Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni:
- Vitate - maneno yanayotatiza kimatamshi. ⇒ '' Vitate hutatiza kimatamshi
- Vitawe - maneno yenye maana zaidi ya moja. ⇒ Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi
- Visawe - maneno tofauti yenye maana sawa. ⇒ Visawe huwa na maanasawa
Vitate
Maneno yanayotatiza kimatamshi.
- ndoa na doa :
- ndoa ⇒ kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke
- doa ⇒ alama ya uchafu, kasoro au dosari
- baba ⇒ mzazi wa kiume
- papa ⇒ mnyama wa baharini
- fua ⇒ osha nguo, tengeneza vyuma
- vua ⇒ shika samaki kutoka majini; toa nguo
- faa ⇒ inayostahili, inayopaswa
- vaa ⇒ weka nguo juu ya mwili
- ngoma ⇒ ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa
- goma ⇒ acha kufanya kazi
- shinda ⇒ ongoza katika makabiliano, mashindano
- shida ⇒ taabu au matatizo
- shindano ⇒ makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza
- sindano ⇒ kifaa kinachotumika kushonea vitu
- pinga ⇒ kutokubaliana na jambo fulani
- piga ⇒ kugonga au kuchapa
- fahali ⇒ ng'ombe wa kiume. pia ndume
- fahari ⇒ kujivunia, furaha
- haba ⇒ kisichokuwa kingi
- hapa ⇒ mahali karibu
- }
Vitawe
Mano yenye maana zaidi ya moja
- paa :
- kwea (enda juu)
- mnyama wa porini anayefanana na mbuzi
- sehemu ya juu ya nyumba
- kaa au ishi mahali/wakati fulani
- ongoza katika shindano
- tupu
- sehemu yenye moto ya kuni
- mnyama wa majini
- keti chini
- kuwa mahali fulani kwa muda
- mnyama anayefugwa kama ng'ombe
- chombo cha kukunia nazi
- ukoo au watu wenye asili smoja
- sehemu ya kuingia kwenye nyumba
- kitu kinachotumika kifunga nyumba
- unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma
- osha nguo
- toa nguo kutoka mwilini
- toa samaki kwenye maji
- mnyama mkubwa wa baharini
- silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga
- aina ya ndovu
- aina ya pombe
- }
Visawe
Maneno tofauti yenye maana sawa.
- msichana au banati : ⇒ kijana wa jinsia ya kike
- mvulana au ghulamu : ⇒ kijana wa jinsia ya kiume
- huzuni au majonzi : ⇒ hali ya kilio na huruma
- mazishi au matanga : ⇒ shughuli za kumzika marehemu
- wakati au mwia : ⇒ wakati au muda
- mtu au mja : ⇒ mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki
- barua au waraka : ⇒ kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani
- siri au faragha : ⇒ jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine
- macho au maninga : ⇒ sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona
- mwangaza au nuru : ⇒ miyale inayowezesha watu kuona vitu
- Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : ⇒ Majina ya Mwenyezi Mungu