UHAKIKI WA RIWAYA
RIWAYA YA TAKADINI
Mwandishi : BEN HANSON
Mchapishaji : Mathews bookstore
UTANGULIZI
TAKADINI ni riwaya inayoeleza
maisha ya jamii za kiafrika na tamaduni zake.Riwaya hii inaeleza namna jamii nyingi za kiafrika
zinavyowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye ulemavu kutokana na mila potofu.Katika
riwaya hii mwandishi amemtumia kijana Takadini aliyezaliwa sope alivyowakilisha
waathirika wa mila hizo potofu.
MAUDHUI
DHAMIRA KUU ; UKOMBOZI
Mwandishi ameeleza kuwa ili
tuweze kupata ukombozi wa kweli na
kujenga jamii mpya tunapaswa kuachana na mila potofu na kukomboka kifikra na
kiutamaduni.Miongoni mwa mila hizo ni mauaji kwa watu wenye ulemavu.Takadini
alizaliwa sope aliamriwa auawe siku ya
pili tu toka atoke tumboni mwa mamaye Sekai.
Aidha makwati anasikitika baada ya kuletewa
taarifa kuwa mtoto aliyezaliwa ni sope anasema.....hilositalielewa......itakuwaje....aliuliza maswali mengi (uk 12).Bila ngozi?,Sope?ni nini ulichokileta hapa
kwetu? maswali haya yanaonyesha
namna walemavu wasivyothaminiwa.Suala hili lilimsononesha sana Sekai inaonyesha
dhahiri mtoto sope katika jamii ya Makwati hakustahili kuishi.
DHAMIRA NDOGO NDOGO
1.
MAPENZI
Mwandishi anaonyesha mapenzi
katika sura mbili tofauti yale ya dhati na ya uongo.Mapenzi ya dhati hayachagui
hali wala mali pia kabila dini wala rangi.Kila mtu ana haki ya kupendwa na
kupenda ,
v
Mapenzi
ya dhati kati ya Sekai na mwanae
,Sekai alikuwa radhi auawe ilimradi furaha yake itimie ya kubaki na mwanawe
sope,hakuogopa kufa alimlinda takadini na kuamua atoroke baada ya makwati
kuruhusu wazee wamwangamize
v
Mapenzi
ya dhati kati ya Sekai na Tendai
hawa ni marafiki wa kweli walifarijiana baada ya kuelezana matatizo
yao,Tendai mke mdogo wa mtemi masasa aliyelazimishwa kuolewa na mzee wa rika la
baba yake.
v
Mapenzi
ya dhati kati ya Mzee Chivero na Sekai,mzee
Chivero alimpokea Sekai na mwanawe Takadini na kuwachukulia kama wanawe (familia
yake) licha ya wanakijiji wengine kuwatenga
Mapenzi ya dhati baina ya
Takadini na Shingai
,Shingai alimpenda Takadini licha ya kuwa na ulemavu wa ngozi (sope) pia
mlemavu wa mguu (alitembea kwa msaada wa gongo) kama anavyokiri mwenyewe “huyu
ndiye mwanaume ninayetaka anioe”
Mapenzi ya uongo ni baina ya
Makwati na Takadini ,Nhamo na Shangai ,Sekai na wake wenza isipokuwa Pindai
2.
NDOA
ZA MITARA
Mwandishi ameeleza athari za
ndoa za mitara kuwa ni pamoja na chuki baina ya wanawake na hivyo kusababisha migogoro
ndani ya familia.Mfano Sekai anasengenywa na wake wenza wake Dedirai,na
Rumbidzai na kudai ni mchawi
Aidha wake wa Mtemi Masasa wanamdharau Tendai
na kuchukulia kama mtoto wao na si mke mwenzao kwa sababu ya umri wake mdogo
3.
MILA
POTOFU
Dhamira hii imetazamwa katika
sura tofauti kama vile:-
v
Wazazi
kuwachagulia watoto wao wenza (wake/waume)Tendai na Shingai wanalazimishwa
kuolewa na watu wasiowataka,hii ni mila potofu zilizopitwa na wakati.
v
Mauaji
kwa walemavu ,mwandishi anaonyesha kuwa watu wenye ulemavu hawakustahili kuishi
katika himaya ya akina Makwati na mtemi
Masasa na ndiyo maana kuzaliwa na kuishi kwa Takadini kulileta mzozo.
4. NAFASI YA MWANAMKE
Jamii nyingi za kiafrika
zinamkandamiza mwanamke na kumfanya mtu duni katika Nyanja mbalimbali za maisha,kama
ifuatavyo;
·
Mwanamke
hana maamuzi yake binafsi,watoto wa kike hawapati haki sawa na watoto wa kiume.mfano
Tendai anaonekana kutofurahishwa na tendo la kuolewa na mume mwenye umri mkubwa
(mzee Masasa)alisema “ni heshima kuwa mke wa mtemi mwenye nguvu
kama Masasa lakini namchukulia kama baba yangu kuliko mume wangu”.......’’(uk 47) hapa inaonyesha mwanamke hana nafasi ya kuongea kama mtu
mwingine.
·
Mwanamke amechorwa kama chombo cha starehe,hili
linaonyeshwa kwa mzee Makwati na Mtemi Masasa kuwa na wanawake wengi kwa ajili
ya kujifurahisha na hili linajitokeza bayana pale(uk 40) aliletwa mtoto kumpa
joto mzee angehisi msisimko wowote ule wa mapenzi.
·
Mwanamke anachorwa kama mwanamapinduzi ,haya
yanajionyesha wazi kwa Sekai na Shingai ni wanawake walioleta mabadiliko katika
jamii.mfano Sekai alikuwa wa kwanza kuvunja mila na desturi kwa kukataa
Takadini asiuawe na kuamua kutorokea kijiji cha jirani pia alileta mabdiliko
akiwa uhamishoni
Shingai
naye mwanamapinduzi kwani alipingana na suala kuchaguliwa mchumba aliamini kuwa
ndoa ya kweli inahusisha watu wawili waliopendana na waliochaguana alisema “ Si
kwamba ninamchukia Nhamo ,la hasha isipokuwa sidhani kama nitakuwa furaha ya
kuishi naye”(UK 110) mwisho
mwandishi anaonyesha Shingai ameolewa na Takadini na wamezaa mtoto asiye sope.
5. UMOJA NA MSHIKAMANO
Umoja na mshikamano ni moja
kati ya nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko na ukombozi wa
kiutamaduni,mshikamano mzuri ulionyeshwa na mzee Chivero,Tendai,mtemi Masasa ulisaidia
kumlinda Takadini dhidi ya unyanyapaa na hatari ya kupoteza maisha katika
mapambano yoyote yenye umoja na nguvu utengano ni udhaifu
6.
UJASIRI
Mwandishi ameonyesha kuwa Sekai
ni mwanamke jasiri aliepambana kufa na kupona kumlinda mwanae Takadini dhidi ya
mila na desturi za kikatili hatima yake kuleta ukombozi katika jamii.
·
Shingai
naye ni mwanamke aliyepambana na matatizo ya kuchaguliwa mchumba,mila
zinazokandamiza wanawake.
7. SUALA LA MALEZI
Malezi
ya watoto yanapaswa kusimamiwa kwa pamoja yaani baba na mama.Katika kitabu hiki
malezi yanaonekana ya upande mmoja mfano Sekai ndio mlezi mkuu wa familia
hususani malezi ya Takadini
·
Shingai
naye anapata malezi kwa mama,shangazi na bibi hata anapokata shauri la kutorokea
kwa Takadini ,anaulizwa kuwa ndivyo ulivyolelewa?mzee Nhariswa anampiga mkewe
na kusema “umefanya nini wewe mwanamke tangu mwanao alivyopeleka maji kwa Sekai
umefuatilia kujua anachokifanya ...uliona dalili kwanini hukutafuta dawa?
UJUMBE
Ø
Walemavu
wana haki sawa ya kuishi kama watu wengine hivyo wathaminiwe.
Ø
Malezi
yanahusisha pande zote mbili yaani baba na mama hivyo kila mmoja awajibike.
Ø
Wanawake
wawe na maamuzi katika jamii hiyo ili wasinyanyaswe
Ø
Ndoa
ni baina ya watu wawili wapendanao hivyo haipaswi kuingiliwa na mtu yoyote
Ø
Umoja
na mshikamano ni jambo muhimu katika ukombozi wa jamii yeyote ile.
MTAZAMO WA MWANDISHI
Mwandishi ana mtazamo wa
kiyakinifu,anaona kuwa matatizo yanayotokana na mila na desturi yanaweza kukataliwa na watu
wengine kwa kuchukua hatua za kujikomboa kama alivyofanya Sekai na wenzake.
MSIMAMO WA MWANDISHI
Mwandishi ana msimamo wa
kimapinduzi kwani ameeleza udhaifu wa baadhi ya mila na desturi zinazokandamiza
watu hivyo anataka jamii ijikomboe dhidi ya mila desturi hizo.
FALSAFA
Mwandishi anaamini kuwa
binadamu wote ni sawa hata kama kuna tofauti za kimaumbile lakini kila mtu ana
haki ya kuishi .
MIGOGORO
Migogoro imejitokeza sehemu
mbalimbali katika riwaya hii ya TAKADINI
kama ifuatavyo;
Ø
Mgogoro
kati ya Makwati na Sekai,chanzo cha mgogoro huu ni (mila na imani potofu) baada ya Sekai kuzaa mtoto
sope,mtoto huyo alipaswa auawe ,mwandishi anasema suala hili halikuungwa mkono
na Sekai,suluhisho sekai aliamua kutoroka kijijini ili kunusuru maisha ya mtoto
Takadini.
Ø
Mgogoro
wa Shingai na wazazi wake,Chanzo cha mgogoro huu ni mila potofu wa kuchaguliwa
mchumba ambaye ni Nhamo ambapo wazazi
walikasirika hata kumtolea maneno mabaya,suluhisho ni Shingai anaamua kutorokea kwa Takadini.
Ø
Mgogoro
kati ya Sekai na wake wenzake,chanzo cha mgogoro huu ni Makwati kuzidisha
upendo kwa Sekai hivyo waliamini kuwa Sekai ni mchawi
Ø
Mgogoro
wa nafsi huu unajitokeza kwa Tendai ambaye aliozwa kwa mzee Masasa ambaye
alikuwa na umri mkubwa
Ø
Mgogoro
wa kijamii,chanzo cha mgogoro ni kuzaliwa mtoto mlemavu(sope)kulizuka mgogoro
baina ya wanajamii ,wao walitaka Sekai na mtoto wake wafukuzwe.
FANI
MUUNDO
Mwandishi ametumia muundo wa
msago (moja kwa moja).Mwandishi ameanza mwanzo kuonyesha mimba ya Sekai ambayo
inazua chuki kwa wake wenza pia anapozaa mtoto wa kiume (sope)
v
Sekai
anaamua kutoroka ili kuokoa maisha ya mtoto,anaishi ugenini siku nyingi hata
sope anakuwa mkubwa na kupata mke na mwisho kabisa mwandishi anaonyesha Sekai
akipanga kurudi kwao.
MTINDO
Mwandishi anatumia mtindo wa
masimulizi vilevile kuna matumizi ya dayalojia (UK 4)Dadirai na Rumbidzai
wanajibizana
Je
na yule mbuzi wako uliepewa na baba mzee Makwati amekupa watoto wangapi?
Tangu
nimepata ni miaka miwili sasa na tayari ana watoto wawili nabado anatarajia
mwingine.
Pia mwandishi ametumia nyimbo
(UK 2)
Mashamba
yote yamelimwa mbegu zote zimepandwa zimechipua na kumea,sisi watatu tumepata
mavuno yetu.,Mheshimiwa wetu amemiliki mavuno kwa mikono yake halisi kutoka
mashamba yetu yote lakini ni kipi alichoambulia kutoka ardhi ile isiyomea
kitu?...........
MATUMIZI YA LUGHA
Mwandishi ametumia lugha rahisi
inayotumika kwa watu wengi,pia ametumia tamathali za semi,nahau,misemo na mbinu
nyingi za kisanaa.
MISEMO NA NAHAU
Misemo na nahau imetumika
katika riwaya hii ili kuipamba kazi yake
·
“Habari
njema kuchechemea kwa mguu mmoja lakini mbaya kukimbia kama sungura.Msemo huu
unamaanisha kwamba habari njema hazienei haraka ila mbaya huenea haraka sana
Pia kuna misemo mingi kama
·
Pokea
upewacho
·
Maosha
ni matamu
·
Kanga
hawezi kutua kwenye bua la mtama
·
Mume
ni kiungo kwa mwanamke
TAMATHALI ZA SEMI
Tashibiha
Matumizi ya tashibiha
yamejitokeza sehemu mbalimbali
v
Giza
jepesi lilibakia ukutani kama mgeni asiyekaribishwa na asiyetaka kuondoka
v
Muda
huenda polepole sana mithili ya mwendo wa kakakuona (UK 6)
Tashihisi
Mwandishi wa riwaya ya Takadini
ametumia tashihisi sehemu mbalimbal; kama vile’
·
Ubongo
wake uliathiriwa kwa mawazo yaliofukuza usingizi wake
·
Fikra
zilizopingana zilijichomeka katika nafsi yake
·
Mwanga
wa jua ungaavu za novemba uliingia ndani na kulifukuza giza totoro.
Dhihaka
Mwandishi ametumia tamathali iliyoonyesha
dharau na yenye lengo la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi lakini kwa
mbinu ya mafumbo (uk 2)
v
“Naamini
ulichobeba sasa ni mtoto na si dubwasha”
Haya maneno yalimlenga Sekai kwakuwa siku
zote waliamini hazai Tafsida
Mwandishi ametumia tamathali
hii kuficha ukali wa maneno (uk 83)
v
Akashambulia
hata sehemu za siri (UK 17)walifanya tendo la ndoa
v
Akajivuta
karibu zaidi naye chini ya guza hawakuzungumza wakafanya kile ambacho kilitokea
kwa asili ya maumbile ,wakakata kiu ya hisia zilizowavuta pamoja miezi mingi (uk
117)
Takriri
v
Wewe
ni sope,sope,sope
v
Najua
,najua (UK 79)
Mdokezo
v
Siku
moja sijui lini ....lakini hivi (UK 75)
v
Sukuma
mara moja tena ....(UK 125)
v
Mtu
mzima kama watu wengine na ameoa
WAHUSIKA
Takadini
·
Huyu
ndiye mhusika mkuu wa riwaya hii
·
Ni
mtoto wa Sekai
·
Ni
mlemavu wa mguu na ngozi (zeruzeru )
·
Kijana
wa kiume
·
Ni
mchapakazi na anayependa kujituma
·
Ni
mtiifu
·
Ni
jasiri
·
Ni
mwathirika wa mila na desturi mbaya au zilizopitwa na wakati
·
Anafaa
kuigwa na jamii
Sekai
v
Ni
mhisika mkuu
v
Ni
mama yake Takadini
v
Ni
mke wa kwanza wa Makwati
v
Mwanamapinduzi
v
Mwathirika
wa mila na desturi zilizopitwa na wakati
v
Jasiri
v
Ni
mwenye huruma
v
Ni
mwenye upendo
Makwati





Chivero







Mtemi masasa






Shingai









Tendai





Dadirai





MANDHARI
Mwandishi ametumia mandhari ya
kijijini.Mandhari hii inawakilisha vijiji mbalimbali hapa Tanzania na Bara la
Afrika.Kwa ujumla mahala ambapo hakuna elimu kuhusu ulemavu wa ngozi
haijaeleweka vema au hakuna kabisa.Pia vijiji ambavyo huduma kama shule hakuna
JINA LA KITABU
TAKADINI linasanifu yaliyomo
kuwa kuna neno TAKADINI lina maana ya sisi tumefanya nini?Swali ambalo wahusika
wengi wanajiuliza mfana Sekai na wanawake wasiozaa na hata vijana au watu wenye
ulemavu
No comments:
Post a Comment