UHAKIKI
WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
TAMTHILIYA
YA KILIO CHETU
MTUNZI:
MEDICAL AID FOUNDATION
WACHAPISHAJI:
TPH
CHAPA
YA 1: 1996
UTANGULIZI
KILIO CHETU ni
tamthiliya inayojaribu kuvunja ukimya uliotawala miongoni mwa wanajamiii katika
kutatua matatizo mbali mbali yanayotokana na mahusiano ya kijinsia,matatizo
ambayo yasipopata ufumbuzi thabiti yanaweza kuliangamiza taifa.
MAUDHUI : DHAMIRA
(i). ELIMU YA
JINSIA
Hii ni dhamira
ambayo imetawala katika tamthiliya hii ambapo
wazazi na walezi wengi inaonesha wako tayari kuvunja ukimya uliopo kati
yao na watoto wao na kuzungumza waziwazi juu ya mahusiano ya kijinsia.Baba na
Mama Anna na mjomba wahusika hawa wamejitoa mhanga ili kuwanusuru watoto
wanaoathirika na ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa sababu ya kukosa elimu.
Baba na mama
Anna wanapeana majukumu ya kuongea na watoto (baba na watoto wa kiume na mama
na watoto wakike) kama uk 10 unavyoeleza. “Baba Anna:hili ndilo nimefaulu mwenzenu Nimekwambia,Mama
Anna akae na mabinti zake”.Kwa upande mwingine kuna wazazi na walezi
ambao wanaamini kuwa kuwaeleza watoto ni kuvunja mila na desturi pia ni
kuwafundisha umalaya.Mama Suzi na baba Joti wanawasilisha kundi hili wao
wanaamini kuwa viboko na vitisho ndio njia sahihi ya kuwafunza watoto tabia
njema.
Matokeo
ya misimamo yote miwili imeonekana bayana kwenye tamthiliya hii ambapo,watoto
waliopata elimu mfano Anna wanajieleza na wana majibu sahihi
kuhusu mahusiano ya jinsia na wale wasio na elimu mfano Joti na Suzi
wanapata maradhi mfano Joti alipata Ugonjwa wa UKIMWI na Suzi anapata
mimba.kutokana na hali hii elimu ya jinsia ni jambo muhimu sana kwa maisha ya
jamii ya sasa,kuendeleza mila kuna liangamiza taifa letu
(ii) MAPENZI
KATIKA UMRI MDOGO
Mwandishi
ameonyesha jinsi vijana wanavyoshiriki mapenzi katika umri mdogo,jambo hili ni
hatari katika maisha yao.Matokeo ya jambo hili ni kupata mimba za utotoni na maambukizi
ya virusi vya UKIMWI.Msanii amewatumia wahusika Joti na Suzi kama waathirika na
mapenzi katika umri mdogo.Aidha ameonyesha pia tabia ya vijana wadogo kushiriki
ngono na watu waliowazidi umri,hali hii pia inazidi kuwaingiza kwenye hatari ya
kupata magonjwa.Joti ana mahusiano ya kimapenzi na chausiku (mtu mzima)ambae
pia ana mpenzi wake mpemba(uk 23)
Suala
la mapenzi katika umri mdogo (kujamiiana) linachangiwa na kuzagaa kwa picha za
X na picha za utupu zilizozagaa mitaani(kwenye magazeti,mitandao nk).Vijana na
watoto wengi hupenda kuangalia vitu hivyo na kujikuta wakishawishika kufanya
ngono .
(iii)MALEZI
Suala la malezi
limezungumziwa katika mitazamo tofauti tofauti ambapo kuna wanaoamini kuwa
malezi ya watoto ni kuwapiga viboko na kuwatisha,mwandishi amewatumia mama Suzi
na baba Joti ambao wanaamini kuwa viboko vinaweza kuwaadabisha watoto wao,
matokeo ya mtazamo huu ni watoto kuwa na nidhamu ya woga na kushindwa
kuyakabiri majaribu mfano Suzi anashindwa kumkatalia Joti kufanya ngono na
matokeo yake anapata mimba
Aidha kuna
wazazi ambao wanaamini malezi bora kwa watoto ni kuwaelimisha na kuwapa mifano
halisi ya maisha badala ya kuwatisha,Mjomba,baba na mama Anna wanaamini mfano
huu.Anna ameelimishwa na kuelimika hakuna anayemdanganya mfano anamweleza
Mwarami kuwa kwa sasa wanatakiwa kuzingatia masomo na si vinginevyo.
Aidha anamweleza
Mwarami madhara ya ngono katika umri mdogo pia ni pamoja na kupata magonjwa
kama kaswende,kisonono na UKIMWI hivyo wasiogope mimba tu kama
walivyodanganyana wao kwa kupeana vidonge vya kuzuia mimba .
Hivyo
suala la malezi litazamwe kama jukumu la jamii nzima na kila mwanajamii aone
kuwa ana wajibu wa kushiriki malezi.
(IV) UKIMWI NA TIBA YAKE
Mpaka sasa
hakuna tiba kamili ya UKIMWI ambayo imethibitishwa kinachotolewa mpaka sasa ni
dawa za kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI pamoja na magonjwa nyemelezi
(ARV).Dawa hizi hutolewa kwenye vituo vya afya vilivyoidhinishwa na serikali au
mamlaka husika.Pamoja na hayo kumekuwapo na matangazo kadha wa kadha kwenye
magazeti, runinga au mabango yanayoeleza kuwepo kwa watu wanaodai kutibu
UKIMWI, ukweli utabaki kuwa hakuna tiba kama mwandishi alivyoeleza (uk 34),
ugonjwa huu hauna tiba ushahidi upo wazi kwani kadri tunavyoona watu walioupata
ugonjwa huu, tunajua ukweli kwa hiyo matangazo yanayotolewa mengi hulenga
kutuongezea matatizo na pengine kuleta uhasama miongoni mwetu.
(V) NAFASI YA
MWANAMKE
katika jamii
zetu za kiafrika mwanamke hutazamwa katika sura tofauti mathalani katika
tamthiliya hii mwanamke ameonyeshwa katika sura tofautin kama ifuatavyo;
Mosi,malaya,mtazamo huu
umethihirishwa na chausiku ambaye licha ya kuhusiana kimapenzi na joti alikuwa
na mpenzi mwingine. (mpemba muuza duka).Suzi naye licha ya kuwa mwanafunzi wa
shule ya msingi alijihusisha na uzinzi.
Pili,Mnyonge hana sauti,mwanamke pia ameonyeshwa kama
mtu duni na asiyefaa,asiye na sauti ya kutetea haki zake zote.Mfano mama joti
baada ya kubaini mume wake kutokuwa mwaminifu anashindwa kumuuliza badala yake
ananunua khanga kuwasema wabaya wake.
Tatu,Mlezi
wa familia,mwandishi
ameonyesha kuwa mwanamke ni mtu muhimu sana katika malezi mfano,mama suzi yuko
mstari wa mbele kumlea mwanawe suzi na kuhakikisha anafuata njia njema impasayo
mtoto mwema. Mama Anna naye ameonyesha kumlea vema bintiye Anna na kumwezesha
ashinde vishawishi toka kwenye jamii inayomzunguka.
Nne,Mwenye
msimamo thabiti,mwanamke
pia ameonekana kuwa mwenye msimamo katika maamuzi yake,Mfano Anna anapotongozwa
na mwarami anajibu kwa ujasiri kuwa wao bado ni wanafunzi wazingatie masomo
anasikika akisema “ya nini kukimbilia suti na nepi hujavaa”.
Tano,mshauri,katika tamthiliya hii mwanamke
ameoneshwa kama mshauri bora,mfano Anna anamshauri suzi kutotoa mimba bali
amueleze mama yake kuhusu swala hilo.
(VI)
MAPENZI NA NDOA
Mwandishi
ameonyesha kutokuwepo kwa uaminifu katika suala la mapenzi na ndoa kwa ujumla.Baba
Joti ameoneshwa kuwa na wanawake wengi.Joti na Chausiku wana wapenzi zaidi ya
mmoja hali inayohatarisha maisha yao hasa kipindi hiki cha ukimwi hivyo
uaminifu ni muhimu sana katika mapenzi.
MIGOGORO
Katika tamthiliya
hii kuna migogoro mbalimbali imejitokeza ambayo ni;
Mosi,mgogoro kati
ya Suzi na mama yake,Chanzo
cha mgogoro huu ni vidonge vya kuzuia mimba kwenye sketi yake ya shule jambo
ambalo mama yake hakiliafiki na suuhisho ni mama suzi kumwadhibu Suzi.
Pili,mgogoro kati ya mama Suzi na mjomba,Chanzo
cha mgogoro huu ni tofauti za mtazamo kuhusu elimu ya jinsia,mama Suzi aliamini
kuwa kumwelimisha Suzi kuhusu mahusiano ya kimapenzi ni kumfundisha
umalaya,mjomba anapingana na hilo kwa kumwambia mama Suzi viboko havisaidii
Tatu,mgogoro
kati ya Joti na Chausiku,Chanzo cha mgogoro huu ni tabia ya Joti kuwa
na wasichana wengi na kutumia vitu vya Chausiku kuwahonga wasichana
wengine,suluhisho ni Chausiku kumkalipia joti.
Nne,mgogoro kati Mwarami na rafiki zake,(Chogo,Joti
na Jumbe) wanamlaumu Mwarami kutochangamka na kuwa na mpenzi wanamwambia kama
hachangamki watamtoa umemba.Kauli hiyo ilimfanya Mwarami amfuate Anna na
kumtaka kimapenzi.
Tano,mgogoro kati ya Anna na Mwarami,Chanzo cha mgogoro huu ni
tofauti za misimamo,Mwarami anataka Anna akubali kufanya ngono,Anna anakataa na
kumweleza kuwa wasome kwanza mambo ya ngono yana muda wake.
UJUMBE
Ø
Si
busara kuchanganya mapenzi na masomo kwani kufanya hivyo huleta madhara(Suzi
alipata mimba ,Joti alipata UKIMWI)
Ø
Elimu
ya jinsia ni haki na stahiki si halali kwa watoto (vijana) kuwanyima elimu hiyo
kwani kufanya hivyo ni kuwaangamiza
Ø
Wazazi
wabadilike kulingana na wakati wasing’ang’anie mila ambazo haziisaidii jamii.
Ø
Elimu
stahiki kuhusu UKIMWI itolewe kwa wanajamii wote ili wasihusishe UKIMWI na
mambo ya kishirikina.
Ø
Wazazi
wavunje ukimya na wao bayana kuhusu mabadiliko ya miili yao ili iwe rahisi
kushinda majaribu mbalimbali
FALSAFA
Mwandishini
anaamini kuwa kuwapa watoto elimu ya jinsia ni kuwafanya wajitambue na
kujielewa barabara na kuepuka madhara ya kujiingiza kwenye ngono katika umri
mdogo.Elimu ndio njia pekee ya kuwaepusha dhidi ya VVU/UKIMWI.
FANI
MUUNDO
Mwandishi wa
tamthilia ya KILIO CHETU ametumia muundo wa moja kwa moja (msago),mchezo unaanza
sehemu ya kwanza ambapo dubwana linaingia kisiwani.
Ø
Sehemu
ya pili na ya tatu tunajulisha kifo cha fausta na Suzi kujihusishwa katika
mapenzi na kukutwa na vidonge vya kuzuia mimba.Na katika sehemu hii mjomba
anawaeleza wazazi wa Suzi na Joti elimu ya jinsia kwa vijana.
Ø Sehemu ya nne watoto
wanajihusisha ngono na wasichana wanaowazidi umri kama Chausiku Aidha mtoto
Anna anaonyesha jinsi alivyopatiwa elimu kuhusu jinsia hivyo kushindwa
vishawishi
Ø Sehemu ya mwisho Suzi
anagundulika kuwa ana ujauzito wa Joti ambaye amedhihirika kuwa ana ugonjwa wa
UKIMWI
MTINDO
Mwandishi
ametumia baadhi ya vipengele vya sanaa za maonyesho ya kiafrika.
Mfano;
Ø
Matumizi ya nyimbo (uk 21 na
25)
Kiongozi; tunaangamia x4
Wote;tunakwishwax2
(wanainuka huku wanaendelea na wimbo)
Ø
Pia
mwandishi anatumia mwanzo na mwisho wa hadithi ambao ni mwanzo wa hadithi za
fasihi simuluzi mfano ‘Paukwa........pakawa
Mtambaji:niendelee nisiendelee
Wote: endelea
Ø
Mwandishi
pia ametumia mtindo wa monolojia pale mtambaji anapotoa maneno ya utangulizi kuhusu
matendo yanayohusika/yanayotokea
Ø Pia kuna matumizi ya dayalojia
yenye maneno machache lakini yaliyopangwa kwa ufundi na ustadi mkubwa .
MATUMIZI
YA LUGHA
Mwandishi
anaonyesha ustadi mkubwa katika matumizi ya lugha inayofanya wasomaji
watafakari kwa makini ametumia lugha nyepesi inayoeleweka kwa walengwa(watu wa
kawaida) ambao ni watoto na wazazi(walezi).Lugha iliyosheheni tamathali za semi
,misemo nahau matumizi ya lugha za kiingereza na lugha ya kiasili(kibantu)na
pia matumizi ya taswira
TAMATHALI ZA SEMI
Tashbiha
·
Walipukutika
kama majani(UK 1)
·
Miti
inayoungua kama mabua(UK 6)
·
Mbona
unakuwa mgumu kama mpingo(uk 5)
·
Unakuwa
nyuma nyuma kama koti
Sitiara
·
Ndio
mwisho wa kumvumilia huyu nguru anaechimba ndoa yangu(uk2)
·
Huyu
kinyago wako anakimbia nini?(uk 20)
Tashihisi
·
Huyu
kinyago anakimbia (uk 20)
TANAKALI ZA SAUTI
·
Wacha
moyo nipute pwi pwi(uk16)
·
Basi
vup nikamdaka(uk 16)
Takriri
·
Pigadomo
,piga domo( uk 16)
·
Watu
watapukutika kama majani ya kiangazi
·
Hodi
hidi mwenye nyumba (uk 13)
Misemo
·
Na
wewe utakuwa nyuma kama koti (uk 4)
·
Mtakatifu
wa usoni (uk 9)
·
Mapenzi
ni tiba (uk 22)
·
Kukimbilia
suti na hali nepi hujavaa (uk 20)
·
Kukausha
(uk 9)
·
Anadunda
(Uk 8)
·
Umekula
wa chuya (Uk 25)
·
Makapera
kibao (Uk 7)
·
Kujikaza
kisabuni (Uk 21)
·
Kushika
hatamu (Uk 22)
Methali
·
Wembamba
wa reli treni inapita (Uk 6)
·
Shukrani
ya punda ni mateke
·
Asiyefundwa
na mamaye hufundwa ulimwengu (Uk 30)
Nahau
·
Kufa
kwa kukanyaga miwaya (Uk 9)
LUGHA YA
KIINGEREZA NA LUGHA YA ASILI
Kwa kiasi kidogo
mwandishi anachanganya lugha ya kiingereza na Kiswahili kutambulisha namna ya
vijana wengi wa siku hizi wanavyoongea kwa kuchanganya lugha. Mfano
JOTI;Ndio
umecome sio?,maneno mengine ni
·
Stori
(uk 16)
·
Umemba(Uk
24)
·
Gest(Uk18)
·
Chips(Uk16)
·
Tuition(Uk
21)
·
Mabuku(Uk1)
Ø
Mwandishi
ametumia lugha ya asili katika wimbo wa maombolezo
·
Kiongozi:Jiti
afitwe sanda salauyax3
·
Wote:Ena,ena,ena
salauya
·
Kiongozi
:umwana afitwe sanda x3
·
Wote
:ena,ena,ena salauyax3
UTEUZI WA TASWIRA
Mwandishi
ametumia taswira la dubwana lililoleta balaa kisiwani (Uk 1)mwandishi anasema
kila aliyegusa wakaharisha mara nywele kunyonyoka na vifo vikafuataHaya ni
maelezo yanayofanya msomaji ajenge woga na kupata picha halisi ya dubwana yaani
UKIMWI
MANDHARI
Mwandishi
ametumia mandhari ya mjini hii imedhihirika pale jirani aliposema ‘mie toka
siku ile niwaone pale shamba sijakaa tena mjini,nilienda zangu shamba kupambana
na nyani wala nafaka’
Pia sinema za x zinadhihirisha
mandhari ya mjini
Jumbe:leo si
ndio picha
Choggo:ndio
tulisahau(Uk 7)
Pia Anna
anapoimba (Uk 20)anasema’ pesa zenu,lifti zenu niache mie’wimbo huo
umedhihirisha mandhari ya mjini kwani lifti kwa wakina dada hasa wanafunzi
zinapatikana mjini kuliko vijijini.
WAHUSIKA
MAMA SUZI
·
Ni
mhusika mkuu msaidizi
·
Mama
yake suzi
·
Ana
msimamo wa kizamani kuwa mzazi hawezi kuongea na mwanae maswala ya kujamiiana
au elimu ya kijinsia haamini kuwa watoto wadogo wanaweza kujihusisha na mapenzi
Mfano Fausta
alikuwa mtoto mdogo wa darasa la tano mambo hayo asingeyajua anaamini kuwa njia
pekee ya kumfunza mtoto ni kumuadhibu
SUZI
·
Ni
mhusika mkuu
·
Ni
mtoto wa mama Suzi,
·
Ni
binti mdogo wa darasa la sita aliyejihusisha kimapenzi na Joti kinyume na
matarajio ya mama yake.
·
Alikutwa
na vidonge vya kuzuia mimba,
·
Hakupatiwa
elimu ya kijinsia na wazazi wake,
·
Anapata
mimba kutokana na wepesi wa kushawishika
BABA JOTI
·
Ni
jirani yake mama Suzi bado ameshikiria ukale kwamba wazazi hawawezi kukaa na
watoto wao kuwaeleza habari za ngono anaamini kuwa dawa pekee ya kuthibiti ni
viboko na mijeledi (Uk 21)sio mwaminifu katika ndoa yake kwani ana mwanamke
mwingine nje ya ndoa
MAMA JOTI
·
Ni
mke wa baba Joti
·
Anaamini
kuwa watoto wangejua makubwa kwa kutumia methali ‘wembamba wa reli treni
inapita (Uk 6).
·
Ndoa
yake matatani kwa kuingiliwa na nyumba ndogo .anafikiri suluhisho la tatizo ni
kununua kanga za mafumbo
MJOMBA
·
Kaka
yake na mama Suzi
·
Ana
uelewa mpana na upeo wa kufahamu mambo ya ulimwengu wa sasa ulivyo hivyo
anashauri watoto wapatiwe elimu ya jinsia hawatajihusisha na mambo ya
kujamiiana mhusika huyu anafaa kuigwa na jamii
BABA ANNA
·
Ni
jirani yake na baba Joti
·
Pia
ana upeo wa kuelewa mambo na anamwambia mkewe
(mama Anna)akae na watoto wao na kuwaelimisha kufamya mapenzi katika umri mdogo.
·
Anaamini
wapo watoto wataelimishwa kamwe hawatajihusisha na kujamiiana
JIRANI
·
Ni
jirani yake na baba Joti,
·
Hana
uhakika na vipimo vya hospitali anashauri Joti apelekwe kwa fundi(waganga wa
jadi) kwa tiba.
·
Anawakilisha
watu wengi ambao hawaamini kuwa kuna UKIMWI na mtu akiupata ni kwamba amerogwa.
·
Hafai
kuigwa katika jamii
ANNA
·
Ni
msichana mdogo ambaye bado ni mwanafunzi amepata elimu ya jinsia na wazazi
wake.
·
Huyu
ana msimamo na maamuzi ya haraka kuhusiana na maswala ya kujamiiana mfano
Uk21......hujui kama kuna madhara mengine....hujui kisonono na mengine kedekede
·
Kutokana
na elimu ya jinsia aliyopewa kuepukana na kushinda vishawishi vingi.
·
Pia
ni mshauri mzuri, alimshauri suzi asitoe mimba kwani ni hatari (uk 20)
·
Anafaa kuigwa katika jamii
JOTI
·
Ni
mwanafunzi wa shule ya msingi anasoma darasa moja na Suzi,
·
Ana
uhusiano wa kimapenzi na wasichana wengi akiwemo Suzi,Chausiku,Yoranda,Gelda na
sikujua ,
·
Alipata
UKIMWI kwa sababu wazazi wake hawakumpatia elimu ya jinsia yaathari za
kujamiiana
JINA LA KITABU
Jina la kitabu KILIO
CHETU linasadifu maudhui
yaliyomo ndani ,mwandishi ameonyesha kilio cha watoto wakiwalaumu wazazi na
walezi wao kwa kutowapatia elimu ya jinsia ili waweze kujikinga na janga hili
la UKIMWI.Hiki ni kilio cha jamii nzima ‘wimbo huu unathibitisha
Kiongozo:tunaangamiax4
Watu:tunakishax2
Pia
wimbo wa maombolezo kutokana na kilio chetu juu ya janga hili la UKIMWI hSWA
WATOTO
KIONGOZI:Joti
afwite sanda salauyax3
WATU:Ena
ena ena salayax3
No comments:
Post a Comment