NGOSWE -PENZI
KITOVU CHA UZEMBE
MTUNZI: EDWINI
SEMZABA
MCHAPISHAJI:THE
GENERAL BOOKSELLERS LTD
CHAPA YA 1-1988
UTANGULIZI
Ngoswe-penzi Kitvu cha Uzembe inaonyesha namna jamii inapaswa kushiriki
mipango mbalimbali ikiwepo ya kisiasa kiuchumi na kiutamaduni.Mafanikio ya
mipango hiyo inategemea na kujulikana kwa idadi ya watu utayari,uelewa wa watu
hao kuhusu mipango husika
Tamthiliya hii inaonyesha kazi
ya kuhesabu watu ilivyokwama kijijini kwa mzee mitomingi ngengemkeni kutokana
na uzembe wa afisa wa kuhesabu sensa Ngoswe.
DHAMIRA
1. MAPENZI
Mwandishi Edwin semzaba ameonyesha
jinsi mapenzi yalivyo kitovu cha uzembe,wahusika Ngoswe na Mazoea wametumiwa na
mwandishi kufafanua dhamira hii
Ngoswe baada ya kufika kwa mzee
Mitomingi anashindwa kuitawala nafsi yake mara anapomuona Mazoea,Ngoswe aliamua
kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Mazoea hali iliyomfanya ashindwe kuimudu
kazi yake na mapenzi kwa wakati mmoja.
Ngoswe anamtorosha Mazoea
kitendo hiki kinamuudhi balozi Mitomingi Ngengemkeni (baba mzazi wa mazoea)na
kuamua kuchoma moto karatasi muhimu za serikali.Ngoswe anaonekani ni mzembe kwa
kuwa alishindwa kutofautisha kazi na mapenzi kama msomi (afisa wa sensa
)alitakiwa ajue umuhimu wa kazi iliyompeleka kijijini.
2. ULEVI NA ADHARI ZAKE
Katika tamthiliya ya ngoswe
penzi kitovu cha uzembe mwandishi anaonyesha
namna ulevi ulivyoleta madhara,mfano kuchelewesha kazi.Wahusika Mitomingi na
Ngoswe wanashindwa kukamilisha kazi kwa vile wahusika (wahesabiwa)wapo kwenye
Pombe kama maneno haya yanavyothibitisha;
Mitomingi:Haya ni matatizo yote
hii shauri ya pombe nadhani yupo kilabuni
Ngoswe
:hawezi kwenda kuitwa?
Mitomongi:haitosaidia
mkewe tu hana habari ya kuhesabiwa sembuse hao wengine kwa leo haitowezekana
Licha ya kuchelewesha kazi
ulevi huaribu kazi.Mfano:ngoswe anaunguza karatasi za sensa baada ya kulewa
pombe ya mnazi.
3. ELIMU
Elimu ni chombo cha ukombozi kama
itatumiwa vizuri ipaswavyo,mwandishi wa tamthiliya hii amemuonyesha kijana
Ngoswe (msanii)alivyoshindwa kutumia elimu yake hususani katika kujua namna
ambavyo maisha ya mjini yanavyotofautiana
na maisha ya kijijini,Ngoswe anajikuta akiharibu kazi yake kwa kukosa maarifa.
Mwandishi ameonyesha elimu katika
familia ya mito mingi haikupewa thamani yoyote ile wananchi wengi hawakuwa na
elimu kwa kisingizio cha shule kuwa mbali,ukosefu wa elimu ulichangia
ukosekanaji wa huduma muhimu kama vile hospitali ,miundo mbinu na maji ili
kupata maendeleo,suala la elimu lazima litiliwe maanani watu wakieleweshwa
wataweza kujua wajibu wao :-
Mfano:kujali kazi na kuacha
ulevi “kutumia vema hospitali badala ya kutegemea mitishamba
4. UCHAWI NA USHIRIKINA
Mwandishi wa tamthiliya hii
ameonyesha jinsi watu wengi ndani ya jamii walivyo na imani juu ya uchawi,wanajamii
hawa wameweka vikwazo kuhusu sensa wakiamini kuwa mtu anayewahesabu wenzake ni
mchawi
Mfano:mama anasema mchawi ndiyo
huhesabu watoto wa wenzake ili awaroge sasa wewe ni mchawi? hata kama si mchawi
siwezi kukubali unihesabu maana sijui nia yako kama ni mbaya au nzuri.Imani
hizo ni za kishirikina zinachangia kukwama kwa zoezi la sensa pia maendeleo kwa
ujumla kuwachini,watu wakiugua hawapelekwi hospitali badala yake wanapelekwa
kwa mganga wa kienyeji wakidhani kuwa amerogwa.
5. NAFASI YA MWANAMKE
Katika tamthiliya hii mwanamke ametazamwa
katika mitizamo tofauti kama ifuatavyo;
Ø
Mwanamke
amechorwa kama chombo cha starehe,mwandishi
amemuonyesha mzee mitomingi kuwa na wake wengi (mitala)bila kuoyesha bayana
kazi zao.
Ø
Mwanamke
amechorwa kama mtu asiye na sauti
mfano:Mazoea na mama yake
hawakushirikishwa katika mipango ya kutaka kuolewa mazoea kwa vile walionekana
hawana mchango wowote katika maamuzi hayo
Ø
Mwanamke
amechorwa kama mlezi,
katika tamthiliya hii inamchora
mwanamke kama mtu mwenye majukumu ya malezi ya watoto,baada ya Mazoea kuwa na
mahusiano na Ngoswe mzee Mitomingi anamlaumu mama yake Mazoea kuwa hakuona
dalili ya mahusiano ya kimapenzi kwa kuwa ni jukumu la mama kumwangalia binti
yake.
5. NDOA NA MALEZI
Mwandishi wa tamthiliya hii
ameonyesha suala la ndoa ni suala la hiyari na si kufuata matakwa ya wazazi,Mazoea
alichaguliwa mchumba na wazazi wake (baba yake)hali iliyomfanya kutoroka na
ngoswe
Hali kadhalika katika tamthiliya
hii wanaume wengi wana mke zaidi ya mmoja hali hii inapelekea familia kuwa
kubwa na kushindwa kuzitunza.
Mfano:Mzee Mitomingi ana wake
wawili ambao ni mama Mazoea na mama Mainda,wazazi hawa wanatofautiana katika
malezi hasa kwa Mazoea hali iliyopelekea kuwa na tabia mbaya.
Kwa upande mwingine ndoa zenye mke zaidi ya
mmoja haziwi na upendo ndani ya familia hivyo kuwa kikwazo kwenye malezi.
6. UVIVU NA ATHARI ZAKE
Wanakijiji wa Ngengemkeni mitomingi wengi ni
wavivu muda mwingi wanautumia kwenye ulevi na uvuvi,unawafanya wakose huduma
muhimu kama shule,barabara na hospitali huduma hizi zingepatikana kama wananchi
wenyewe wanajitolea.
Siku zote wavivu wanatafuta visingizio,vifo
vingine vinatokea sababu ya uzembe na uvivu kisha sababu hutafutwa.
Mfano:wanawake wawili walidai mume wao
amerogwa ili hali wenyewe hawakumpeleka hospitali
MIGOGORO
Ni hali ya kutoelewana baina ya
pande mbili zenye mitazamo tofauti Katika tamthilia ya Ngoswe penzi kitovu cha uzembe kuna migogoro mingi ambayo imeweza
kujitokeza kama ilivyoonyeshwa na mwandishi
Ø
Mgogoro
kati ya Ngoswe na wazazi wa Mazoea
chanzo cha mgogoro huu umetokana na
Ngoswe kumtorosha Mazoea,suluhisho wazazi kumfukuza Ngoswe na Mazoea kuchoma
karatasi na kumwadhibu Mazoea
Ø
Mgogoro
kati ya Mazoea na wazazi wake,chanzo cha mgogoro huu ni baada ya Mazoea
kutoroka na Ngoswe ili hali Mazoea tayari ana mchumba wake,suluhisho ni
mitomingi kumchapa mazoea na kuchoma karatasi za sensa.
Ø
Mgogoro
kati ya Ngoswe na serikali,chanzo cha mgogoro huu ni Ngoswe kuharibu kazi ya
sensa na hivyo kusababishia serikali ishindwe kupanga mipango ya
maendeleo,suluhisho halijapatikana hadi mwisho.
UJUMBE
Ø
Si
jambo zuri kuchanganya suala la kazi na starehe au mapenzi,wakati wa kazi uwe
wa kazi na wakati wa starehe uwe wa starehe
Ø
Wavulana
wanaovuruga wasichana siku moja watakamatwa na wasichana wenyewe wanapewa
tahadhali wasiwe na maamuzi bila kufikilia.
Ø
Elimu
ni kitu cha muhimu sana katika jamii na jamii isipokuwa na watu walioelimika
hawawezi kuwa na maendeleo maana ili tuwe na maendeleo tunatakiwa tutupilie
mbali ulevi na uvivu katika jamii yoyote
Ø
uchawi
na ushirikina ni kikwazo kikubwa katika maendeleo
FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa ni
rahisi jamii kuingia kwenye matatizo kama itachanganya mambo mengi kwa wakati
mmoja hivyo ikumbukwe kuwa kila jambo na wakati wake.
FANI
Vipengele vya fani katika kazi
ya fasihi ni muundo ,mtindo,madhari ,wahusika na matumizi ya lugha
MUUNDO
Muundo uliotumika katika tamthiliya
ni wa muundo wa moja kwa moja ambapo kazi nzima ipo katika sehemu
tano ambazo mwandishi amezipa majina ya kitwasira kulingana na ukubwa wa tatizo
linalozungumziwa ,yaani ameonyesha kuingia kwa Ngoswe kijijini mazingira yanayoashiria
hali ngumu ya maisha(kijito)
Ø
Sehemu
ya pili inaonyesha kazi ya kuhesabu watu imeanza na watu hawana utayari na
uelewa juu ya sensa (vijito)
Ø
Sehemu
ya tatu inaonyesha Ngoswe ameanza kujihusisha na mapenzi na ulevi,ambavyo ni
viashiria vya kuharibu kazi yake (mto)
Ø
Sehemu
ya nne inaonyesha kazi aliyopewa Ngoswe tayari imekosa mwelekeo,Ngoswe amebobea
kwenye mapenzi na ulevi, karatasi zinachomwa moto baada ya kumtorosha Mazoea (jito)
Ø
Sehemu
ya tano inaonyesha serikali ikimuhukumu Ngoswe juu ya takwimu zilizoungua moto
na Ngoswe asingizia kuwa kijijini kuna shida ya kuhesabu kwani nyumba
zimejitenga na watu wenyewe kutoelewa (baharini)
MTINDO
Mtindo uliotumika ni wa kidayalojia
ambapo wahusika wake wanazungumza kwa kujibizana
Pia kuna matumizi ya nafsi zote
tatu na nafsi hizo zimetumika katika sehemu mbalimbali.Mfano sehemu ya tano kwa
matumizi ya nafsi ya kwanza pale Ngoswe anapoulizwa na serikali kuhusu takwimu
akajibu “usemi sinao”
MANDHARI
Kitabu hiki kimejengwa katika
mandhari ya kijijini,hii inadhihirishwa na ukosefu wa huduma muhimu kama vile
shule hospitali na miundo mbinu
Tabia za wahusika pia
zinaonyesha mandhari ya kijijini mfano,ulevi wa pombe za mnazi,watu kutojali
elimu,kun’gan’gania mila zilizopitwa na wakati
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha
nyepesi na yenye kueleweka pia mwandishi ametumia tamathali za semi,misemo na mbinu
nyingi za kisanaa.
Tamathali za semi
Hizi ni semi au kauli
zitumiwazo na mwandishi katika kazi ya fasihi ili kuongeza ladha katika kazi
husika
Tashibiha
Ni tamathali ilinganishayo vitu viwili au zaidi
kwa kutumia viunganishi kama mithili ya ,kama,mfano wa
Mfano,Ngoswe anaposhangaa ardhi
ya kijijini kwa balozi Mitomingi anasema
·
Udongo
mwekundu kama ugoro wa sabiani
·
Tazama
suruali yake kama kengele ya bomani
·
Nikitoka
hapa najitupa kitandani kama gogo
Tafsida
Ni tamathali itumiwayo
kupunguza ukali wa maneno
mfano Mainda anasema labda
anajisaidia(Uk 21)
Takriri
ni tamathali inayorudiarudia
neno ili kuweka mkazo juu ya kile kinachosemwa
Mfano; karibu,karibu(pale
Ngoswe alipokuwa akikaribishwa)
Mdokezo
Ni tamathali ambayo hueleza
jambo kwa kukatakata maelezo
Mfano Mazoea anasema
sijui......sijui......siwezi namwogopa baba (Uk 22)
Tanakali za sauti
Ni tamathali inayoiga mlio wa
vitu
mfano Ngoswe alishindwa
kujizuia akacheka ha ha ha ha
Methali
Ngoswe anamwambia Mazoea
v “Penye nia pana njia” (uk 22)
Misemo
v
Hebu
keti tutupe mawe pangoni
v
Kupeleka
chakula ndio unafanya makambi
Taswira/Jazanda
Taswira mbalimbali zimetumiwa
na mwandishi katika tamthiliya hii. Msanii ametumia taswira ya mtu kwa kuhusisha
na matukio ya wahusika.Mwandishi analinganisha mwanzo wa mchezo ni kijito ni
mto mdogo sana hivyo maelezo ya sehemu hii yanategemewa kuwa madogo sana
v
Sehemu
inayofuata ya vijito,sehemu ya vijito inaonyesha kuwa masuala yanashughulikiwa
na kujadiliwa hapa yanaongeza uzito ingawa sio mazito sana
v
sehemu
ya mto inaonyesha ukubwa wa shughuli ya
Ngoswe yuko kazini (yuko mtoni)tayari yupo ndani ya jukwaa bila shaka maji ya mto
ni mengi (matatizo mengi)na hivyo yeyote atakayeingia mtoni yampasa awe
mwangalifu
v
sehemu
ya jito inaashiria kuna hatari, kuna matatizo mengi, katika jito kulivika si
kazi rahisi hatimaye tunaonyeshwa Ngoswe amezama baharini ambapo kuzama kwa
Ngoswe ni baada ya makaratasi kuchomwa moto.
WAHUSIKA
Wahusika ni watu walioshiriki
katika mchezo au tamthiliya husika.
Mwandishi amegawa wahusika
katika makundi mawili yaani mhusika mkuu na wahusika wasaidizi
MHUSIKA MKUU
NGOSWE
Ni msomi anayependa kazi ya
kuhesabu watu lakini kutokana na tamaa ya mwili wake anaharibu kazi baada ya
takwimu zote kuchomwa moto na Mitomingi kutokana na kitendo cha kujaribu
kumtorosha mazoea .
WAHUSIKA WADOGO
Mazoea
v
Msichana
mwenye umri wa miaka 18-20
v
Ni
mtoto wa balozi (Mitimingi)
v
Anawakilisha
wanawake wasio na msimamo katika mapenzi
Ngengemkeni mitomingi
v
Huyu
ni balozi
v
Baba
yake Mazoea
v
Anachoma
karatasi za takwimu kutokana na Ngoswe kutaka kumtorosha Mazoea
v
Ni
mzee aliyeshikilia ukale na anapenda ndoa za mitara
JINA LA KITABU
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe
jina hilo la kitabu linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu ,kwani msanii kwa kiasi
kikubwa amejaribu kujadili na kuonyesha matatizo yanayoikumba jamii katika
shughuli za kijamii,matatizo hayo ni kama uchawi ulevi uzembe na dhana nyingine
potofu
KUFAULU NA KUTOFAULU KWA
MWANDISHI
Mwandishi katika tamthiliya hii
amefeli kwa kuwa ameonyesha matatizo yaliyomo katika jamii bila kuonyesha mbinu
mbadala ya kuyatatua.
No comments:
Post a Comment