ORODHA
Mtunzi; Steve REYNOLDS
Mchapishaji;Macmillan
Chapa
ya 1;2006
UTANGULIZI
ORODHA ni
miongoni mwa tamthiliya ambazo zinaonyesha namna jamii hususani watoto na
vijana wanavyoangamia kutokana na UKIMWI.Vijana wengi wanaangamia kwa sababu ya
ukosefu wa elimu sahihi kuhusu UKIMWI hali hii yaweza kusababisha ongezeko la
waathirika,Binti mdogo furaha kwa kutokujua athari za UKIMWI anajiingiza kwenye
vitendo vya ulevi na uzinzi kama alivyoshauriwa na rafiki yake Marry na
kujikuta akipata UKIMWI mapema hivyo ni vyema asasi kama za dini zihusike
katika kutoa elimu hiyo
MAUDHUI
DHAMIRAKUU : MAPAMBANO
DHIDI YA UKIMWI
Mwandishi wa
tamthiliya hii amezungumzia kwa kina suala la ugonjwa wa UKIMWI haswa kwa
mazingira ya vijijini,mwandishi amebainisha kuwa chanzo kikubwa cha maambukizi
ya UKIMWI ni umasikini na ukosefu wa elimu sahihi kuhusu VVU/UKIMWI.Pia
mmomonyoko wa maadili,kukosekana kwa uadilifu, ukimya/kukosekana kwa uwazi na
hata upendo wa kweli.
Mwandishi licha ya kuzungumza mambo haya
kuwa chanzo cha UKIMWI,ameonyesha mambo ambayo kama yatazingatiwa na jamii
inaweza kujiepusha na janga hili la UKIMWI,mambo hayo ni kama ngono salama,uadilifu,elimu,uamiifu,ukweli,upendo,uelewa
na uwazi.Kwa ufupi ni kwamba endapo jamii
itazingatia hayo UKIMWI utakwisha, pamoja na dhamira hiyo kuu ya mapambano
dhidi ya UKIMWI ,dhamira nyingine ni :-
1 KUKOSEKANA KWA
ELIMU
Ujinga humfanya
mtu akose maarifa ya kupambana na maisha.Mwandishi wa tamthiliya hii ameonyesha
kuwa ujinga na ukosefu wa elimu ya VVU/UKIMWI ni kikwazo cha mapambano dhidi ya
ugonjwa huu,elimu hii itolewe kwa watu wa vijijini yaani wajue UKIMWI ni
nini,unaenezwa vipi ,unaweza kuepukwa vipi,huduma kwa wagonjwa iweje na je tiba
ipo?
Mwandishi ameonyesha kuwa kwenye kijiji
anachoishi binti Furaha hajui UKIMWI ni
nini,rejea na mazungumzo ya wahusika hawa;
Mwanakijiji
wa kwanza :Ndio lakini kwenye ofisi ya daktari kaambiwa anaugonjwa wa AIDS
Mwanakijiji
wa 4:hicho si kitu kizuri
Mwanakijiji
wa 1:wanauita slimu kwa sababu ugonjwa wenyewe unakondesha
Mwanakijiji
wa 3:lakini unawezaje kupata ugonjwa kama huo?
Mwanakijiji
wa 1:nahisi kuna mtu kamroga pengine rafiki msichana mwenye wivu
Mwanakijiji
wa 2:nasikia unapata kwa kugusana tu
Mwanakijiji
wa 4:au hata kwa kuwa nao chumba kimoja
2
. UMASIKINI
Umasikini ni
hali ya jamii kukosa mahitaji muhimu katika tamthiliya hii umasikini umeonyeshwa
kama sababu ya wasichana kujiingiza kwenye vitendo vya ulevi na akina bwana
Ecko ili wapate vitu vizuri kama vile viatu,magauni na begi.Umasikini humfanya
mtu ashindwe kufanya maamuzi ya busara.Ili kufanikisha zoezi la kupambana na
UKIMWI ni vema kwanza wanakijiji wakawezeshwa kiuchumi. Mwanandishi ameonyesha
kuwa mwanakijiji akikombolewa kiuchumi atashiriki vema kupambana na UKIMWI
3 .MMOMONYOKO WA MAADILI
Mwandishi wa
tamthiliya hii ameonyesha namna jamii inachangia maambukizi ya VVU/UKIMWI
Mfano:furaha na
Marry wanatoroka usiku na kwenda kwenye ulevi (baa) na hata kujihusisha katika
vitendo vya uzinzi kama kauli ya baba yake anavyodhihirisha “anilichokuwa
nafahamu....na hadi sasa Furaha .......ni kwamba amekuwa akitoroka nyumbani usiku
wa manane ......kutoroka bila ruhusa .....baa .... ‘wanaume” “wewe”.....
“Malaya”....asiye na shukrani’’
Mmomonyoko wa
maadili pia umedhihirishwa kwa watu wazima ambao wamekabidhiwa majukumu muhimu
katika jamii kama Padri James ni miongoni mwa watu waliopoteza mwelekeo na
kujiingiza katika uzinzi na waumini wakeHoja hii imedhihirishwa na padri James
mwenyewe anasema “Furaha alikuja kama alivyoagizwa na .....ee.....Ekaristi
takatifu ilipatikana,lazima uelewi jinsi
ilivyo vigumu kwa mtu wa hadhi yangu na wadhifu wangu.......?
Kwa ufupi ni kwamba bwana Ecko,Juma,Kitunda
na Padri James ni watu waliotakiwa kuwasaidia wakina Marry na Furaha kufuata
mwenendo mwema kwa kuwa kiumri walistahili kuwa baba zao lakini ndio wana
uhusiano wa kimapenzi
4
. MAPENZI
Mapenzi kwenye tamthiliya hii yameonyeshwa
kwa namna mbili; Kwanza,mapenzi ya
ulaghai baina ya wanandoa na wanajamii kwa ujumla.Mapenzi haya ni yamekwamisha
mapambano na mafanikio dhidi ya UKIMWI .
Pili,mapenzi
ya ulahai baina ya wanandoa ambapo Bwana Ecko si mwaminifu katika ndoa yake na
wanawake wengine wa kijiji chao wana wanaume wengi hali hii inaweka kijiji chao
katika hatari ya maambukizi ya VVU/UKIMWI
Juhudi ya
kutafuta barua ya orodha ziliwafanya Padri James na wenzake ni ishara ya hofu
ya kutambulika kuwa ni waathirika wa UKIMWI kwa sababu walikuwa uhusiano wa
kimapenzi na Furaha
5. SUALA LA UWAZI
NA UKWELI.
Katika mapambano
dhidi ya UKIMWI suala la uwazi ni muhimu sana katika tamthiliya hii.Furaha
baada ya kutambua ana maambukizi ya UKIMWI aliamua kuandika barua ya ORODHA
kuwataadharisha wanakijiji kuhusu UKIMWI
Furaha alimwambia mpenzi wake Salim kuwa ana
UKIMWI “nina UKIMWI salim’’ zaidi ya hayo,Furaha katika barua yake alitaja
mambo ambayo aliamini wanakijiji wakizingatia wataepuka maambukizi ya UKIMWI
Mama Furaha nae
alijua bayana sababu ya kifo cha mwanae Furaha kuwa ni UKIMWI.Mama huyu
alitambua kuwa ukweli na uwazi ni silaha madhubuti katika mapambano dhidi ya
VVU/UKIMWI
6. UKOSEFU
WA HUDUMA ZA AFYA
Katika tamthiliya
hii mwandishi ameonyesha kuwa ukosefu wa huduma za afya unachangia kwa kiasi
kikubwa katika kupoteza maisha ya watu,katika kijiji cha akina Furaha hakukua
na huduma za afya ndio maana ililazimu daktari wa Furaha achukue vipimo na
kupeleka mjini ambako ndipo huduma hizo zinapatikana ili kubaini tatizo
lililokuwa linamsumbua Furaha
Maisha ya waathirika kama Furaha yalihitaji
huduma za afya ziwe bora na karibu na makazi yao.Huduma hizo zitawasaidia
kuwapa elimu ya magonjwa kama Malaria pamoja na kifua kikuu
Pia upatikanaji wa huduma za afya husaidia
kuwashirikisha wananchi dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI
Mwandishi wa
tamthiliya hii ameonyesha kuwa suala la ukosefu wa huduma za afya linachangia
suala la unyanyapaa kwa wagonjwa wa UKIMWI kuongezeka siku hadi siku na hivyo
kuwafanya watu walioathirika wasiwe tayari kujitangaza
7. TIBA YA UKIMWI
Mwandishi wa
tamthiliya hii ameonyesha kuwa mpaka sasa hakuna tiba ya kitaalamu ambayo
inapatikana,kutokana na hali hiyo watu wengi wamekuwa wakizua tiba mbalimbali mfano
imedaiwa kuwa mtu mwenye virusi vya UKIMWI akifanya mapenzi na mtu mwenye
bikira hupona kama ilivyoeleza Bwana Ecko
Ukweli ni kwamba hakuna tiba ya ugonjwa wa
UKIMWI kinachotolewa kwa sasa ni dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo na si kutibu
Kwa mantiki hiyo ni busara kwa jamii
kuhakikisha kwamba inaepuka njia zote ambazo zinaweza kusababisha maambukizi ya
virusi vya UKIMWI
(B) MIGOGORO
Ni hali ya
kutoelewana baina ya pande mbili au zaidi zenye mitazamo tofauti.Katika
tamthiliya hii kuna migogoro mbalimbali kama ifuatavyo;
Mosi,Mgogoro kati ya mama Furaha na Padri
James,chanzo cha mgogoro ni Padri James kupinga
mama Furaha asisome Orodha hiyo, suluhisho ni mama furaha anamwonyesha kuwa
Padri hana cha kuficha hivyo aliisoma hiyo barua kwa nguvu
Pili,Mgogoro kati ya Furaha na dada mdogo
katika harakati za kutoroka usiku kwenda baa,dada mdogo hapendezwi na tabia
hiyo na suluhisho ni dada mdogo kumtisha
kwenda kusema kwa mama yao
Tatu,Mgogoro kati ya baba na Furaha kuhusu
kutoroka bila ruhusa ya wazazi na pia kujihusisha na
ulevi na umalaya,suluhisho la tatizo hilo ni baba kumpiga mwanae na kumwonya
kwa maneno makali
Nne,Mgogoro
kati ya mama Furaha na Salim kuhusu orodha,Salim kutokukubaliana na mama
Furaha na kulazimika kuipora orodha na kuichana vipande,suluhisho ni mama
Furaha kumkumbusha fadhila za Furaha kwa Salim na kuamua kusoma karatasi
iliyobaki na kuokota vipande vile kuviunganisha na kuisoma orodha
C. UJUMBE
Mwandishi wa
tamthiliya hii anatoa ujumbe kwamba;
Ø Elimu ni silaha muhimu katika
mapambano dhidi ya UKIMWI
Ø Umasikini na ulevi ni vyanzo
vingine vya ongezeko la maambukuzi mapya ya VVU/UKIMWI
Ø Asiyesikia la mkuu huvunjika
guu,Furaha hakusikia maonyo ya wazazi wake akapata UKIMWI
Ø Tamaa mbele mauti nyuma,vijana
wengi wanaendekeza tamaa za fedha au vitu matokeo yake ni kupata matatizo mfano
Furaha alipata UKIMWI
Ø Umdhaniaye ndiye kumbe siye,Furaha
alikuwa anamwamini Padri James kama mlezi wa kiroho matokeo yake akamwingiza
kwenye uzinzi
Ø
Uadilifu,upendo,uaminifu,uwajibikaji
na matumizi ya kinga(kondomu) ni baadhi ya mambo yanayoweza kutuepusha na
UKIMWI
D. FALSAFA
Mwandishi
anaamini kuwa mapambano dhidi ya UKIMWI ni jukumu la watu wote hivyo uadilifu
,uwajibikaji ,upendo,uaminifu ni nyenzo bora katika mapambano hayo
KUFAULU
NA KUTOFAULU KWA MWANDISHI
Kimaudhui,Mwandishi amefaulu kufikisha
ujumbe wake kwa walegwa.Mwandishi ameweza kujadili vyema tatizo la UKIMWI
kwa kutumia mazingira ya kijijini
Mwandishi
ameeleza wasiwasi wake kuhusu uelewa wa watu waishio kijijini kuhusu ugonjwa waUKIMWI
lakini pia ameweza kueleza mambo ya msingi ya kuzingatia katika mapambano kwa
kutumia mbinu ya waraka (barua ya orodha yenye mambo hayo muhimu ya kuzingatia).Barua
ile imetumika kama wosia unasomwa siku ya mazishi siku yenye huzuni na hofu
miongoni mwa watu ili kuleta athari za uoga kuhusu UKIMWI
Mwandishi
ametumia wahusika wachache ambao hawamchanganyi msomaji.Wahusika wa rika na
jinsia mbalimbali wametumika kuwasilisha mawazo ya watu mbalimbali kuhusu
UKIMWI kutokana na uzito wa tatizo linalojadiliwa mwandishi amefaulu kutumia
lugha inayoeleweka kwa urahisi iliyojaa ucheshi tamathali za semi na mbinu
mbalimbali za kisanaa
Vilevile
mwandishi amekuwa makini kujadii utamaduni wa jamii husika kwa kutumia tafsida
kulinda miiko ya utamaduni wetu katika kutumia lugha
Pia mwandishi
amefaulu kupangilia matatizo kutokana na ukubwa wa tukio linalozungumziwa,mwandishi
anaanza na msiba kuwa jambo lililopo mbele yetu ni msiba wa jamii na anamaliza
na sehemu ya mwisho kwa msiba kuonyesha msisitizo wa dhamira kuu
Kwa ujumla
mwandishi amefaulu kwa kimaudhui kufikisha ujumbe kama ilivyokusudiwa kwa jamii
KUTOFAULU KWA
MWANDISHI
Mwandishi
ameshindwa kuelewa njia mbalimbali zinazoeneza UKIMWI toka mwanzo hadi mwisho
wa kitabu mwandishi ameonyesha njia moja tu ambayo ni kufanya mapenzi yasiyo
salama
Hii ni muhimu
ili kupunguza unyanyapaa.
Mwandishi
ameshindwa kugawa kitabu katika maonyesho mbalimbali kitabu kizima kina onyesho
moja lenye sehemu ishirini,mwandishi angeweza kuweka shemu katika maonyesho
matatu.Hiii ingeweza kufuatilia matukio kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasa.
FANI
Mwandishi
amewagawa wahusika katika makundi mawili yaani wahusika wakuu na wahusika
wasaidizi
A. WAHUSIKA WAKUU
·
Mhusika
mkuu katika tamthiliya hii ni Furaha,
·
Msichana
aliehitimu darasa la saba,
·
Furaha
alijihusisha katika mambo ya uzinzi akiwa na umri mdogo
·
Furaha
hakuwa mtiifu kwa wazazi wake kwani licha ya kukatazwa tabia ya utoro wa usiku
na ulevi hakuacha tabia hiyo bali aliendelea mpaka alipopata maambukizi ya VVU
·
Hakuwa
mwaminifu kwa mpenzi wake Salim,alikuwa muongo kwani alimdanganya Salim hana
mwanaume mwingine zaidi yake,
·
Alijihusisha
kimapenzi na watu waliomzidi umri ambao sawa na baba yake mfano bwana Ecko na Padri James
·
Alikuwa
na tama ya pesa na vitu ,alidanganyika kirahisi mfano Marry alimdanganya kuwa
mwema kwa akina bwana Ecko.
·
Si mwaminifu,
·
Muwazi,
·
Mwenye
upendo yuko mstari wa mbele kupambana na VVU/UKIMWI
B. WAHUSIKA WASAIDIZI
Mama Furaha
·
Ni
mama mzazi wa Furaha
·
Ni
mchapakazi
·
Ni
mpole
·
Ni
mama mwenye upendo
·
Mkweli
·
Ni
muwazi
·
Ana
msimamo
·
Anafaa
kuigwa na jamii kwani ni mama aliyeejishughulisha katika ulezi wa watoto na familia nzima
Baba Furaha
·
Ni
baba mzazi wa Furaha
·
Ni
mkali
·
Ana
upendo
·
Ana
lugha kali kwa wanae
Marry
·
Ni
msichana
·
Ni
rafiki yake Furaha
·
Ni
Malaya
·
Mlevi
·
Hafai
kuigwa na jamii
Bwana Ecko
·
Ni
mwanaume mtu mzima
·
Ni
mfanya biashara
·
Ni
mlevi
·
Hafai
kuigwa na jamii,sio mwadilifu katika ndoa yake,ni mwathirika wa UKIMWI
Bwana Juma
·
Ni
mwanaume mtu mzima
·
Ni
rafiki yake na bwana Ecko
·
Ni
mzinzi
·
Ni
mtu mwenye tama
·
Ana
lugha chafu hafai
·
Hafai
kuigwa na jamii
Kitunda
·
Ni
kijana wa mtaani
·
Ni
rafiki yake na Furaha
·
Ni
msanii
·
Sio
mwadilifu
·
Sio
muwazi
·
Sio
mkweli
·
Anaweza
kuwa mwathirika wa UKIMWI japokuwa alitumia kondomu baadhi ya siku alizokutana
na Furaha
MTINDO
Mwandishi wa tamthiliya
hii ametumia mitindo mbalimbali katika kazi yake mfano matumizi ya majibizano
(dayaloji) Mtindo huo huruhusu wahusika wake kuzungumza kwa kujibizana mfano
mazungumzo kati ya Furaha na Kitunda
Furaha:kuvuta
nini lako........(anarudi nyuma)
Kitunda:Mezea
mtoto lazima ujifunze lugha za mitaani
MUUNDO
Mwandishi wa
tamthiliya hii ametumia mtindo wa onyesho ambao sehemu hizo zipo kwenye makundi
matatu ambayo yamejipambanua kutokana na matukio mfano sehemu 1-2 ni mazishi ya
Furaha ,sehemu ya 3-16 ni makuzi ya maisha ya Furaha kwa ujumla ikihusisha
kuugua na kifo chake ,sehemu ya 17-20 ni mwendelezo wa mazishi ya Furaha
ikiwemo mchakato wa kutafuta barua ya furaha (orodha)mchakato unaofanywa a
Bwana Ecko,Padri James na Salim na mwiso wa mazishi ulioamatana na kusomwa
barua ya orodha
MANDHARI
Mwandishi
ametumia mandhari ya kijijini.Hii inawakilisha vijiji mbalimbali hapa Tanzania
na Bara la Afrika kwa ujumla ,mahala ambapo elimu kuhusu UKIMWI haijaeleweka
vema au hakuna kabisa pia huduma za afya kama hospitali hakuna kabisa
MATUMIZI YA LUGHA
Lugha
iliyotumika ni ya kawaida inaeleweka na inazingatia maadili ya kitanzania na
kueleweka vema kwa walengwa na kwa kiasi fulani tamathali za semi na mbinu
nyingine za kisanaa
Misemo/Nahau
Misemo iliyotumika
kwenye tamthiliya hii ni kama ifuatavyo ,
v
“Shuga
dadi”mwandishi akiwa anamaanisha wanaume wenye umri mkubwa wanaopenda
kutembea na wasichana wadogo umri sawa na binti zao
v
“mshamba
“mtu ambae hajui mambo ya mjini au mambo ya kileo
v
“furaha
anavuna mbegu ya kifo aliyoipanda”kuvuna ni msemo unaomaanisha kupata
kitu kutokana na matenyo au maandalizi ,msemo huu ni sawa na “utavuna
ulichopanda”
Ø
MISIMU
Mwandishi
ameweza kutumia lugha ya misimu ili kuweza kumtambulisha muhusika ,misimu
iliyotumika ni ile ya mitaani au ya vijana kutoka kijiweni ,lugha hii tunaweza
kuona ikitumika katika mazungumzo kati ya Kitunda na Furaha mfano
mshikaji,mchizi ,bomba ,poa majani,nitakulinda ,mwanangu ,kuvinjari haya ni
baadhi ya maneno yanayotumika mitaani hususani maneno haya hutumika na vijana
wa kijiweni katika mji
Maana ya
maneno hayo
Mshikaji-rafiki/jamaa
Bomba
mchizi –sawa rafiki/ndugu
Poa-vizuri
/sawa
Ganja,majani-bangi
Nitakilinda-nitakusaidia
Mwanangu-mtu
wa karibu/rafiki yangu
Kuvinjari-kuzunguka/kutalii
TAMATHALI ZA SEMI
Mfano ....yeye
ni kama punda wa kijiji tamathalii hii ilitumiwa kumfananisha Furaha na punda
wa kijiji ambae kila mwaname anampenda ,ilitokana na tabia ya Furaha kuwa
uhusiano wa kimapenzi na wanaume mbalimbali
Pia Kitunda
anafananisha jiji la Dar-es salam sawa na jiji la New york anasema....kisura
sawa na jiji la New york
Pia mwandishi
anapoonyesha namna vipande vya karatasi vilipoanguka baada ya barua ya orodha
kuchanwa na Salim anasema.....vipande vikaanguka kama theruji
Ø
SITIARI
Tamthiliya hii imetumiwa
na baba Furaha anapofananisha watoto wake ma mbu wanyonyao damu wasioweza
kujitegemea anasema “nyie mbu wadogo”
Ø
KIJEMBE
Mwandishi
ametumia kejeli kati ya Marry na bwana Juma anasema
Marry:nieleze wewe
ni mzee wa kutosha kuwa baba angu
Ø
TAFSIDA
Pia mwandishi
ametumia tafsida ili kupunguza ukali wa maneno aliyoyatumia
Mfano :Bwana Ecko:Juma hebu mwangalie yule
msichana anavyotingisha kile alichopewa na mama yake
Bwana
Juma:kama ulivyofanya wewe mishikaki yangu midogo
Tamathali
hiyo(tafsida)imetumiwa badala ya kutaja sehemu zake za siri anazozizungumzia
Ø
TASWIRA
Mwandisha pia
ametumia lugha ya picha(taswira)
Mfano,karibu nitakufa njaa hali nyie mbu wadogo
mnainyonya damu yangu yote,mbu ni taswira inayoonyesha hali ya utegemezi
JINA LA KITABU
Kitabu hiki
kinaitwa ORODHA (The list) neno
lenye maana la mfuatano au mfululizo wa vitabu au mambo.Kitabu hiki kinaonyesha
orodha zifuatazo
Mosi,Orodha
ambayo Furaha alibainisha mambo ambayo yalisababisha kifo chake.mfano;ngono zembe,ukosefu
wa elimu,kukosekana kwa uaminifu,umasikini.
Pili,kuna
orodha ambayo ina mambo ambayo jamii inapazwa kujazingatia ili waepuke UKIMWI
ambayo ni ngono salama,uadilifu,uaminifu,elimu sahihi kuhusuVVU?UKIMWI
Mwisho,orodha
inadhihirika kwa kuitafuta orodha iliyoandikwa na kuachwa na furaha ili isomwe
kwenye mazishi yake
No comments:
Post a Comment