MADA MPYA 3: KUHAKIKI KAZI YA FASIHI ANDISHI
MADA NDOGO-1: MAENDELEO YA FASIHI ANDISHI.
A.Mwelekeo wa kazi za
fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar wakati wa ukoloni.
Kimaudhui Kazi nyingi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar
zilishughulikia masuala mbalimbali ya kimaisha lakini kazi nyingi zilikuwa na
mambo ya mila na tabia kama njia ya kufundisha maadili .vile vile
zilishughulikia utamaduni, mawaidha, dini, maadili mema na maonyo na kazi
zilizoopinga ukoloni
Senkoro (1976) anaonyesha kuwa maandishi ya kwanza ya nathari
yaliyotokana na waafrika wenyewe na kama vile“Uhuru wa watumwa ‘(1934)
cha James Mbotela kinashughulikia uhusiano baina ya mataifa ya
magharibi na ya Afrika.Katika kitabu hiki mwarabu na muislam wanalaumiwa kwa
utumwa uliokuwepo Afrika Mashariki wakati mkoloni anasifiwa kwa kuleta uhuru japokuwa
utumwa ulitiliwa nguvu na ukoloni.
Kwa ujumla hadithi ya uhuru wa watumwa inaonyesha ubaya wa
biashara ya utumwa iliyoendeshwa na waarabu na papo hapo inaonyesha matukio
yaliyowapata watumwa mambo yaliyowaumiza na uchungu ulowapata watumwa hao.
Mwandishi anaeleza mateso ya watumwa kwa watumwa kwa uchungu
na mchomo mkali.Pia hadithi hii inawatukuza wakoloni wa Kiingereza, ikijaribu
kumfanya mwafrika akubali kutawaliwa.Hadithi hii inausuta utumwa wa kimwili uku
ukiusanifu ule wa akili na mawazo ambao ni utumwa ulio mbaya zaidi.
Senkoro anaendelea kusema kuwa baada ya mwaka 1949-1960 kazi
nyingi za fasihi za Kiswahili hasa riwaya zilifuata mkondo wa ngano na fasihi
simulizi kama za Paukwa pakawa…hapo zamani za kale palitokea kimaudhui fasihi
simulizi zilijali maadili ya kufuatwa katika kujenga jamii inayofaa katika
maisha.Mfano mzuri wa vitabu hivi ni Adili na Nduguzi (1952) utenzi wa
mwanakupona (1858) na Al-inkishafi (1890).
Katika Adili na Nduguze mwandishi alitumia visasili vya jadi ya
kiarabu kama vile matumizi ya majini anaonya dhidi ya uchoyo na kuhimiza moyo
wa wema, usamehevu na kutosheka.Katika utenzi wa mwanakupona,mama anatoa
mafunzo kwa binti yake.Humo ndani ya utenzi mwanamke anapaswa kujitazama kwa nyenzo
tatu
Ø Yeye ni nyenzo ya starehe ya mume
wake hivyo inampasa ajitahidi mno kumfurahisha ili apate rehema zake, kwani Mungu hata acha kumtia hatiani kwa kutotimiza huu mume
atakapomkana mbele ya Mungu.
Ø Inampasa mwanamke awanyenyekee
wanaume wote isipokuwa watumwa tu.Aonyeshe kilicho na heshima kubwa kwao.
Ø Mwanamke ajione kuwa yu mmoja wa
matajiri au maskini (watumwa).Binti anayeandikiwa shairi hili ni tajiri naye
anaaswa asichanganyike na watumwa, watu duni waliodharauliwa duniani
Shughuli za kisiasa zilizopamba moto
miaka ya 1950-1960 ilisababisha
kuibuka kwa fasihi ya kisiasa ambayo wasanii wake walizitumia kumpinga mkoloni.
Shaaban Robert pamoja na matatizo yake yote,
alionyesha upinzani wake hasa katika riwaya zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika
(1967) ambamo zaidi ya kuwatetea wajumbe mbalimbali walikuwa wakiutetea
uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Pia mwandishi anaitetea serikali ya kikoloni kwa kejeli kubwa
kwani ilikuwa inainyonya Tanganyika na Zanzibar kwa ajili tu ya kukidhi “Uguma
na Utasa” wa mfalme na malkia.Ugumba na Utasa ambao Shaaban Robert kautumia kwa
ishara tu ya mahitaji ya wakoloni.
Katika “Kusadikika” mwandishi
anajali suala la haki ya watu dhidi ya uongozi kandamizi wa kiimla utawala usio
na kiasi wala mpaka ni utawala ambao hatimaye hukwamisha maendeleo ya nchi na
watu wake.Kwa sababu huwanyima huwanyima watu uhuru wa kufikiri na kuchangia
katika maendeleo ya nchi yao kwa kutumia mbinu
ya kejeli, tashtiti, misemo, nahau.
Mwandishi amejitahidi kufikisha lengo lake la kuonyesha hasara ya kuyakwamisha
maendeleo ya nchi.
Ukoloni wa kiutamaduni ni mwanzo tu wa ukoloni wa siasa na
uchumi. Hata katika riwaya ya Tafsiri ya hadithi ya ”Chinua Achebe”Shujaa Okonkwo (1932) ambapo wamisionari walitangulia
kuja ili baadae watawala waje na kuiteka nchi yote. Hivyo wamisionari walishirikiana
na watawala katika kuwanyanyasa na kuwanyonya watu.
Mhusika wa zamani, hasa mhusika mkuu alikuwani halisi mwenye
sifa zisizo za kawaida ambaye alisanifiwa na msanii kwa makusudi mazima ya
kuumba. Mfano bora wa kuigwa na kumfanya awe kielelezo cha ukweli na ukamilifu
wa maisha na mwenye kupigania na kuleta mambo hayo bila kuwa na dosari. Mhusika
mkuu wa zamani alitafakari maisha ya jamii kwa njia ya matendo makubwa na lugha
teule. Mhusika huyo japo kuwa alijitokeza
kuwa mtendaji mkuu kiasi hicho lakini hakuwa na saikolojia wala hisia.
Sifa hizi za upungufu wa saikolojia na hisia katika mhusika mkuu wa zamani
ndizo zilizomtofautisha na mhusika mkuu wa kisasa.
Tofauti nyingine ya msingi ni ile inayohusu uhusianao kati ya
mhusika mkuu huyo na wakati. Mhusika mkuu wa zamani kama vile wa kwenye hadithi
ya kifasihi alijitokeza kama mhusika mkuu wa wa wakati wote. Kwa msanii wa
namna hiyo ya wahusika, dhana za wakati na ukweli uliokamilika zilikuwa katika
hali ya kutobadilika wakati na ukweli vilikuwa na vitu vilivyotitia pamoja.
Kwa jinsi hiyo maandishi ya kisanii yaliyopewa jukumu la
kuzibeba sifa hizo yalilengwa kuwa ni ya wakati wote, yasizeeke. Lakini kinyume
chake mhusika mkuu wa kisasa anayaona maswala yasiyotulia bali ni maswala
ambayo yana badilika pamoja na jamii. Na baadhi ya wasanii wa kisasa wanaona
kuwa, swala la ukweli uliokamilika kwa kiasi kikubwa ni ndoto iliyomo katika
vichwa vya watu tu, na wala si maisha
halisi.
Mhusika mkuu wa kisasayuko katika wakati maalumu wa
kihistoria ambapo anayazamia maisha kwa undani na kuyatafakari. Lakini kadri
Shaban Robert alivyozidi kuandika kama Maisha
yangu na baada ya mwaka Hamsini(1966) Wasifu
wa Siti binti Saad(1967) Siku ya utenzi wote(1968) ndivyo alivyozidi kuwapa
wahusika wake sifa zinazokaribia au zinazoelekeana katika hali halisi ya
maisha. Hii ina maana kwamba mkabala wake ulizidi kuelekea katika hali ya
kueleza ukweli kwa kutumia mbinu za kisanii ambazo hazikutenga kazi ya Sanaa
kwa kiasi kikubwa na uyakinifu wa maisha.
Kwa ujumla fasihi Andishi ya awali ilihusu zaidi maadili na
masuala ya kidini kama katika”Adili na nduguze”.
Pili mvutano ulikuwepo baina ya wakoloni na waafrika, Ulikuwa unadhihirishwa katika baadhi
ya kazi za fasihi Andishi za awali.Pia maandishi mengine ya fasihi yalihusu
matarajio ya jamii itakiwayo baada ya ukoloni, kama katika kufikirika na
kusadikika, katika kipindi hiki tanzu za fasihi andishi zilizokuwapo ni riwaya
na ushairi. Baada ya uhuru, tamthiliya zote za Kiswahili zilizochapishwa
zilikuwa zimeandikwa na wakenya, watanzania, hawakujitokeza katika uwanja huu
hadi baada ya uhuru.
B: Mwelekeo w kazi za fasihi Andishi nchini Tanzania baada ya
uhuru
Baada ya uhuru
kulikuwa na fasihi mchangamano ambayo ni vigumu kuainisha hadi tukio kuu la
kutangazwa kwa Azimio la Arusha, kabla ya hapo fasihi kwa kiasi kikubwa,
ilikuwa ya kushangilia uhuru uliopatikana hasa katika magazeti ambako mashairi
na hadithi nyingi zilionyesha hoi hoi ya lelemama za uhuru.
Kwa upande wa mashairi, vitabu kama vile Utenzi wa uhuru wa Tanganyika(1967) na utenzi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania(1968) viliandikwa wakati
huo. Ni kipindi hicho cha uhuru utanzu wa tamthiliya ulijitokeza kwa mara ya
kwanza kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar.
Mwandishi maarufu wa tamthiliya aliyejitokeza kipindi hicho
Ebrahim Hussein ambaye tamthiliya yake ya kwanza “wakati ukuta”(1969)
ilichapishwa ikifuatiwa na tamthiliya ya “Kinjekitile”(1969)
Fasihi ya Kiswahili imepevuka zaidi kwenye miak ya 1970.
Mulokozi(1996) anasema karibu tanzu zote za fasihi Andishi ya Kiswahili
zimepata wawakilishi. Hali hii imejitokeza fasihi za mokondo mbali mbali.
Kimaudhui, fasihi andishi nchini Tanzania baada ya uhuru
imejadili dhamira mbali mbali ambazo zinatokana na matukio mbali mbali ya kihistoria yaliyojitokeza
katika jamii yetu ya Tanzania.
Kipindi maalumu cha maisha kina matukio yake maalumu ambayo
huigusa jamii kwa uzuri au ubaya na kuwa dundo la moyo la kipindi hicho ndichi
kinachojenga kilele. Aidha tukio linapokuwa dundo la moyo la kipindi fulani cha
maisha huwa pia mada kuu(muhimu) ya wakati huo kwa jamii inayohusika.Mada hiyo
uweza kujitokeza kinagaubaga katika taaluma mbali mbali za jamii na fasihi
ikachukua nafasi muhimu.
Kihistoria masuala makuu ya miaka ya 1960 yalikuwa ni ukombozi wa bara la
Afrika na ujenzi wa jamii mpya baada ya uhuru. Masuala haya makuu
yaliyojitokeza katika fasihi andishi ya
Tanzania wakati huo. Hivyo palitokea fasihi andishi za kisiasa na kifalsafa zilizojadili
kuhusiana na maisha, utawala na ujenzi
wa jamii mpya.Kazi nyingi za fasihi zilipingana
na ukandamizaji, ubinafsi na pamoja na unyama mwingine uliokuwa
unafanywa.Pia zilieleza mkondo wa ubanadamu usawa na ustawi. Baadhi ya kazi
hizo ni za Shaaban Robert, Utu bora
mkulima (1987) na siku ya watenzi wote(1968)
Kwa upande wa ukombozi, riwaya ya kiimbila “Lila na Fila” (1966) iligusa dhamira
hiyo kiishara na Tamthiliya ya E.
Hussein”Kinjekitile” (1969). Katika
kipindi cha miaka ya sitini ilitokea fasihi ya tabia na maadili ambayo
imejadili maadili mema na maonyo.
Fasihi hii ya tabia na maadili inawakilishwa na J.M Somba “kuishi
kwingi kuona mengi”(1968) “Alipanda
upepo akavuna tufani” (1968) Mathias Mnyapala “Diwani
ya mnyapala”(1965) S.A Kandoro “Mashairi ya Saadan”(1972), Akili mali “Dwani
ya Akili Mali”(1967)
Aina nyingine ya fasihi iliyojitokeza katika kipande hiki ni
ile riwaya na hadithi fupi za upelelezi na za mapenzi. Fasihi ya aina hii
ilizuka kutokana na nguvu mbali mbali za jamii.
Katika Tanzania, aina hii ya fasihi ililetwa kwa mara ya
kwanza na M.S Abdulla alipoandika riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale”(1959) na miaka ya 1960 aliandika riwaya ya “kisima ch giningi”(1968) akafuatiwa na
katalumbwa aliyeandika kitabu cha “Simu
ya Kingo”(1965)
Mwisho kazi za fasihi zilijitokeza miaka ya sitini ni fasihi
ya mila na utamaduni inayowakilishwa na M.S Farsy “Kurwa na Dotto”(1960) F.Nkwera “Mzishi wa baba ana radhi zake” (1968)
Mwaka 1967, Azimio la Arusha lilitangazwa. Azimio hilo
lilionekana kwa wanasiasa na wananchi wengi kuwa ndio dira ya kuitetea jamii ya
Tanzania katika maisha bora ya ufanisi na maendeleo kwa hiyo kipindi cha miaka
mitano hivi baada ya Azimio la Arusha kilikuwa
na fasihi ambayo ilitukuzwa maadili na awali zilitokana na tamko la Arusha.
Maudhui yaliyotawala fasihi ya kipindi hiki ni ujenzi wa
jamii mpya kwa kupitia nguzo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kazi hizi
zilizosisita mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni,
zilizopigania jamii mpya Ijapokuwa bila kuonyesha kimantiki (kiyakinifu) vipi
jambo hilo lingewezekana. Mfano wa kazi hizi ni:-Mashairi ya miaka kumi ya Azimio
la Arusha (1977),Mashairi ya Azimio la Arusha
(1970),Utenzi wa zinduko la ujamaa (1972),Utenzi wa kumbukumbu za Azimio
la Arusha (1970),Matunda ya Azimio la Arusha (1980),Liwazo la ujamaa (1978),Mtu
ni utu (1971),Ndoto ya Ndana (1976),Njozi za usiku (1970),Kijiji chetu (1971)
n.k
Pia kutokana na Azimio la Arusha pamoja na siasa yake iliyosisitizakuhusu umuhimu wa
vijiji na umuhimu wa kilimo, zilitokea kazi za fasihi ambazo zilihubiri kuhusu
maisha bora wa vijiji yaliyo linganishwa na yale ya mjini.
Suala ambalo liliwahi kuangaliwa na Shaaban Robert katika
riwaya yake ya “Utubora Mkulima”(1968). Sasa ilipata damu mpya katika kazi kama
za Penina Muhando,”Hatia” (1971)
Balisidiyo Shida (1975) Mnyampala, Ngonjera
za ukuta (1968) Mbogo “Giza limeingia”(1980) mashairi mbali
mbali katika magazeti n.k katika kazi hizi mvutano baina ya mji na kijiji ambao
ulileta matatizo ya wizi, ujambazi, umalaya na mengine ya aina hiyo yalitolewa
dawa moja, kurudi vijijini. Jawabu
hili halikuwa sahihi kwani linakwepa kiini hasa cha tatizo na lilipotosha
maana halisi ya kijiji na kilichotakiwa kuundwa katika jamii ya Tanzani.Kijiji
kilionekana kuwa mahali pa kuwalundika wahuni walioshindwa maisha ya mjini.
Katika kipindi hiki cha 1970-1980 zilijitokeza kazi ambazo zilitazama suala
lakujenga jamii mpya kwa kutafakari na kujiuliza na hata kwa mashaka na wasi
wasi pia. Hususani baada ya kubaini utata, migongano ya kitabaka na ukuaji wa haraka
wa ubepari wa kimji. Mfano Kiu (1972) Kichwa maji (1974),Gamba la
nyoka (1979),Nyota ya Rehema (1978) Dunia uwanja wa fujo (1979) ( Madumulla 1988)
Kwa ujumla miaka ya 1980 riwaya ya Kiswahili imeshuhudia
jaribio la muundo wa riwaya ya kifalsafa. Lakini kama ilivyogusiwa kwa kiasi
kikubwa mikondo ya riwaya imeendelea kuwa ile ile ya miaka ya sabini. Riwaya ya
ukasuku katika upande wa riwaya dhati imepotea. Badala yake kuwa riwaya
inayopevuka nakutumia ukweli wa mambo. Inayojaribu kubainisha migongano ya
kijamii katika vipengele mbali mbali vya maisha hususani vya kiuchumiu ijapokuwa
waandishi wanafanya hivyo katika mkabala au mitazamo ya maisha
inayotufautiana,mikabala hiyo ni kama vile;Mfumo wa vyama vingi,Utandawazi
Kipindi hiki mfumo wa chama kimoja ulifutika na mfumo wa
vyama vingi ukaanzishwa hapa nchini ambapo uliambatana na kuanzishwa kwa
utitiri wa vyama vingi. Fasihi andishi iliyojitokeza kipindi hiki ilizungumzia
mfumo wa vyama vingi na athari zake kwa jamii yake. Mfano wa kazi hizo ni
riwaya ya “Nyuma ya pazia” (1996),
na mashairi mbali mbali yaliyokuwa yanaandikwa kwenye magazeti.
Kwa upande wa utandawazi ambao unaenda sambamba na
ubinafsishaji wa soko huria umewaathiri sana waandishi wa fasihi ya Kiswahili.
Katika fasihi ya Kiswahili utandawazi
umesababisha kuzuka kwa fasihi mpya ya Kiswahili ambayo imezaliwa mwanzoni mwa
miaka ya 1990, muda mfupi baada ya neno utandawazi kuingia masikioni na kuzama
akilini mwetu kuanzia 1980.
Utandwazi ni neno dhahania lenye maana nyingi tata kutegemea
msisitizo wa anayelitumia. Pamoja na tofauti za maana na matumizi ya neno hili
wataalamu wakubliana kwamba ni neno linaloelezea mfungamano na uhusiano
uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita, hasa katika biashara na uchumi. Lakini
pia katika utamaduni, miongoni mwa jamii tofauti za dunia zimekuwa na mfungamano
na uhusiano uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita hasa katika biashara na
uchumi,na kiutamaduni. Mfungamano na uhusiano huu unaotofautishwa na uhusiano mwingine wa aina hii uliojitokeza
kabla, kwasababu utandawazi umepata kazi kubwa ya kuwekeza mitaji na kuvuna
faida kubwa kiuchumi kiutamaduni, ikisaidiwa na maendeleo makubwa ya
kiteknolojia yaliyopatikana karibuni hasa ya vyombo vya habari vya masafa marefu.
Utandawazi unahusishwa na kuenea kwa tamaduni za kimataifa (Marekani na Ulaya)
kwa njia ya biashara (kama vile vinywaji vya Cocacola, bia na pombe kali ambazo
zamani zilikuwa hazijulikani). Mtiririko wa muziki na taswira kupitia
video,luninga,mitandao ya kompyuta/Tanakilishi na simu,CD, DVD na VCD.Mfano wa fasihi
ya Kiswahili ni kama vile Nagona(1990), Mzingile(1990), Zirani na
zraili(1999), Babu alipofufuka(2001). Makundi wa soko huria(200), Baria-
Adam(2002), Dunia yao(2005), Mkamaduma(2005) zimeathiriwa sana na
utandawazi wa kimagharibi, sifa moja kubwa ya kimaudhui miongoni mwa kazi hizi
ni ile ya kushughulikia kwa kina matatizo ambayo yana kabili ulimwengu wetu
leo. Ingawa bado riwaya hii inajishughulisha kwa kiwango fulani na matatizo ya
ndani ya nchi na jamii husika kwa kiasi kikubwa imekiuka mipaka ya kitaifa na
kuenea kwa kiasi kikubwa inachunguza si jamii ya Tanzania tu bali dunia yote
huku ikionyesha athari za utandawazi kwa jamii hizo.
Katika Babu alipofufuka (2001), Dunia yao(2003) na
hata Bina- Adamu (2002), Suala zima linaloshughulikiwa kifalsafa ni
siasa. Nini maana ya kuishi? Nini maana
ya uhuru? Nini maana ya maendeleo? Nini maana ya uraia wa mtu? Nini maana ya
uzalendo? Kwanini kikundi kidogo cha watu wapange maisha ya watu wengi
katikavjamii fulani nan je ya jamii hiyo? Kuna dunia ngapi katika dunia moja ya
jamii fulani? Mipaka ya dunia hizo ni
miembamba au mipana kwa kiasi gani? Nini maana ya kijo? Nini maana ya kuishi?
Inawezekana mtu anayeishi akawa amekufa? Nguvu zipi zinaongoza limwengu wetu?
Zinaongoza kwa mslahi ya nani na kwa taathira?.Athari hizi za utandawazi
katika jamii na maisha halisi zimehitimishwa na Chachage, ambaye riwaya yake ya
“Makuadi
wa soko huria”(2002) inavua nguo na kusambaratisha utandawazi na
utetezi wake wa ndani.
Kwa jumla maendeleo ya
fasihi Andishi nchini Tanzania baada ya uhuru ni makubwa sana ukilinganisha na wakati
wa ukoloni. Tanzu zote za fasihi Andishi,
riwaya, hadithi fupi ushairi na tamthiliya zimepanuka sana. Vile vile kama
waandishi wengi sana wa tanzu hizo na uandishi wao umekuwa ukibadilika kulingana
na mabadiliko mbali mbali yanayoitokeza katika jamii. Kila tukio la kihistoria
lililotokea katika jamii limezaa kazi zake za fasihi.
MADA NDOGO 2; KUHAKIKI USHAIRI
USHAIRI
Ushairi ni Sanaa
inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye muwala,kwa
lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi
ya wimbo ili kueleza tukio, wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi
fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.Kutokana
na maana hiyo kuna mambo muhimu yanayojitokeza katika ushairi:
Ø Ushairi ni Sanaa yaani kazi
iliyobuniwa na mtunzi mahususi.
Ø Ushairi una ufungamano na hisia.
Ø Ushairi una mpangilio wa aina fulani
kuanzia kiwango cha sauti, neno, sentesi hadi ubeti.
Ø Ushairi huchota hisia na tafakari
zake kutoka katika ulimwengu halisi wa maisha ya jamii na mara nyingi
hufungamana na falsafa ya jamii fulani.
Ø Ushairi hutumia lugha ya mkato yenye
kueleza mambo mengine kwa maneno machache kwa kutumia mbinu za taswira na
tamathali za semi.
Ø Ushairi huzingatia sana dhana ya urari
(ulinganifu wa vitu) kimuundo.
Ø Ushairi una uhusiano na muziki
(nidhimu) ngoma na uchoraji (mchoraji) hutumia rangi na brashi mshairi hutumia
taswira na maneno.
AINA (KUMBO) KUU ZA
MASHAIRI YA KISWAHILI
MULOKOZI(1996) Ameainisha aina tatu za ushairi waKiswahili.Aina
hizo ni:-
I)
USHAIRI WA KIMAPOKEO
Ni mashairi na tenzi za kijadi zenye
kufuata kanuni za urari wa mzani na mpangilio wa vina vya mwisho au kati.Katika
ushairi wa kimapokeo kuna mambo ya msingi ambayo yanasemekana kuwa ni mti wa
mgongo wa ushairi wa Kiswahili.
Kwa
mujibu wa wanamapokeo.Shairi la
Kiswahili lazima liwe na vina na mizani,mistari ubeti na kituo.
Katika utenzi (aina pia ya ushairi wa
kimapokeo) kuna kuwa na bahari katika mstari wake wa mwisho.
Ushairi wa kimapokeo unaweza kugawanyika katika sehemu
kuu mbili yani Tenzin na Mashairi
a) TENZI
Ni utungo ambao kimaudhui huelezea tukio fulani linalotokea
katika jamii au liliwahi kutokea.Pengine huweza kuwa maelezo juu ya wasifu wa
mtu fulani, jambo fulani la kihistoria au jambo lolote zito linaloelezwa kwa
maelezo marefu.Utenzi ni masimulizi marefu juu ya jambo fulani maalumu
Katika upande wa fani
utenzi una sifa za pekee kabisa
v Utenzi unakuwa na beti nyingi kuliko
yalivyo mashairi au aina nyingine yoyote ya ushairi.Beti hizi zaweza kuwa 100,
200, 300 au zaidi kutegemeana na ufundi wa mshairi mwenyewe.
v Utenzi huwa hauna mizani ndefu,tenzi
zilizo shamiri sana katika jamii hii ni zile zenye mzani nane nane katika kila
mistari zaweza pia kwenda zaidi ya nane kufikia kumi na moja lakini hazuii
zaidi ya hapo
v Katika utenzi kila ubeti huwa na
mistari minne, mistari mitatu ya kwanza ikiwa ina vina vyenye urari sawa na ule
wa mwisho ikiwa na kina tofauti ingawa vina vya mistari mitatu ya kwanza huwa
na vina vyenye urari sawa lakini vina hivyo hubadilika badilika toka ubeti
mmoja hadi mwingine.
v Katika utenzi kina cha mwisho katika
msitari wa mwisho wa kila ubeti huwa hakibadiliki badiliki, kina cha mwisho
wataalamu wengi wa ushairi hukiita bahari kwa sababu huwa kimetenda na
kuongelewa katika utenzi mzima Mfano wa
tenzi: S.Robert, Mapenzi bora,A.Abdilatif, Utenzi wa maisha ya Adam na Hawa
(1971) J.K.Nyerere, Utenzi wa Injili
kadiri ya utungo wa Luka (1996).Mfano Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK)
Ubeti
6: Liyongo Kitamkali
Akabalighi vijali
Akawa mtu wa kweli
Na
hiba huongeya
Ubeti 7: Kilimo kama utukufu
Mpana sana mrefu
Majimboni yu maarufu
Watu hujakumwangalia
Ubeti 10: Sultani pate Bwana,
Papo nae akanena,
Wagala mumemwona,
Liyongo kuwatokeya
b) MASHAIRI
Shairi kama sehemu ya ushairi, ni utungo ambao
huelezea kwa ufupi mambo fulani kuhusu binadamu na mazingira yake.Aghalabu mashairi
huelezea mambo yanamhusu binadamu na maisha yake ya kila siku.Mashairi ya
kimapokeo yanapoandikwa hufuata kanuni za vina, mizani, mistari, ubeti na kituo
mfano:-
KUNTU SAUTI
YA KIZA (FUNGATE YA UHURU-UK 38)
Nyuki ni mtanashati, umbo na zake tabia,
Yeye yu kila wakati, vichafu huvikimbia,
Mchana na kulati, hatui kwa kukosea,
Kuntu sauti za kiza, Nyuki hapendi vichafu.
Ni inzi na sio nyuki, Nadhafa hajazoea,
Kwa uchafu ni ashiki, hawezi kuuachia,
Vianzavyo humiliki, fahari hujonea,
Kuntu Sauti za kiza, Nyuki hanyoni vichafu.
U WAPI UZURI
WAKO
U wapi uzuri wako, haupo umepotea,
Ya wapi maringo yako, na hashuo za dunia,
Leo upo peke yako, sote tumekukimbia.
Sasa ni chano cha maji, watu wajichanyatia,
Umekwisha ujuwaji, haya zimekupatia,
Yale usoyatarajia kwako yamekuhamia.
DAFINA
Paa ni kuruka angani, kama ndege wa tiara
Paa ni mnyama porini, ni mwenye nyingi, Papara
Paa ni kuteka mengine, moto uwako imara
Paa ni toa migombani, Samaki atie sura
Paa Pia ni la nyumba, makuti au kurara
Mgodi wa Kiswahili ni dafina isiyokwisha
2. USHAIRI
WA MAIGIZO
Ushairi huu unahusisha ngonjera na ushairi wa kidrama
v NGONJERA
Ni ushairi wa majibizano ulioanzishwa na Mathias
Mnyapara miaka 1960 ili kueleza siasa ya ujamaa na kujitegemea kabla ya hapo
ulikuwepo ushairi wa majibizano lakini ulikuwa unatambwa tu.
Ø Katika ngonjera kuna pande mbili zinazojibizana kuhusu
mambo fulani upande mmoja huwa sahihi na wa pili huwa umepotoka.
Lengo la mabishano ni kuushawishi upande uliopotoka
ukubaliane na upande wenye msimamo sahihi baada ya kuelimishwa. Hili
linapotokea ngonjera huwa imefikia kilele chake. Mfano wa ngonjera ni Ngonjera za ukuta 1 na 2 (Mnyapara
1970-1972)
Ushairi wa kidrama ni ule unaotumika katika baadhi ya
tamthiliya. Ushairi huo ni sehemu tu ya mchezo wa kuigiza ni mtindo wa kuandika
mazungumzo ya wahusika katika tamthiliya hivyo hauwezi kutenganishwa na hiyo
fani ya tamthiliya. Kwa mfano tafsiri Shaspare, Mabepari wa Verusi Julius
Kaizari (Nyerere) 1969, Mfalme Epidope (Mushi 1971)
Mfano:
Juma: Naam na nitampa bure bila ya fidia
Pokeeni na Jeshika kutika kwa Myahudi
Hati maalum ya hiba, baada ya kifo chake
Ataacha kwenu nyingi, kila atakachokiacha
Baraka: Mabibi wema, mwaonyesha maana kwa walagai
Neema: Kunakaribia kucha, lakini nina hakika
Bado hamjaridhika, kabisa na mambo hayo
Kwanza na twendeni ndani, kisha huko tuhajiri
Nasi tutawajibuni, mambo yote sawa sawa
(W.
Shakespare, Mabepari wa virusi 1969)
Katika mfano huu ushairi huu una mizani 16 kwa
mshororo bila urari wa vina, kanuni ya utoshelezi imekiukwa wazo la mshororo
mmoja linaendelezwa katika mshororo unaofuata.
3.
USHAIRI WA
MLEGEZO / KISASA / MASIVINA
Ni mashairi yasiofuata urari wa vina na mizani, Vina
vinaweza kutoka lakini si lazima katika mistari. Pia mapigo yanaweza kuwa sawa
kwa idadi katika mfululizo wa vipande kadhaa lakini si katika tungo nzima.
Mfano:
CHAI YA JIONI
Wakati tunywapo chai hapa upenuni
Na kuwatazama watotowetu
Wakicheza bembea kwa furaha
Tujue kamba ya bembea yetu
Imeshalika na imeanza kuoza
Na bado kidogo tutaporomoka
Kulikuwa na wakati uinisukuma juu
Nikaenda zaidi ya nusu duara
Kulikua na wakati nilidaka
Ulipokimbia na kuanguka
Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza kutekeleza tena
Tumalize machicha ya chai yetu ya jioni
Bila kutema tena na kuwa tabasamu
Baada ya hapo tujilambe lambe utamu utamu
Uliobakia kwenye midomo yetu
Tukikumbuka siku ilee ya kwanza
Tulipoutana jioni chini ya mwembe
Tukifunga bembea yetu
Naye umbwa samba akikusubiri
Lakini kabla hatujaondoka kimya kimya
Kukamilisha nusu duara iliyobakia
Tuhakikishe vikombe vyetu visafi
(Kazilahabi 1988)
VIJENZI VYA USHAIRI WA KISWAHILI
Ushairi wa Kiswahili unajengwa na vipengele
vifuatavyo:-
1. Mpangilio wa
maneno
Maneno ya ushairi hupangwa ili kuleta maana fulani,
sauti za aina fulani au urari fulani wa mizani.
Katika shairi la Kazilahabi “Kisu mdomoni” , kisu
mdomoni (kiuchumi) uk 10 kuna mstari ufuatao.
“Ya nyuma sana nisijali ya mbele sana niyakabili. Hapa
neno “sana” limewekwa makusudi kati ya “nyuma” na “nisijali” ili kupata maana
mbili. Mambo ya zamani sana (ya nyuma sana) na kutojali jambo neno (sana
nisijali) kama neno sana kinga kuja baada ya nisijali maana hizo mbili
zisingalitokeza. Vivyo hivyo uwili huu wa maana tunaupata katika kipande cha
pili cha mstari huo “ya mbele sana niyakabili” kutokana na mpangilio wa maneno.
2.
Takriri na
Ridhimu au wizani
Takriri ni mbinu ya kurudia rudia jambo kwa kusudi maalumu,
vina na urari wa mizani ni aina ya takriri. Mtunzi anaweza pia kurudia rudia
maneno fulani au silabi fulani kwa shabaha malumu. Kwa mfano katika shairi la “
Kufa moyo” Shaaban Robert anatumia mbinu ya takriri kwa kurudi rudia kifungu
cha maneno “ siku ya ………. Kwa msisitizo:-
Siku ya panga kufuta, mashujaa kwenda kona
Siku ya kuja matata, kwa damu kwenda mdundo
Siku ya watu kuteta, kufa moyo mfundo
Siku ya kung’ara nyota za watenzi wa mtindo
(Shaaban
Robert 1991 : 48-49)
Takriri hutumika sana katika nyimbo na mashairi ili
kutia msisitizo.
Ridhimu ni mapigo asili ya lugha , kila lugha ina
mapigo yake. Mawimbi ya sauti yenye kupanda na kushuka na yanayofunga maana na
mfuatano wa sauti usio na maana yoyote.
Ridhimu ya ushairi wa muziki hutokana na mlingano wa
vipande vya mapigo ya lugha au sauti . Katika muziki vipande hivyo vya mapigoni
lazima vilingane kabisa katika ushairi.Vinaweza kupitana kidogo ili kupunguza
maudhi masikioni.
3.
Taswira au
Picha
Taswira ni mbinu ya kuumba picha ya jambo katika mawazo
ya msomaji au msikilizaji wa tungo hilo kwa kutumia maneno. Picha ya maneno
ikichorwa vizuri mtu huweza kuhisi, kuona, na hata kunusa kile
kinachozungumzwa.
Mfano:
Amina umejenga, umekufa umetangulia
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga, peponi kukubaliwa
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
(S. Robert Amina 1966: 3)
Katika ubeti huu, mshairi analinganisha maisha ya
mauti ya Amina kwa njia ya picha na ua mbalo limekuwa likichanua na kisha
likafunga au kunyauka.
4.
Tamathali za
Semi
Tamathari ni umithilishaji yaani uwakilishaji wa jambo
kwa kulinganisha au kulifananisha na jingine.Kwa mfano badala ya kusema “Juma
alikuja mbio sana” Mshairi atasema “Juma alikuja kama umeme” Tamathari nzuri
hupanua, huyadumisha na huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayoelezwa,
huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au msikilizaji wa shairi na athari ya
kudumu katika hisia na mawazo yake.
Tamathari zinazotumika zaidi katika ushairi ni
Tashbiha, tafsida, tashhisi, mbalagha, kejeli, sitiari n.k.
5.
Hisia za kishairi
Hisia hizi hutokana na msukumo wa ndani wa moyoni
alionao mshairi wakati anapotunga shairi lake na hujidhihirisha katika uteuzi
na mpangilio mzuri wa maneno yenye kuwakilisha maudhui husika kwa mfano,
maudhui ya huzuni hudhihirika katika maneno yanayotumika ambayo aghalabu
yanadokeza hali ya huzuni, vina vyenye sauti ya kilio.Mfano ee, lel, lel, lel,
ea, aa, ya n.k.
Mfano mzuri ni shairi la Shaaban Robert la AMINA
ambazo linaomboleza kifo cha mkewe.Hisia za furaha pia huweza kuwasilishwa kwa
njia hizo hizo
Mfano:-Shairi la Cheka kwa furaha
Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha!, ndio ada duniani,
Basu cheka kwa! kwa!, usifike moyo wako.
(Robert, kielelezo cha fasihi 1968:16)
6.
Lugha ya
mkato.
Shairi huzungumza mambo wa ufupi kuliko ulivyo katika
maongezi ya kawaida. Hivyo ni muhimu kwa mtunzi kujua namna ya kueleza jambo
kwa Lugha ya mkato.Hii inawezekana kwa kutumia taswira na tamathali badala ya
maelezo marefu.
7.
Mchezo wa
maneno
Mbinu ya kuchezea maneno hutumiwa na washairi ili
kutoa maana ya kile kisemwako na kuongeza utamu wa usemaji mara nyingi maneno
yenye umbile moja lakini maana tofauti hutumiwa kwa ajili hii mfano katika
Shairi la M.Mulokozi la “wale, wale” maana tatu za neno wake (yaani kundi la
watu na hao watafune na kumeza chakula “na” “wale”wale” kwa maana ya “hao hao”
si wengine zinachezewa ili kuleta ujumbe fulani.Mshairi anaona kuwa hakuna
mabadiliko ya msingi yaliyotokea .Kundi lile la walaji limerejea katika
madaraka kadharika maneno “kura” na “kula” yamewekwa sambamba ili kuonyesha
uhusiano uliopo kati ya uchaguzi (kupiga kura) ulaji.
Wale wale
Wale wale ndiyo wao
Bado wapo palepale
Wao wale wenye vyao
Na vya kwao vile vile
Wala kale wala leo
Kura huko kule kule
Mwendo huu ndiyo huo
Bado tupo pale pale
(Mulokozi 1990)
FANI NA MAUDHUI
Ushairi kama Sanaa hujengwa na mambo mawili ambayo ni
fani na maudhui.Maudhui ni mambo yaliyomo (yanayozungumzwa) ndani ya shairi na
fani ni njia anazozitumia mtunzi kuyasawirisha maudhui yake kwa hadhira
yake.Fani na maudhui huingiliana hutegemeana na kukamilishana.Ni mambo ambayo
hayatunganiki, fani hubeba maudhui, na maudhui huathiriwa na fani.Uwiano wa
fani na maudhui ndiyo kigezo bora cha ndani cha ubora wa shairi.
Katika fani kuna mambo yafuatayo:- Muundo, mtindo,
matumizi ya lugha na jina la kitabu katika kipengele cha lugha kuna mpangilio
wa maneno, tamathali za semi, methali, misemo, picha n.k.
Maudhui ni mawazo yanayosemwa ndani kazi ya Sanaa.Mada
kuu inayayozungumziwa katika shairi huitwa dhamira.Dhamira inapounganishwa na
mtazamo wa mtunzi, Shabaha na ujumbe hupatikana yanaweza kuhusu jambo lolote
linalohusika.Maudhui yanaweza kuhusu jambo lolote linalomkera mwanadamu kwa
mfano maana ya maisha, mapenzi, mauti, ndoa, elimu, kazi, dini, ukombozi,
usaliti n.k.
UHAKIKI WA
VIPENGELE VYA FANI
a) Mtindo wa
mashairi
Masharti ya Kiswahili yana mtindo mingi sana katika
utungaji wake kwa hakika si rahisi kutambua ama au idadi ya aina za utungaji wa
ushairi, kwani hii hususani kutegemeana sana na ufundi wa mtungaji
mwenyewe.Baadhi ya mtindo ya utungaji wa ushairi ni kama ifuatavyo
a) Mtindo wa
pindu
Katika
utungaji wa aina hii silabi mbil za mwisho wa mstari hurudiwa rudiwa kwa mfano:
kama mstari wa kwanza uliishia na neno “fahamu” basi mstari wa pili utaanza na
silabi mbili za mwisho, yaani “hamu” wakati mwingine huitwa “Mkufu”
Mfano: Zipokeeni Salamu, lamu kila na mvita,
Vita kwa wanadamu, damu zinawezachonyota,
Nyota njema ni agumu, gumu jema
kulipata,
Pata kwa kuyafuata, fuata mambo mazuri.
Zuri katika dunia, nia mama yanaleta,
Leta kila la sheria, ria huleta matata,
Tata watu hujifia, fia ipo kwa kupita,
Pita usije kupita, pita katika mazuri.
(waniitila,
kichocheo cha fasihi simulizi na andishi Uk 224)
b) Mtindo wa
msisitizo
Kuna
msisitizo wa aina mbili, kuna msisitizo wa wima na msisitizo wa ulalo
Msisitizo
wa wima ni kule kuwa na neno moja likawa linatokea mwanzoni na linarudiwa
katika kila mistari wa shairi zima
Mfano: Ua langu la moyo, nitunzo nipowe
Ua langu usinitunze, ua nitunze nitowe
Ua nikae shingoni, ua usinichambue
Ua la moyo ua, Ua lichanue kwangu
(Diwani ya Akilimani 1973:63)
Msisitizo
wa ulalo ni ule wa kutumia kibwagizo kama kiini cha habari yote inayozungumziwa
katika shairi lote na ikawa hicho kibwagizo cha rudiwa rudiwa katika kila ubeti
wa shairi
Mfano: Kokoni kucha kuchile, risala enenda hima,
Kufika similatile, ulitimavu si mwema,
Kumbe nao watambule, haya ninayoyasema,
Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
Sipendelei kusudi, na manji mno kusema,
Nendapo hijitahidi, kimya change hatuzamu,
Kanama sio mwadi, watu wengine si wema,
Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.
(fani na taratibu za ushairi wa
Kiswahili 1939:18)
c) Mtindo wa
beti kubadilisha vina.
Iwapo
katika ubeti wa kwanza kina cha kati kilikuwa “na” na ile ile cha mwisho
kilikuwa “ma” basi katika ubeti unaofuata kina cha kati kitakuwa “ma” na kile
cha mwisho kitakuwa “na”.
Mfano: Kila shairi nalia, chozi latoka machoni,
Na ninyi mwangalia, wala hamniponzeni,
Mpenzi kankimbia, naudhika simwoni
Nirudie we mwandani, roho ipate tulia.
Nakuomba samahani, magoti nakupigia,
Nisamehe nuksani, zote nilo kutendea,
Naapa kwa yangu dini, kamwe sitayarudia,
Narudia we mwandani, roho ipate tulia.
d) Mtindo wa
kubadilisha vina vya kati toka ubeti ili hali vile vina vya mwisho katika ubeti
vikibaki vile vile
Katika
ubeti wa kina kina cha mwisho kilikuwa “za” basi kina hicho kitaendelea kujitokeza
ubeti mmoja hadi ubeti mwingine wakati vile vya kati vitaendelea
kubadilikabadilika.
Mfano: Jalali wangu mchunga, nikidhi yako rehema,
Niweke natangatanga, nitabaruku kwa wema,
Niweke kwenye kiunga,cha malisho ya uzima,
Na majani ya rehema, na vijito vyenye
raha.
Tabaruku moyo wangu,
nisifikwe na zahama,
Pasinifike machungu, kwani u mwenye hunena,
Nakutegemea tangu, wala sinayo tahuma,
Uniongoze kwa wema, nami nitakutukuza.
(fani na taratibu za ushairi wa
Kiswahili 1986:38-39)
e) Mtindo wa
kidato
Katika
muundo huu baadhi ya mistari na maneno yake au silabi zake zina maneno machache
au zimefupishwa tofauti na mistari mingine ambayo huwa na silabi au maneno
mengi.Ufupishaji huu wa maneno au silabi katika baadhi ya mistari hufanywa kwa
lengo maalumu.
Mfano:Tohara,
kwa wanawake ni hatari
Madhara, kwa wake uke, hushamiri
Hasara, ya peke yake, hudhurika
Zinduka
(Wasakatonge 2004:02)
f) Mtindo wa
kuhoji
Huu
ni mtindo unaotumiwa na mwandishi wa kuuliza maswali ambayo aidha majibu yake
yako wazi au hayako wazi hivyo mtindo huu unaweza kutumika kama tashtiti.
Mfano: Si wewe?
Ukinijia mapema kama ukidayatema,
Nikawa kama wako baba na mama,
Kakulea kwa ugonjwa na uzima,
Ni wewe uso hisani.
Si wewe?
Niliyekunyima chungu kukutafutia tamu,
Kila kichota hakisishi hamu,
Ukazoa bila kufahamu,
Kuhujua kuichota,
Ni wewe ujilaumu.
(Fungate la uhuru 1996:42-43)
g) Mtindo
binafsi
Huu
ni mtindo ambao mwandishi anaweza kutumia nafsi ya umoja au wingi au nafsi
kundi kila nafsi ina maana yake kimaudhui.Nafsi moja huzungumzia mambo fulani
yanayomkabili mtu mmoja tu.Mara nyingi huwa ni maonyo, mawaidha au sifa.
Mfano: Umeshapwelea nchi kavu,
Wako werevu umekwisha,
Sasa tunatweta,
Utaabani,
Ni wewe ulo mrafi,
Si wewe?
(Wasakatonge 2004:21-22)
Nafsi
nyingi hutokea pale mashairi anapozungumzia na kundi fulani la watu huku na
yeye akiwa mmojawapo.
Mfano: Hatukubali tena,
Kwetu kurudisha ubwana,
Kwetu kuurejesha utwana,
Kwetu kuurejesha utumwa.
Hatukubali katu,
Ndani ya nchi yetu.
Hiyo huru.
(Wasakaonge 2004:30-31)
Lakini
nafsi kundi hutoka pale ambapo mwandishi au msanii anapozungumza na kundi la
watu huku yeye akiwa ama msimulizi.Hutoa masimulizi kama hadithi au hotuba
fulani.
Mfano: Jua kali ni wasakatonge.
Wao ni wengi ulimwenguni
Tabaka lisilo ahueni
Siku zote wako matesoni
Ziada ya pato hawaoni
Lakini watakomboka lini?
(Wasakatonge 2004:5)
h) Mtindo ambao
unaruhusu kipande kizima cha mstari wa mwisho wa ubeti kuweza kurudiwa, kikiwa
ni chanzo cha huo ubeti unaofuata:-
Iwapo
mstari wa mwisho wa ubeti wa kwanza ulikuwa kama “Uwanjani nayanena, leo wote
wataona” Basi ule mstari wa kwanza na ubeti wa pili utaanza na “leo wote
wataona”
Mfano: Chochote ulichonacho, kilikuwa kwa
mwenzako,
Leo yeye hako nacho, kimesha hamia kwako,
Huenda utokwe nacho, kiende kwa mwingine huko,
Kiumbe wacha vituko, sione ulichonacho.
Sione ulichonacho, ukaendesha vituko,
Na upambwe chokochoko, mwishowe ni
pukutiko,
Malao akupambacho, kilipambiwa mwenzako
Kiumbe wacha vituko,sione ulichonacho.
(Sheria za kutungo mashairi na Diwani
ya Amri 1967:30)
Kimsingi mitindo katika ushairi ni mingi sana na
hutegemea ufundi wa mshairi katika kuunda mashairi yake na ushair unaweza kuwa
wa kimapokeo au wa kisasa.
ii) Miundo ya Mashairi
Muundo ni neno pana ambalo hujumlisha mjengo wa shairi
yaani jinsi ulionekana.Mashairi yana mundo mbalimbali kutegemea ufundi wa
mshairi mwenyewe kimsingi Shairi linaweza kuwa la kimapokeo au likawa Shairi
huni (kisasa) Shairi la kimapokeo huwa na mpangilio maalumu wa vina na mizani,
silabi, vituo, beti n.k.Idadi ya mistari huzaa aina mbalimbali za mashairi.
a) Muundo wa
Tarbia
Kila
ubeti wa shairi huwa na mistari mine na kila mstari huwa na mizani kumi na sita
(16) vile vile katika muundo huu kila mstari unakua umegawanika katika viande
viwili vilivyo na mizani sawa kila kipande kukiwa na mizani nane.
Mfano: Amkeni kumekucha, wakubwa hata wadogo,
Wadoho siku waacha, kwa kuogopa kinyongo,
Kinyongo sikuficha, kukificha ni uongo,
Mnapowacha madogo, na makubwa mtawaacha.
Na wakubwa mtawaacha, mnapoacha madogo,
Mfano kama kuchacha, chakula japo kidogo,
Kidogo kinapochacha, kikubwa hakina kingo,
Mnapowacha madogo, na wakubwa mtawaacha.
(Masahiri ya Saadani 1972:25)
b) Muundo wa
Tathnia
Kila
ubeti wa shairi huwa na mistari miwili muundo huu unatiwa zaidi katika nyimbo
si muundo ambao hutumika sana katika mashairi ya kawaida ya kusomwa kam
mashairi au ya kuimbiwa.
Mfano: Mjamzito, umelazwa “Thieta”
Lazima kupasuliwa
Chake kitoto tumbo kinatweta
Hawezi kujifungua
Mwili u moto, tumbo linamkeketa
Kwa kite anaunguwa
Jasho na Joto, kiungo cha mpwita
Na mauti yanamwita
Ni jambo zito, daktari kufata
Wauguzi waameitwa
(Fungate
la uhuru 1988:08)
c) Muundo wa
Tathilitha
Kila
ubeti wa shairi unakuwa na mistari mitatu
Mfano: Kujitawala si kwema, kuliko kutawaliwa,
Kujitawala ni umma, kila yao kuamua,
Kujitawala si kama, wanguzi na rushwa.
Kujitawala khatamu, na umma kushikiliwa,
Kujitawala hukumu, makosa kushitakiwa,
Kujitawala si sumu, mara kwa mara kuuwa.
Kujitawala kisomo, kupiga kubwa hatua,
Kujitawala kilimo, njaa na kuondoa,
Kujitawala si somo, njiani kusimuliwa.
d) Muundo wa
Takhimisa
Kila
ubeti wa shairi unakuwa na mistari, mitano
Mfano: Hao nyani wanaruka, mara hapa mara kule,
Hao nyani wanabweka, hawaoni soga mbele,
Hao nyani wanaanguka, waingiwa na ndwele,
Nyani wanababaika,misitu una upele
Msitu haukaliki, nyani wanahangaika.
Msitu wawaka moto, kufukuzwa hao nyani,
Umeligundua pato, la nyani lenye utani,
Moto waziona kwato, zilizoko mapangoni,
Nyani watupa watoto, hawakubaliki mwituni
Msitu haukaliki, Nyani wanahangaika.
e) Muundo wa
Sabilia
Katika
muundo huu mtunzi au mshairi anakuwa na uhuru wa kuweka zaidi ya mistari mitano
katika kila ubeti, ubeti unakuwa na mistari sita na kuendelea
Mfano: Mmea unapokuwa, huifurahisha mvua.
Lakini siposogea, hulisingizia jua
Uliamini ni mola, hata maji kukupatia
Ulikubali kabila, haliishi bila mila
Mwanadamu kadhalika, kukua
kufurahika
Huupenda uhakika, wa nyota yake kufika
Umri wa kuridhisha, huhitaji kujitwisha
Hapa, ukiufikisha, huona, kufanikiwa
Maisha ya hupenda, ni, mazuri ya kwenda
Na siyo yenye kupinda, haya daima hupenda
(Diwani ya Mloka 2002:18)
f) Muundo wa mistari
mine
Muundo
huu unaweza kuwa na mizani nane au pungufu.Muundo huu ni wa Abdilatifu Abdalla
(1973) mfano ametumia katika mashairi yake ya “Kamili wazi” “mnazi” “Jana na leo na kesho” na “Njia panda” mara nyingi huo mstari wa
mwisho kina chake huwa ni sawa na kina cha mwisho wa mstari mwingine katika
ubeti wao
Mfano: Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika.
Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika
Kimeingoa mibuyu, minazi kunusurika
Nyoyo zilifadhaika
(Kimbunga 1995:01)
iii) Matumizi ya Lugha.
Hiki ni kipengele muhimu sana katika kazi yeyote ile
ya Sanaa ya kifasihi. Matumizi ya Lugha ndiyo yanayofanya kazi fulani ionekane
tofauti na nyingine au itofautishe kazi ya Sanaa ya kifasihi na ile isiyo ya
kifasihi.Luha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi kwani fasihi ni kazi ya Sanaa
inayotoa maudhui ya kutumia Lugha ya maneno.Matumizi ya Lugha katika kazi ya
fasihi yako ya aina mbalimbali
a) Methali,
misemo na nahau
Mhakiki
anapaswa avifahamu na ajue kuvichambua katika ushairi.Vipengele hivyo vina kazi
ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi
METHALI
Ni
kazi ya Sanaa ya kifasihi inayotumia mafumbo kwa kwaida semi zote zina hakima
ndani yake.Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha hali ambapo methali
hutumika.Methali pia ina kazi ya kufurahisha, kutisha, kuonya nakadhalika,
waandishi hutumia methali katika kazi zao nani jukumu la mhakiki kuzitambua
hizo
MISEMO NA NAHAU
Matumizi
ya misemo na nahau hushabihana na yale ya methali.Misemo, misimu na nahau
huzaliwa, hukua nap engine hufa
-Sekela amenipaka mafuta kwa mgongo wa
chupa (sekela amenipa sifa zilizostahili)
-Juma katutangulia (Juma amekufa)
b) Tamathali za
Semi
Mulokozi & Kahigi wanasema kuwa tamathali za semi
ni maneno, nahau au semi ambazo hutumiwa [H1] na
waandishi wa fasihi ili kutia nguvu na msisitizo katika maana, mtindo, na
pengine sauti katika maandishi hayo.Tamathali za semi zinatumiwa pia [H2] kuipamba
kazi ya Sanaa ya kifasihi kwa kuongeza utamu wa Lugha.
Baadhi ya tamathali za semi ni:-
Ø Tashbiha
Hii ni
tamathali ya ufananisha au mlinganisha wa vitu viwili au zaidi katika tashbiha
kama ilivyo katika sitiari huwa kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo
wataalamu wameviita kuzungumzwa, kufananisha na kiungo.Katika tashbiha hakuna
maana dhahania bali kuna ulinganishaji wa vitu viwili vilivyobayana.
Mfano: Kweli ni sawa na radi, inapotoa kauli…
Kweli kinywnani ikiwa sawa na moto wa
nili
Kweli kama msumeno hukoreza sawa kweli
Ø Tashhisi
(uhaishaji)
Washairi
mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa na uhai sifa za kitu chenye uhai,
hasa sifa za binadamu, kisanaa maelezo ya kitashhisi huwa na upekee unaomwingia
msomaji akilini haraka, kwani si jambo a kawaida, mathalani kuona mti
“Ukimpungia mtu mkono” au “nyumba ikimkodolea macho mgeni”
Mfano: kimya hakineni jambo si kimya chawatazama…
Kimya chajazua mambo, pasiwe mwenye kusema.
Kimya kipimeni sana, msione kutosema.
Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama.
Kimya chaja watukana, na kizuwe yalozama.
Katika
ubeti huu “kimya” (ambayo ni nomino dhahania) kimepewa sifa za binadamu
kinaweza kunena, kutazama, kuzua mambo, kusimama na kutukana.
Ø Metonumia
Hii
ni tamathali inayotumia neno (au semi) kuwakilisha neno, kitu, mtu au dhana
nyingine yenye kuhusiana nalo neno hilo huweza kutumiwa kwa kuwa dhana
inayozungumziwa au kwa kuwa linataja ktu ambacho ni sehemu na kuwakilisha cha
kitu kingine kikubwa zaidi.
Mfano
neno “kitambi” huweza kutumiwa kuwakilisha tajiri au kabila “meno” huweza
kuwakilisha kicheko
Ø Mubalagha
Ni
matumizi ya lugha yaliyotiwa chumvi ili kuongeza utamu na kuleta athari fulani
katika ushairi wa majigambo, tamathili hii hutumika sana maana huo ni ushairi
wa kujitapa na mtu mwenye kujitapa aghalabu hujilimbikizia sifa. Mara nyingi
mubalagha hutumika katika tenzi zenye kusimulia habari za mashujaa.
Mfano:
katika utenzi wa fumo Lyongo kuna mfano unaokusudiwa kuonyesha ukubwa wa (kimo
na umbo) na nguvu za Lyongo.
“Ruhu zikienda kishindo
Zima zao hukoma ondo
Huyo ni bwana wa kondo
Ashindaye jeshi miya
Ingawa
wagala wanajulikana kuwa ni watu warefu akini vimo vyao vilifika magotini tu
(ondo) pia Lyongo
Ø Kejeli
Ni
usemi ambao maana ya ndani ni kinyume cha maanayake halisi. Ni usemi wa kebehi
ambamo kisemwacho na msemaji. Pia kejeli ni tukio ambalo ni kinyume cha lile
linatazamiwa au lililotakiwa na ambalo kutokea kwake huwa ni namna ya dhihaka
Katika
shairi la “Ibada na Haki” Shabaan Robert anatumia usemi wa kejeli kukebehi watu
wanothamini fedha kuliko dini.
Anasema
hivi: Huifanya fedha mungu wao
Itazame adha na Imani yao!
Na mwenye akili kama hana fedha
Hatajwi mahali ila kwa rakadha
Na kuadhiriwa kuwa mtu chini,
Tazama dunia ilivyo na dini
Katika
mstari wa pili “Itazame adha na Imani yako!” kuna kejeli, mshairi anachotaka
kutuambia ni kwamba watu hao hawana adha wala Imani katika mstariwa mwisho
“Tazama dunia ilivyo na dini” Anakusudia kutuambia
“Tazama
dunia ilivyo na dini kwa hiyo semi hizo ni kejeli kinachosemwa ni kinyume na
maana yake halisi kadha toka alama za mshangao!) zimetumika kusisitiza hali ya
kejeli.
MBINU
ZA KISANAA
Kuna mbinu mbalimbali za kisanaa ambazo hutumika
katika kazi za kifasihi ya ushairi na ambazo mhakiki atatakiwa azitambue na
kuzifafanua mbinu hizo ni kama vile
Ø Takriri
Ni kurudia rudia neno, sauti, herufi au wazo katika
kazi ya Sanaa ya kifasihi.
Mfano: kweli kito mhabubu, mwenyezi nijaze kweli
Kweli siri ya ajabu, huwapa watu fadhili
Kweli chimbo la johari, linahimili la kweli
Kweli inatafakari, husema na kujadili
Katika ubeti huu neno “kweli” limerudiwa rudiwa. Neno
hili linasisitiza wazo kuu la mwandishi
Ø Onomatopea
Ni mwigo wa sauti. Hutumiwa na washairi kutoa picha au
dhana ya kile kinachowakilishwa au kupambanuliwa na sauti hizo. Mfano tukisema
“maji yalimwagika mwaaa!” neno mwaaa! Ni onomatopea linawakilisha sauti au
kishindo cha maji yanayomwagika. Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa
sehemu za msamiati wa kawaida. Mfano: pikipiki, bomboni, kata n.k.
Katika shairi la “Cheke kwa furaha” Shabaan Robert
ametumia onomatopea ili kuleta dhana ya kucheka
“Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha! ha! Ndiyo ada duniani
Basi cheka kwa! kwa! kwa! Usafike moyo
wote
Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko
Maneno ha! ha! ha! na kwa! kwa! kwa! Ni onomatopea yanayotoa sauti ya kusikika ya
sauti ya mtu anayecheka. Huu ni mpangilio maalumu wa sauti ili kutoa picha ya
kusikika ya dhana inayozungumzwa
Ø Mjalizo
Ni kuunganisha maneno yanayofwatana bila kutumia viunganishi
mfano: bila kutumia “na, kwa” n.k. Mfano:
Nilikaa, nikashangaa, nikachoka
Niliimba, nikanuna, nikacheka
Ø Mdokezo
Hii ni mbinu ya kisanaa ambapo mwandishi anaukatiza
usemi fulani na kumuacha msomaji. Aghalabu pana vielekezi vinavyoweza kumsaidia
msomaji katika kukamilisha.
Mfano: wimbo
la mauaji limezidi
Mashaka…ah! Shida tupu
Maneno…tena anyway…
Labda tusubiri.
Ø Tashtiti
Ni matumizi ya maswali ambayo majibu yake kwa kawaida
yanakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa kwa
ajili ya msisitizo tu au mshangao.
Mfano: Mtu
anayemfahamu amekufa anauliza
-Adela ameachana nami?
Au mtu
anayemfahamu amekutembelea
- Jamani hata Luiza naye kaja?
-Aisee ni wewe?
Ø Usambamba
Ni takriri ya sentensi au kifungu vya maneno vyenye
kufanana kimaana au kimuundo. Usambamba huonekena sana katika ushairi simulizi
Shabaan Robert amekitumia kipengele hiki mara kwa mara
atika mashairi yake katika shairi lake “kinyume” anasema
Tulifululiza
mwendo lakini sana twasita
Tulikwenda
kwa mshindo lakini sana twanyata
Katika mistari yote miwili wazo linalosisitiza ni moja
maneno tu ndiyo yanabadilika uwezo wao wa zamani katika utendaji mambo
unalinganishwa na udhaifu “wao” wa sasa.
c) Taswira au
Picha
Dhana hii hutumiwa kueleza neno, kirai au maelezo
ambayo yanaunda picha fulani katika akili ya msomaji. Taswira zinaweza kuwa za
kimaelezo (yaani maelezo fulani yanaunda picha) au za ki-ishara (zinazounda
picha ambayo inaashiria jambo fulani au imeficha ujumbe mwingine). Taswira
huweza kuundwakwa matumizi ya tamathali za semi hasa tashbiha na sitiari.
Kimsingi taswira nyingi ni taswira za uoni (yaani
zinamchochea msomaji kuona picha fulani)
Mfano: Neno
lenye mzunguko, halipatikani mwisho,
Wa huku
hafiki huko,wala halina matisha.
Halishibishi huchosha, wala hapati utuvu,
Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka.
Na milima akapanda, apendako akafika,
Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dinani
Hupati kupenda bara, na hushuki baharini
Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia
Katika shairi hili tunapewa picha tatu mahususi picha
ya kwanza ni neno linalozunguka mshairi anatuambia kuwa neno ambalo halifuati
njia iliyonyooka neno lenye mzunguko halifiki mwisho wake na halileti mradi
uliokusudiwa “Halina malisho”
Hapa neno limefanya kuwa kitu chenye uwezo wa kutembea
na kuzunguka
Picha ya pili ni ya mtu aendaye safari ngumu kwa
ujasiri na moyo wa dhati akipanda milima na kushuka na mabonde akipenya misitu
na kuvuka mito hadi kufika kule anapokwenda. Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo
anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu, alimradi anajua kuwa itamfikisha kwenye
lengo lake. Ni mtu anayepamana na matatizo badala ya kuyakimbia mtu wa kwenda
njia iliyonyooka
Piha ya tatu ni dira, dira ni chombo kitumiwacho na
mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha majira yao, wasipotee njia. Dira ni
chombo cha mviringo na mshale wake aghalabu huzungukia palepale ulipo, katu
hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo la mwandishi kuwa njia yenye
kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye lengolake. Mshale wa dira huzunguka
daima lakini haufiki kokote.
Picha hizi tatu kwa pamoja zimefaulu kufikisha ujumbe
wa mwandishi kuhusu maisha na namna ya kuyakabili tuyakabili kwa juhudi na
ujasiri na nia.
JINA LA
KITABU
Jina la kitabu ni vyema liwiane na yale yaliyomo ndani
ya kitabu hicho. Mfano: “Fungate la uhuru” (1988) jina hili linawiana vipi na
yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?
PICHA YA
JALADA KATIKA UCHAMBUZI
Kazi ya kifasihi kuwa na picha au michoro fulani
kwenye majalada yao. Inawezekana majalada hayo yakawa na uhusiano fulani na
dhamira na maudhui ya kazi zinazohusika. Picha hizi huweza kuwa kielelezo
muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi. Hata hivyo si kazi zote
za kifasihi ambazo zinaonyesha uwiano kati ya majalada yake na yaliyomo.
UHAKIKI WA
VIPENGELE VYA MAUDHUI
Maudhui katika mashairi hupatikana baada ya mhakiki
kupitia beti zote za shairi lile ili kupata ujumbe wa shairi lazima itambidi mhakiki
ajumlishe yaliyo katika beti mbalimbali za shairi lile.
Kwa ufupi katika ushairi uchambuzi wa maudhui mhakiki
anapaswa kuangalia:
Ø DHAMIRA
Ni wazo kuu katika kazi ya fasihi.
Ø UJUMBE
Ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya
kusoma kazifulani ya fasihi.
Ø FALSAFA YA
MWANDISHI
Ni wazo ambalo mtu anaamini lina ukweli fulani
unaitawala maisha yake.
Ø MSIMAMO WA
MWANDISHI
Ni hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia
jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na wengi, lakini yeye
atalishikilia tu.
Ø MTAZAMO WA
MWANDISHI
Ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia
mazingira aliyonayo msanii mwenyewe
HATUA ZA
UCHAMBUZI WA USHAIRI
Katika uchambuzi huu wa vitendo, kielelezo tutatumia
shairi la “Wauwaji wa Albino wapigwe vita” Shairi hilo linasema hivi:
Kwa kweli inashangaza, ni mambo hufikirika,
Ukijaribu kuwaza, wenzetu wanatutukana
Albino wanaweza, kifo kimeshawafikia
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Ni unyama wa kuzidi, albino kuwashika
Huu wote ni ukaidi, utajiri kuusaka
Tena ni kwa makusudi, maovu umeyashika
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Mikononi wanawakata, kwa mashoka na mapanga
Kuwasema sita sita, huu wote ni ujinga
Kwa vitisho wajikita, kusikiliza waganga
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Albino tuwalinde, wamekuwa almasi
Wasakwa kila upande, sababu ya ibilisi
Yatupasa tuwalinde, binadamu kama sisi
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Majumba kuyabomoa, pande zote kuzunguka
Damu isiyo hatia, kwa wingi inamwagika
Mola inamlilia, hukumu ipo hakika
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Albino ni wenzetu, uzao wao ni halisi
Acha tofauti zetu, tena tuwape nafasi
Tujenge taifa letu, tuuache ukakasi
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Ujinga na upumbavu, kuwaua albino
Wajawa maumivu, mikono na visigino
Sahitaji utulivu, upole mshikamano
Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.
Zamu yako inakuja, mwisho wao utafika
Wenyewe watajitaja, tena bila ya mashaka
Sote tuwe na umoja, kufungua mashtaka
Kuwasaka wauwaji, kusudi wahukumiwe.
HATUA ZA
KUCHAMBUA SHAIRI
1.
Lisome shairi
zima toka manzo hadi mwisho ili upate picha ya jumla, kimaana na kiumbo ya
shairi hilo. Katika hatua hii kama shairi ni gumu linaweza lisieleweke, kwa
bahati shairi la “wauwaji wa albino wapigwe vita” linaeleweka bila tatizo
2.
Rudia kulisoma
tena shairi hilo polepole, andika maana ya jumla unayoipata. Unaweza kupata
maana zaidi ya moja katika “Wauwaji wa albino wapigwe vita” maana ya jumla
inayojitokeza ni maombolezo ya mauwaji ya Albino
3.
Huku ukiwa na
kalamu yako ya risasi, rudia kulisoma tena shairi hilo mstari baada ya mstari.
Pigia kila neno usemi, sentensi au kipengele kinachoelekea kuwa na umuhimu au
dhima maalumu ya kifani au kimaudhui.
Katika shairi ili pengine utayapigie mstari mafungu ya
maneno yafuatayo:
-Albino
wanaweza kifo kimeshawafikia
-Ni
wauwaji wabaya vikali walaaniwe
-wasakwa
kila upande sababu ya ibilisi
-damu
isiyo hatia kwa wingi inamwagika
-Albino
ni wenzetu uzao wao ni halisi
4.
Jaribu kufanya
kisisisi maneno hayo yalyopigiwa mstari au kuorodheshwa katika hatua ya tatu bila
shaka yapo mambo ambayo undani wake hutauelewa katika hatua hii, hivyo aghalabu
itabidi
a)
Urejee mambo hayo
yalivyotumika
b) Urejee katika muktadha wa shairi hilo kama una ufahamu
kwa upande wa wauwaji wa Albino wapigwe vita, muktadha huo ni mauaji ya Albino
Jiulize semi, sentesi hizi zinasema/zinaonyesha au
zinadokeza nini? Kwa nini mtunzi kaamua kutumia maneno hayo na si mengine? Je
yanahusiana vipi na maana ya jumla uliyopata katika hatua ya pili.
5.
Chunguza
vipengele vingine vya kisanaa na kimuundo alivyovitumia mtunzi. Jiulize kama
vinaoana na madokezo ya maana uliyoyapata katika hatua ya nne. Vipengele
unavyoweza kuchunguza katika hatua hii ni muundo wa shairi, vina, mizani,
wizani, takriri, milio ya maneno, tamathali n.k. kwa mfano hadhihirika kuwa
muundo wa shairi ni kijadi ambao hautuambii lolote kuhusu maana ya shairi hili
vifanye uchambuzi vipengele vya kisanaa ulivyovipambanua
6.
Husisha ufafanuzi
wake hadi hatua hiina maana ya shairi iliyokwisha kujitokeza kuona kama mambo
hayo yanaoana barabara au bado kuna pengo au mkinzano.
Baada ya hatua hii utakuwa umepata maana kamili ya
shairi ambayo unaweza kuitetea kifasihi kwa kurejea katika shairi lenyewe si
lazima maana unayopata/unazopata ioane/zioane na maana watakazopata wengine
jambo muhimu ni kuwa na ushahidi wa kutosha kuweza kutetea hoja zako.
Maana ambayo umepata hadi sasa yaweza kuelezwa iwe:
Mshairi anaomboleza mauaji ya Albino ambayo yanafanywa
na watu mbalimbali kwa Imani za
kishirikina anaonyesha kuwa kuua binadamu wenzetu ni unyama na ni ukatili.
Anamwomba Mungu awaepushie Albino na mates ohayo.
7.
Hadi hatua
hii umepata maana ya shairi lakini bado hujapata maudhui yake. Ili kupata maudhui unatakiwa upambanue dhamir kuu
ya/za shairi hili na uonyeshe mtazamo wa mshairi kuhusu dhamira hizo. Katika
shairi hili ni dhahiri dhamira kuu ni “Mauaji ya Albino” mtunzi anasawiri tukio
la mauaji ya Albino mwandishi anaonyesha kuwa mauaji ya albino ni tukio lenye
kuleta majonzi na kilio. Mtazamo wake kuhusu mauaji ya Albino ni kwamba
wanaofanya hivyo hawana utu hivyo ni sawa na wanyama wa porini na anaonyesha
kuwa kuwaua albino ni kinyume cha utu
Mtunzi anazungumzia pia dhamira ya ujinga. Mwandishi
anaonyesha kuwa ujinga ni kikwazo cha maendeleo ya jamii kwani wote
wanaojihusisha na mauaji ya albino ni wajinga na wanataka kupata utajiri kwa
njia za mkato.
8.
Katika hatua
hii mchambuzi ana uhuru wa kuithamini kusifu au kwaani. Baada ya kulichambua na kulielewa vizuri shairi hilo
katika hatua saba zilizotangulia sasa unaweza kulitolea tathmini ya kifani na
kimaudhui katika kufanya tathmini ni muhimu kuzingatia muktadha wa wakati
lilipotungwa na wakati wa leo.
Tathmini yako itazingatia muktadha yote miwili unaweza
kusema kuwa, shairi hilo lilipotungwa ulikuwa na umuhimu wake leo labda
umepungua kwa kuwa muktadha huo wa vifo vya Albino umepita. Hata hivyo labda
shairi limebaki na umuhimu wa kihisia na kifalsafa kuhusu tatizo la maisha na
mauti na ufumbuzi wake.
HISTORIA NA
MAENDELEO YA KISHAIRI WA KISWAHILI
Wataalamu wengi wanakubali kuwa ushairi wa Kiswahili
ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo. Kabla ya karne ya 10 BK ushairi wa
Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kugharura kwa ghibu bila kuandikwa.
Kuanzia mwaka 1000 B, mambo mawili yaliletwa na
kuathiri ushairi, mambo hayo ni Dini ya kiislamu na Uandishi wa hati ya kiarabu
waswahili wengi walijifunza kusoma na kuandika hati za kiarabu, hali hiyo ilienda
sambamba na ustawi wa miji ya Pwani katika biashara na majengo ya mawe mashujaa
mashuhuri wa miji ya Pwani wanokumbukwa katika tendi na masimulizihuenda
waliishi katika hicho ni Fumo Lyongo wa Shangapate kaskazini mwa upwa wa Kenya
kati ya karne ya 8 na 9
Katika kipindi hiko washairi wengi walitunga mashairi
mengi kwa ghiba kwa sababu hayakukusudiwa kuhifadhiwa kwa maandishi kwa kipindi
kirefu ni tarihi na baadhi ya mswada hiyo imepotea. Tungo zilizosalia ni Fumo
Lyongo ambayo ilandikwa 1500 BK kutoka katika mapokeo ya mdomo.
-“kumswifu” yanga au suifa ya mwana ning utingo wa
mwanzo kuhifadhiwa kwa maandishi.
Mwaka 1500-1700 BK kulikuwa ni kipindi cha uvamizi wa
maneno katika kipindi hicho tungo chache zilihifadhiwa zikiwasifia maneno
mashairi yaliyo wasifia wareno> mfano
-mzungu
mgeli} 1630
-Portugezi
Afala} 1630
Lakini tungo mashuhuri za wakati huo ni:
· Utendi wa Hamziyya (Seyyid Aidamis bin Athumani 1652)
· Siri lasirari (Binti Lamba 1668)
· Utendi wa Tambika (Taboka) {Mwango bin Athumani 1728}
· Siri Lasirari ni kisa cha kubuni
· Hamliyya ni tafsiri ya utendi wa kiarabu kuhusu maisha
ya Mtume Muhamadi
· Tabuta (tambuka) ulihusu vita kati ya waislamu na
warumi walikuwa chini ya mfalme Hela kali
1750-1900
kipindi cha waarabu
Sehemu kubwa za tendi mashuhuri za wakati ambazo mpaka
leo zipo ni:
· Tendi za
dini na vitu
-
Utenzi wa Shufaka
-
Utenzi wa
masahibu
-
Utenzi wa kijamaa
-
Utenzi wa mayasa
na mikidadi
-
Utenzi wa Ras L
Ghuli (unahusu vita vya waarabu kati ya waislam na makafiri-{1855})
· Tungo za
kitamaduni, mawaidha na Tumbuiza
Tungo
hizi zilikuwa nyingi na zilikuwa katika maandishi na zilihusu (maudhui yake)
kueleza mandhari ya Afrika Mashariki mfano tungo hizi ni:
-
Utenzi wa Inkishafi (1810)
Mtunzi: Seyyid Abdallah bin Nasri.
Utenzi
huu unazungumzia matokeo ya uvamizi wa waarabu na wareno ambapo matokeo yake ni
kuporomoka kwa mji wa Pate.
-
Utenzi wa Mwana kupona (1858)
Unahusu
utamaduni na misingi ya Dini. Utenzi huu uliandikwa kama wosia kwa binti yake
na kwa kiasi kikubwa unahusu unyumba pia ndani yake kuna mafundisho ya unyago
kwa watu wa Pwani.
Kundi jingine kubwa ni mashairi ya siasa kundi hili
liliwakilisha/lilisimamiwa na akina Muyaka bin Haji wa Mombasa. Huyo alitunga
mashairi ya kupinga waarabu wa Oman mfano;Suid
bin Said (1810-1876),Kibabina (1776-1834) na wengine.
Wote hawa walitunga mashairi yaliyohusu harakati za
kisiasa na kijamii za wakati huo, wa baadhi yao walifungwa au kuuwawa gerezani
kwa sababu ya kupinga kutawaliwa. Mchango mkubwa wa hawa ni kuendeleza mashairi
ya unne (tarbia)
Kwa ujumla katika kipindi hiki mambo yaliyojitokeza
katika maendelezo ya ushairi ni manne:
i)
Umbo la tarbia
(unne) ulifika kilele
ii)
Utendi
iii)
Kanuni ya utunzi
ziliwekwa wakati huo
iv)Hati
ya maandishi (Kiswahili n kiarabu) ilisanifiwa kuzingatia sauti za lugha ya
Kiswahili.
1885-1918
USHAIRI WAKATI WA UKOLONI WA KIJERUMANI
Ushairi wa wakati huo unaweza kugawanyika katika
makundi matatu.
i)
Ushairi wa
kawaida-mashairi haya yalihusu mawaidha, mapenzi na dini.
ii)
Ushairi wakusifu
wakoloni- huu uliandikwa kwenye magazeti na vitabu mfano kitabu maarufu cha Dr.
C
Velter (1907) Prose and Poesie der Sua heli
Kitabu hiki kilisifu utawala wa kidachi
iii)
Ushairi wa
upinzani.
Huu ulipinga utawala wa kikoloni.
Mfano: utenzi wa vita vya wadachi (H.Abdallah)
Utenzi
wa vita vya majimaji
Katika kipindi hiki mambo matatu yalitokea katika
ushairi kwa upande wa Tanzania.
a.
Kuandika kwa
kutumia hati ya kirumi hati hii ulienea kwa kupitia Elimu kanisa na ilianza
kutumiwa na watunzi baada ya hati ya kirabu
b.
Utafiti kuhusu
ushairi ulianza wakati huo na wachambuzi maarufu walikuwa C.Velter Buttner na
K.Mein holf n.k
Hawa
walisaidiwa na waafrika kama vile Mohamed Kajunwa, utenzi wa Fumo Lyongo
Rev.Taylor ndiye aliyekusanya mashairi ya Fumo Lyongo.
1918-1961
UKOLONI WA KIINGEREZA
Kipindi hiki kiliambatana na mambo matatu mapya:-
a) Elimu .Hii ilieneza lugha ya Kiswahili na ushairi katika
maeneo ya bara kupitia shuleni maarifa ya kusoma na kuandika. Hati ya maandishi
ya kirumi ilienea kupitia elimu
b) Kuanzishwa
kwa mashirika ya uchapishwaji.Katika
kipindi hiki magazeti mengi yalichapwa kwa lugha ya Kiswahili na kusambazwa.
Baadhi ya magazeti yalikuwa na kurasa maalumu ya ushairi ambapo ulisaidia
kuwakutanisha watunzi kutoka Afrika Mashariki.
Mfano: Gazeti la “Mambo leo” 1923 kupitia gazeti hilo
watunzi maarufu kama S.Robert, Mdanzi Hamasa, Mzee Waziri (kijana) walipata
umaarufu kupitia mambo leo
Pia kuanzishwa kwa shirika la wachapishaji vitabu
Afrika Mashariki (E.A.L.B) kulisaidia sana kukuza na kueneza Sanaa ya ushairi.
c) Shughuli za
siasa za kudai Uhuru ziliibua ushairi
wa kisiasa mnamo mwaka 1950-1960.
Mfano: S.Kandoro alitunga mashairi mengi pia kipindi
hicho ushairi ulikuwa wa aina.
1.
Mashairi
yaliyosaili mfumo wa uchumi wa kikoloni. Matatizo ya kazi, umanamba, mshahara
mdogo n.k haya yote yalitolewa na gazeti la mamba leo.
2.
Mashairi
yaliyohusu utaifa yalianza miaka 1930. Haya yalijiuliza mwafrika ni nani? kwa
nini mzungu yupo hapa?
Mfano:
S.Robert- mashairi ya kutetea weusi mfano Shairi la Rangi zetu,S.Kandoro
kwetu ni kwao kwa nini
Pia kulikuwa na
mashairi ya kutetea Lugha mfano S.Robert
(Titi la mama li Tamu) S.Kandoro
(Kitumie Kiswahili)
3.
Mashairi ya
kisiasa ambayo yalihimiza watu waungane ili waweze kujitawala wenyewe S.Kandoro
shairi la siafu wamekazana
4.
Pia kipindi hiki
walitokea wachunguzi wengi sana wa ushairi wa Kiswahili.
Mfano: Withchens (1930), A.Wine, B.E.Damman (1930-50)
Lumbart, H.Cory W.Whitely n.k. “wazungu”. Waafrika Sr. Mbarak Hisway, Hamis
Kitumbey
USHAIRI BAADA YA UHURU
Baada ya uhuru ushairi ulisambaa zaidi kutokana na
msukumo wa kisiasa fani mpya mfano Ngonjera na mtiririko au tungo huru
zilizanziashwa ili kuzingatia mahitaji mapya ya kisiasa na kisanaa. Ushairi wa
Kiswahili baada ya uhuru ulikuwa wa aina kuu mbili
1.
Mashairi ya kawaida: Haya yalitungwa sana magazetini na vitabu vya mashairi mbalimbali
vilichapishwa ambapo Dhamira za malezi, mapenzi , dini, mawaidha n.k.
o Akilimali snow- white
o Mwinyi khatibu- Mohamed
o Andanenga
o S.Kandoro
o S.Robert
2.
Mashairi ya kisiasa: Hapa kuna makundi mbalimbali ya mashairi ya
kushangilia Uhuru.
Mfano:
Utenzi wa uhuru wa Tanganyika
Utenzi wa jamhuri wa Tanzania
Utenzi wa uhuru wa Kenya.
a)
Mashairi yanayojadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya. Katika mashairi yao walisisitiza watu wafanye kazi ili
kuinua pato.
Mfano: S.Kandoro katika shairi la kujitawala
J.K.Nyerere-chombo
cha taifa letu
b) Mashairi ya
Ujamaa
Hayo yalitokea baada ya Azimio la Arusha ambalo
yalisisitiza siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambapo walipinga unyonyaji, ukupe,
ukabila na ubepari. Walitukuza kilimo na kuwashawishi watu kurudi shamba
(kijijini)
Mfano: Mashairi ya Azimio la Arusha (kamaji), Ngonjera
za Matias Mnyapara, Mashairi ya miaka 10 ya Azimio la Arusha ( Abdulah)
Tatizo kubwa lilijitokeza katika hiki ni ukasuku ambapo
waandishi wengi walikariri hotuba za viongozi bila kuzifanyia uchambuzi na
kuziandikia mashairi.
c)
Mashairi yaliyohakikii siasa yaliyokuwepo na hawa
walikuwa na mitazamo mbalimbali.
· Wanauhalisia
Walihakiki
dhana ya ujamaa na ukombozi na kuchambua mafanikio ya matatizo yake hasa katika
utekelezaji wa malengo ya Azimio la Arusha. Waandishi hao ni E.Kezilahabi,
E.Husein, Z.Mochiwa na T.A.Mvungi.
· Washairi wa
Malengo wa kushoto
Hawa
walikuwa na mambo yafuatayo walichukua msimamo wa kufanya kazi na mkabala wa
kitabaka katika kutolea tungo zao
· Waliona
usoshalist kama suluhisho la matatizo yao.
Ili
usoshalist upatikane waliona ni lazima kumwaga damu (kutumia nguvu). Kundi hili
lilikuw na K.Kahigi, na M.Mulokozi, Ally Salehe, M.S.Khatibu, A.Abdullah na
S.A.Mohamed.
Hivyo
Sanaa hii ambayo ilianza upwa wa Kenya na Tanzania katika kare ya 10-15 sasa
imeenea Afrika Mashariki nzima hadi Rwanda, Burundi na Kongo
MGOGORO KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI
Mgogogro huu ulianza mwisho mwa miaka ya sitini (1968)
na mwanzoni mwa miaka ya sabini. Mgogoro ulihusisha pande mbili washairi wa
kimapokeo (wasiokubali mabadiliko hawa walisisitiza kuwa vina na mizani ni uti
wa mgongo wa shairi la Kiswahili) wanamabadiliko waliona kuwa si lazima shairi
liwe na vina na mizani.
Sababu kuu zilizozua utata ni mbili
i.
Maana ushairi kwa
ujumla
ii.
Maana ya shairi
la Kiswahili
Mvutano huu unahusisha na mabadiliko ya kidunia
yaliyotokea miaka ya Sitiari na Sabini katika Nyanja mbalimbali za maisha hata
kupelekea washairi nao kuhitaji mabadiliko katika tasnia ya ushairi kwa upande
wa fani
Msukumo huu wa kuleta mabadiliko katika tasnia ya
ushairi uliletwa na wanazuoni akina E.Kezilabahi, Jared Angira na E.Husein
wasomi hawa walijishughulisha na utunzi wa mashairi hivyo baada ya kusoma
fasihi za nchi mbalimbali waligundua kuwa vina na mizani ni wazo zilizofuatwa
na washauri wote duniani hivyo waliamua kuasi sharia hizo ili kuleta mabadiliko
ya kuondoa minyororo iliyowafunga kuhusu utungaji wa shairi la Kiswahili kwa
pamoja waandishi hawa waliweza kutunga mashairi mengi au tungo zisizofuata
niaza ya vina na mizani na pia waliungwa mkono na watunzi wengi kama vile
M.M.Mulokozi, K.K.Kahigi miaka ya themanini washairi wengi waliibuka kuungana
na kundi hilo. Mfano: Henry MhanikanaT.Mvungi
Madai ya wana mabadiliko kutunga tungo zao yalikuwa
kama ifuatavyo:
1.
Mbinu na njia za
kutunga mashairi ya Kiswahili zilikuwa chache mno.
2.
Kutunga kwa
kufuata taratibu za muundo wa tungo za Kiswahili (mapokeo) kuliwanyimia uhuru
walidai kuwa hakuna sharia za utunzi wa mashairi katika (diwani ya Amri)
(sharia za kutunga mashairi).
3.
Muundo wa tungo
zao zisizofuata kaida ni wa kiasilia. Hii ina maana kwa ushairi wa mwanzo
haukuwa na mizani wala vina.
Kwa namna nyingine tunaweza kusema kuwa mgogoro huo
ulijitokeza baina ya wazee akina Kuluta Amri Saadam Kandoro, Ustadhi,
Andamenga, Shihabdini chira hdin n.k na vijana akina E.Kezilahabi na Uanza.
MADA NDOGO ;KUHAKIKI
RIWAYA
Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawaidha,
lugha ya nathari, mchanganyiko wa visa, wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa
kimantiki yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na maisha halisi.
SIFA ZA RIWAYA
1.
Urefu, Riwaya kwa kawaida huwa ndefu ikilinganishwa na tanzu
nyingine za kinathari kama vile hadithi fupi. Mfano wa Riwaya ya Bwana
Mnyombokera na Bibi Bagomoka (198 ) iliyoandikwa na Kiterezi, Hii ina mamia ya
kurasa
2.
Matukio,Riwaya humulika hali halisi ya maisha ya binadamu
ingawa matukio ya riwaya si lazima yawe ya kweli yametokea, yanaweza kupatikana
katika ulimwengu halisi wa binadamu matukio kama vile rushwa, wizi wa mali ya
umma, matabaka, uongozi mbaya, athari za pesa katika ndoa na mapenzi na tatizo
la usafiri Dar-es-salaam katika “Pepo ya
mabwegwe” (1981) iliyoandikwa na Mwakyembe, mambo yaliyoandikwa yamo katika
jamii yetu kwa sasa.
3.
Muundo,Riwaya huwa na miundo changamano ukilinganisha na
kazi nyingine za kinathari. Riwaya inaweza kua na muundo wa msago, rejea au
rukia, wakati mwingine inaweza kuwa na muundo changamano yaani inakuwa na
muundo miwili katika kazi moja.
4.
Mandhari yake
ni pana
Mandhari
ya riwaya ni mapana na kikamilifu kwani riwaya hushughurikia mawazo mengi,
hujishughulisha na vipengele vingi vya maisha ambavyo hupatikana katika nyakati
na mahali tofauti kama vile shuleni, mijini, vijijini, nyumbani, barabarani
n.k. ili kushughulikia mazingira mapana mwandishi hutumia kipindi kirefu cha
wakati ikilinganishwa kazi nyingine kama vile hadithi fupi ambayo huweza
kuchukua kipindi kimoja tu kukuamilika.
5.
Wahusika ,Wahusika wa riwaya ni wengi na waliokuwa zaidi. Riwaya
hushughulikia masuala mengi huwa na wahusika wengi wanaomwezesha mwandishi
kukidhi haja hiyo kuna wahusika wanaobadilika kwa lengo la kuonyesha hali
halisi ya maisha kuna wale wasiobadilika ili kutumiwa kukashifu au kuhimiza
hali fulani n.k. Riwaya ya Ziraili na Ua la faraja na Mkufya na Makuadi wa Soko
Huira iliyoandikwa na Chacha Gezina wahusika wengi.
6.
Mtindo,Riwaya hutumia mtindo wa wasimulizi, monolojia au
dayolojia na nafsi zote tatu. Mwandishi anaweza kuwa ndiye msimulizi au mhusika
fulani akawa ndiye anayesimulia au wahusika wakawa wanajibizana wao kwa wao.
Mfano:
Njama (1981), Uchu (2000), Kikosi cha Kisasi(1979) vya musiba ametumia zaidi
mtindo wa monolojia na dayolojia kidogo.
AINA/TANZU
ZA RIWAYA
Kuna
michepuo miwili ya riwaya ambayo ni;
A. RIWAYA YA DHATI
Riwaya
dhati ni riwaya yenye kuchambua masuala mazito ya kijamii, kutafuta sababu zake
athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na
kumfikirisha msomaji, sio kumstarehesha mtu.
MATAWI
YA RIWAYA YA DHATI
1.
Riwaya ya kijamii
Ni
riwaaya inayosawiri maisha na matatizo ya kawaida ya jamii. Matatizo haya
huweza kuwa ya kifamilia, kiuhusiano wa kitabaka ya kisasa ya kiutamaduni n.k.
Utanzu huu ndiyo wenye idadi kubwa zaidi ya riwaya.
Mfano:
-Shabaan Robert “Siku ya watenzi wote” (1968)
-M.S.Moamed “Nyota ya Rehema” (1978)
-S.A..Mohamed “Dunia mti mkavu” (1980)
-E.Kezilahabi “Rosa mistika” (1971)
-J.N.Somba “Alipanda upepo Akavuna Tufan” (1969)
-Alex Banzi “Titi la mkwe” (1972)
2.
Riwaya ya kisaikolojia
Ni
riwaya inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia, mawazo, Imani, hofu, mashaka
na matumaini na matamanio yake binafsi na athari za mambo hayo kwake binafsi na
labda jamii yake. Baadhi ya watunzi waliojipambua katika utanzu huu ni
-E.Kezilahabi “Kichwa maji” (1974)
-M.S.Mohamed “Kiu” (1972)
-S.A.Mohamed “Tata za Asumini” (1990)
-K.G.Mkangi “Ukiwa” (1973)
3.
Riwaya ya kitawasifu
Ni
riwaya ambayo husimulia habari za maandishi tangu kuzaliwa kwakwe hadi pale
inapokomea au hadi kufa.
Mfano: -Shabaan Robert “Maisha Baada ya miaka
Hamsini” (1966)
-Maisha ya Hemed Bin Muhamed “Tipu Tipu” (1950)
4.
Istiara
Ni
riwaya ya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara au kuwakilisha tu cha jambo
jingine.
Mfano: -Riwaya ya Nathanuel Swift (1926)
-Safari za Gulliver (Mfasiri F.Johnson)
(1945)
-Shamba la wanyama (Msafiri F.Mkwegere)
Ni
ishara ya mfumo wa utawala wa dikteta wa kisovieti wa enzi za Staliri. Yaelekea
pia riwaya Shabaan Robert (1951) kusadikika ni ishara kuhusu utawala na mabavu
wa kikolono.
5.
Riwaya ya kigano
Ni
riwaya yenye umbo la mtindo wa ngano mathalani huweza kuwa na wahusika wanyama,
visa vya ajabu ajabu, mandhari ya kubuni na visa vyenye kutendeka nje ya wakati
wa kihistoria.
Mfano: -Shabaan Robert (1952) “Adui na nduguze”
-J.K.Kimbila (1966) “Lila na fila”
6.
Riwaya teti
Ni
riwaya inayosimulia vituko na masahibu ya watu, wapuuzi, walaghai, wajanja na
kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Aghalabu hao huwa ni watu wanaovutia wa
tabaka la chini na bapa. Matukio ya Riwaya hii hayana msukumo ulioshikamana
vizuri shabaha yake mojawapo ni kuziteta na kuzikejeli tabia za matabaka na
watu mbalimbali katika jamii.
Mfano: -Hadithi za “Hekaya za Abunuasi na Hadithi
nyingine (1915) imefanana na vituko vya riwaya teti.
7.
Riwaya ya wasifu
Ni
riwaya inayoandikwa na mtu mwingine kuhusu maisha ya mtu mwingine tangu
kuzaliwa hadi kufa kwake.
Mfano: -J.Makabarah “Maisha ya Salum Abdallah”
(1975)
-S.Robert “Wasifu wa Siti bint Saad” (1967)
8.
Riwaya chuku
Ni
riwaya ya vituko na masaibu yasiyokuwa ya kawaida ni riwaya isiyozingatia
uhalisia mara nyingi masaibu ya Riwaya chuku huambatana na mapenzi, mfano;
baadhi ya hadithi za Alfu-lela-Ulela (1929) ni chuku katika fasihi ya Kiswahili.
Riwaya za Shabaan Robert za “Adili na Nduguze” (1952) na “Kusadikika” (1951)
zinaingia katika kundi hili.
9.
Riwaya ya kihistoria
Hii
huchanganya historia halisi na Sanaa kwa makusudi ili kutoa maudhui fulani.
Mara nyingi riwaya hii hujikita kwenye matukio makuu ya kihistoria yalioathiri
mwenendo na mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika na historia ya kubuni,
matukio ya kweli na ya kubuni. Hata hivyo riwaya hiyo inazingatia zaidi namna
matukio makuu ya kihistoria yalivyomwathiri na yalivyoathiriwa na matendo ya
mtu binafsi aliyeyashiriki baadhi watunzi mashuhuri wa riwaya za kihistoria ni
Mfano: -Olef Msewa “Kifo cha ugenini” (1977)
-M.Karuthi “Kaburi bila msalaba” (1971)
-S.A.Shafi “Kuli” (1979)
-A.Lihamba “Wimbo wa Sokomoko” (1990)
-B.Mapalala “kwa heri iselemaguzi” (1992)
-G.Ruhumbika “Miradi Bubu ya wazalendo” (1992)
10.
Riwaya ya kimaadili.
Ni
riwaya inayowapa watu maadili mema na wengine maadili hayo ni ya kidini wausika
wanakuwa na sifa za kudumu kama vile upendo wa ukarimu.
Mfano: -Shabaan Robert “Adili na Nduguze” (1952)
-M.Mnyapala “Mrina Sali na wenzake wawili” (1961)
-G.Mhina “Mtu ni Utu” (1971)
11.
Riwaya ya kimapinduzi
Ni
riwaya inayojadili matatizo ya kisiasa katika jamii. Riwaya hii ni mwelekeo
fulani wa kuleta mabadiliko ya kisiasa katika jamii.
Mfano:
wa riwaya hizi ni “kuli” (1978), Kabwela (1978), Mzalendo (1977) Ubeberu
Utawashinda (1971) n.k.
12.
Riwaya ya kifalsafa
Ni
riwaya zinazojadili migogoro ya kimaisha kifalsafa. Riwaya hizi hujuliza
maswali kama vile
-
Ukweli ni nini?
-
Maisha ni nini?
-
Kifo ni nini?
-
Kuwepo na
kutokuwepo ni nini? n.k
Muundo
wa riwaya hizi ni wa kimchangamano au a mviringo na wahusika huvunjwa vunjwa
hivyo mhusika wa riwaya hizi ni wazo tu au hawapo kabisa
Mfano: E.Kezilahabi- “Nagona” (1987) Mzingile
(1991)
S.Mohamed- “Kiza katika nune” (1988)
K.G.Mkangi- “Mafuta” (1984) n.k
13.
Riwaya Barua
Ni
riwaya ambayo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia ya barua wanazoandikiana
baadhi ya wahusika.
Mfano: -Mariam Ba “Barua ndefu kama hii “(1980)
Msafiri Maganda
-Walter Tribisch “Nampenda mvulana. Barua ya siri” (1964)
14.
Riwaya ya vitisho
Ni
riwaya yenye visa vya kutisha na kusisimua damu mara nyingi visa hivyo
huambatana na mambo ya ajabu au miujiza
Mfano: -C.Mung’ong’o “Mirathi ya Hatari” (1977)
-N.J.Kuboja mbojo Simba-mtu (1971)
15.
Riwaya pendwa
Ni
riwaya iliyokusudiwa kuwastarehesha na kuburudisha msomaji tu lengo hili
kulihimiza kwa kusawiri visa na vituko vya kusisimuwa damu
Mfano:
Vituko vya majambazi na uhalifu, ususi na mahaba ya waziwazi.
Riwaya
pendwa huwa na mafunzo kidogo kama lengo la ziada katika Tanzania aina hii ya
riwaya ililetwa kwa mara ya kwanza na Abdull alipoandika riwaya ya “Mzimu wa
watu wa kale“ (1957/8) na miaka ya 1960
-
Katalambwa (1965) simu ya kifo
SIFA ZA
RIWAYA PENDWA
1. Matumizi
makubwa ya taharuki na utendaji
Taharuki hutumika kuelezea hamu kubwa anayokuwa nayo
msomaji katika kujua yatakayotokea katika hadithi fulani. Taharuki hutokea pale
ambapo msomaji ana hamu kubwa au anajua yanayoweza kutokea laikini hajui jinsi
yatakavyotokea.
Riwaya pendwa ni riwaya ya taharuki kwa sababu ya
kimsingi ya fani yake hujiweka katika mbinu ya kisanaa ya taharuki. Taharuki
imepewa nafasi kubwa katika aina hii ya riwaya kwa njia ya vituko vya kusisimua
vinavyojibainisha kwa njia ya mkingano iliyosukwa kwa namna ya ufundi usiokuwa
wa kawaida.
Kwa upande wa utendaji wahusika wake n hodari sana
katika kutenda, katika kuwindana, kupigana kwa silaha na mikono mitupu na
kufanya matukio yake utendaji unaojitokeza humu unaziteka nafsi za wasomaji
wake.
2. Hutumia
wahusika walewale.
Riwaya pendwa inasifa ya kutumia wahusika walewale
hivyo ikawa na uwezo wa kujiendeza katika vijitabu kadhaa. Karibu kila
mwandishi maarufu wa aina hii ya riwaya ameandika vitabu zaidi ya kimoja. Sifa
hiyo ya kuwatumia wahusika walewale imefanya kijitabu kimoja katika mfuatano wa
vitabu kadhaa vya mwandishi mmoja kionekane kama tukio linalojitegemea katika
mfululizo wa matukio. Ili kuustawisha na kuwisisitiza mfuatano huo, baadhi ya
waandishi wameweza hata kudondoa kazi za nyuma katika kazi zao za baadae mfano Abdallah
“Kosa la bwana Musa”,Hofu (1988) musiba,Salamu Toka Kuzimu (1993) Mtobwa,Tutarudi
na roho zetu?? (1987)
3. Mhusika mkuu
hupewa sifa zisizo za kawaida
Mhusika mkuu ameumbwa juu ya wahusika wengine
anatawaliwa, hivyo ana sifa ya ubabe sifa ya kuwa kielelezo chenye ukamilifu,
yaani kutokana na dosari.
Mfano: Abdallah “ Kosa la Bwana Musa”
Mhusika mkuu ndiye mshindi hata apitapo katika taabu
na mashaka ya aina gani tunajua hatimaye ni mshindi katika mambo yake. Wahusika
hawa wakuu hutenda na kuendesha mambo yao kama miungu wadogo pasi na kukosea
hata wakawa wasioaminika.
4. Mandhari
yake huundwa kwa namna ya pekee
Wasanii wa riwaya pendwa wanatumia mandhari ya
kitanzania au kiafrika, lakini sehemu kubwa ya matukio ama imo ndani ya vichwa
vya wasanii au filamu za upelelezi, uhalifu na mapenzi za kigeni.
5. Upangaji
holela wa matukio
Katika riwaya pendwa kuna upangaji wa haraka wa
mtiririko wa matukio kiasi kwamba sehemu zingine zinakosa upatanifu na mantiki.
6. Kuenzi
jinsia ya kike kama chombo cha anasa na uhalifu.
Riwaya pendwa hua zina mapenzi ndani yake kana kwamba
upelelezi au shughuli inayofanyika haiwezi kusisimua bila mapenzi, yaani hazina
dawa, dawa ya kazi ni mapenzi.
7. Hutumia
lugha ya kila siku
Mara nyingi riwaya pendwa hutumia mitindo wa
masimulizi na monolojia na kwa kiasi kidogo dayolojia. Lugha yake ni rahisi ya
mazungumzo ya kila siku.
ATHARI ZA
RIWAYA PENDWA
1. Hudumaza
vipaji vya waandishi wetu kwani huiga kila kitu.
Kazi hizi zinadhihirisha jinsi gani fasihi pendwa za
kigeni pamoja na filamu zinaathiri waandishi wetu. Riwaya pendwa ni matokeo ya
mwigo ambayo yameathiri uasili wa waandishi wetu katika ubunifu kimaudhui na
kifani kazi hizi zinashindwa kabisa kudhihirisha umahiri wa waandishi wetu
katika kubuni kazi na sanaa zenye mawazo yao wenyewe.
2. Hufundisha
majangili na wahalifu mbinu mpya katika shughuli zao za kufanya uhalifu.
Riwaya pendwa husababisha uhalifu katika jamii.Mfano:
Athari mbaya za tamaduni za kigeni zinazokuja kwa njia ya filamu na riwaya
pendwa ni kama vile kuzuka kwa makundi ya kiharamia hapa nchini ambayo
yanavamia benki, baa, maduka na kuwaibia watu kwa kutumia silaha mbalimbali.
3. Hazichambui
kwa undani misingi ya matatizo ya jamii.
Riwaya hizi haziingi kwa undani katika misingi ya
matatizo ya jamii kama kuna tatizo linalosababisha upelelezi je kiini chake ni
nini? Riwaya hizi zinataja juu ya wivu, tamaa, uovu wa aina hiyo bila kuyahusisha
vilivyo mazingira ya jamii (mfano filamu zinaitwa 24)
AINA ZA
RIWAYA PENDWA
1. Riwaya ya
Mahaba
Ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati ya
mvulana na msichana au mwanaume na mwanamke. Siku hizi zipo zenye kusawiri
mapenzi haramu pia.Kwa mfano: Mapenzi baina ya watu wa jinsia moja (mashoga)
Mfano: J.Simbamwene “Mwisho wa mapenzi” (1972),J.D.Kiango
“Jeraha la moyo” (1974),S.M.Komba “Pete” (1978),J.Simbamwene “Kweli unanipenda”
(1978)
2. Riwaya ya
Uhalifu/Ujambazi
Ni riwaya zinazosimulia vituko vya uhalifu. Mfano:
wizi, ujambazi, uuaji, magendo, utapeli, n.k. Aghalabu polisi huhusishwa katika
kuwasaka na kuwadhibiti wahalifu hao.
Mfano:J.Simbamwene
(1972) “Kwa sababu ya pesa”,H.Katalambula (1975) “Buriani”,L.O.Omolo (1970)
“Mtu mwenye miwani meusi”,S.J.Chadhoro (1972) “Kifo change ni fedheha”,Hammie
Rajab (1979) “Ufunguo wa Bandia”
3. Riwaya ya
Upelelezi
Riwaya hii huelezea mambo mawili kosa au uhalifu na
upelelezi wa uhalifu huo hadi mwalifu anapopatikana.
Hivyo wahusika wake ni wahalifu, wadhulumiwa
(waliotendewa kosa) na upelelezi wakiwemo polisi. Mtunzi wa kwanza wa riwaya ya
upelelezi nchini Tanzania ni mfano;M.S.Abdallah
na riwaya zake ni:-Mzimu wa watu wa kale (1958),Kisima cha giningi(1968),Duniani
kuna watu (1973),Siri ya sifuri (1974),Mwana wa yungi Hulewa (1976),Kosa la
Bwana Musa (1984),Watunzi wengine wa
riwaya ya upelelezi ni:-H.Katalambwa na E.Ganzile,Simbamwene (1984) “Dimbwi la
Damu”,E.Ganzele (1980) “Kijasho chembamba”
4. Riwaya ya
Ujasusi
Ni riwaya ya upelelezi wa kimataifa majasusi ni
wapelelezi wanaotumwa na nchi, serikali au waajiri wao kwenda katika nchi nyingine
kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi (silaha walizonazo) siri za kisayansi
na kiuchumi n.k ili taarifa hizo ziwanufaishe waliowatuma wakati Fulani hutumwa
kwenda kuharibu silaha zao au nyenzo za uchumi na maadui
Mfano wa riwaya za ujasusi ni:-E.Musiba (1979) “Kikosi
cha kisasi”,E.Musiba (1981) “Njama”,K.M.Kassani (1982) “Mpango”,Mtobwa (1987)
“Je tutarudi na roho zetu?”,Hammie Rajab (1984) “Roho mkononi”
UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI
Vipengele vya fani ni kama vile:-
a)
Muundo
Muundo hutumika kueleza mpangilio wa kazi ya kifasihi.
Mpangilo huu hujionyesha kwenye maumbo ya kazi za kifasihi kama hadithi fupi au
riwaya. Muundo ni namna au jinsi kazi za fasihi inavyoonekana yaani umbo lake,
ilivyogawanyika. Mfano sura, mfuatano wa matukio yake (mtiririko wa matukio),
msuko n.k. matukio yanaweza kufuatana kwa njia sahihi nay a moja kwa moja
(msuko sahahi) au yakawa na uchangamano ambao unahusisha kwenda mbele na kurudi
nyuma (msuko changamano)
b) Mtindo
Ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mandishi kuwasilisha
ujumbe wake.Mtindo huelezea jinsi mwandishi anavyoiunda kazi yake.Dhana hii
inarejesha sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo
hujionyesha kwenye fani yake. Mazoea hayo ya mwandishi yanapambanua msanii huyu
na wenzake kiasi kwamba msomaji anaweza kusema hii ni kazi inayoandikwa na
fulani kwa kusoma tu katika mtindo wa riwaya kuna vipengele vifuatavyo
· Matumizi ya Lugha
· Usimulizi wa nafsi (Msanii anaweza kusimulia matukio
kwa kutumia nafsi ya 1,2 na ya 3)
· Matumizi ya masimulizi (msanii hutoa masimulizi yake
juu ya mfululizo wa matukio kama yalivyotokea katika kipindi fulani cha maisha
ya wahusika. Msanii husema nini kilitokea jinsi gani kilitokea na mahali ambapo
hayo yalitokea
· Matumizi ya monolojia ni masimulizi yanayofanywa na
mhusika mmoja katika hadithi au kazi nyingine za kisanaa katika mbinu hii,
hadithi inayojitokeza kama inasimuliwa na mhusika aliye hadithini. Mwandishi
anaonekana kuwa hayupo. Pia hadithi inaweza kujitokeza ikisimuliwa katikaa
nyakati mbalimbali.
· Matumizi ya dayolojia, ni mazungumzo baina ya wahusika
wawili au zaidi katika riwaya.
· Matumizi ya tanzu nyingine za kifasihi simulizi kama
vile nyimbo, mashairi, majigambo, hadithi matumizi ya barua n.k.
· Uteuzi wa wahusika na ujengaji wa mandhari.
c)
Wahusika
Ni viumbe wa sanaa wanabuniwa kutokana na mazingira ya
msanii. Hatua ya kwanza katika utungaji wa kazi ya sanaa ni wazo, wazo kutokana
na hali halisi anayoiona msanii ili kueleza fikra rai au falsafa yake kuhusu
kile akionacho anaichukua Lugha na kuifinyanga.
Wahusika wake pia huwaweka katika mandhari
yatakayomsaidia kuwakilisha hoja zake kutokana na vitendo, maingiliano na fikra
zao kuna wasanii wanaotumia wanyama au wadudu kama wahusika kwa lengo la
kufikisha maudhui fulani kwa jamii au dhamira, mitazamo yao, kwa jamii.
d) Mandhari
Ni mahali au makazi maalumu yaliyojengwa na mtunzi na
yanamatokeo, matukio mbalimbali ya fasihi. Mandhari ni mazingira ya wahusika na
matukio na inahusu mahali wanamokaa wahusika na kuingiliana, mazingira ya
kijamii na kiuchumi ya wahusika hao na nafasi zao za kitabaka kufahamu mandhari
kunatusaidia kuelewa hisia, imani, tabia, na maumbile ya wahusika. Mandhari
hutupatia mwelekeo kuhusu maudhui.
e)
Matumizi ya Lugha
Lugha ina nafasi kubwa sana katika fasihi kwa kuwa
fasihi yenyewe ni sanaa ya lugha. Lugha hiyo ndiyo nyenzo inayotofautisha
fasihi na sanaa nyingine kama uchoraji, ufinyanzi, udarizi n.k
Lugha ni nguzo kuu ya kazi za kifasihi na uchunguzi
wowote wa kazi hizo hauna budi kuangalia suala la lugha kazi ya kifasihi huyawasilisha
maudhui yake, dhamira yake kwa kutegemea lugha. Baadhi ya wahakiki wa
fasihi wa kwanza kuwa fasihi hutumia
lugha kwa namna maalumu, inayozoea lugha ambayo inajulukana kama lugha ya
kifasihi. Katika matumizi ya lugha kuna vipengele kama:-
Tamadhali za semi, kama vile tashibiha, sitiari,
tafsida, tashihisi, kejeli, mubalagha, dhihaka n.k
· Mbinu nyingine za kisanaa ni kama vile takriri,
tanakali sauti, mdokezo, tashititi, mjalizo n.k
· Matumizi ya majali maana ya watu aghalabu huwa na
maana. Wasomaji wa riwaya ni vyema tuyachunguze majina na kuyahusisha na
matukio, dhamira, maudhui na ujumbe wa riwaya husika. Mfano wa riwaya ni “Adili
na Nduguze” (1952) mhusika Adili ni mwadilifu
· Matumizi ya jazanda au Taswira ni mafumbo ambamo ndani
maana ya kitu imejificha na mfano katika riwaya ya “Dunia mti mkavu” (1980)
mvua inatumiwa kama jazanda na matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.
· Uteuzi na mpangilio wa maneno. Lugha ni nyenzo ya
kimsingi ya msanii na jinsi anavyotumia huathiri jinsi msomaji atakavyoisoma,
kuielewa na kuathiriwa na riwaya fulani mfano wa matumizi ya miundo fulani
huweza kuathiriwa na maswala yanayozungumzwa.
· Matumizi ya semi, kama vile methali, misemo, nahau,
misimu mafumbo n.k vipengele hivi vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya
fasihi
· Matumizi ya taharuki. Hii ni mbinu inayotumiwa na
watunzi wa kazi za kubuni ili kutetea hisia na hamu ya msomaji ili kujenga
taharuki. Mtunzi husuka matukio yenye mshikamano na kutiririka kwa muwala ambao
unamfanya msomaji asiitue kazi hiyo hadi kikomo chake kazi yenye taharuki
haichoki kuisoma bali inaburudani ndani yake.
JINA LA KITABU
Jina la kitabu ni vyema lisadifu yale yaliyomo ndani
ya kitabu. Mfano Je Shetani msalabani (1982) linasadifu vipi yale yaliyomo
ndani ya riwaya hiyo?
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui ya riwaya kama kazi yoyote nyingine ya fasihi
yaweza kuwa kitu, mtu, tukio au jambo lolote katika maisha yetu. Maudhui
hudhihirika baada ya kuangalia mambo mengi, mathalani tukio mbalimbali
Kwa ujumla, maudhui ni muhimu katika riwaya hasa ndiyo
msingi wa riwaya kwa hivyo ni lazima tutegemee mambo yaliyojitokeza katika ile
riwaya yaani maudhui lazima itoke ndani ya riwaya na sio nje.
Katika bahari hii ya maudhui, hatuna budi kuichunguza jumuiya iliyozungumzwa. Matokeo
yote katika utunzi ule yatapimwa kwa mujibu wa hali ya jumuiya. Mhakiki
astahili kuichunguza jumuiya ili kuweza kuhukumu kama mtunzi amezingatia kutoa
hali halisi ya jumuiya yake.
Maudhui huwa ni ya aina mbalimbali kwa ujumla huwa
yanalenga migogoro na mikinzano katika jamii. Baadhi ya maudhui ya kazi zote za
riwaya na sanaa kwa jumla ni kama vile:-
-
Mgongano wa
tabaka kati ya watawala na watawaliwa
-
Migongano kati ya
wenye elimu na wasiopata elimu
-
Migongano kati ya
walio na mali na wasionayo
-
Migongano kati ya
mwenye kupigania usawa kati ya mume ne mke na wenye kupinga usawa huu n.k
Kwa ujumla maudhui hutupa mafunzo, ujumbe na
kutufahamisha falsafa
MADA NDOGO ;UHAKIKI WA TAMTHILIYA
Tamthiliya ni utungo wa kidrama ambao ni aina mojawapo
ya maandishi ya sanaa za maonyesho. Ni sanaa inayoonyeshwa kwa vitendo katika
sanaa hii ili mtu apate maadili au utamu uliomo katika sanaa mpaka asome
vitendo vya wahusika waliotumiwa na msanii na kuvitafakari kwa makini.
Tamthiliya huonyesha matendo ya wanajamii kwa njia ya
kuigiza, maigizo ambayo hatimaye huweza kuonyeshwa kwenye majukwaa katika sanaa
za maonyesho wahusika wake huonyesha matendo waziwazi kwa njia ya kuigiza.
Wausika hawa huzungumzia nafsi zao wakati zamu zao za kuongea zinapowafikia ili
mradi kila mmoja hujaribu kuonyesha waziwazi kuridhika au kutoridhika kwake
kufutana na nafasi anayoiwakilisha katika jamii inayohusika.
Sifa za
tamthiliya
Tamthiliya huwa na sifa za kawaida za sanaa za
maonyesho, sifa hizo ni:
· Dhana
inayotendeka
Dhana inayotendeka ni kile kinachoongelewa katika
tamthiliya na kinaweza kuwa cha kubuni au cha kweli. Dhana inayotendeka kwa
kawaida huhusu mzozo fulani unaohusisha pande mbili. Kwa mfano, katika
tamthiliya ya “Kilio chetu” (1995),
dhana inayotendeka ni “Vita dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI”
· Kuwepo kwa
mtendaji
Hapa ni wale wanaotenda ile dhana, yaani wahusika. Ili
tamthiliya ikamilike lazima wawepo wale wanaotenda lile tendo ambao wanaitwa
wahusika. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Mashetani” (Hussein) watendaji wakuu
ni: Juma na Kitaru na watendaji wadogo ni: Mama Kitaru, Baba Kitaru, Daktari,
Bibi, Mama Juma, n.k
· Kuwa na
uwanja maalumu wa kutendea
Tamthiliya huigizwa sehemu fulani. Hapa kuna jukwaa
ambako wahusika wanaingiliana katika uigizaji wao. Ukubwa au upana wa eneo hilo
ni muhimu sio tu kwa athari, bali pia kwa kuupitisha ujumbe fulani.
· Kuwepo kwa
watazamaji
Hawa hutazama dhana inayotendeka. Kwa tamthiliya
iliyoandikwa, watazamaji hapa ni wasomaji, yaani wale wanaosoma kazi hiyo ya
sanaa. Kwa hiyo, tamthiliya inaingizwa mbele ya watazamaji (hadhira).
· Kusudio la
kisanaa.
Hili hutupa uhakika kuwa kinachotendeka hapo
kimedhamiriwa kuwa sanaa na si kitu kingine kwa mujibu wa kanuni za jamii
inayohusika.
vi.
Muktadha wa kisanaa
Ni sifa nyingine ya tamthiliya. Muktadha wa kisanaa unafafanua mazingira ya tukio hilo.
Kwa mfano, ugomvi wa walevi kilabuni au baa si sanaa za maonyesho kwa sababu
muktadha wa tukio hilo haulipokei kama sanaa.
vii.
Tamthiliya ni kazi ya kubuni kama kazi nyingine za
kifasihi.
Hii ni muhimu ili kutofautisha kati ya tendo la dhati
katika maisha na tendo la sanaa.
viii. Matukio ya
tamthiliya huigizwa kwa hadhira hai.
Hapa basi pana mawasiliano ya moja kwa moja kati ya
wahusika, ambao ni vipaza sauti vya mtunzi na hadhira.
ix.
Tamthiliya, hadithi yake imegawika kimuundo katika
matendo na maonyesho
Matendo na maonyesho huonyesha matukio mbalimbali.
Kila tendo huzingatia tendo moja kuu ndani ya mchezo; na hugawanyika katika
sehemu ndogo ziitwazo maonyesho. Onyesho moja kwa kawaida huwasilisha tuko moja
linalotendeka mahali pamoja.
x.
Mgogoro wa tamthiliya huwa mwanzoni
Mwandishi hana wakati wa kutoa maelezo mengi. Kwa
mfano, katika tamthiliya ya “Kifo
Kisimani “ ya Kathaka wa Mberia, mgogoro kati ya Mtukufu Bokona na wanyonge
unajitokeza mwanzoni
AINA ZA
TAMTHILIYA
1.
Tanzia
Tanzia
ni ile inayohusika na mambo yenye uzito, kifikirika na kihisia katika maisha ya
binadamu. Mhusika mkuu ambaye hupewa sifa nyingi zinazovutia, hukabiliwa na
shida au tatizo;tatizo ambalo linaweza kumkabili mtu yeyote. Lakini namna
anavyojitahidi kulitanua tatizo hili, namna anavyopigana vita kushinda shida
inayomkabili, hali ya ulimwenguni na tabia za binadamu, zinamfanya asiweze
kufaulu na mwishowe anashindwa katika vita hii. Kwa mfano, tamthiliya ya “Mzalendo Kimathi” (1978) “Kinjekitile” (1969), “Pungwa” (1988), “Kilio cha haki” (1981) ni mfano wa tanzia. Katika tamthiliya zote
hizi mhusika mkuu anashindwa na hata anakufa au anauawa, lakini kifo chake si
kile cha ajali barabarani, bali ni kifo kinachokuja baada ya mapambano marefu,
mapambano yanayochepuza hisia za ushujaa wa binadamu
2.
Ramsa (komedia)
Ramsa
ni ile inayokusudiwa kufurahisha au inayochekeshachekesha na yenye mwisho
mwema. Aina hii ya tamthiliya ni kwamba hutuchorea picha yakini ya maisha yetu,
huwa haijaribu kuisawiri picha hiyo kwa undani na uzito kama uleunaojitokeza
katika tanzia. Mfano wa ramsa ni tamthiliya ya Aliyeonja Pepo (1973)
3.
Melodrama na vichekesho
Melodrama
inafanana sana na tanzia, ingawa mara nyingi mhusika mkuu wa meleodrama
humaliza kwa ushindi, matokeo yake huwa yanasisimua sana, na mwendo wa msuko
wake huwa ni wa harakaharaka zaidi.
Vichekesho,
kwa upande mwingine; huwa vinakusudia
kutuonyesha vituko vitakavyotuchekesha tu. Ujenzi wa wahusika huwa ni muhimu,
matukio huwa hayawekewi sababu zozote au sababu za kuturidhisha na msuko wake
huwa hauna uchangamano mzuri. Tamthiliya nyingi zinazoonyeshwa katika
televisheni ni vichekesho.
4.
Tamthiliya ya kihistoria
Hii
ni aina ya tamthiliya inayoelezea tukio fulani la kihistoria katika jamii
fulani. Msomaji wa tamthiliya hii huweza kukutana na sifa za tanzia pamoja na
tamthiliya chekeshi. Mhusika mkuu wa tamthiliya hii mara nyingi huwa ni shujaa
aliyejitoa mhanga kuipigania na kuitetea jamii yake ili iweze kuondokana na
matatizo yanayoiandama, hususani ya kisiasa na kiuchumi.
Tukio la
kihistoria linaloelezewa kwenye tamthiliya hii huwa limeiathiri jamii husika
kwa kiasi kikubwa na hivyo huwa si rahisi kusahaulika. Vitabu vya tamthiliya
vinavyoelezea matukio ya kihistoria ni kama vile Kinjekitile, Mzalendo Kimathi, Mkwawa wa Uhehe (1979) pamoja na Tone la Mwisho.
UHAKIKI WA
VIPENGELE VYA FANI
Uhakiki wa tamthliya kimsingi huzingatia kanuni na
misingi ileile ya uhakiki wa Riwaya. Kuna mambo ya msingi yz hizo tanzu mbili
kufanana na kutofautiana. Mambo muhimu yanayochunguzwa wakati wa kuhakiki fani
ya tamthiliya ni:
a)
Utendaji/tukio/tendo.
Kitu muhimu sana katika ujenzi wa tamthiliya ni tukio.
Kutokana na tukio moja, msanii anao uwezo wa kuibua dhamira mbalimbali.
Wataalamu wa taaluma hii husisitiza umuhimu wa tendo au tukio katika tamthiliya
kwa kusema “drama ni tendon a wahusika ni tendo”
Tendo huanza pale mhusika anapoulza, “Ninataka nini?
Je, lengo langu ni nini?” Kwa kawaida, aina ya tendo/tukio litaathiri matokeo
ya tamthiliya itakayoandikwa.
Mwandishi mwenyewe anapaswa kuamua juu ya aina ya
tamthiliya anayotaka kuandika, lugha, mtindo, wahusika au mandhari anayotumia.
Kwa hali hiyo, uteuzi wa tendo/tukio la kuandikia tamthiliya lazima uende
pamoja na uteuzi mzuri wa vipengele vingine vya kisanaa kama vile lugha,
wahusika, mandhari, n.k.
b) Lugha
Lugha ndiyo nyenzo kuu ya kazi ya fasihi. Dhamira na
maudhui ya kazi ya kifasihi haziwezi kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya
kuwako kwa lugha. Uchunguzi wa matumizi ya lugha ni muhimu katika uhakiki wa
tamthiliya. Je, mambo gani ya kuchunguza hapa? Hapa tunachunguza:
-
Matumizi ya nahau
na misemo.
-
Uteuzi na
mpangilio wa maneno/msamiati.
-
Tamathali za
semi. Kwa mfano, sitiari, tashibiha, tafsida, tashihisi, n.k.
-
Mbinu nyingine za
matumizi ya lugha. Kwa mfano, takriri, tanakali sauti, majazi, mdokezo, mjalizo
n.k.
-
Matumizi ya
taswira na ishara mbalimbali.
-
Matumizi ya mkopo
na kutohoa.
c)
Wahusika
Katika tamthiliya, wahusika ni nguzo muhimu sana.
Wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuniwa, wenye sifa muhimu za
binadamu. Wahusika huwa na athari kubwa kwa hadhira kutokana na sababu mbalimbali:-
-
Wahusika
wanabebeshwa sifa nyingi tofauti ambazo zinawakilisha maisha halisi ya watu
hai.
-
Mwandishi wa
tamthiliya hulazimika kumjenga mhusika mmoja kwa kuvutia na kumpa mbinu za
ki-drama, mambo ya kushangaza au mbinu yoyote ile anayoichagua mwandishi. Kama
tamthiliya inaigizwa jukwaani, wale waongozaji wa tamthiliya hiyo wanaweza
kuathiri mchezo huo pia. Kama ilivyo katika riwaya, tamthiliya huwa na wahusika
wakuu na wahusika wadogo.
d) Muundo wa
tamthiliya
Muundo katika tamthiliya humaanisha msuko wa vitendo
na mgogoro kuanzia mwanzo wa mchezo, kuingia kwenye kilele (upeo) na
kuhitimisha kwenye ufumbuzi/masuluhisho ya mchezo huo (mwisho). Kwa upande
mwingine, muundo huonyesha mpangilio wa maonesho kutoka mwanzo hadi mwisho wa
tamthiliya.
Kwa ujumla, tamthiliya inakuwa na mwanzo unaomwelekeza
msomaji kwenye wahusika na migogoro au mkinzano unaokuwa na kufikia upeo kasha msuko
wa aina fulani kabla ya kufikia ufumbuzi. Muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja
au muundo wa rejea.
e)
Maelekezo ya jukwaani
Haya ni yale maelezo ambayo huandikwa kwa mabano
katika tamthiliya na huandikwa kwa hati ya mlazo. Je, maelezo hayo hufanya kazi
gani?
-
Hueleza mienendo
na miondoko ya wahusika.
-
Hutoa maelezo
kuhusu wasifu wa wahusika, mavazi, lugha ya ishara za uso, n.k.
-
Hutoa maelezo
kuhusu mandhari au mahali pa mchezo.
-
Hufafanua matendo
mbalimbali yanayotokea jukwaani.
-
Hueleza wasifu wa
mazingira na hata malebaya wahusika.
-
Hutoa vielekezi
vy jinsi ya kuandaa jukwaa kwa ajili ya uigizaji
-
Hutoa tathmini ya
matendo ya wahusika au lugha; kwa kuonyesha wapi pana kinaya, n.k
f)
Mandhari
Madhari hutumiwa kuelezea sehemu ambako tendo fulani
hutendeka. Neon hili huweza kutumiwa kwa mapana kuelezea pia mazingira ya
kisaikolojia ya tendo fulani. Mandhari huweza kurejelea yale mazingira ya
jukwaani na hata wakati wenyewe katika tamthiliya. Mandhari yanaweza kuwa ya
kubuni au ya kweli (halisi)
g)
Upeo/kilele
Upeo ni sehemu ya tamthiliya ambamo taharuki na matamanio ya hadhira hufikia kilele.sehemu
ambapo hadhira huanza kupata suluhisho la mgogoro uliomo katika tamthiliya. Peo
katika tamthiliya ni za aina mbili upeo wa juu na wa chini
i.
Upeo wa juu ni ule ambao unakidhi haja za hadhira au jamii
inayoipokea. Katika sehemu hii, jamii hupata majawabu muhimu ambayo tamthiliya
huwa imeyachelewesha kwa kutumia mbinu kama vile za taharuki, mbinu rejeshi,
mtindo telezi, n.k. Sehemu hizi mara nyingi husisimua hadhira kwa hali ya juu
sana.
ii.
Upeo wa chini ni ule ambao haukidhi haja ya wasomaji wa tamthiliya
inayohusika. Katika baadhi ya kazi za tamthiliya upeo wa chini huonyesha
udhaifu wa kazi ya sanaa ya msanii anayehusika. Wakati mwingine upeo wa chini
umekusudiwa na msanii na huutumia sana katika hadithi fupi na lengo kubwa huwa
ni kuipa hadhira mshangao.
h) Jina la
kitabu na jalada lake
Kama ilivyo kwenye uhakiki wa riwaya, katika
tamthiliya vilevile tunaangalia uhusiano wa jian la kitabu na yaliyomo katika
kitabu, hali kadhalika jalada na uhusiano wake na maudhui ya kazi inayohusika.
i)
Mtindo katika tamthiliya.
Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao
ni mazungumzo au dayolojia. Mazungumzo/dayolojia hutumiwa kuelezea majibizano
baina ya wahusika wawili au zaidi waliopo kwenye jukwaa au katika tamthiliya
maongezi au majibizano si kwa ajili ya kujibizana tu. Hata hivyo ni muhimu
kutambua kuwa, mazungumzo hayo si mazungumzo tu, lazima yaendeleze tendo kuu
katika tamthiliya. Mazungumzo ndiyo nguzo ya kukuza dhamira na maudhui.
-
Mazungumzo mazuri
yana uhalisia na uthabiti.
-
Mazungumzo sio
maelezo tu bali yanaonyesha matendo ya ndani.
-
Mazungumzo mazuri
hukuza na kuendeleza tendo kuu na msuko
-
Mazungumzo sio
maongezi yanayovutia tu, lazima yawe na lengo.
-
Ikiwa mazungumzo
yanakuza na kuendeleza tendo kuu, basi yanatekeleza jukumu la kidrama.
-
Mazungumzo
yanaweza kutokea sambamba; kwa kuwako kwa wahusika kadhaa jukwaani.
-
Mazungumzo na
uzungumzi nafsi wa wahusika huchukuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya tamthiliya
kwa sababu ya kuliendeleza tendo kuu.
-
Mazungumzo huweza
kuonyesha sifa zisizokuwa za kawaida katika maongezi ya kila siku ikiwa
mwandishi anataka kulimulika jambo fulani.
-
Mazungumzo ya
mhusika yanaweza kuyavunja mtarajio fulani wa wasomaji au hadhira katika hali
fulani kwa ajili ya kupitisha ujumbe fulani.
-
Mazungumzo ndiyo
njia kuu ya kuindeleza hadithi iliyopo katika tamthiliya kwa kuwa mwandishi
hana uhuru wa kutumia mbinu za usimilizi, isipokuwa katika maelezo ya jukwaani.
Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni dayolojia.
Dayolojia ndiyo mtindo mkuu wa tamthiliya nyingi.
Dayolojia ni majibizano baina ya wahusika wawili au
zaidi, ambao hujadili jambo fulani.
UHAKIKI WA MAUDHUI
Maudhui hutujulisha lile lililomgusa mwandishi mpaka
kuunda ile kazi yake. Hili linaweza kuwa ni wazo tu au aliloshuhudia au hata
likawa ni jumuisho la mambo mengi.
Maudhui pia hutuangazia jinsi jumuiya ya mwandishi
ilivyo kwa kuwa fasihi ni kioo cha jamii. Kupitia maudhui, tunaweza kugundua
mazingira ya mwandishi yalivyo.
Mwandishi hutumia maudhui yake kutudhihirishia
mivutano, misuguano na pia maendeleo ya jamii yake. Maudhui ndiyo lengo la
mwandishi. Ndicho chombo chake cha
kutuonyesha furaha na matatizo ya jumuiya iliyomzingira na kuwathiri kimawazo.
Kuathirika huku kwa mwandishi hasa hujitokeza zaidi baada ya kusoma kazi zake
nyingi.
Kwa hivyo, basi maudhui ya kazi yoyote ile ya fasihi
yatahusu mambo ambayo yalimsukuma mwandishi hadi akaiunda kazi ile. Pia
yatahusu mafunzo ambayo mwandishi aliliengea hadhira yake. Zaidi ya haya, kwa
kuwa maudhui hayatenganishwi na mazingira na jamii, itambidi mwenye kuyachambua
ayalinganishe na hali ya jamii ya mwandishi katika vipengele mbalimbali vya
maisha. Mathalani, itambidi achunguze siasa, uchumi, utamaduni, n.k.
Mwanafasihi mmoja, Senkoro (1981), amefafanua maudhui
kama yanayojumlisha mawazo nap engine mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma
mtunzinama msanii hadi akatunga kazi fulani ya sanaa. Huwa msanii huyo
amekusudia hadhira yake ya wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji wayapate
mawazo au mafunzo hayo. Kwa hiyo, haya twaweza kuyaita kuwa ni lengo la msanii
kwa hadhira. Mawazo na mafunzo haya hayazuki hivi hivi tu. Kwa hiyo, kuna
umuhimu wakati wa kuyachambua na kujadili yahusishwe na hali halisi ya jamii.
Mhakiki anachunguza maudhui ya kazi ya fasihi anaweza
kuongozwa na maswali yafuatayo:-
-
Je, wazo kuu la
msanii n nini?
-
Je, msanii
ametazamia hadhira ya aina gani?
-
Je, kuna kundi
lolote analoliunga mkono?
-
Je, kuna kundi
analolibeza?
-
Je, msanii ameipa
hadhira yake mbinu zipi za kuitatua migogoro aliyoichunguza?
Katika tamthiliya ya Kiswahili, kuna dhamira
mbalimbali ambazo waandishi wamezishughulikia kwa mujibu wa Mulokozi (1996).
Dhamira hizo ni:-
1. Migongano ya
kiutamaduni
Hizi
zinonyesha mvutano kati ya utamaduni wa jadi wa Kiafrika na utamaduni wa
Kizungu au kati ya mji na shamba. Suala hili limejadiliwa kwa dhati zaidi
katika
-
E.Hussein “Wakati
Ukuta” (1969)
-
E.Hussein “Kwenye
Ukingo wa Thim” (1989)
-
P.Mhando “Hatia”
-
J.Ngugi
“Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi” (1961)
-
H.M.Liyoka “Dunia
Imeharibika” (1978)
-
C.Riwa na
M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!” (1976) n.k
2. Matatizo ya
kijamii
Kwa
mfano, mapenzi, ndoa, ufukara na urithi. Karibu
tamthiliya zote za mawazo zilihusu kipengele hiki. Kwa mfano, Nakupenda Lakini…(1957) na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (1961),
zilizungumzia matatizo ya mapenzi yanayokumbana na vikwazo vya kiuchumi na
vinginevyo. Tamthiliya za Hyslope zilihusu matatizo ya urithi, rushwa, fitina
na tama. Tatizo la mimba limejitokeza katika Hatia, katika Mke Mwenza (1982),
tunakutana na tatizo la wivu katika ndoa za mitala.
3. Dini
Hizi
ziko katika makundi mawili:
· Tamthiliya za kanisani zenye kufundisha dini. Kwa
mfano, zile tamthiliya zinazoingizwa kanisani kukiwa na shughuli au sherehe
fulani.
· Tamthiliya zinazochambua na kuhakiki asasi na
maundisho ya dini kifasihi. Hizi ni kama vile
-
F.Topan
“Aliyeonja Pepo” (1973)
-
Muba-“Maalimu”
(1980)
-
Mulokozi “Mkwawa
wa Uhehe” (1979).
Hawa wanaonyesha mikinzano iliyomo ndani
ya mafundisho ya kidini, hasa pale mafundisho hayo yanapogongana na maisha
halisi, sayansi au mantiki. Tamthiliya nyingine zinazoonyesha mgongano huo ni Kinjekitile (1969) na Njia Panda (1981).
4. Ukombozi
Hizi
zinazungumzia juu ya harakati za kumwondoa mkoloni hapa Afrika. Mfano wa
tamthiliya hizo ni Nkwera “Mkwawa Mahinya” katika “Johari Ndogo” (1968),
E.Hussein “Kinjekitile” (1969) na “Mashetani” (1971), M.Mulokozi “Mkwawa wa
Uhehe” (1979), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), P.Muhando, N.Balisidya na
A.Lihamba “Harakati za Ukombozi” (1972) na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na
Paulo! Paulo!” (1976), n.k. Tamthiliya hizi licha ya kujadili ukombozi wa
kisiasa, vile vile zinajadili ukombozi wa kiuchumi na kiutamaduni.
5. Ujenzi wa
jamii mpya
Baadhi
ya tamthiliya zinazojadiliwa zinazojadili suala hili ni za Ngahyoma “Kijiji
Chetu” na M.Rutashobya “Nuru Mpya” (1980). Hawa walipendekeza marekebisho
katika mfumo uliopo. Baadhi wameonyesha tu kuwa mambo siyo sawa. Mfano: Mbogo- Giza Limeingia (1980) na Hussein- “Mashetani” (1971) na wengineo
wanalitazama suala hili kitabaka na kuhimiza mapambano ya wafanyakazi dhidi ya
mabepari na ubepari- Kahigi na Ngemera- “Mwanzo
wa Tufani” (1976) na Mazrui “Kilio
cha Haki” (1981).
6. Uke na
matatizo ya kijinsia
Hawa
wanaonyesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya sasa, kutafuta sababu za hali
hiyo na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya tamthiliya hizo ni P.Muhando-“Nguzo
Mama” (1982), Ngozi-“Machozi ya Mwanamke” (1977), Mulokozi-“Mkwawa wa Uhehe”
(1979), Mazrui “Kilio cha Haki” (1981),
E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989).
7. Uchawi,
uganga na itikadi za jadi
Suala
hili limejitokeza katika tamthiliya kadhaa. Kwa mfano, Mhanika-“Njia Panda”
(1981), Mbogo “Ngoma ya Ng’wanamalundi” (1988), Hussein “Kinjekitile” (1969) na
Kitsao “Mfarakano” (1975). Kwa ujumla, uganga na itikadi za jadi katika
tamthiliya hizi husawiriwankama amali muhimu za jamii zifaazo kutatua baadhi ya
matatizo ya kimaisha.
8. Tatizo la
ugonjwa wa UKIMWI
Hawa
wanaonyesha madhara yanayotokana na ugonjwa wa UKIMWI kwa jamii. Tamthiliya
hizo ni Ushuhuda wa Mifupa (1990), Mwalimu Rose (2007), Orodha (2006) na Kilio Chetu (1995).
TOFAUTI KATI
YA TENZI NA MASHAIRI
Tenzi na mashairi hutofautiana, hasa katika vipengele
muhimu vifuatavyo:
1. Muundo,tenzi hutumia muundo wa tarbia tu katika beti zake
ambapo mashairi yana uhuru wa kutumia miundo mingine tofauti kama vile
tathlitha, takhmisa n.k
2. Urefu,tenzi kwa kawaida huwa ni ndefu kwa vile hutokea zikiwa katika mtindo
wa usimulizi, na hivyo kuwa na beti nyingi sana ili kkamilisha usimulizi wa
kisa ambapo mashairi kwa kawaida hutumia beti chache
3. Vina,tenzi zina vina vya mwisho tu; hazina vina vya kati
ambapo mashairi yana vina vya kati na vya mwisho.
4. Urefu na
mistari ,tenzi mistari yake ni
mifupi; haigawanyiki katika nusu ya kwanza nay a pili, mashairi yake ni mirefu;
na hugawanyika mara mbili, nusu ya kwanza na nusu ya pili (huitwa vipande).
5. Idadi ya
mizani, tenzi katika mistari yake huwa na mizani nane tu,
mashairi huwa na mizani 16 katika mistari yake.
6. Kituo,kituo cha tenzi hubadilikabadilika kutoka ubeti mmoja
hadi mwingine. Kituo cha shairi kinaweza kubadilika au kutokubadilika.
KANUNI ZA
UTUNZI WA NGONJERA
Ngonjera ni tungo za kishairi zinazowasilishwa kwa
kutumia mazungumzo ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi. Mazungumzo hayo
huwa na mjadala wa malumbano yenye lengo la kutoa ujumbe maalumu kwa
wasikilizaji
Katika majibizano hayo, mhusika mmoja hueleza jambo
fulani kwa ubeti mmoja, mhusika wa pili naye hujibu kwa kupinga au kuunga mkono
hoja za mhusika aliyetangulia. Mwishoni mwa ngonjera wahusika hao huwa
wanaondoa tofauti zao na kuwa na msimamo mmoja. Hali hiyo hutokea pale mhusika
mmoja anakubali kulegeza msimamo wake na kukubaliana na mtazamo wa mwenzake.
Kanuni za utungaji wa ngonjera hazitofautiani na
kanuni za utungaji wa mashairi ya kimapokezi. Ngonjera sharti iwe na kichwa,
beti, vina, mizani, muwala, utoshelezi, kituo na urari wa mistari ya beti.
Ngonjera pia, hutakiwa kutumia lugha ya kisanaa kama ilivyo kwa mashairi.
Mfano wa
ngonjera: Mwenye nyumba na mhitaji
MWENYE
NYUMBA: Nakwambieni jamaa, vya nyumbani mwangu visa,
Mpangaji amekaa, huu mwezi wa tisa,
Mpangaki ana baa, atoapo zangu pesa,
Hivi sasa nimenusa, nataka
kumfukuza.
MHITAJI: Taibu maneno yako, yananipata
kabisa,
Mimi mhitaji kwako, chumba sina
nimekosa,
Sema kodi iliyoko, unayopokea sasa,
Name nitakupa pesa, upate kumfukza.
MWENYE
NYUMBA: Kwa hesabu iliyoko, mimi sipati halasa,
Thelethini ndizo ziko, alipazo Bwana
Musa,
Kinipa sitini zako, atatoka hivi
sasa,
Himiza unipe pesa, nipate kumfukuza.
MHITAJI:
Sitini ni hizi hapa, pokea ni
kama posa,
Na kodi hasa talipa, daima bila
kukosa,
Tena Wallahi naapa, kulipa sitakutesa,
Nenda kafanye mkasa, upate kumfukuza.
(Kutoka: Ngonjera za UKUTA, uk 86-87)
TOFAUTI KATI
YA NGONJERA NA MASHAIRI
Ngonjera hutofutiana na mashairi katika vipengele
vine, navyo ni wahusika, namna ya uwasilishaji, kituo, na matumizi ya lugha.
1. Wahusika,ngonjera hutumia wahusika wanaojibizana. Wahusika hao
wanaweza kuwa wawili au zaidi, ambapo
shairi hutumia mhusika mmoja tu anayezungumza au anayetoa mawazo yake pasipo
kujibizana na mtu.
2. Uwasilishaji, ngonjera huwasilishwa kwa njia ya uzungumzaji wa
kujibizana, mashairi huwasilishwa kwa njia ya uimbaji.
3. Kituo,ngonjera huwa na vituo tofauti kwa vile kila mzungumzaji
huwa na ktuo chake, lakini shairi huwa na kituo kimoja tu na hata kama
kitabadilikabadilika huwa hakilengi kuonyesha mtazamo wa ukinzani wa mada
inayojadiliwa kama ilivyo kwa vituo vya ngonjera.
4. Matumizi ya
lugha, ngonjera hutumia sana lugha
rahisi lakini mashairi hutumia sana lugha ya kuzama.
No comments:
Post a Comment