.
Ø Kulinda na kutetea maslahi
yawadhamini wao. Hii inatokea zaidi kama mdhamini ni wa tabaka tawala. Kama
tabaka linalo tawala ni la mabepari kazi za fasihi zitatetea tabaka hilo.
Ø Kujulikana au kuipendekeza. Baadhi ya
waandishi hudhaminiwa kwasababu ya kutakakujulikaa na kwa upande mwingine
mdhamini anawadhamini waandishi kwa lengo hilo.
Ø Kupata fedha za haraka. Hawa huandika
vitabu vyenye kujaa wahusika wakuu, mafundi wa kufanya mahaba, kutumia madawa
ya kulevya na kufanya mapenzi kwa kutumia mipira ya kiume na kike bila kujali
staha utamaduni wa jamii yake. Mwandishi anachojali hapa ni pesa na sio matakwa
ya jamii yake.
Ø Kulazimishwa na tabaka tawala.
Waandishi hawa wanakubali udhamini huo kwa kuogopa udhabiti wa kazi zao na
tabaka tawala. Waandishi hawa wakikataa udhamini huo kazi zao zitadhibitiwa na
kupigwa marufuku zisisomwe au kuchapishwa kabisa.
UMUHIMU
WA UDHAMINI
· Husaidia waandishi chipukizi katika
kuchapisha kazi zao.
· Husaidia waandishi katika kufanya
utafiti wa mambo mbalimbali yatakiwayo katika Sanaa hiyo ya fasihi.
· Husaidia jamii kupata kazi mbali
mbali za kifasihi.
· Husaidia kuleta ushindani wa ubora wa
kazi katika soko la kazi za fasihi.
· Husaidia kuinua vipaji hasa vya
waandishi chipukizi.
ATHARI ZA UDHAMINI
Ø Mwandishi anayedhaminiwa anatakiwa
kuandika yale tu ambayo mdhamini wake anayataka. Msanii hatakuwa na uhuru wa
kuandika kitu chochote na kwa njia anayotaka.
Ø Mapana ya uandishi wake kidata, kigiografia na kimaudhui huamuliwa na
mdhamini na kutegemea
mahitaji yake na kiwango cha fedha alichonacho mdhamini.
Ø Ufafanuzi wa data na maudhui ya kazi ya fasihi lazima ulingane na mtazamo
wa itikadi ya mdhamini.Hii ina maana kuwa mwandishi wa kazi ya fasihi hawezi kufanya ufafanuzi
wa data na maudhui mwenyewe bila kumshirikisha mdhamini.
Ø Matokeo ya uandishi wa kazi za fasihi mara nyingi ni mali ya mdhamini na
hutumia kuendeleza
maslahi yake mabayo sio lazima yalingane na malengo ya mwandishi.
Ø Wasanii au waandishi wengi kutokana na kudhaminiwa huanza kuandika kazi
zao kwa kupenda pesa
hii huwafanya waandishi kuwa makasuku kwasababu ya kuandika yale tu yasemwayo
na mdhamini wake bila kuyafanyia uchambuzi wa kina.
Ø Udhamini hukuza utabaka katika jamii, hapa tunakuwa na tabaka la wenye nacho (mdhamini) na
tabaka la wasionacho (msanii) mdhamini humnyonya msanii.
Ø Kuzuka kwa fasihi pendwa (riwaya ya pendwa).Hapa waandishi huandika kazi zao kwa
lengo la kupata pesa za haraka, huandika riwaya pendwa ambazo zina soko kubwa
hapa nchini hasa kwa vijana na wakati huo huo riwaya hizo hazifunzi lolote
jamii Zaidi ya kuburudisha.
Ø Huchochea rushwa, hii ni kwa sababu waandishi wengi wanataka udhamini huo na matokeo yake
wale wanapata udhamini huo lazima watoe chochote (rushwa) kwa mdhamini.
No comments:
Post a Comment